Ingia

Sema Jambo

Unsplashb
750+ Trending Pictures | Download Free Images on gonga94
  Afande sele ft Belle 9 dini tumeletewa

Siri Ya Mvuvi Na Bahari akaniambia kwamba ukimuona Riziki mwambie awahi hospitali kuja kumuona mama yake... Inaendelea... Sehemu Ya 06

3rd Aug, 2025 Views 2



Sasa nikaona hapa mambo yatakuwa magumu kama zitapita siku tatu Riziki hajaonekana inamaana kwamba kesi itaniangukia, siku inayofuata yule ndugu yake na Riziki alikuja mpaka nyumbani kwetu, nikamwambia Riziki aliondoka na Goma yule kiongozi wetu wa kazi na walienda kununua nyavu mjini kwahiyo bado hawajarudi lakini wakirudi nitamwambia na atakuja huko nyumbani, ikabidi nimdanganye namna hiyo, yule ndugu wa Riziki alipoondoka mama akaniulia kwani Riziki mara ya mwisho ulimuacha wapi? nikamwambia mama kwamba Riziki waliondoka na mkubwa wetu wa kazi kwenda kununua nyavu kwahiyo bado hawajarudi, mama akaniambia wewe sema nyavu maana nasikia huko baharini watu wanazidi kupotea,

Badae nikaenda kule ambapo huwa tunapaki ule mtumbwi nilifika na kuanza kuuangalia hadi nikawa najiuliza hivi huu mtumbwi una nini hasa maana inaonekana kama vile ni mtumbwi wa zamani harafu unagombaniwa na watu,harafu bado watu wanapotea kupitia ule mtumbwi, nikawa sina majibu, lakini nikakumbuka Salha aliniambia kwamba nikikosa kile ninachokitafuta, nimtafute yeye ili anipe msaada,

Nikawa nimeelekea kule ambapo mara nyingi huwa nakutana na Salha, nilipofika nikawa nimekutana,nae nikamwambia kuna marafiki zangu wametoweka ghafla na sijui wapo wapi Salha akaniambia kama unataka nikusaidie basi ni lazima twende kwetu ukajitambulishe, harafu tukitoka huko nitakupeleka walipo marafiki zako, nikawaza huu mbona kama vile ni mtego,harafu inakuwa vipi Salha ajue kule walipo wenzangu harafu kingine, wakati huo nilikuwa tayari nimeshajitambulisha nyumbani kwao na kina Latifa, harafu Salha nae anasema nikajitambulishe kwao. nikamuuliza Salha kwani nyumbani kwenu ni wapi, Salha akaniambia sio mbali sana wala sio karibu sana lakini twende utaenda kupajuwa ukifika,

Nikawaza au Salha ni jini maana simwelewi kabisa, lakini nikaona acha nikajitambulishe ili niwaokoe wenzangu, tukaondoka na Salha lakini cha ajabu tukaenda kuchukuwa ule mtumbwi ambao uliwapoteza Riziki na Goma, mimi nikamwambia Salha tuchukuwe mtumbwi mwingine, Salha akasema hapana huu ndio mtumbwi mzuri. kweli tukapanda kisha tukaelekea katikati ya kina kirefu cha maji lakini wakati tunazidi kwenda ghafla nilianza kuona tunaingia ndani ya mji tukiwa baharini, lakini tunavyozidi kwenda nilianza kuona majumba mazuri magari ya kifahari treni za umeme, ule mji wa ndani ya bahari ulikuwa ni mji mzuri ambao una kila kitu, lakini ile bahari ilikuwa imeunganikana hadi na bahari ya huko chini, wakati tunazidi kwenda ule mtumbwi wetu ulianza kubadirika rangi na kuwa na mwonekano wa rangi ya dhahabu,lakini pia ulikuwa ukijiendesha wenyewe, tulienda hadi sehemu ambayo wamepaki mitumbwi na boti, Salha akaniambia usiwe na hofu huku ndio kwetu, barabara zao zilikuwa ni zakisasa zaidi ambazo kwa dunia yetu ya kawaida bado hatujazifikia sababu zina mwonekano tofauti sana,

Tuliingia kwenye jumba moja kubwa na lakifahari, lilikuwa kama jengo la kifalme kisha Salha akanishika mkono hadi mule ndani, ndani ya lile jumba la kifahari walikuwemo watu wengi na wasichana wazuri kuliko hata Salha, nilianza kushangaa lakini sielewi napelekwa wapi, tukafika hadi kwa viongozi wa lile jumba, Salha akaniambia hawa ndio wazazi wangu, nikawasalimia, wakaitikia vizuri tu, wakati bado nimeduwaa nikisubiri kinachofuata, alisogea mtu mmoja na kuja kunikata katika paji langu la uso damu ikatoka yule mtu alipangusa damu yangu na kuilamba kisha akaipikicha katika mikono yake, alipoipikicha akawaambia wale viongozi wa lile eneo kwamba ndio ni yeye, lakini mimi nikawa sielewi ni yeye kivipi,

