NAISHIWA PAWA SEHEMU YA "2"💘 nilimpa Jordan mkono wangu kwa lengo la kuagana naye alipoushika mkono wangu
Niliendesha gari mdogo mdogo hadi nyumbani kwangu nilikopanga nilikuwa naishi tu peke yangu nilioga nikamaliza nikapika chakula chepesi cha usiku nilipomaliza kula nilielekea chumbani kwangu nikasali nilimuomba Mungu amponye Mr Jordan ili aweze kurudi katika hali yake ya kawaida miguu yake ipate uwezo wa kutembea baada ya kusali niliingia kulala ili kesho mapema nisije Chelewa kazini.....usiku mkubwa nilipoamka kwenda kukojoa niliishika simu yangu kutizama saa baada ya kuangalia ni saa ngapi ndipo nilipogundua kuwa kwenye simu yangu kuna ujumbe mfupi ambao haujafunguliwa niliifungua ile msg ilikuwa ni msg ya kunitakia usiku mwema ilitoka kwa Jordan kwa kuwa usiku ulikuwa umeshakuwa mkubwa sikuijibu niliipotezea kwani usiku huo nilijua tayari Jordan kaishalala sikutaka kumsumbua nilipanga kesho kukikucha nitamuomba samahani kwa kuwa msg yake nilichelewa kuiona....... nilirudi kitandani nikalala na kesho yake kulipokucha nilijiandaa kwa ajili ya kwenda kazini nilipomaliza kujiandaa ndipo nilipoishika simu na kukuta msg nyingine kutoka kwa Jordan......
""Hello pink....Good morning.... how was your night?!.....I hope you woke up safe I wish you a nice day, have a good job please take care......""
"""Wow nilipousoma huo ujumbe nilijikuta natabasamu..... nimekuwa single kwa muda mrefu huwa nalala na kuamka kama kuku hakuna mtu wa kuniwish usiku mwema wala asubuhi njema hatimaye leo kwa mara ya kwanza nimefeel ile raha ya kuambiwa take care😉😉 nikaulizwa usiku wangu ulikuwaje😊😊 lol leo nimewishiwa kazi njema🤣🤣🤣nilijisikia raha ya tofauti sana......nilimjibu Jordan nilianza na salamu.....
""Hello Jordan...... samahani jana sikuweza kuijibu msg yako kwa sababu niliiona usiku ukiwa umeshakuwa mkubwa...... asante kwa kujali nakutakia siku njema pia nikiwahi kutoka kazini nitapita nyumbani kwako nikuletee koti yako..... niliituma hiyo msg baada ya hapo niliuchukua mkoba wangu nikatoka kuelekea kazini.......
Nilipofika ofisini nilitia saini kisha nikaelekea kwenye sehemu yangu ya kazi hata nilipoifungua computer yangu ili nianze kazi mawazo yangu yote bado yalikuwa yanauwaza ule ujumbe niliotumiwa na mr Jordan niliachana na swala la kufanya kazi ikabidi niichukue simu yangu nianze kuusoma ule ujumbe kwa kuurudia rudia😜😜 tabasam mwanana lilinijaa usoni kwangu nilitamani nianze kumchatisha Jordan lakini naanzaje🙈🙈niliendelea kuusoma ule ujumbe huku taswira ya sura ya Jordan ikiwa imeitawala akili yangu..
nikiwa sina hili wala lile ghafla nilishangaa nakanyagwa mguu na mfanyakazi mwenzangu nilipoinua macho kumuuliza ana shida gani ndipo aliponikonyeza kwa ishara ya kuniambia tizama nyuma yako wewe😩😩 haraka nililigeuza shingo langu huku nikiwa nimeyakodoa macho yangu kwa wasiwasi nilishangaa kumuona Boss Hance akiwa ameikunja sura yake kwa hasira huku akiwa ananitizama mimi😳😳😳 mkononi kwake alikuwa kashikilia file alilirusha mezani kwangu kisha akaondoka huku ameikunja mikono yake kwa hasira🙄🙄🙄🙄🙄mmmhhh kwani huyu kafika hapa sangapi?!..... nilijiuliza😩😩😩 hazikupita hata sekunde simu ya mezani kwangu iliita nilipokea alikuwa ni Boss Hance.....hello Boss..... 🗣️🗣️🗣️njoo ofisini kwangu haraka....... nti nti ntiiiii simu ikakatwa nilinyanyuka upesi nikaelekea ofisini kwa Boss ili nikamsikilize🏃♀️🏃♀️...
