VYOTE NDANI GONGA94
MY TRUE LOVE STORY SEHEMU YA 15
Usimulizi huu ni wa watu wazima. Chukua muda wako, tulia, kisha usome kwa utulivu kama machapisho yetu yanayoendelea moja kwa moja.
Basi nabil alikuwa anakuja kulala na mimi usiku licha ya shenaiza kulala nae chumba kimoja, ila alikuwa anaenda kule kuchukua nguo tu, na sijui hata alimpanga nini shenaizah akawa anakubali tu, ila sasa anakubali kumuachia omari wangu kuja kulala na mimi mpaka asubuh ila omari akiondoka tu kwenda kazini, alikuwa ananionesha joto ya jiwe..
Yaan alivyo na tabia za hovyo akaanza mpaka kunifulisha nguo za ndani za kwake, sikuweka hiyana kwa sababu ndio sina namna, na Yule mama bado hakuwa ananipenda hata kidogo..
Nilijipa moyo konde na kuamin kuwa hata kama kumekuwa giza kiasi gani, haimaanishi kuwa hakutakucha, yaan ni lazima kukuche tu…
Basi maisha yakawa yanaendelea, sasa huyu shenaiza akajichanganya siku moja, ndio akajua rangi yangu ya kweli..
Watu wote nyumban walikuwa wameondoka na nilikuwa nimebaki mimi na yeye tu, mara akaja shoga yake mmoja, wakaanza kunituma kwa kunikomoa, sikuwa na namna zaidi ya kuwakubalia kila wanachoniagiza….
Basi kuna muda akaniagiza juice alafu shoga yake akaimwaga makusudi chini, kisha akanambia nifute..
Aisee niliwakata jicho kisha nikamuambia “ sifuti na naomba aliemwaga afute mwenyewe, mimi ni mfanya kazi wa ndani na sio mtumwa wenu…
Si ndio shenaizah akaniweka kibao, aisee hapo ndipo alijichanganya, sijui hakuwa anajua kuwa mimi ni mtoto wa kijijini na nilikuwa nimelelewa kwa mihogo na magimbi, hizo nguvu ambazo nilikuwa nazo nahisi labda wakusanyane ukoo mzima, aisee nilimpiga kisawa sawa, mpaka akaanza kulia na mlinzi akaja kuamua, na wakati huo huyo shoga yake nae akawa anataka kujichanganya, nikawaunganisha wote, nikawachapa balaa, mwisho mpaka wakajisogeza wenyewe, kisha kwa sauti ya ukali nikasema “ nyie pia ni wanawake, na majukum ya wanawake yanajulikana kwa wote, kama ni kazi ya nyumba hii niiteni nitafanya, ila kama ni ujinga wenu msisinisumbue kuniita, maana mtakuwa mmeita moto nan i lazima utawaunguza…
Wakaniangalia kisha hata sikusema nao nikaenda zangu nje kukaa na mlinzi, ila wakati nawapasua nikamalizia na hasira zangu za kutaka kumchukua omari wangu…
Basi nimefika kwa mlinzi,mlinzi ni ananipongeza tu kuwa nimefanya kazi nzuri sana maana shenaiza alikuwa na madharau sana, na kuna namna anaonekana kama alikuwa anataka kumuendesha kila mtu kwenye ile nyumba…
Kwenye majira ya kama saa nane, wakaja watu wakapamba, nikawa nashangaa wanapamba nini hawa, ndio nikaja kugundua kuwa walikuwa wanaandaa harusi ya kupakana hina…
Kiukweli nilihisi kuchanganyikiwa kabisa, yaan niliona kama mambo yanaenda haraka haraka sana, kiasi kwamba nikawa hata mimi sina muelekeo wowote na sijui kuhusu penzi langu na nabil lilikuwa linaishia wapi, nikamtumia sms nabil juu ya kinachoendelea, akanambia nisiwe na mashaka, maana kama ni kuoa ni lazima mtu atakae muoa atakuwa ni mimi tu, hivyo akanitaka sana nipunguze wasiwasi na mawazo yasiyokuwa na msingi kabisa…
Basi kweli kwenye majira ya kama saa kumi na mbili jion, suala la party ya hina likawa linaendelea, nikamwambia omari ananiambia nisijali, na akawa ananitoa wasiwasi kama ambavyo huwa anafanya kila wakati…
Basi omari akarudi kwenye kama saa tatu kasoro, akakuta na mimi nafanya kazi, na mama akasema kuwa nisiishi kama mwanafamilia bali niishi kama mfanyakazi asiekuwa na hadhi kabisa …
Sasa nabil amerudi amekuta natengea watu chakula, akanishika mkono kisha akanambia “ usifanye hii kabisa zinura..
“ lakin mama amenambia niishi kama mfanyakazi kwneye hii nyumba na sio mwanafamilia, nikasema…
Nikashangaa nabil ameenda kubadilisha nguo, kisha akaanza kufanya yeye zile kazi ambazo nimepewa nifanye mimi…
ITAENDELEA ………………….
Umesoma kwa utulivu · dakika chache tu Asante Endelea kusoma chagua hapo chini
Umependezwa ?? Asante Soma Zaidi my-true-love-story-sehemu-ya
