*NIMEKOMA MIMI 🙌* *SEHEMU YA KUMI NA NANE* Basi lile busu lilikuwa tamu sana kama chokoleti, yani lilinipeleka mbali kabisa dunia nyingine. Nikajikuta Nampa
Nilikuwa tayari kufanya na Bishop! Na Hatukuwa tunajali kitu chochote, wala mtu yeyote. Ilikuwa mara yangu ya kwanza kufurala ile kitu na kuhisi kama niko peponi. Ndiyo hapo nikagundua nimeanza kumpenda Bishop.
Tulifanya mpaka tulipo ridhika kisha Akanikumbatia kwa nguvu akaniambia "Nakupenda, Nataka tuwe pamoja. Je utakubali kuwa na mimi ?....... Mimi ni mtu hatari, Polisi wananisaka na wanataka kunifunga. Nina maadui wengi alafu Nafanya kazi chafu na zisizo halali. Watu wanaserna sina huruma, sisamehi kirahisi, Naumiza watu na nina tabia mbaya nyingi. So je, utakuwa na mwanaume kama mimi? Kama hutaki kuwa nami, nitaelewa, nitakuacha uende. Lakini kama unataka kuwa nami licha ya yote hayo, nitafurahi na nitakupenda milele. Sema chochote nakusikiliza
Alinipa nafasi ya kumchagua au kumkataa. Na kama unavyojua, mimi nimekuwa na bahati mbaya sana kwenye mapenzi. Lakini Bishop alikuwa mtu wa kwanza kunionyesha mapenzi ya kweli, hata kama ni kwa siku moja tu.
Namna alivyonitazama, alivyonionesha wivu, alivyonipigania mbele ya Michael nilijua hii ndio nafasi yangu ya pekee ya kufurahia aina ya upendo ambao nimekuwa nikiutamani kwa muda mrefu. Nilikuwa tayari kuwa naye, hata kama polisi wanamtafuta au ana maadui kila kona.
Nikamuambia "Niko tayari kuwa na wewe. Sijali watu watasema nini. Cha msingi niko nawe na nina amani, basi!"
Alishindwa kuamini, Akanitazama kama vile mtu anayetaka kulia. "Wanawake wengi waliniacha kwa sababu ya vitu walivyosikia au walivyoona juu yangu. Nimeumia sana kwa sababu ya kuachwa au kusalitiwa. Ndio maana nilijizuia sana kuwa na mwanamke. Niliepuka hata kuwa na wafanyakazi wanawake, wala kufanya. biashara nao. Nilikuwa naogopa kuangukia mapenzi halafu mwisho wa siku niachwe! Kazi ninayo fanya Imenikosesha sana nafasi ya ku-enjoy mapenzi. Lakini wewe umebadilisha kila kitu. Nimefurahi sana kusikia uko tayari kuwa pamoja na mimi
"Niko tayari, lakini lazima nifanye kazi. Familia yangu Inanitegemea"
"Hilo halina shida. Nitakuwa natuma pesa kila mwezi kwa familia yako. Nitahakikisha wanaishi vizuri, na wewe pia uishi vizuri. Mimi niko tayari kukufanya uwe na furaha, nitapigania haya mapenzi kwa sababu nakupenda kweli"
Nikacheka & nikamkumbatia "Na wewe je? Unayo familia?"
"Hili tutaliongea jioni tukitoka dinner. Sasa hivi tuenjoy hii moment
"Ok! Ila utamuachia Michael aende?"
"Namna unavyoongea kuhusu ex wako wivu unani washa akakunja sura
"Najua lakini mwache aende. Sitaki kuishi nyumba moja na huyo mtu. Mwache tu aondoke"
"Sawa, nitamwachia" Tukaendelea kukumbatiana pale pale tukifurahia kila dakika.
Na kweli Bishop alimwachia Michael. Lakini kabla hajaondoka, alimwambia kwa ukali asinisogelee lasivyo atamvunja meno. Weeeh! Michael aliogopa vibaya sana. Alipotoka pale, alikimbia kama chizi. Nilifurahia kuona jinsi alivyo fundishwa adabu mpaka akakaa kwenye mstari.
Basi Jioni ile Bishop wangu alitaka tutoke outing kidogo Akaninunulia wig, gauni jipya na viatu. Nikajipodoa vizuri nikawa kama Malaika. Then tukaenda dinner kwenye hoteli nzuri sana. Tulikula, tukanywa, tukacheza muziki wa taratibu, halafu tukaanza kuongea.
Ndipo akanifungukia kuhusu familia yake. Akaniambia baba yake alimwacha akiwa mdogo sana, akalelewa na mama yake peke yake. Ila baadae mama yake alianza kuugua vibaya mpaka akashindwa kufanya kazi, Ikawa Bishop ndiye anatakiwa kutafuta hela za kuwatunza.
Kabla hajaanza kufanya kazi, aliwaza kurudi kwa baba yake kuomba msaada. Wakati huo baba yake alikuwa tayari ameoa mwanamke mwingine ambaye alikuwa mjamzito.
Bishop alipofika kumuomba baba yake, baba yake hakumsikiliza. Alimfukuza na kumwambia achague moja, aishi naye au akaendelee kuishi na mama yake mgonjwa.
Bishop akaamua kubaki na mama yake. Akawa anafanya kazi za mtaani kutafuta hela, lakini pesa haikutosha, Kodi, chakula, dawa vyote vilimaliza vijisenti alivyokua anavipata.
Hapo ndipo akaingia kwenye kundi la watu wanaofanya biashara haramu ambazo ni wizi, dawa za kulevya hata biashara ya silaha.
Siku moja alipata dili la kusafirisha silaha kwa ajili ya kupata pesa ya kumtibu mama yake. Alifanya kazi hiyo na akalipwa, lakini aliporudi nyumbani, akakuta mama yake amekufa. Ilimuumiza sana. Alilia na akamzika mama yake, kisha akabaki mwenyewe. Akakata tamaa ya shule, akaamua kuendelea na biashara hizo haramu.
Kwa muda akaendelea hivyo, hadi akawa na biashara zake mwenyewe. Akaanza kusaidia watoto wa mitaani. Kwaiyo Wale vijana wote tunaoishi nao pale nyumbani, wale ni watoto wa mitaani aliowasaidia.
Hata Tobias ni mmoja wao japo Tobias hakumuokota mtaani. Ndio maana wanamuheshimu sana, hawamgeuki na Wako loyal kwake. Alikiri kwangu kabisa kwamba bado anauza silaha haramu na mambo mengine, hakunificha kitu na mimi nilimuelewa.
Baada ya kumaliza kuniambia yote, alibaki kimya akiwa mwenye mawazo. Nikamkumbatia, nikamwambia "Nakupenda jinsi ulivyo. Asante kwa kuniambia ukweli wako Akafurahia, akanibusu.
Baadaye akaenda kuninunulia ice cream na vitu baadhi nilivyo vitaka ndipo tukarudi nyumbani tukiwa tumefurahia sana.
Nakuja........
Makala nyingine zinazocheza na ladha yako
Mapendekezo haya yanatokana na kile unachosoma sasa + Endelea kugundua zaidi