Simulizi za john
0789 824 178 ,
1000
Nikasema, โMama, hakuna chochote, baba alikuwa anaangalia vidonda tu.โ Akasema, โUnasemaje? Baba? Baba gani? Babako yule? Unamudu ili unibadilishe uishi kwenye ghorofa hii, si ndiyo? Unaona ninafaidi, unataka kuwa mke mwenza, si ndiyo? Ulimuonyesha nini huko chini?โ Nikasema, โMama, mbona unaniambia maneno ambayo sielewi? Unanionea!โ Akasema, โNani anakunea?โ Alinishika, akanibamiza ukutani, akasema, โNitakuua!โ Nilipasuka kichwani kisogoni, damu zikamwagika. Mama hakustuka, akaendelea kunipiga, kisha akasema, โToka kwangu, toka!โ Akanisukuma nje huku navuja damu, nalia, bila kusema nisameheโnilishaamua kuondoka, bora nikafie mbali.
Nikimkumbuka mama na bibi yangu, nilitamani kurudi, lakini baba yangu ni mkatili, ataniua. Nje ya nyumba kuna kibaraza chenye ngazi, akanisukuma, nikabiringika kama mzigo, nikatua chini. Masai aliona, akaja akikimbia, lakini mama aliniokota, akaanza kunipiga tena, akisema, โOndoka kwangu, mshenzi!โ Nikaskia sauti, โMama Zawadi, mshenzi wewe, mwache mtoto wa watu!โ Alikuwa Baba Zawadi. Masai alinishika, nikiwa navuja damu puani na mdomoni, bila nguvu. Baba akasema, โMasai, kampakie kwenye gari haraka! Na wewe, mwanamke mkatili, nikirudi nisikukuteโuna roho mbaya kama paka!โ
Masai alinibeba, nikatolewa nje ya geti kwenye gari la baba. Baba alipanda, akasema, โMasai, hakikisha nikirudi simkuti yule mwanamke, nitamuua!โ Aliwasha gari. Nakohoa damu, baba akaogopa, akasema, โZawadi, nakupeleka hospitali, sawa?โ Sikuweza kusema. Alipita kwa polisi, akachukua karatasi, tukafika hospitali. Alinibeba, akipiga kelele, โNesi, daktari, nisaidieni mtoto huyu!โ Walinipokea, nikawekwa kwenye kitanda cha emergensi. Nilitibiwa, lakini sikusikia maumivu, kama sielewi kinachoendelea. Nilipopewa dawa, nikapitiwa na usingizi.
Niliamka niko kitandani, bila nguo, nimefunikwa shuka. Nikajiona niko hospitali, chumbani chenye vitanda vinne, lakini hakuna mtu. Nilianza kukumbuka yaliyonipata, machozi yakanitoka. Nesi akaja, akasema, โMuda wa dawa, binti mzuri, umeamka?โ Nikasema, โNdiyo.โ Akasema, โUnajisikiaje?โ Nikasema, โNafuu.โ Akasema, โKakako anakuja, yupo njiani.โ Nikashangaa, โKakangu gani?โ Nikauliza, โKaka?โ Akasema, โYule aliyekuleta, kwani sio kakako? Si babako, bado mdogo.โ Nikajua ni Baba Zawadi. Nikakaa kimya. Alinipa dawa, nikanywa, drip liliisha, akaweka lingine, akatoka.
Nikiwa na mawazo, โMama akirudi, itakuwaje? Bora nitoroke.โ Nilitamani kumtafuta Neema, lakini sikuwa na mawasiliano naye. Nikapanga kutoroka nikipata nafasi. Nikiwa nimelala, Baba Zawadi akaniita, โZawadi!โ Nikaitika, โAbee,โ nikafumbua macho. Akasema, โUnajisikiaje?โ Nikasema, โNaendelea vizuri.โ Akasema, โPole sana.โ Nikasema, โAsante, baba.โ Akasema, โNimekuletea nguo uvae, ile ilichafuka, ilitupwa.โ Nikasema, โBaba, asante, lakini nitaifua.โ Niliongea nalia.
Baba alinishika, akasema, โZawadi, naomba unisamehe kwa yaliokufanyia mke wangu. Alikufanyia kitu cha kinyama. Nitafanya kila kitu kwa ajili yako, nitakupa chochote unachotaka. Nina watoto, nawaza kama sipo, wataishije? Nisamehe, nitakulea kama mwanangu.โ Nikasema, โBaba, naogopa, siwezi kurudi, yule mama ataniua.โ Akasema, โHayupo, hatorudi kabisa kwangu. Uwe na amani, nitakusaidia, nitatafuta msichana wa kazi, sawa? Naomba unipe muda.โ Nikasema, โMmmh, nifanyaje? Nimepigwa hadi nakohoa damu, safari hii ataniua. Je, ni kweli hatorudi?โ Nikawaza, โNikubali au iwaje?โ Itaendelea.