????
NASEMA KWA MAMA
SEHEMU YA 13 na 14*
*****
Lidya aligeuza gari aliyokuwa anaiendesha na kuanza safari ya kuelekea Kibaha..
Akiwa njiani alishika simu yake na kumtumia Frenk ujumbe ili apate picha za huyo mama ambae alipaswa kuonana nae..
"" "Picha zake sina labdaa niende sebuleni kupiga baadhi ya picha zilizopo ukutani.." "" "
Frenk alijibu ujumbe...
" "" "Sasa hilo ni lakuniambia mimi kweli au ulipaswa kujiongeza tu na kunitumia hizo picha.. Hembu changamka.." ""
Lidy alijibu ujumbe kwa haraka huku anaendelea kuendesha gari...
Dakika kadhaa baadae alitumiwa pich alizohitaji.. Alizitazama na kuikariri sura ya huyo mama...
Aliendelea kukimbuza gari hadi kibaha.. Alifika na kukuta gari la polisi linambeba huyo mama kwaajili ya kumpeleka Mochwari....
Lidya alisimamisha gari lake na kuawafuata wale polisi, aliwasogelea na kuwaonyesha kitambulisho chake kuwa yeye ni afisa wa usalama na alitaka kuukagua huo mwili...
Alipata ruhusa na kufunguliwa mlango wa nyuma wa gari la polisi....
Lidya aliwasha tochi kwenye simu yake na kiingia ili kuutazama mwili...
Aliukagua vizuri na kubaini kweli ndiye mama alietakiwa kuonana nae..
Lidya alimshika yule mama mshipa wake wa fahamu shingoni na mkononi na kubaini kuwa bado yupo hai yule mama na hakuwa amekufa kama alivyosikia..
"" "" mnampeleka wapi sasa.??? Aliuliza lidya....
"" "" tunampeleka Mochwari hapo kwenye Hospitali ya Kimara mwisho... Alijibu askari mmoja kwa kujiamini..
"" "" "Hamna akili wapuuzi nyie... Hivi mnampeleka mochwari mtu aliekuwa hai...
Inamaana huwa hamkagui miili kwa umakini eti..
Mbona mnakuwa watu wa ajabu kiasi hicho.???..
Aliongea lidya na kwenda kuushika mwili wa yule mama na kuuvuta ili auhamishie kwenye gari lake...
Baadhi ya maaskari walimsaidia na wengine waliendelea na safari zao...
Wawili walipanda gari ya Lidya na kuongozana nae kwenda Hospitali ya Taifa Muhimbili...
Gari lilikimbizwa sana na baada ya dakika kama 25 walikuwa wameshafika hospitalini...
Baadhi ya manesi na madaktari walimpokea mgonjwa na kumpeleka kwenye chumba cha wagonjwa mahututi.
Walimuwekea mashine ya kupumulia na kifaa cha kupima mapigo yake ya moyo ili kujua kama yupo hai au amesha kufa...
Kifaa kiliwekwa kifuani huku wanaangalia mistari kwenye Computer kubwa ukutani....
Mistari ilikuwa ikipanda na kushuka taratibu sana ikimaanisha ni muda mfupi tu anaweza kupoteza maisha endapo mstari wa kwenye compyuta ukanyooka.,.
Madaktari walichukua mashine ya kushtua mapigo ya moyo na kuanza kumkandamizia kifuani...
Baada ya mda kidogo mapigo yaliongezeka...
Madaktari walipata amani kidogo na kuanza kumpatia huduma zingine yule mgonjwa....
******
******
Muda ulikuwa umeenda sana, kulianza kusikika Adhana kwenye baadhi ya misikiti ikimaanisha Alfajiri imefika..
Hadi muda huo lidya alikuwa amekaa tu akisubiri majibu kutoka kwa Madktari...
****
Nusu saa baadae alitoka daktari mmoja kwenye chumba alipo mgonjwa wa Lidya..
Kwa haraka lidya aliinuka na kumfuata Daktari hadi mlangoni..
"" Vipi hali ya mgonjwa wangu.. Aluuliza Lidya..
"" "" Ni njema, alipata fahamu ila kwasasa amepumzika.. Unaweza kuendelea na majukumu yako alafu ukaja baadae kumuona..
Aliongea Dokta..
Lidya alimpa mkono daktari kisha kuondoka..
**********
Lidya alifika nyumbani kwake na kuoga vizuri kisha kuvaa nguo zake za kiofisi kisha kwenda kazini kwake kama Secretary...
Alifika kazini na kuendelea na majukumu yake kama kufanya usafi kwenye ofisi ya boss wake na kumuandalia chai...
Baada ya hapo lidya alirudi mezani kwake...
Kwa siku ya leo boss alichelewa kufika kazini...
Lidya aliamua kuinuka pale na kwenda kukaa karibu na wenzie ili apige nao story mbili tatu...
"" ""haaaaah secretary mbona umeumia umia mwilini.??? Au ulikuwa unabakwa.????
Aliongea dada mmoja kwa masanifu kwasababu walihisi yale majeraha yalisababishwa na boss wao kwasababu wanamjua kwamba akikataliwa huwa anabaka kwa nguvu..
" "" "Hapana. Nipo sawa ndugu.. Kuna vibaka walitaka kunivamia tu kwa usiku wa jana.. Nilipambana nao nikawamudu.. Ila nipo sawa kabisaa..
Aliongea Lidyaaa..
Baada ya Muda wakiwa wanaongea.. Aliingia Boss wao akiwa na majeraha baadhi pia..
Wale wadada walianzaa kukonyezana na kucheka kwa masanifu..
