💋ILA BOSS ANAJUA KUPELEKA MOTO 💋 (MWISHO SEASON 1) 19 -- 20
19
Aliingia kaka yake na Glad Mimi ndio nilikuwa namalizia kupika jikoni, G nimekuletea ice-cream 🍨🍦 unayopenda nilinyamaza kimya hadi alipokuja jikoni.
Glad ametoka mara moja nipo mimi peke yangu nilikuwa namalizia kupika niliongea huku nikijiuma uma je kama akiniuliza ameenda wapi ? Nitajibu nini .
Oh Sawa nilijua yupo ice cream 🍨 hii hapa basi utakula wewe...
Nilichukua ile ice cream 🍨 nikamshukuru 🙏 alivyotoka tu nikaanza kuila kama mwendaazimu na ilivyokuwa tamu 😋.
Nilimaliza kula nikatoka hadi sebuleni nilimkuta amekaa kwenye sofa anachezea PC sijui anaandika mambo ya kazini kwao mimi sijui.
Kaka nimemaliza ngoja mimi niende usiku 🌃 umeshaingia...
Mbona unaondoka bila ya kula, na umesema huna hali ngumu nenda kapakue chakula 🥗 🍲 ule ndio uondoke sawa...
Sawa kaka nilimjibu nikaenda jikoni kupakua chakula nilipakua kidogo tu kuona haya 😌 nikala haraka haraka nikasafisha chombo nilicholia nikatoka jikoni.
Kaka asante 🙏 nashukuru sana nimeshiba mimi naenda.
Ngoja aliingiza mkono mfukoni akatoa wallet yake akanipatia elfu kumi, hiyo ya nauli usiku 🌃 mwema kuwa makini...
Asante 🙏 niliondoka nikaanza safari ya kurudi ghetto usiku kama mnavyojua foleni inakuwa inapungua nilifika ubungo mawasiliano mapema tu nikafikia kulala 😴 na hivi nilichoka sana. Asubuhi 🌅 na mapema niliamka nikajiandaa nikaenda zangu chuo nilikaa kidogo Glad naye akawa amekuja.
Jana nilikuuza sikurudi vipi kaka hajakuuliza nimeenda wapi 🤔.
Nashukuru hata hajaniuliza maana sijui ningemjibu nini nilikula nikaondoka, Sawa wewe jitahidi kufanya kazi vizuri kaka yangu hana shida yule kwanza ana upendo 💕 na kila mtu nampenda sana Glavin wangu his my best friend sio kaka tu..
Sijawahi kuona watu wamefuatana wakapendana nyie wa ajabu sana 😂 na uzungu unachangia natamani kama na mimi ningekuwa na ndugu wa kunipenda..
Usijali Nelly I'm here for you now ni mabest friends ila nakuona kama ndugu kwangu ukiwa na shida yoyote usisite kuniambia nina uwezo nacho nitakusaidia..
Asante 🙏 sana Glad lecture huyo kaa vizuri, maana alikuwa amekaa juu ya meza.
Glad alikaa vizuri tukaanza kipindi hadi mida ya saa saba mchana tulikuwa tushamaliza kusoma...
Nilichukua mkoba wangu nikamfuata Glad, mimi naenda bunju kwa kaka yako nikafanye usafi ili niwahi kurudi nyumbani 🏡 mapema..
Sawa kuna mahali naenda ningekuwa sina inshu ningekupeleka, usijali Glad nauli ninayo. Haya sawa niliondoka nikaelekea nyumbani 🏡 kwa kaka yake na Glad, hata jina nilikuwa simfahamu kumbe ni Glavin jina zuri limekaa kisomi tuachane na hayo tuendelee na story yetu 😅.
Nilifika getini niligonga mlinzi alikuja kunifungulia kwa kuwa alipewa maagizo kuwa nitaenda akanipatia funguo.
Niliingia ndani nikaanz
Itaendeleaaaaaaa
ILA BOSS ANAJUA KUPELEKA MOTO
SEHEMU YA 20
Nilikaa kama dakika tano ndipo ujumbe ukarudi kwenye simu yangu. Yah nipikie chakula cha jana kilikuwa kitamu sana angalia humo kwenye friji kuna kuku pika na wali.. Niliishia kutabasamu nilivyosoma hiyo meseji nikaenda jikoni nikaanza kupika...
Mara nikasikia mlango unafunguliwa nikajua labda ni kaka Glavin karudi tu mapema..
Kumbe sio yeye alikuwa ni mdada tena sura sio ngeni nilishawahi kumuona chuoni tena ofisini alikuwa anaongea na lecture...
Enhee wewe nani tena mbona sura sio ngeni? Yule dada aliniuliza.... Mimi sikumshangaa sana kwa kuwa Glad alishanipa taarifa zake kuwa kaka Glavin ana mpenzi anasoma..
Mimi ni mfanyakazi nilimjibu huku naendelea kumuandaa kuku... Mfanyakazi kivipi wewe sio mwanachuo tena unasoma na Glad...
Ndio nasoma nae ni rafiki yangu nilimjibu... Mhh sawa kama umekuja kufanya kazi kweli jitahidi ufanye kilichokuleta sijui unanielewa..... Yule dada aliongea
Sawa nimekuelewa nilimjibu. Aliniangalia akanipandisha akanishusha akaondoka zake .
Moyoni nikasema ondoa wivu dada mimi nina shida ya hela hapa nina mambo kibao yananisubiri mbele... Nilipika nilivyomaliza nikafunika vizuri nikapakua nikala kisha nikaondoka nikamuacha bibie yupo sebuleni anaangalia movie
.
Nilifika nyumbani nikaenda kuoga nikajilalia zangu maana kama kula nishakula kilichobaki ni kulala tu.
Asubuhi nilienda zangu chuo, nikamkuta Glad tayari amefika. Shoga mh jana yalinikuta mambo mwenzio si amenikuta mpenzi wake na kaka Glavin mdada ana nyodo hatari.
Kwani ulikuwa hujui hapo kashaisi unatembea na mpenzi wake yeye hata kufagia tu hawezi kanajidai slay queen mimi na yeye hata haziivagi sana anatakaga aniendeshe kama gari bovu hiyo nafasi siwezi kumpa kabisa .
Utafanyaje sasa ndio wifi
yako tena inabidi tu
ukubaliane na hali..
Mh ngoja tuonehawa ndio wanafanya mawifi tuonekane ni watu wabaya kumbe hata.
Haya rafiki yangu ngoja mimi niende kuna mahali napitia Glad aliniaga akaondoka zake nikiwa nimekaa nikasikia naitwa nyuma... Mwisho wa season one usikose season 2 ipo tayarii nichangie tupate Leo 0768304821 omary luambano 🙏
Makala nyingine zinazocheza na ladha yako
Mapendekezo haya yanatokana na kile unachosoma sasa + Endelea kugundua zaidi
Maoni