NAKUPENDA BILA MIPAKA 151 -- 157
Kwenye akili yako vuta picha zile Abaya za kituruki, halafu ziwe tatu, nzuriiiiiii, rangi nyeusi, rangi nyeupe, na zambarau fulani imechanganyika, halafu kuna gauni mbili za ukali, eenh, eenh sijui nirudie tena kutoa ushuhuda wangu.
Natamani sana ila nitawezaje sasa mnielewe, ni Mr Gallen ameninunulia. Mimi sasa naangali nakumbatia, na viatu vya chinichini halafu mafuta ya kupaka, halafu na nguo za ndani. Ninatabasamu nikisema “oooh!!, oooh jamani, jamani.”
Nikaona tu bora nikaoge kwanza, nitoe kwanza msisimuko wa Busu. Tena busu lenyewe hata mswaki, nisiseme sana si mnajua sijaoga. Sijui hata amefurahia ila mimi nimefurahia balaa. Nilipoingia bafuni, mimi nafanya hata vitu sijawahi kufanya.
Nilijikuta napiga mswaki nawaza tu, hata nilipoanza kuoga nilisema “Nilikuomba Mungu, kibali kila mahali, najua maombi yangu uliyasikia, ni kazi sana kukumbushia kila siku. Nipo hapa nakukumbusha tena na tena. Mungu kwenye mahusiano, nipate kibali isivyo kawaida. Naomba ndoto hii iwe kweli. Nakuomba.”
Nilimaliza kuoga, nikatoka jamani kwanza ungeziona bra zangu za mwanzo halafu hizi nimeletewa unaweza kukaa chini ucheke. Kuna braaa nzuri jamani, mwanzo nilikuwa navaa kishikilia kifua tu halafu sasa hizi ndiyo braa.
Nilijiweka sawa halafu sasa nikaweka Abaya langu black, halafu mtandio ule nikajifunga mtindo fulani simple wa kupendeza halafu nikajiangalia kwa kioo.
Nimependeza sana, mimi kumbe mzuri ni nguo tu zinafanya usinizingati. Ndugu yangu nunua nguo, nguo hubadilisha mambo, nguo za kuvutia na nzuri huvuta neema nakuambia.
Nilikuwa kama sio Nazwi mimi, nimependeza balaa. Acha kabisa hata mimi najishangaa najiambia “kumbe mimi ni mzuri hivi jamani, sikuwa najua hili, nimependeza saana.”
NAKUPENDA BILA MIPAKA:152
Nikatabasamu, na kusema “wacha nikashtue watu sasa.”
Niliweka vitu vyangu vizuri kabisa halafu nikatoka.
Nilipofika jikoni Maria alishangaa akisema “wewe, ni wewe Nazwiiiiiii, Mungu wangu!!. Mdogo wangu ako kamwili chako kazuri, kaumbo chako sasa kalivyo, eenh Hii gauni usiwahi kuvua kama uvae kila siku. Umependeza sana, umependeza mno. Ujue nilikuwa nikusahau. Hapa nishaelewa dokta ana macho ya ndani, alielewa mapema sana.”
Nikacheka na kusema “dada Maria ujue una mdomo sana niache eenh, supu yangu si tayari.”
Alitabasamu akisema “Wallah umependeza kaka akikuona lazima atakusifia, hakuna mtu anakufahamu asikusifie. Hili gauni tamuuu.”
Nikacheka nikisema “dada tamu tena, halafu sawa gauni ila hili lina jina lake, linaitwa Abaya.”
Alitabasamu, ananitazama anatabasamu tu akisema “Mungu, Mungu aanh kuna watu ni wazuri. Wewe ni kazuri sana. Mungu wangu.”
Dada Maria tu sasa anataka kichwa kipasuke sio kwa sifa hizi. Mimi nilisogea na kuanza andaa chakula kisha nilisema “Boss ana njaa muhudumie supu hii na ndizi hizo hapo, hii napeleka kwa mama sasa.”
Alitabasamu, nilianza kwenda. Dada Maria aliita “nesi!!”
Nilisimama na kumtazama, alisema “tumefurahi upo hapa asante. Ilikuwa mbaya.”