Boss alipita na kuingia Ofisi kwake bila ya kuongea na mtu..
Lidya aliinuka kwenye kiti kwa hofu na kwenda kukaa kwenye sehemu yake ya kazi yaani kwenye meza ya Secretary.
Aliwasha komputa yake na kuanza kupitia baadhi ya vitu. Dakika kama mbili baadae aliinuka na kwenda ofisi kwa boss kama vile haelewi chochote.
************
"" "Shkamoo boss.. Aliongea Lidya.
" "" Jamboo.. Vuta hicho kiti kaa hapo. Aliongea boss na lidya alienda kukaa....
"" "Hivi Juzi kilitokea nini.??? Nilikuja kupata fahamu karibu na asubuhi...
Yaani hata sielewi nini kilinikuta. Nilishangaa nipo msituni sana huko kibaha na nilikuwa nimefungwa kwenye mti...
Mlinzi wangu mmoja sikumuona ila kuna mwingine alienda kutoa taarifa kituo cha polisi kuwa tulivamiwa.
Hapa nawaza hao watu waliingilia kwa wapi na ilikiwaje nikapoteza fahamu bila kujua chochote kinachoendelea..
Aliongea Boss huku anamtazama Lidyaa machoni.....
"" "" Pole jamani My Boss kumbe ndio maana jana hukuja kazini... Poleeee....
"" "" " Alafu Bosssss.. Sitaki tena Apointment za kushtukiza kama zile.. Alafu mazingira yenyewe si salama.. Je tungeuliwa juzi Boss..
Aliongea Lidya kwa hasira sana na kutaka kuinuka ili arudi njeee kwenye sehemu yake ya kazi...
" "" "Basi nisamehe mrembo kweli naona umeumia hapo.. Naomba nisamehe kwasababu ya uzembe wangu.. Siwezi rudia kukualika mazingira kama yale tena...
Aliongea Boss na kuinuka kwenda kumshika mkono Lidyaa..
Bos alimuinua lidya na kumkumbatia kisha kumbusu huku akimuomba radhi..
Boss alifugua moja ya Droo za Ofisini kwake na kutoa Noti 15 za elfu kumi kumi na kumpa lidya ili akitoka pale aende hospitali..
Lidya alipokea huku anatabasamu kisha kurudi njee kwenye meza yake...
Aliendelea na kazi zake na wafanyakazi wengine walikuwa bize na kazi zao pia..
Walikuwa wakisanifiana tu Lidya na Boss wake...
Boss alishajua kabisa kuwa Muhusika wa yote huenda ni Lidya kwahiyo alikuwa akimtengenezea mtego ili Lidya aingie kwenye kumi na nane zake....
Lidya pia alihisi huenda Boss wake ndio alicheza mchezo wa kumteka mgeni wake alietoka moshi na kwenda kumtupa msituni kibaha...
"" "" "Kama boss hausiki" "" kwanini sasa yule mama baada ya kutekwa jana alienda kutupwa kwenye Mti ule ule niliomfunga boss juzi.??? Aliwaza mwenyewe lidya na kutabasam tu....
*****
*****
Huko hospitalini Mama yake Dayana alikuwa amepata Fahamu na kujikuta yupo hospitali akiwa na njaa sana....
Aliangalia kila kona na kumuona nesi yupo pembeni yake...
Yule mama hakutaka kukurupuka kwasababu alikuwa ni msomi na anajielewa..
Ilibidi akae kimya hadi alipochomwa sindano na yule nesi ili kupunguza maumivu..
"" "" "" "Nipatie kidonge cha Tramadol, nipe na maji madogo na chakula.. Kisha niletee Ice na Pamba pamoja na spirity...." ""
Aliongea mama yake Dayana akimwagiza Nesi.....
Nesi alishtuka kidogo baada ya kusikia yule mama kaagiza dawa kali sana za kutuliza maamivu.. Pia aliongea kwa lugha ya kidaktari utadhani anataka kujitibu mwenyewe......
"" "" "Hivyo vidonge vya Tramadol ulivijua wapi.????? Aliongea nesi..
"""""""Nesi hembu changamka unapo agizwa.. Najisikia vibaya sana.. Pia sindano yenyewe hujui kushika umenichoma vibaya hadi umeniumiza mkono.
Bora ningejichoma tu mwenyewe.....
Aliongea mama yake Dayana na kukaa pale kitandani..
Ilibisi nesi atoke na kwenda kumuita Daktari kwasababu alikuwa hamuelewi kabisa yule mgonjwa..
Wakati anatoka Lidya pia alikuwa anaingia kwenye Wodi ya mgonjwa wake..
"" "" Shkamoo mama... Aliongea lidya....
"" "" Marahaba hujambo binti..... Wewe ndio umenileta hapa.???
Aliongea Mama yake Dayana.
"" "Ndio.. Mimi naitwa Lidya.. Ndie Mwanamke ulielekezwa na Frenk kuja kuonana nae huku Dar....
Aliongea lidya na kumsogelea yule mama.....
" "" Frenk ntamuua nasema. Inamaana kaja kuniuza huku mjini mimi.. Nateseka nusu kufa..
Yaani najua yeye ndio mhusika mkubwa wa mipango yote ya mimi kutekwa...
Binti naomba uondoke. Kwasasa mimi siamini msichana hata mmoja hapa mjini.. Ondokaaaaaaa nasema ondoka we mwanamkeeee......
Aliongea kwa ukali sana mama yake Dayana hadi madaktari wakaingia kwenye ile wodi kujua kuna nini tena kimetokea......
ENDELEA....
.
Maoni