JAMANI NIPE CHANCE KIDOGO 14&15* "Abisai kwanini unakuwa sio muelewa, Erick ni rafiki yangu wa kawaida tu, kwani wewe haujawahi kuwa na marafiki wakike?
Niliacha nao siku nyingi baada ya kuona hawana maana kwenye maisha yangu. Na hata wale niliowabakiza niliamua kuachana nao kabisa baada ya kupata wewe mwanamke ambae tunaendana.
Leyna hivi umeshawahi kujiuliza pamoja na mambo yako ya kuvunja moyo na kukatisha tamaa lakini bado nilikuwa sikati tamaa ya kuwa na wewe?
Leyna alimuangalia bila kusema chochote.
"Kama ulikuwa hujui basi leo nakwambia.
Sababu nakupenda Leyna, baada ya kuteseka
sana kwenye mahusiano yangu huko nyuma sikutamani kupenda tena. Hata nilipo ondoka na wewe pale club ilikuwa napitia tu baada ya hapo naendelea na mambo yangu lakini upendo
wangu ukanifanya niwe king'ang'anizi kwako. Abisai aliongea kwa hisia sana mpaka Leyna akisikia vibaya.
Basi mume wangu tuachane na mambo yaliyopita tufurahie ndoa yetu.
Kesho yake kulipokucha Abisai aliamka mapema na kwenda kusimama nje upepo wa bahari ukimpuliza huku akiwa anaangalia mawimbi ya bahari.
Leyna alifumbua macho yake alipoangalia pembeni hakumuona Abisai, aliponyanyuka akakaa ndipo akamuona Abisai akiwa kasimama nje. Alinyanyuka pale kitandani huku akiwa amevalia night dress yake nyeupe na kumfuata
mume wake. Akimkumbatia kwa nyuma na kumlaza kichwa chake mgongoni huku mikono yake ikiwa kifuani kwa Abisai.
Abisai aligeuza shingo kumuangalia huku akitabasamu.
* Umeamkaje mpenzi?
"Salama, vipi wewe mume wangu.
"Mimi niko poa.
"Ukaniacha mwenyewe kitandani?
"Nilitoka tu kitandani lakini niро hapa nilikuwa na kuangalia.
Basi baada ya hapo walienda bafuni kuoga huku wakionesha na kucheza michezo yao ya kimahaba. Walipofika bafuni na kuvaa nguo Abisai
alitaka kupiga simu aagize wapelekewe kifungua kinywa chumbani kwao lakini Leyna alikataa.
*Hapana mpenzi leo naomba tutoke tukaangalie na mazingira ya huko nje.
"Sawa hakuna shida.
Wakitoka chumbani kwao huku wakiwa
wameshikana mikono mpaka restaurant. Waliagiza kufungua kwenye kinywa muhudumu aliyekuja kuwahudumia alionekana kumfananisha Leyna.
"Samahani dada ni kama nakufanisha vile.
Abisai alikuwa kashika simu yake lakini kusikia hivyo aliweka pembeni na kumuangalia yule muhudumu.
Wakati huo Leyna alikuwa akimuangalia kwa makini.
*Umenifananisha na nani?
Dada mmoja hivi anaitwa Leyna walikuwa mapacha.
"Kwani wewe ni nani?
"Nasibu
*Nasibu tuliwahi kuonana wapi? Kule pembe la ng'ombe kwa bibi mmoja
anaitwa mama selemani. "Huyo ni bibi yangu ila bado sijakukumbuka.
Tulikuwa tunakaa karibu na bibi yako kwenye ile nyumba ya zamani iliyojengwa kwa mawe.
"Jamaniiii nimeshakumbuka. "Leyna umebadilika sana umekuwa mrembo.
*Wewe bro hivi upo hapa kwaajili ya kufanya kazi yako au kutaka kujua mambo ya watu?
Jamani mume wangu huyu ni kama kaka
yangu. "Ni kama na sio kaka yako.
Kijana naomba nikuulize swali moja. Hivi una mke nyumbani kwako?
"Ndio nina mke na watoto
Vipi kama mimi nikimsifia mke wako mbele
yako.
Hiyo mbona ni kawaida tu..
"Kawaida kwako lakini kwangu sitaki.
Yule muhudumu walimuangalia Leyna ambae alikuwa kimya.
Samahani boss wangu.
Yule muhudumu aliondoka, Leyna alimuangalia Abisai kwa hasira kisha akanyanyuka kwa hasira na kuondoka
Wewe unaenda wapi? Abisai aliuliza lakini Leyna hakujisumbua kugeuka nyuma.
Alienda kukaa ufukweni kwa bahari akiangalia
maji, alipiga picha na kuziweka instagram, facebook na hata status. Watu wengi wali comment kwenye chapisho lake.
Watu wa karibu wa Abisai alipoona post za Leyna walimpigia simu Abisal kumpa hongera. "Naona Fungate imenoga, shemeji yetu anazidi kung'aa.
Abisai aliamua kuingia instagram na kukutana na picha za Leyna.
Huyu mwanamke sio muelewa kabisa sijui kwanini anajuanikachuvi kwenye mitandao. Alianza kufuatilia comment watu walivyokuwa walimsifia hasa wanaume na maneno yao ya kichokozi.
Abisai alijikuta anapata na wivu. *Wanaume wengi ndio wame comment lazima akaifute hii picha.
Alitoka pale restaurant huku akimpigia simu lakini simu ya Leyna ilikuwa ikitumika. Anatumika wameshaanza kumpigia simu.
Itaendelea........
Offer offer
Soma yote kwa sh 800
Whatsp 0784468229
Makala nyingine zinazocheza na ladha yako
Mapendekezo haya yanatokana na kile unachosoma sasa + Endelea kugundua zaidi



Maoni
14&15*
"Abisai kwanini unakuwa sio muelewa, Erick ni rafiki yangu wa kawaida tu, kwani wewe haujawahi kuwa na marafiki wakike?