USIKU MMOJA TU ALIDATA SEHEMU YA 10
ENDELEA........
"Sitaenda mtoni kwa Mfalme, waamshe mabinti wote waje ukumbini. Kwa vyovyote vile mhalifu atapatikana" Malkia aliongea akionekana kuvurugika.
Nilijitia bize na mtoto lakini Kijakazi wa Malkia Shamsa alinidaka.
"Wewe pia ni Mwanamke, njoo hivyo hivyo tena bahati nzuri nguo zako zimelowana na kamtindo ka nywele zako sasa utadhani ni mdogo wake Malkia" Tunu aliongea, ana mdomo huyu acha tu.
Basi alinisaidia kubeba mtoto tukaelekea kwenye kusanyiko lililoitishwa na Malkia Shamsa.
Hata Ada Mama wa Mfalme alikuja kujionea kinacho endelea si unajua tena Wanawake tuna asili ya uongo.
"Kuna Mbweha mmoja alikuwa anaoga na Mfalme kwenye mto ambao hatakiwi kuingia. Sitaki kutumia nguvu nyingi naomba awe mwaminifu kwa kupita mbele adhabu yake itapungua " Malkia Shamsa aliongea.
"Hebu subiri kwanza, kuna mtu kaingia kwenye mto tofauti na wewe " Malkia Ada aliuliza.
"Ndiyo Mama, sielewi hata kwanini unacheka hili jambo halifurahishi hata kidogo sielewi kwanini unacheka " Malkia Shamsa aliongea.
"Wala huna haja ya kupaniki kila kitu kitaenda sawa, na hata hivyo kuna mtu kalowa..... Yaya wa Ivan pita mbele " Malkia Ada aliongea akiwa kakunja sura yake. Huyu naye huwa haelewiki dakika mbili zilizopita alikuwa anacheka ghafla tena kabadilika.
Nilipita mbele kwa aibu,
"Wakati na kuletea Ivan wangu ulikuwa katika hiyo hali " Malkia Shamsa aliuliza.
Nilitikisa kichwa kuashiria ndiyo.
"Kwahiyo wewe ndio ulikuwa unaoga mtoni na Mfalme " Malkia Ada alinidaka kwa mara nyingine tena.
Nilikosa jibu, sikujua nazungumza nini na ukizingatia Mimi ndio mkosefu.
"Ukimya ni jibu tosha, afungwe miguu yake huku na kule kisha farasi liondolewe " Malkia Ada alifunga mjadala.
Sikuwa tayari kufa, nilianguka kifudifudi ili niombe rehema lakini jibu la ghafla lilikuja kichwani mwangu.
"Sikuwa na mpango wa kusema lakini Mfalme Pangani aliniita nimsaidie kutafuta pete yake iliyokuwa imedondokea mtoni....haikuwa rahisi kuipata lakini nilifanikiwa " Nilitunga maneno ya uongo.
"Muite Mfalme Pangani aje kuthibitisha maneno ya Sadia " Malkia Shamsa alitoa amri.
Basi Kijakazi wake Tunu aliondoka kwa kukimbia.
Dakika mbili hazikupita Mfalme Pangani alifika.
"Ni kweli ulidondosha Pete kwenye mto wetu na huyu Yaya wa Ivan alikusaidia kuipata?" Malkia Shamsa aliuliza.
Mfalme alitikisa kichwa chake kuashiria ndiyo.
Niliwaona watu wote wametulia kutokana na ushahidi wa Mfalme. Kwa kuwa ilikuwa ni usiku wote tulitawanyika.
Nilienda chumbani kwangu kubadili nguo, Ivan alikuwa ana sumbua sumbua hivyo nilimuweka Mgongoni.
Haikuchukua muda alilala, ile namtoa Mgongoni nimlaze kitandani Malkia Shamsa alikuja.
Alinipokonya mtoto kisha akamuweka kitandani.
"Pete unayosema ilikuwa mtoni ni hii hapa....alinipatia Mimi kitambo tu. Kwahiyo wewe na Mfalme mmeongea uongo.....naomba ulale kitandani ni kague sehemu zako. Naufahamu vizuri udhaifu wa Mume wangu " Malkia Shamsa aliongea.
Eeh jamani eti nilale kitandani anikague........
Makala nyingine zinazocheza na ladha yako
Mapendekezo haya yanatokana na kile unachosoma sasa + Endelea kugundua zaidi
Maoni