USIKU MMOJA TU ALIDATA SEHEMU YA 11
ENDELEA.......
"Nimesema lala ni kukague au nikuitie nguvu kazi " Malkia Shamsa alifoka.
Nguvu kazi tena jamani nilianguka chini kuomba msamaha.
"Leo siyo siku ya kusamehe naomba uache kuongea neno nisamehe 😠" Malkia Shamsa alifoka huku akinirushia teke.
Nilijitia kuumia kumtia moyo lakini ukweli kutoka moyoni sikuumia.
"Malkia, kila kitu kimetokea kwa bahati mbaya, naomba unisamehe tafadhali, kama utaniua nitaweka wapi sura yangu " Niliomboleza.
"Kesho asubuhi na mapema utaondoka hapa....kwa usiku mzima nitakesha nikifikiria kosa litakalo kufaa na hata hivyo na rahisisha mambo kwa sababu ya Baba yako. Kanifundisha sana mambo mengi kabla sijaja hapa hivyo nitakupunguzia adhabu " Malkia Shamsa aliongea kisha akasepa na mtoto wake.
Walikuja Vijakazi wake wanne wakaniwekea Ulinzi nisije kutoroka kabla ya kupatiwa adhabu.
Mwanzo walikuwa imara, yaani kila nilipogeuka nilikutana nao sura lakini kadri masaa yalivyoenda mmoja baada mwingine alifumba macho yake sababu ya usingizi.
Nilijiweka tayari kwa kutoroka, nilikusanya vitu vyangu vya thamani bila kusahau kanguo ka Ivan mwana wa Mfalme....nilihitaji kuwa nako kama ukumbusho kuwa nililea mtoto wa Mfalme. Laiti kama ningejua nisingefanya hivi.
Nilianza kunyata taratibu ile nataka kufungua mlango nilidakwa na Tunu (Kijakazi wa Malkia) huyu binti anakuwaga na balaa sana naweza kumuita shetani mwekundu kwa sababu matendo yake huwa ni magumu sana.
"Wapi unaenda Mbwa pori wewe, hivi unafikiri tulikuwa tumelala hii mbinu niliwafundisha wenzangu ni kijua fika utaingia mkenge kubabake. Hebu nijibu, nini kimekusibu ukaipakia nguo ya Mwana wa Mfalme kwenye nguo zako " Tunu aliniuliza.
Vile anaongea sasa utadhani yeye ndio Malkia Shamsa. Nilikuwa na mpango wa kumjibu lakini nilimpuuzia.
"Huyu hana mdomo wa kujitetea, hebu leteni hizo hereni za Malkia Ada tumuongezee kwenye furushi lake. Hapo kinguo cha Ivan kule hereni za Malkia Ada. Hakika siku ya kesho patanoga " Tunu aliongea huku akicheka.
Basi hereni za Malkia Ada ziliwekwa ndani ya furushi.
Kulivyo pambazuka asubuhi Malkia Shamsa alikuja akiwa bado kafura.
"Malkia wangu huyu Yaya ni mwizi mkubwa, tulizuga kulala wacha aiibe nguo ya Mwana wa Mfalme. Pia ana hereni za Malkia Ada " Tunu alipigilia msumari.
"Mwizi?.... ulitaka ukaifanyie nini nguo ya mwanangu pamoja na hereni za Malkia Ada. Kubabake bila shaka ulifikiria kufanya vitu vya kishirikina " Malkia Shamsa aliongea.
Mdomo wangu Mimi ulikuwa mzito, sikuweza kujitetea wala kuongeza neno lolote.
Malkia Ada aliletwa kuthibitisha hereni nilizo nazo ni zake au la.
"Hereni zangu zimefikaje mikononi mwako ....hakuna mtu mwenye ujasiri hapa Ikulu wa kuingia malangoni kwangu bila ruhusa yangu, inaonekana wewe ni kibaka uliyekomaa. Huyu achapwe viboko 50 kisha aondolewe hapa akiwa kavaa matambara 😠" Malkia Ada aliongea.
Basi nilinyweshwa fimbo 50 za makalio kisha ni kavalishwa matambara.
Kama utani hivi niliondolewa Ikulu, na kwetu mie hivyo sikutaka kutanga tanga hata kidogo nilinyooka moja kwa moja nyumbani.
Ile nafika tu Baba naye alifika akiwa amelewa chakali.
"Ikulu inahitaji watu Wahuni na si wastaarabu. Kama hujui kucheza michezo ya pata poteza kila iitwayo leo utakuwa unalia tu, ahsante kwa kurudi nyumbani " Baba yangu aliongea.
Nilitaka kuangua kilio lakini niliona ujinga hivi, niliingia ndani kulala.
Sikumbuki ilikuaje lakini nilikuja kushtuliwa na Mama yangu kuwa nahitajika nje.
"Mb...wa wewe, yaani unafuatwa kabisa nyumbani na Wanaume. Hebu nenda ukawasikilize kabla Baba yako hajaamka likawa balaa " Mama aliongea..
Wanaume wapi hao tena? mbona Mimi sina marafiki wa kiume wala mashemeji .
Ile natoka nje nilishtuka kumuona Mfalme akiwa na Mlinzi wake.
Nilidondoka chini kumpa heshima , sijui ilikuaje familia yangu yote ilikuja nje kutoa heshima bila shaka walikuwa wanachungulia dirishani.
"Tunarudi wote Ikulu, kwa wakati huu hautakuwa Yaya wa Kijana wangu badala yake utakuwa Kijakazi katika malango yangu " Mfalme aliongea.
"Tunashukuru ee Mtukufu Mfalme " Watu wa familia yangu walinisaidia kujibu kwa sababu nilikuwa nimepigwa na butwaaa........
ITAENDELEA..........
Makala nyingine zinazocheza na ladha yako
Mapendekezo haya yanatokana na kile unachosoma sasa + Endelea kugundua zaidi
Maoni