Nilimtazama na kutabasamu tu halafu nikaendelea na safari.
Nilifika mpaka chumbani kwa mama, mama alikuwa ameamka, ile naingia mama alishangaa hata aliachia mdomo. Nikasimama na kusema “mama jamani.”
Alishangaa akisema “ni wewe binti yangu Nazwi?”
Nilicheka kidogo na kusema “ila mama, haya jiandae supu nzuri ipo tayari.”
Mama alinishangaa bado na alisema “mwanangu umependeza. Weka supu hapa simama hapo.”
NAKUPENDA BILA MIPAKA:153
Nilitabasamu na kufanya alichotaka, akasema “ebu zunguka, eenh zunguka. Eenh Mungu nna binti mzuri sana. Hii nguo imekupendeza mno. Uzuri wako umeonekana vizuri kabisa. Mwanangu jamani, wewe ni mrembo sana. Nafurahia kukuona hapa. Nashukuru sana mwanangu.”
Nilitabasamu na kusema “mama nashukuru sana kwa upendo. Tule sasa.”
Mama alitabasamu, halafu alisema “ukweli lazima niseme, mwanangu wewe aaah wewe chombo tena chombo saafi. Nashindwa hata niseme nini. Nishushie tu supu, vipi mwanangu amekuona?”
Nilitabasamu tu nikisema “mama lakini upoje.”
Akacheka na kusema “nitakupa umbea nile kwanza.”
Nikacheka huku nikisema “mama ushaanza mimi sitaki. Nakulisha huku unaniambia eneh niambie.”
Mama akasema akicheka “dokta kabale nikiwa hospitali walifikiri nimelala. Akawa ana mshauri Gallen. Tutafute nesi mwingine, huyu naona mjuaji sana anaweza sababisha tatizo.”
Gallen sasa anasema “hapana, Nazwi hapaswi kuacha kazi ni mtu pekee anaongea lugha moja na mama.”
kabla Dokta hajasema kitu nikafungua macho na sauti ikatoka nikisema “sitaki yeyote, binti yangu arudi na mna maelezo ya kuniambia kwanini sio yeye. Namtaka Nazwi.”
Dokta niliona sura yake, ikawa inatisha ila anatabasamu. Nikacheka na kusema “ila mama, kwahiyo umbea umeishia hapo?”
Akacheka na kusema “najikaza mwanangu, kwasababu wewe upo. Ila sipo vizuri.”
Nikamwambia kwa upole “kula mama ndiyo utapata nguvu.”
Mama alitabasamu na kusema “umependeza sana mwanangu. Nitakununulia nyingi kama hizi. Nazwi asante upo hapa. Nashukuru kwa msaada wako binti.
NAKUPENDA BILA MIPAKA:154
Hakuna kiwango cha pesa nitakupa kitatosha. Lakini mwanangu nataka ujue ya kuwa nakupenda sana. Nitahakikisha una furaha wakati wote.”
Nilitabasamu na kusema “asante sana mama.”
Aliniambia kwa upole “niahidi hutoniacha binti yangu.”
Nilitabasamu na kusema “Nakuahidi mama. Sitakuacha hata iweje.”
Alitabasamu na kusema “Supu tamu, asante sana. Na nakupenda mwanangu.”
Nikatabasamu pia na kusema “Nakupenda mama.”
Huyu mama anaumwa, ukimtazama tu unajua kabisa anaumwa ila ni mtu Imara sana. Ni imara. Alilala tena nikiwa namtazama huku natabasamu tu, nikamuweka sawa, nikatoa vyombo na kurudi kumtazama.
Nimekaa pale kwenye kochi, na nguo yangu mpya. Najitazama natabasamu tu, siamini, siamini kila kinacho nitokea.Sijui ni ndoto naota, sijui ni ukweli huu au nijizabue ndiyo nijue haya yote ni ukweli na sioti ni uhalisia.
Mambo mengi sana yametokea, mengi sana. Nikisema mambo mengi namaanisha mambo mengi sana. Lakini katika mambo mengi yaliyotokea hili la leo, hili la busu ni jambo kubwa kuwahi kutokea kwangu tangu dunia yangu iumbwe.