Nilifika ofisini kwa Boss nikaanza kugonga mlango ngo ngo ngooo..... 🗣️🗣️get in....... aliongea Hance kwa sauti iliyodhihirisha wazi kuwa ana hasira nyingi.....Niliingia ofisini huku macho yangu nikiwa nimeyainamisha chini kwa uoga.....naaaam Boss😞😞.....nilimuitikia Boss huku nikiwa navikunja kunja vidole vyangu😩😩😩🫢 naona umeshaichoka kazi?! Kwanini Boss?..... yani muda wa kazi wewe ndo unautumia kuchezea simu😡😡😡?! Samahani Boss lakini kwenye simu nilikuwa naangalia tu mambo ya kazini na si vinginevyo😫😫.... una uhakika?! Lol uhakika sina🤣🤣🤣 sikujibu nilikaa kimya...... nipatie simu yako🗣️😒 lol simu tena🤭🤭🤭......🗣️🗣️ nipatie simu yako Pink😡..... sasa Boss anataka simu yangu ili afanyie nini😂😂😂🙈 hivi mnamuelewa kweli🥳🥳 alafu kachukia hadi kawa mwekundu nyooo🙈🙈 na anavyojikuta mr serious au kadata kwangu🤪🤪🤪 mbona simuelewi yani anaongea hadi anataka kulia😹😹😹 sijamzoea hivi😃😃pink I need your phone🗣️🗣️ lol aliongea kwa sauti ikabidi nichomoke mbio kwenda kuifuata simu🏃♀️🏃♀️🏃♀️nilikwenda mezani kwangu nikachukua simu yangu mbio nikaanza kurudi ofisini kwa Boss🏃♀️🏃♀️🏃♀️🏃♀️ kabla sijaingia nikawaza mmmhh au kaona ile msg ya Jordan🤔🤔🤔🤔 sijui niifute lakini sitaki kuifuta natamani niwe naisoma tu muda wote😩😩😩 sikuifuta ile msg niliingia ofisini nikamkabidhi Boss Hance simu bila kumtolea lock🤣🤣🤣🤣 alivyoishika akairudisha kwangu na kuniamuru nimtolee lock nikatoa nikampa ndani ya dakika tatu akanirudishia sikujua alichotaka kukiona kwenye simu yangu mimi nilivyorudishiwa simu yangu nikaambiwa nenda ukaendelee na kazi nikaondoka nilipofika mlangoni kugeuka nyuma nikakuta Boss kainamisha kicha chake kwenye meza kama mtu mwenye maumivu makali ya kichwa ikabidi nirudi kumuona kama yuko sawa😂😂😂
Boss is everything ok?!🤔🤔🤔....Pink please leave me alone😞😞😞😞.....lol mie huyooooo nikaondoka zangu🏃♀️🏃♀️🏃♀️🏃♀️ Nikaenda kuendelea na kazi si akaja rafiki yangu mumbea mwenzangu🤣🤣 karafiki kangu kakikorea kanaitwa soo_ah kanaongea kama chiriku😩😩😩😩 Hey Pink nini kinaendelea kati yako na Boss Hance😃😃😃 nahisi ninyi wawili mnadate?! Yani alikuwa anakutizama kwa wivu sana na wivu wake ulizidi kiasi baada ya kukuona wewe uko busy na simu yako alihisi huenda unamsaliti mbona hujawahi kunitambulisha bwana😞😞soo_ha unaongea nini ?! Mimi sina mahusiano na Boss Hance mtu mwenyewe alivyo mr serious hajawahi hata kunionyesha dariri za kunitaka☺️☺️☺️ tulia nishakwambia shemeji yako ni Leeminho kila siku nakwambiaga Leeminho ndo crush wangu lazima niolewe kwenu Korea huko uwe wifi yangu🤣🤣 basi tukaishia kucheka ghafla tukamuona Boss Hance anatokea ofisini kwake lol kila mmoja akafunga bakuli lake tukajidai tuko busy na kazi🙈🙈🙈 soo_ha si akawa ananikanyaga miguu ili nimwangalie nikimwangalia ananikonyeza et nimwangalie Boss Hance anavyoniangalia tu mimi muda wote yani ni kambea karafiki kangu🤣🤣🤣
