USIKU MMOJA TU ALIDATA SEHEMU YA 15
ENDELEA.......
"Hizo dhana ni za nini " Malkia Shamsa aliuliza akionekana kuogopa.
"Swali la ajabu sana Mkwe umeleta malalamiko kuwa Sadia katembea na Mumeo hii ni mara ya pili. Kinachotakiwa kufanyika muda huu ni kumuadhibu. Nadhani adhabu zangu zina fahamika.....nitaichana chana hiyo K yake " Malkia Ada aliongea kwa msisitizo.
Nilianguka chini kuomba huruma, mie nisiye kuwa hata na mtoto mmoja niliomba kuhurumiwa.
"Nitakuhurumia baada ya kuichinja K yako..... naomba mmlaze hapo juu ya meza " Alitoa amri akiwa kafura kupita maelezo.
Mie Sadia ndio niliamini kuwa kilo zangu hazina tofauti na zile za karatasi.
Nilibebwa juu juu kisha ni katupwa kwenye meza.
Nilivuliwa nguo zote ni kabakia kama nilivyo zaliwa.
Miguu yangu ilifungwa kikatili aisee mmoja magharibi mmoja mashariki. Yaani hata ningefurukuta vipi isingekuwa rahisi kutoboa.
"Malkia Ada, tafadhali sana kabla hujatoa hukumu yako nina ujumbe wako kutoka kwa miungu " Mtabiri Mkuu aliingilia kati.
"Ujumbe kutoka kwa miungu hasa baada ya kuona nataka kutoa adhabu kwa huyu binti mtukutu basi miungu wakakuletea ujumbe hebu naomba uzungumze huo ujumbe" Malkia Ada aliongea kwa kebehi.
"Hili Taifa haliwezi kuwa na Malkia tu isipokuwa Mfalme anahitaji kuwa na pisi kali wa kumliwaza....na Sadia ndio kachaguliwa kuwa Pisi kali wa Mfalme Pangani " Mtabiri Mkuu aliongea.
"Pisi kali ? yaani hata miungu wanaijua hiyo misemo ya kihuni!....hii ni ajabu sana. Lakini na kumbuka nimewahi kukuuliza kuhusu huyu binti ukasema hakuna maono umeona na pindi utakapoona utaniambia. Kwahiyo umeona maono siku ya leo...." Malkia Ada aliongea kisha akamsogelea Mtabiri Mkuu
"Tangu ufike hapa unaonekana kuwa na roho mbaya juu ya Shamsa. Kuna namna huwa unahisi kama anaupiga mwingi. Unajua hata huwa siyaamini maono yako nitaongea na Mfalme tutafute mtu mwenye mawazo chanya juu ya Taifa hili na si hayo yako " Malkia Ada aliongea.
Mtabiri Mkuu alidondoka chini akawa kapiga magoti.
"Nisamehe kwa kusema hivi lakini kisheria Malkia haruhusiwi kuwa na wivu. Ni haki ya Mfalme kuwa na Wanawake zaidi ya mia. Na mabinti wote wanaopatikana Ikulu ni mali ya Mfalme hivyo hata akionekana yupo na Mwanamke mwingine tofauti na Malkia watu hawatakiwi kunong'ona au kuongea chochote " Mtabiri Mkuu aliongea.
"Kubabake " Malkia Shamsa alifoka, hakuishia hapo alishika mkasi akazikata nywele za Mtabiri Mkuu Kwa kifupi hakuwa na utofauti na Mwanaume.
"Mpelekeni kwenye kiwanda cha ngano, maisha yake yote yatakuwa huko...."
"Nitaenda kwenye kiwanda cha ngano, na nitatumikia adhabu yangu maisha yangu yote lakini naomba msiyashike maneno yangu nyie wote hapa kuwa Mfalme hatoweza kuwa na Mwanamke mmoja maisha yake yote hivyo itapendeza kama Malkia Shamsa atajiandaa kiakili......Sadia ni chaguo la miungu kuwa atakuwa mke wa pili wa Mfalme " Mtabiri Mkuu aliongea.
"Hebu niondoleeni huyo kivuruge hapa nisije kumtoboa macho " Malkia Shamsa alifoka.
Basi Malkia Ada alishika kisu kikali airarue K yangu.
📢Mfalme kafika simama mtoe heshima📢 Sauti ilisikika.
Basi shughuli zote zilizokuwa zinaendelea zilisitishwa.
"Kitu gani kinaendelea mahali hapa " Mfalme Pangani aliuliza.
"Kwanza kabisa nimemuadhibu Mtabiri Mkuu, atasaga ngano maisha yake yote. Lakini pia nitashirikiana na Malkia Ada kuirarua K ya Sadia kwa kosa la kunidharau Mimi " Malkia Shamsa aliongea.
"Ni vile nilichelewa tu kutangaza lakini Sadia ni pisi kali wangu....siku tatu zijazo sherehe kubwa itafanyika. Natumaini Malkia Ada utaniunga mkono katika hili. Naomba aondolewe mara moja juu ya hiyo meza " Mfalme alitoa amri........
ITAENDELEA.........
Makala nyingine zinazocheza na ladha yako
Mapendekezo haya yanatokana na kile unachosoma sasa + Endelea kugundua zaidi
Maoni