VYOTE NDANI GONGA94
MZUNGU TULIA MOYO HAUNA RANGI SEHEMU YA 5
Usimulizi huu ni wa watu wazima. Chukua muda wako, tulia, kisha usome kwa utulivu kama machapisho yetu yanayoendelea moja kwa moja.
Sikusubiri Sada aniulize nilizama ndani ya gari nae akanifuata.
"Love, kuna nini lakini?" aliniuliza baada ya kunikuta mule
"Ah! da Sada jamani🤦! hii kazi balaa! dereva ebu ongeza mwendo basi!" nilisema kwa upole. Yule kijana alitabasamu kisha akalipiga gari fimbo. Punde tuliwasili hapo kazini. Tukashuka na kuanza majukumu yetu sasa. Niwe mkweli, maandazi yangu yaliopendwa sana kiasi ya kwamba nilikuwa napika hadi napika tena. Ila kulikuwa na wanaume wanakanda unga, ni mimi nawaelekeza viungo. Sasa kuna mdada akaja, Zai kama mnakumbuka alinikuta jikoni.
"Love, samahani! naona una kazi lakini kuna mtu anataka kukuona" Zai alisema akiashiria kule nje
"Zai nani tena na unaona kabisa kuna wateja bado wanahitaji maandazi" nilisema nikimuonyeshea maandazi
"Nae pia ni mteja ila ameshakula tayari" alisema Zai. Nikatoka hivo hivo na dera langu. Lakini kumbuka msomaji kuwa: boss alinisainisha mkataba, kisha akasema kama nataka kubaki na dera kazini, nijitahidi nsitoke jikoni hadi nitakapo maliza kazi. Sasa hapo masharti shwaaa yanavunjika.
"Ndio, nimeitikia wito" nilisema baada ya kumfikiliza mteja huyo. Alikuwa mzee hivi wa kizungu. Akanisifia pale kwa kingereza kisha akanipa pesa. Nilikataa ila baadae nikachukuwa. Nikarudi zangu jikoni.
Nikiwa naendelea na kazi, simu yangu iliita namba ngeni, nikapokea.
"Njoo haraka ofisini" alisema boss, na ndie alikuwa kanipigia simu. Tena hakusubiri jibu langu, alikata moja kwa moja. Nishaanza kumzoea boss wangu hivo hakunipa shida. Nilimkuta ofinisi, akiwa na Sonia tena Sonia, alikuwa kamkalia boss mapajani.
"Wewe tena! unaingia bila kubisha hodi" kilisema ki Sonia. Yaani jibu ningekuwa hili: sasa boss wako si aliniita na alikuwa anajua kuwa nakuja. Hapo nilijibu kimoyomoyo, sikutaka kujibu kwa sauti mwisho nigombezwe na hili li boss.
"Samahani madam haitajirudia tena!" nilisema kwa upole
"Okey. Baby umemwita huyu au?" Sonia alimuuliza boss
"Yeah tuna kikao kidogo" alisema boss. Sonia alituacha, tukiwa na boss. Jamani fanyeni maombi sasa.
"Naam boss, nakusikiliza" niliketi nikiwa mwoga sana lakini hata hakuongea, zaidi alinisogelea akiwa na mfuko; akanikabidhi.
"Ya nini hii boss?" nilimuuliza huku nikimtazama
"Nimechoka kukuona na hizo dera mbili kila siku, haya kuanzia leo uniform zako ni hizo" alisema hivo kisha akaendelea kuangalia laptop yake. Nilifurahi kupata nguo mpya, nikamshukuru kisha nikaondoka zangu. Sada alinikuta nabadili mavazi, kwenye chumba husika.
"Haya naona ndio unajiandaa, mi naondoka" alisema akiwa anasubiri jibu langu
"Sawa ila uniwekee ugali kipenzi" nilimwambia hivo Sada. Nilimsindikiza hadi zilipo boda, akaondoka ndio nikarudi.
Nilijielekeza moja kwa moja hadi kwenye chumba nilichoelekezwa kuna mgonjwa...natakiwa kumfanyia massage.
Niliingia moja kwa moja bila kubisha hodi maana niliambiwa kuwa ni mgonjwa kalala tu kitandani. Ghafla namkuta Sonia.
"Khaaa! we binti, mbona unanifuata sana?" aliniuliza Sonia
"Mimi nakufuata wewe? kwa lipi hasa?" nilimjibu kwa jeuri sasa.
Tuliendelea kuzozana hadi tukasikia kitu kinaanguka chini kama mzigo. Tukageuka kutazama tobaaaa😳 bibi!
To be continued.....💥
MTAKATIFU GEMMA UTUOMBEE SHIRIKA LA MASISTA WA MT GEMMA WA DODOMA
Tunao Wapenda ndio wanao tuua baba
Sikiliza Wimbo Kamili
Umesoma kwa utulivu · dakika chache tu Asante Endelea kusoma chagua hapo chini
Umependezwa ?? Asante Soma Zaidi mzungu-tulia-moyo-hauna-rangi-sehemu-ya