USIKU MMOJA TU ALIDATA SEHEMU YA 6
ENDELEA......
Mfalme aliingia akiwa na Mlinzi wake, buti alilovaa sasa halikuwa tofauti na zile gari za kuchora kwenye karatasi.
Mbavu zangu huwa ni nyepesi kama karatasi aisee, nilishindwa kujizuia Mb....wa mie niliachia kicheko
Eeeh ndipo Mfalme alichungulia uvunguni mwa meza.
Kwa aibu nilitoka nisijue najibu nini
"Huo mpira wa mtoto hujaupata " Mtabiri Mkuu aliongea bila shaka alikuwa ananitetea.
"Si...si...sijaupata " Niliongea kisha ni katoa heshima yangu kwa Mfalme.
Eeh huyu Mfalme bhana, alinyoosha mkono wake akaanza kunifuta futa vumbi nililotoka nalo uvunguni.
"Ivan ni mtoto wangu Mimi, jitahidi kuwa msafi masaa 24 anapokuwa mikononi mwake " Mfalme aliongea.
"Nimeelewa mtukufu Mfalme " Niliongea kwa utii macho yakiwa chini"
"Unaweza kuondoka nahitajika kumhudumia Mfalme, bila shaka ana jambo lake hajaja hapa bure " Mtabiri Mkuu aliongea.
Nilimchukua mtoto ni katega mgongo niondoke lakini Mfalme alinisubirisha.
"Nikumbushe jina lak" Mfalme aliongea.
"Naitwa Sadia "
"Sadia?....jina hili ni zuri itapendeza kama farasi wangu mpya atapatiwa hili jina "
"Yaani jina langu Mimi apatiwe farasi? " Nilijikuta ni kiongea bila kufikiria.
Watu wote walinigeukia, nililitambua kosa langu. Nilitaka kuanguka chini kuomba rehema lakini Mfalme alinizuia.
"Endelea na safari yako "
Basi niliondoka haraka bila kugeuka nyuma. Siku ya leo nilimuona mtoto mwepesi kuliko siku zote.
Wakati nakata kona kuelekea chumbani kwake nilikutana na Ada (Mama wa Mfalme)
Kama kawaida niliinamisha kichwa kutoa heshima.
Sijui nini kilimpata alijikuta akinitazama kwa macho makubwa. Ni kama kuna maono alikuwa anayaona hivi.
"Mida ya saa mbili usiku naomba uje malangoni kwangu " Ada aliongea kisha akaendelea na safari yake.
Nilijikuta ni kikosa amani, isije kuwa Mfalme alinishtakia kwa Mama yake kuhusu kutaka kubandika mchoro wa nyeti zake kwenye mbao za matangazo.
Niliona muda kama hauendi hivi, acha mtoto aanze kulia nilimfunga Mgongoni ni kaelekea bustanini.
Nilianza kumbembeleza kwa kumuimbia nyimbo za kila rangi lakini hakubembelezeka.
Ile nageuka nimpeleke kwa Mama yake akanyonye nilikutana na Mfalme.
"Huyu mtoto hana njaa hata kidogo, mtindo wako wa ubanaji nywele ndio una mkwaza " Mfalme aliongea kisha akanyoosha mkono wake.
Alikitoa kibanio kilichokuwa kimebana nywele zangu zikateremka. Si unajua tena watu wa Nchi yangu tumebarikiwa nywele Wahindi wakasome. Mfalme ana sifa huyu, aliwatuma Vijakazi wake wa kike chanuo pamoja na kitana.
Baada ya vitu kuletwa alinibana mtindo mpya.
"Lakini Mfalme, huu mtindo hubanwa na Malkia tu huoni kama italeta shida " Mlinzi aliongea.
"Ivan kanyamaza, maana yake ni kwamba kavutiwa na huu mtindo tunaweza kuendelea na safari yetu " Mfalme aliongea kisha akaondoka.
Vijakazi wake na Walinzi wake walimfuata kwa nyuma pia.
Nilibaki kushikiria moyo wangu, huyu Mwanaume kaanzaje kunitengeneza nywele vipi kama taarifa zitamfikia Malkia.
JE UNAJUA NINI KILIENDELEA???
Makala nyingine zinazocheza na ladha yako
Mapendekezo haya yanatokana na kile unachosoma sasa + Endelea kugundua zaidi
Maoni