JUA: NYOTA INAYOTUPA UHAI HUKU IKISUBIRI KUTUSAMBARATISHA
Nyota iliyo karibu sana na Dunia, haiko mbali sana, si kwenye galaksi nyingine, bali hapa hapa nyumbani, katikati ya mfumo wetu wa Jua. Adui wetu ndo mlinzi wetu.
Hii nyota imekuwa ikifanya kazi ya kusambaza uwezekano wa kuwepo na maisha Duniani kimya kimya kwa zaidi ya miaka milioni 4.5, bila kupumzika hata sekunde moja. Yenyewe inakadiriwa kuwepo kwa miaka billion 4.6
Kwa macho yetu, Jua huonekana kama duara la kawaida la mwanga. Tunaliamkia kila asubuhi, na kuliona likizama jioni nyuma ya milima, kana kwamba ni sehemu ya ratiba ya kawaida ya maisha.
Lakini ukweli ni kwamba, kile tunachokiona ni moja ya mashine za asili za nishati ya nyuklia zilizopo ulimwenguni. Hachana na Chernobyl, hiki kinu cha kufua umeme cha angani kina umene wa kuwasha sayari zaidi ya 9 na watoto wao wote.
Kisayansi, Jua ni nyota ya daraja la kati. Ndani yake, katikati kabisa, kuna joto la takribani nyuzi joto milioni 15 za Celsius. Katika joto hilo, atom za Hydrogen zinabanwa na nguvu ya gravity mpaka zinachanganyika na kuunda Helium.
Mchakato huo unaofahamika kama "Nuclear Fusion" ndio chanzo cha mwanga, joto, na uhai wote duniani.
Kuungana kwa viindi vya atoms za Hydrogen kuunda Helium kunazalisha nguvu kubwa sana ya mionzi na mionzi hii husafiri kwenye anga tupu mpaka kutufikia huku Duniani.
Lakini hapa kuna jambo lingine la kushangaza. Mwanga tunaouona ukitoka kwenye Jua unakuwa sio wa wakati huo, bali unakuwa ni mwanga wa muda kidogo uliopita.
Iko hivi....
Mwanga pamoja na mionzi yote husafiri kwa mwendokasi wa kilomita Laki tatu kwa sekunde moja (300,000km/s).
Chukulia kutoka Dar mpaka Bukoba, kwenda na kurudi mara 200 ndani ya sekunde moja.!
Jua lipo kilomita Milioni 150 ukitokea duniani, kwa huo umbali mwanga ukitoka kwenye Jua unatakiwa kusafiri kwa dakika 8 njiani ili kufika huku.
Kiuhalisia ni kwamba, unachukua muda wa takribani dakika 8 na sekunde 20 kusafiri kutoka kwenye Jua hadi unafika duniani. Ina maana kwamba kila unapolitazama Jua, unaona taswira ya zamani, unaangalia kile kilichotokea kwenye Jua dakika 8 zilizopita.
Kwa mfano tu, kama Jua lingeweza kuzimika ghafla, Dunia ingeendelea kuwa na mwanga kwa dakika 8 bila kujua hatari inayokuja. Mimea ingeendelea kufanya photosynthesis. Ndege zingekuwa angani.
Watoto wangekuwa wakicheza. Shughuli za kila siku zingekuwa zinaendela kwa sababu mwanga bado upo njiani unakuja, hatujui kama nyuma kuna giza linafuata, mara ghafla tunakumbwa na Giza.
Fikiria hilo kwa sekunde chache. Hilo linatufundisha jambo moja la kina sana:
Maisha yetu yote yanategemea nyota ambayo hatuioni kwa wakati halisi. Yaani dakika 8 zilizopita Jua limeunda nguvu ambayo inanifanya niishi sasa hivi.
Jua pia hupoteza uzito wake kila sekunde– takribani tani milioni 4 za uzito hubadilika kuwa nguvu na nishati safi ya mionzi na mwanga. Hata hivyo, ni kubwa kiasi kwamba upotevu huo hauonekani.
Jua lina uzito mkubwa sana, akiba ya kutosha kuendelea kuwaka kwa zaidi ya miaka bilioni 5 ijayo.
