USIKU MMOJA TU ALIDATA SEHEMU YA 8
ENDELEA..........
"Baba unatafuta nini hapa " Nilishtuka mno baada ya kumuona Baba yangu. Unajua simsemi vibaya lakini kama asingekuwa na familia angekuwa kibaka mkubwa aliyeshindikana.....kuna hadi Mimi huwa ananiibia.
"Yaya wa Mtoto wa Mfalme kwa nyota ipi uliyonayo .....hebu naomba ujielezee haraka kwa sababu nimekutafuta sana huko mtaani hadi magerezani lakini sikuambulia kitu" Baba aliongea.
Vile mwenyewe ni mapengo sasa mtoto alianza kulia.
"Hebu nifuate haraka " Nilimuambia kisha ni kamuingiza chumbani kwangu.
Sikuwa na namna zaidi ya kusimulia mambo yalivyokuwa.
Ile Baba anataka kufungua mdomo wake kuzungumza mlango uligongwa.
Ilinilazimu kumuweka chini ya uvungu.
"Karibu mheshimiwa Malkia " Niliongea kwa unyenyekevu baada ya Malkia Shamsa kuingia ndani.
"Leo nitalala na mwanangu, nimemkumbuka" Malkia aliongea huku akinyoosha mikono.
Nilimpatia mtoto wake na hata ni katamani aondoke haraka. Cha ajabu alivuta kiti akakaa.
"Hebu mbadilishie nguo, nataka kuona namna unavyo mvalishaga "
Mie huyu nilianza kumvalisha mtoto chapu chapu. Nilimrusha huku na kule ndani ya dakika mbili nilimaliza.
"Una ubaya Mb....wa wewe si ungejiunga tu na Jeshi la Nchi" Baba yangu aliropoka kutoka uvunguni, kumbe alikuwa ana chungulia.
Nilianguka chini ni kapiga magoti kuomba msamaha, ni kosa la jinai kuingiza Mwanaume kwenye Ikulu ya Mfalme.
"Mwalimu " Malkia Shamsa aliongea.
"Mwalimu?.... Mwalimu wako nani " Nilijikuta ni kiuliza.
Baba yangu alitoka uvunguni akatoa heshima ya dhati.
"Nafurahi kuona kwa sasa wewe hapo ni Malkia wa Taifa hili "
"Mafundisho yako yalinisaidia kushinda mtihani, kama siyo wewe sidhani kama ningeitwa Malkia . Vipi bado hujaacha tabia yako ya kupenda watoto wadogo " Malkia Shamsa aliuliza.
"Huyu ni binti wangu anaitwa Sadia "
"Aaah nisamehe, imekuwa kama bahati kwake kuwa Yaya wa Kijana wangu "
"Basi naomba niondoke, nilikuja kumsalimia tu." Baba alijieleza.
"Ni rahisi sana kuingia kwenye Ikulu hii lakini kutoka ni changamoto kubwa, fuatana na Mimi nitakutoa " Malkia aliongea
Basi Baba yangu pamoja na Malkia Shamsa waliondoka.
Kubabake nilikuja kushtuka sina bangili za mkononi, Baba yangu Mimi ni balaa kuna muda huwa tuna muita jini upepo kwa sababu huwa anaiba kwa kushtukiza.
Leo ilikuwa ni siku yangu ya kipekee kulala pekee yangu bila mwana wa Mfalme.
Tamaa ya kupata mto niogelee ilikuwa juu sana.
Nasikia mahali hapa huwa kuna mto.
Nilijikokota tararibu mpaka kwenye mto huo.
Nilivua nguo zangu moja baada ya nyingine kisha ni kajitupa kwenye maji.
Sikuwa na hofu yoyote ile.....akili yangu ilikuwa mbali sana hasa nikifikiria eti Baba yangu Mimi ni Mwalimu wa Malkia Shamsa.
Nilishtuka nusu ya kupiga kelele baada ya kushikwa nyonyo kwa mahaba yote. Sijui mnaelewa mikono ilipitishwa kwa nyuma.......
ITAENDELEA..........
Makala nyingine zinazocheza na ladha yako
Mapendekezo haya yanatokana na kile unachosoma sasa + Endelea kugundua zaidi
Maoni