BETWEEN SISTERS AND SECRET ____________________________________* *SEHEMU YA ISHIRINI NA MOJA* Jioni, muda wa kufunga duka, Gael alimfuata Mia.
"Mambo mrembo wangu," Gael aliushika mkono wa Mia.
"Safi tu boss, Madam hakufika hapa leo. Unataka nikusaidie nini?" Mia aliongea kana
kwamba hawajuani.
"Sihitaji huduma yoyote, Mia. Nataka kuongea na
wewe," Gael alisema kwa upole.
"Unaweza kuongea hapa hapa, unachotaka kuongea, nakusikiliza, Mia alimjibu huku akimuangalia usoni.
"Siwezi kuongea hapa, unaonaje tukitoka labda hotelini au sehemu tulivu?"
Mia alitafakari kidogo. "Sawa, nakupa dakika tano tu."
Mia aliongozana na Gael mpaka kwenye hoteli moja maarufu.
"Utapendelea kula chakula gani?" Gael aliangalia menu.
"Kumbuka una dakika tano tu, Gael, na mimi sikuja hapa kula sema ulichoniitia," Mia alisema kwa ukali.
"Mia, nipe nafasi ya kuwa karibu na wewe, hata kidogo. Kwanini umekuwa mkali ghafla?"
"Gael, sitaki tena kuishi na hii siri wala
kugombana na yeyote."
"Siri ipi?" aliuliza Gael.
"Ni kwamba..." kabla Mia hajamaliza, Mira alimkatisha.
"Mimi na Mia ni ndugu, watoto wa baba mmoja
na mama mmoja, ila Mia hakutaka mtu yeyote ajue kama sisi ni ndugu, ndomana hata wewe
nilikuficha," Mira alisema bila aibu.
"What? Hii sio kweli!" Gael alimuangalia Mia, akitafuta jibu.
"Ni kweli, Gael, sisi ni ndugu, Mira ni dada yangu, lakini ni yeye ndo kabla hajamaliza, Gael
alisimama.
"Inatosha sasa! Nilikuona kama mwanamke wa tofauti, lakini kumbe unapenda michezo ya
kijinga. Hata huo upole ni maigizo tu! Nimeshangazwa sana, sikutegemea hili kutoka kwako!"
Gael aliondoka akiwa amekasirika, akawaacha Mira na Mia.
Mira akamuangalia Mia kwa dharau.
"Namjua vizuri sana Gael, huwa hapendi watu waongo. Hesabu umeshamkosa," alisema huku
akicheka na kuondoka.
"Hata siku moja hukuwahi kuwafikilia wengine,
Mira. Wewe ni mbinafsi sana, huoni hata aibu kumuumiza mtu," Mia alisema huku akichukua
pochi yake na kuondoka.
"Nimeshamfanya Gael akuchukie, sasa ni wakati
wangu wa kumfanya anipende mimi peke yangu," Mira alicheka kwa kiburi.
Wakati huo, Gael hakuwa sawa kabisa. Alienda baa, akaagiza pombe, akaanza kunywa
hadi akalegea.
"Kaka, samahani, muda wa kufunga umefika, unatakiwa kuondoka," alisema mhudumu.
"Aaah, niache ninywe kidogo, nataka ninywe
mpaka nishindwe kabisa kukumbuka mimi ni nani," Gael alisema kwa sauti ya kilevi, huku
akiwa amelala mezani.
"Meneja, tutamsaidiaje huyu mtu?" mhudumu
aliuliza.
"Hatuna jinsi, tumpigie mtu wake wa karibu aje kumchukua," meneja alisema.
Alipekua kwenye mfuko wa Gael, akatoa simu, namba ya juu kabisa ilikuwa ya Mira. Walimpigia.
"Samahani dada, tumechukua namba kwa Mr. "Nani mwenzangu?" aliuliza Mira upande wa pili. Gael kama kwenye kitambulisho chake, unaweza
kuja kumchukua hapa baa?"
"Mimi ni mpenzi wake, yupo baa gani?"
"Pacific."
Kusikia hivyo, Mira alifurahi.
"Sawa, nakuja sasa hivi."
Haikuchukua muda, Mira alifika, akamchukua
Gael na kwenda naye nyumbani kwake. "Siwezi kupoteza hii bahati," alisema huku
akimvua nguo zote na kumlaza kitandani. Na yeye pia alipanda akalala pembeni yake.
Asubuhi, Gael aliamka akiwa na maumivu makali ya kichwa.
Offer offer
Soma yote kwa sh 800
Whatsp 0784468229
Makala nyingine zinazocheza na ladha yako
Mapendekezo haya yanatokana na kile unachosoma sasa + Endelea kugundua zaidi
Maoni