Na kweli bwana kila nilipomtizama Boss Hance kwa kuibia😹😹😹nikawa namkuta macho yake yote yako kwangu😳😳😳khee kwani kuna nini na huyu mwanaume🤣🤣🤣basi tukawa tunakonyezana na soo_ha tunaachia cheko la kimoyomoyo kazi zinaendelea mara simu yangu ikaanza kuita nikashindwa kuipokea kwa sababu Boss Hance yuko hapo karibu na anazunguka zunguka kutizama vile wafanyakazi wanavyojituma kufanya kazi za kiofisi oops😫😫😫 nilipokaza jicho kwenye simu kutizama anayenipigia ni Jordan lol😩😩😩 nikatamani nipokee lakini Hance akawa ananikata jicho hatari🙈🙈🙈 simu nayo ikaendelea kuita Boss Hance akasogea hadi pale mezani kwangu akasimama kwa muda lengo lake ilikuwa kutizama mtu anayenipigia simu ni nani na kwa bahati nzuri simu nilikuwa nimeshaigeuza nikailazia screen 🤣🤣🤣 alipoona hivyo akaingia ofisini kwa hasira nami haraka nikaelekea chooni na simu yangu mkononi🏃♀️🏃♀️
Kufika huko nikampigia Jordan..... hello Jordan niliongea kwa sauti ya chini kidogo...... hello Pink samahani kwa usumbufu kuna kitu nataka kukuomba kama hautojali🥲🥲🥲...... bila shaka Jordan niombe kitu chochote nitakupatia..... Asante Pink niko shopping nilikuja kuchukua baadhi ya vitu vyangu nimekupigia kukuomba ruhusa ili niweze kukuchukulia zawadi iwe kama shukurani kwa wema ulionitendea jana.... samahani lakini sifanyi kama malipo bali ni kama shukurani tu🙏 aaaaa..... laalaaaakkkkkk........ mmmmhhhhh.......aaaaa.....niliingiwa na kigugumizi nikashindwa nijibu nini🙈 usijali Pink naomba usinikatalie nimejisikia kuchukua kitu kwa ajili yako nikubalie nakuomba🙏🙏 it's okay Jordan hakuna shida....... nilikubali et😌😌 Jordan alifurahi sana alinishukuru kwa kuikubali zawadi yake jamani moyo wangu ulijawa na furaha sana yani sikutamani Jordan akate simu nilitamani niendelee kuisikia sauti yake kiukweli anaongea vizuri sana baada ya yeye kukata simu nilibakia nalitizama tu jina lake kwenye simu yangu ni kitu gani kimeukuta moyo wangu lol😝😝😝😝
Niliamua kutoka kule washing room nikarudi kuendelea na kazi nilitamani mida isonge haraka jioni ifike ili nitoke nikaione hiyo zawadi aliyoninunulia Jordan ni zawadi gani.....nilifanya kazi haraka haraka na jioni ilipofika niliondoka ofisini nikaelekea nyumbani kwangu nilianza kuchagua nguo ya kuvaa kwani nilijua ni lazima Jordan atanihitaji tutoke ili aende akanipatie zawadi yangu na kweli bwana baada ya muda mfupi Jordan alinipigia simu akaniomba tukutane katika sehemu moja hivi amazing kwa ajili ya dinner na baada ya dinner atanipatia hiyo zawadi yangu nilimkubalia....... mtoto wa kike baada ya simu kukatwa nikaanza maandalizi🥳🥳🥳🥳 lisaaa lizima nikalitumia kwenye kuvaa tu mida ya saa mbili kamili usiku nikawa natoka ndani kuelekea kwenye gari kwa ajili ya kutoka kwenda kukutana na Jordan....... kufika kwenye gari ghafla simu yangu ikawa inaita atakuwa Jordan huyo nahisi anataka kuuliza kama nimeshaondoka😊😊 baada ya kuishika simu ndipo nilipogundua kuwa anayenipigia siyo Jordan bali ni boss Hance😳😳😳 hello Boss...... hello Pink where are you?! Niko nyumbani Boss.......nahitaji kuongea na wewe sasa hivi ni muhimu sana nakuja nyumbani kwako sasa hivi ndani ya dakika chache nitafika hapo......lakini Boss aaaaaammmmmm ninaaaa.....taaaaa......kaaaakuto........kkkkk.........
nti ntiiii ntiiiiii kaishakata lol sa itakuwaje😩😩😩na anataka tuongee nini🤔🤔......
Makala nyingine zinazocheza na ladha yako
Mapendekezo haya yanatokana na kile unachosoma sasa + Endelea kugundua zaidi
Maoni