Hata natamani nifanye tangazo maalumu lakini nafanyia wapi hili na wewe likufikie eenh. Hahahahaaa!!, hahahahahah!!, hahahahaha!!!, eenh nachoka mimi jamani, kila ninachowaza kuhusu busu na Mr serious wangu ni uchizi. Ni uchizi naona kabisa mwenzenu naenda kuchanganyikiwa.
Lakini kadri muda ulivyokuwa unazidi kwenda, kadri nilivyokuwa nazidi kukaa hapa ndiyo nilikuwa nazidi kuumia moyo wangu juu ya ndugu yangu, rafiki yangu kipenzi Dorice. Anateseka sana, anapitia maumivu, anaumia juu ya mama yake, mama yake na matendo yake. Roho yangu ilikuwa ina hangaika hata nikawa nakumbuka vile analia, vile anaumia, vile anasimulia. Ushirikiano wetu, umoja wetu namna tunaishi nilijikuta napoteza hata furaha. Nilikuwa tu natamani nirudi nyumbani nikamuone.
NAKUPENDA BILA MIPAKA:155
Mama alitumia muda mwingi sana kulala, muda wote huo sikuwa nimemuona Boss kabisa. Ni wazi na yeye alienda kupumzika. Ana stahili kupumzika. Amechoka sana. Siku zote hizi ana hangaika juu ya mama yake mpaka analala nje kwetu mchezo. Nilitulia tu.
Ulifika muda nilimwamsha mama, mama alipoamka niliona tu nimsafishe ili azidi kuchangamka. Nilianza kumuhangaika. Mama alikuwa tu ananitazama na aliniambia “pole sana mwanangu.”
Nilitabasamu na kusema “mama wewe ndiyo unastahili pole hii. Unaonekana umechoka sana mwanangu.”
Mama alinitazama akisema “ni kweli mwanangu, ni kweli nachoka. Dawa za safari hii sielewi kabisa. Lakini jambo zuri ni kuwa wewe upo hapa.”
Nilitabasamu, mama aliendelea tu kunitazama huku mimi nikifanya mambo yangu. Sikutaka hata kusema lolote niliacha tu yeye ndiyo ataongea. Mama yangu alisema “Nazwi mwanangu upo sawa kweli?”
Kwa upole nilimjibu “nipo sawa mama yangu.”
Kabla hata mama hajamaliza, dokta huyu hapa. Hajafa tu jamani. Nikajua leo ni kusafirisha maana kwa mbwembwe zake zile na kilichotokea. Aaaah dada ana roho ya paka huyu. Tena anatabasamu kabisa na alinisalimia “Hujambo nesi?”
Nilitabasamu na kusema “Shikamoo Dokta.”
Tena kaja kapendeza, eenh sijui ndiyo ameenda kujiupdate. Au ndiyo sijui tuseme amejipanga upya. Huwa anapendeza. Safari hii. Amependeza kupitiliza.Na hapa nisiwe muongo anapatia sana. Mimi haya sio mambo yangu, sio mambo yangu mimi tu nioge nivae masuala ya kujipodoa hata pakuanzia mimi sijui bora hata rafiki yangu Dorice.
Alitazama na kusema “umependeza nesi.”
Nikatabasamu na kusema “umependeza sana dokta.”
[3/28, 2:51 AM] faraja simulizi nunua: 156 - 165 SEASON FOUR
NAKUPENDA BILA MIPAKA:156
Akapiga hatua akisema “mama yangu mzuri. Unaendeleaje. Nilikumiss sana na sasa uniambie, kwanini ukaondoka hospitali hujaniambia mwanao.”
Mama alimtazama akisema “nisamehe tu binti yangu. Sikutaka kuendelea kukaa pale. Ilipotokea nafasi nikaona tu niondoke zangu.”
Akawa anacheka cheka na mama. Mara Boss akaingia. Alipoingia tu alitabasamu, tukatazamana mimi haraka nikakwepesha macho na kusema “Nimeondoka nyumbani mapema sana bila hata kuaga yeyote. Lazima watakuwa na wasiwasi sana. Kama hamtojali naomba kuondoka sasa.”