Lakini pamoja na utulivu wake, Jua lina tabia nyingine isiyozungumziwa sana, na hii ndo hatari sana, rafiki wetu wa kutupambania kupata maisha anapogeuka kuwa muuwaji wetu.
Jua hutoa milipuko kama huku Duniani tunayoona kama Volcano, kwenye Jua volcano huitwa "Solar Flare" utofauti wa Volcano na Solar Flare ni kwamba huku kwenye volcano mlipuko huanzia kwenye kiini (core) ya gimba, wakati kwenye Flare za Jua mlipuko huwa tu kwenye ganda la juu linaitwa "Chromosphere"
Huu mlipuko huzalisha ujiuji wa moto (hot plasma) na huweza kuruka hadi kutoka kwenye angahewa ya Jua na kuruka juu nje ya Jua hiki kitendo huitwa "Coronal Mass Ejections"
Ni kitendo cha maada za moto kutoka kwenye Corona ya Jua na kupaa mbali zaidi na wakati wa kufanya hivyo husukuma hewa ya moto kutoka kwenye Jua (Solar Wind) kuelekea Sayari za karibu.
Upepo huo mkali wa mionzi na joto kali huweza hadi kufika duniani na kuathiri ukanda wa umeme na sumaku wa Dunia, hii itaathiri mawasiliano, satelaiti, na mifumo ya umeme duniani.
Kwenye makala niliyoandika tarehe 24 mwezi May, 2023 niliwahi kuelezea hizi Solar Flare, Solar Wind na Solar Storm zinavyoathiri mawasiliano ya satellite na internet Duniani na hiyo siku Dunia nzima ilikuwa haina mtandao.
Nakumbuka Jamii Forum 'waliiba' ile makala wakaiweka kwenye platforms zao, kutumia Expert Member kwemoj ya majukwaa yao, nikawa nazozana nao.!
Sio hiyo tu, pia hizi Solar Wind ndo huwa zinasababisha Aurora kwenye North au South Polar Lights, joto la vimbunga hivi kutoka kwenye Jua husababisha "Heat wave" hasa kwenye nchi za Kaskazini na Kusini.
Heat wave ni kitendo cha joto kuongezeka ghafla ndani ya mda mfupi na kuathiri mazingira, jambo ambalo huwa linasababisha moto wa nyika mara kwa mara kwenye misitu ya Marekani, Canada na Urusi, hata India nayo iliwahi kukumbwa na heat wave. Wafatiliaji wa account hii wanajua nishaeleza sana.
Hilo ndo Jua, urafiki wake na Dunia unatupatia mazingira ya kutupa maisha, lakini mara kadhaa lazima tulionje joto la jiwe hilo laini linalolipuka.
Inasadikika baada ya miaka milioni 5 Jua litamaliza akiba yake ya maada za kuunda joto, yaani Hydrogen atoms zitakuwa zimeisha na msawazo wa Helium utakuwa mkubwa sana na italazimisha Jua kulipuka na kusambaratika.
Mlipuko huo huitwa Supernova, kitendo cha Nyota kupasuka baada ya kumaliza akiba yote ya atoms za Hydrogen za kufanya Fusion kuunda joto na mionzi.
Supernova zimesharekodiwa kadhaa kutumia telescope na kutupa ushahidi wa kinachohofiwa kutokea, na kweli kitatokea na hapo itakuwa mwisho wa mfumo wa Jua maana sayari zote zitasambaratishwa na ambazo hazijasambaratika zitapotelea mbali huko kwenye anga.
Enjoy Jua likiwa bado lipo, na kabla halijachanganyikwa kuachia uji wa moto unaohatarisha maisha ya Sayari zote za angani kwenye mfumo huu.
Mimi ni mdadavuaji wako wa Sayansi ngumu kwa lugha rahisi, niite Cekam Cekam's na sasa hivi nimeanza kuunda Video za ma-Alien zitakuwa zinakuja wakati wa mapumziko.
Makala nyingine zinazocheza na ladha yako
Mapendekezo haya yanatokana na kile unachosoma sasa + Endelea kugundua zaidi