MREMBO YATIMA NA KIJANA TAJIRI SEHEMU YA 23* That day niliplan ninywe pombe kidogo cha kushangaza kila nikinywa nikimaliza naongeza nilifanya hivo mpaka nikajikuta nimelewa siwezi hata kuona mbele..
Romy alinibeba akanipeleka chumbani kwangu alinilaza kitandani akanifunika vizuri kisha akaniomba kiss..
The way jamaa alivokuwa anaiomba hiyo kiss dah nikajikuta mwenyewe nimefumba macho nimeachanisha lips zangu Romy akazama mdomoni na kuanza kunila denda💋
Romy baada ya kiss alijilaza palepale pembeni yangu...kwa vile wote tulikuwa hoi na pombe tulipitiwa na usingizi..
Usingizi ulikuwa mzito sana nimeingia kulala huo mchana saa 9 nilikuja shituka usiku mida ya saa tano..
Huo usiku nilitaka kujigeuza nilalie upande wa pili baada ya kujigeuza nikahisi kama kuna mtu pembeni yangu😳😳chumbani ni giza totoro..
Niliwasha bed switch nikiwa na wenge la usingizi mkojo umenibana mpaka nahisi maumivu ya kibofu😴😴 baada ya kuwasha kitaa cha pale kitandani nikashangaa nimelala na Romy kitandani kwangu..
Niliruka kitandani kama chizi😆😆🙈 cha kwanza nikajishika huko chini kama niko uchi nikagundua pako salama😴😴😴nilimcheki na Romy alikuwa kavaa nguo zake vizuri kachomekea😌😌..
Mida hiyo hiyo naye alishtuka akanishangaa like😝 what's going on?.??... nikamwambia unatakiwa uamke ukalale kitandani kwako sikujua kama umelala hapa🙄..
Oops sorry Bella hata mimi sikujua kama nilisinzia hapa 😴😴😴 Romy aliamka na kuanza kujinyoosha huku na kule then akanisogelea na kuniuliza ulihofia kuna kitu ningekufanya???
Nilikaa kimya sikujibu😌😌 alitaka kunikiss tena nikakwepesha mdomo na nikamuomba aende chumbani kwake🤨🤨aliniambia ni sawa but sorry kama nimekukwaza..
Alisema hivo na kisha akatoka nilijifungia mlango then nikakimbia chooni kwanza kupunguza maji mwilini😌😌😌nilipomaliza nikajimwagia na maji ya baridi nitoe hangover kichwani😝
Baada ya kuoga nilirudi chumbani nikakaa pale kitandani nikaanza kuwaza kilichotokea🥺🥺🥺nilikumbuka na ile kiss tuliyopeana na Romy🥲
Hata sikupanga iwe hivo ni pombe tu jamani😞😞niliishia kuzishika lips zangu na kuzipangusa lakini haisaidii kitu tayari nishatiwa kiss na haifutiki hiyo😞
Ila ananyonya vizuri🙄🙄sema tu alikuwa ananuka sana pombe😉😉 nilikumbuka ile siku mimi na Hemed tulipokiss usiku kwenye gari aa ile kiss ilikuwa hot sana💋
Hemed si mlevi wakati ananikiss nilienjoy kiss pamoja na ile harufu nzuri ya marashi aliyokuwa ameipaka💋💋💋..
Bado kichwa changu kilikuwa kinamuwaza Hemed muda wote🥲🥲 he is my first love siwezi kumsahau kirahisi..
Hata hivo usiku huo nilishika simu yangu niangalie huenda lbda Hemed atakuwa kani unblock💔💔 nilicheki nikagundua bado niko blocked😰😰..
Nilichofanya nilimpigia mama yake Hemed lengo langu nilitaka nijue kama Hemed kawaambia chochote kuhusu sisi au laaah...
Kama kawaambia basi nitajua hapo penzi hakuna na kama hajawaambia huenda tukarudiana😴😴 nilisachi namba ya mama nikaipigiaaa😝😝
Mapigo ya moyo yalikuwa yananienda mbio kuliko kawaida😌😌😌simu iliita ikakata bila kupokelewa mtumeeeeeee nikaamini kabisa hapa sina changu bora ni move on maisha yaendelee😌😌...
Niliwaza sana lakini nafsi ikawa inaniambia Hemed hawezi kukuacha anakurusha roho tu😰..
Usingizi ulipotea💔💔niliweka simu pembeni nikaanza kutembea tembea kule chumbani kama chizi sijisikii kula sijisikii kulala namtaka Hemed😰😰..
Nilikwenda nikafungua dirisha nikasimama nikawa nalia tu😰😰😰 nimesimama pale dirishani lisaa lizima sielewi najisikia nilieeeee nilieeeee bila kunyamaza😰😰..
Nililia mpaka nikatosheka nikafunga dirisha nikarudi kitandani kulala...
Asubuhi kulipokucha niliamshwa na simu ya mama yake Hemed😴
Itaendeleaaaaaaa
Makala nyingine zinazocheza na ladha yako
Mapendekezo haya yanatokana na kile unachosoma sasa + Endelea kugundua zaidi





Maoni