Mama alinitazama na kusema “upo sahihi mwanangu, lakini unaonaje unipe supu tena halafu ndiyo uondoke.”
Nilisema kwa upole “bila shaka mama, bila shaka.”
Nikatoka, baada ya kutoka nikaingia jikoni, na dada Maria alinisaidia. Nikarudi chumbani bado Dokta alikuwa hapo, mimi kimya kimya nilianza kumpa mama ile supu. Mama aliinywa vizuri sana, nikampa na maji alimaliza ile niliyokuwa nimeweka.
Alinitazama na kusema “Binti yangu sasa unaweza kwenda, lakini kesho uwahi sawa eemh.”
Nilitabasamu na kusema “upo sahihi mama. Kesho nitawahi.”
Alisema kwa upole “nashukuru sana, nashukuru.”
Nilitabasamu na kuaga. Dokta na yeye alisema “Uwe na siku nzuri nesi eenh.”
Dokta mnafiki huyu, mnafiki kama nini. Nilitabasamu tu huku moyoni nikisema “unaniletea sanaa THT hapa ndiyo jumba la sanaa. Tutanyooshana mnafiki sana wewe.”
Nilitoka mpaka kwa chumba changu cha kubadilishia nguo. Nilikusanya vitu vyangu na kuanza kutoka. Nilipita kumuaga dada Maria maana na yeye hakuwa sawa.
Hivyo niliagana na yeye na kumtaka tu aniambie kama akihitaji msaada hata mtu wa kuongea naye nipo kwaajili yake. Alitabasamu na kusema “Nakupenda mdogo wangu, wewe ni mkarimu.”
Nilimwambia kwa tabasamu “Nakupenda dada maria wangu, cha umbea wangu.”
Angalau akacheka, nilimkumbatia na kuondoka zangu.
NAKUPENDA BILA MIPAKA:157
Sasa naondoka rohoni naumia mimi, naondoka ondoka vipi Mr Gallen hata hajaniambia nimependeza, hajanisifia kweli ni haki jamani. Sasa nifanye nini sina namna inabidi tu niondoke zangu tu. Unajua ile eneh umependeza mwenyewe halafu hukutani na uliyemlenga, au umejiandaa mwenyewe akija akukute umependeza halafu haji. Basi yale maumivu moyoni sasa hapa ndiyo nayahisi.
Nakwambia sasa, nimetoka nje naelekea getini nifunguliwe mimi niondoke zangu. Nimetoka tu getini, ndinga hii hapa.
Nilitabasamu, halafu sio amekaa huko ndani ya gari, ameshuka, amekuja upande wangu kunifungulia. Kwanza sasa tangu nimfahamu sijui ana nguo ipi haijampendeza. Bana ana pendeza huyu, muanko ana vaa huyu mimi ni tabasamu tu.
Subiri!!, subiri taratibu kabla hatujaendelea, eenh nakukumbusha kwanza ni Tajiri, Ni boss, ni mkubwa, ni mtu mwenye misimamo lakini linapokuja suala la mimi, hivi vyote sivioni, anashuka na kunifungulia. Nilipoingia alinitazama na kusema “Hey, naweza kukukumbatia.”
Nilitabasamu, alinikumbatia kwa muda, akanifunga na mkanda wa gari mimi hapo natetemeka kindanindani asijue tu maana niseme ukweli kwake mimi sijiwezi kabisa. Baada ya hapo aliwasha gari hakukaa kimya alitabasamu na kusema “Nazwi umependeza mno.
Hivi si umeelewa, amesema mno, mbele ya sana unajua eemh, nilitabasamu na kusema “nashukuru sana. Nguo zote ni nzuri, lakini Boss ni gharama sana.”
Akatabasamu na kusema “Gharama haina maana kulinganisha na umuhimu wako Nazwi. Umependeza sana.”
Nilitabasamu, unasikia maneno haya, mimi ni bichwa linanielemea kama linapasuka.Ukiniona sasa natabasamu tu nasema “asante sana.”
Makala nyingine zinazocheza na ladha yako
Mapendekezo haya yanatokana na kile unachosoma sasa + Endelea kugundua zaidi



Maoni