Badae yule mzazi wa Salha ambaye ndio kiongozi mkubwa wa pale, alisimama na kusema (tumepata mgeni mpya naamini tutafurahia uwepo wake) mimi nikawa nashangaa mgeni kivipi maana nikakaribishwa kwa heshima kubwa, yule kiongozi wao akasema kwamba huyu ndio mchumba wa binti yangu, watu wote waliokuwepo pale walishangilia kwa furaha, Salha akaniambia usishangae ndio umeshatambulishwa hivyo. badae nikachukuliwa na kupelekwa kwenda kuogeshwa, wale walionichukuwa walikuwa ni wasichana wote,waliponifikisha sehemu ya kuogea walianza kunivulisha nguo zangu zote huku Salha akiwa amesimama pembeni ananiangalia, nikawaambia niacheni nitavua na kuoga mwenyewe, Salha akaniambia usiogope hivi ndivyo wanavyopokelewa wageni, Dah! sikuwa na chakufanya,

Nikaogeshwa na kuvalishwa nguo zingine tofauti na zile nilizokuwa nimevaa, baada hapo tulikaa meza moja na Salha pamoja na wazazi wake, tukala baada ya kumaliza kula Salha akanichukua na kuniingiza kwenye chumba kimoja kikubwa na hakina kitu chochote, Salha akaniambia kwanini una nguvu na hutaki kuzitumia nikamuuliza nguvu kivipi, Salha alinyoosha mkono wake kisha akatoa kitu chenye mwanga mkali na kina mfano wa pete, Salha akaniambia usiogope, alishika kidole cha mkono wangu wa kulia kisha akanivalisha ile pete katika kidole changu cha mwisho,kile kidogo kuliko vyote, ile pete ilianaza kuingia ndani ya kidole changu, lakini kwa maumivu makali, ile pete ilianaza kuzunguka kwenye kidole changu, maumivu yalikuwa ni makali, ile pete ilizunguka ndani ya mwili wangu wote tena kwa maumivu makali sana, nilikuwa napiga kelele lakini Salha yupo kimya, baada ya muda maumivu yakaisha na ile pete, ilitoka kwenye kidole changu na kuanguka chini, Salha alionekana kushangaa,

Salha alitoka na kwenda kuwaita wazazi wake, wazazi wake wakaja kwenye kile chumba na kukuta ile pete bado ipo chini...

Itaendelea...✍🏻

~Daudi~.
   

X
SHARE TO SOCIAL MEDIA

Siri Ya Mvuvi Na Bahari akaniambia kwamba ukimuona Riziki mwambie awahi hospitali kuja kumuona mama yake... Inaendelea... Sehemu Ya 06  >>> https://gonga94.com/semajambo/siri-ya-mvuvi-na-bahari-akaniambia-kwamba-ukimuona-riziki-mwambie-awahi-hospitali-kuja-kumuona-mama-
#Nk #gonga94 #trending #instagood #explore #viral #challenge #simulizi #hadithi #israel #iran #war 

Share on Facebook
Share on Twitter
Share on LinkedIn
Share on Pinterest
 

Afande sele ft Belle 9 dini tumeletewa
SIMULIZI NA SAUTI
gonga94ads - The Best Popunder Adnetwork
offa ya msimu wa nanenane
offa ya msimu wa nanenane

HONGERA WEWE NDIO MSHINDI WA VOCHA YA LEO VOCHA NAMBA (499712343590381) MTANDAO VODACOM TUMA NENO NIMESHINDA KWENDA NAMBA 0768304821


majario rewards 100 Comments 0
 

BLOOD MOON EPISODE 1

mjukuu rewards 100 Comments 0
 

CHANZO NI BOSS 03

mjukuu rewards 100 Comments 0
 

CHANZO NI BOSS 02

mjukuu rewards 100 Comments 0
 

CHANZO NI BOSS 01

majario rewards 100 Comments 0
 

MTOTO WA MAMA LISHE

majario rewards 100 Comments 0
 

MY LUNA SEHEMU YA : 06

majario rewards 100 Comments 0
 

NDOA YA MIE ... 8...

majario rewards 100 Comments 0
 

LUVIE binti wa malaya

Home Login Signup
Top 20 Popular Contact us
Terms & Conditions About us Latest