WHATSAPP 0675137453
FULL STORY TSH1000 TU (VIPANDE 50)
"kinini hiko unachokitazama" alinifuata na kuninyang'anya haraka haraka mkononi mpaka nikaingiwa na wasiwasi
"mme wangu umenunua simu kwani?"
"wewe unataka ujue ili iweje, sijanunua"
"mh sasa hizi earphones na maelekezo ni ya nini?"
"sasa mbona una haraka Rebecca si usubiri au umesahau leo ni siku gani jamani?"
"halafu sipendi unavyoniita Rebecca mimi ni nani wako kwani?"
"aah nisamehe mke wangu kipenzi wakati mwingine nalimisi jina lako halisi nililolizoea wakati ule kama sijakuoa mmwaaah" alinijibu na kunibusu shavuni nikatabasamu
"utakula, nikutengenezee nini?"
"nimeshiba, nitasubiri cha jioni tu mke wangu" alinijibu na muda huohuo tukasikia sebuleni wanaimba wimbo wa happy birthday to you happy birthday to you kana kwamba kuna watu wengi ikabidi nitoke kuja kutazama ni wageni gani hao nikamkuta rafiki yangu Margreth amekuja na wanawake wengine kutoka kwenye Saccoss yetu wameniletea keki nzuri wameiweka mezani na watoto wangu watatu, Theresia, Robert na mdogo wao wa mwisho, Leticia wakiwa wamesharudishwa na gari wakiwa na sare zao za shule
"waaaoh jamaniii!" nilijiziba mdomo baada ya kufanyiwa suprise hiyo na mume wangu nae akatoka, walikuwa wamekuja na makreti ya soda na vitafunwa (bites) na majirani zangu kadhaa nao niliwaona lakini mdogo wangu Diana alikuwa chumbani kwake hakutoka, mume wangu aliwasalimia na kurejea chumbani maana simu yake iliita akaenda kupokea
"maisha marefu Rebecca"
"maisha marefu mama Theresia"
"happy birthday mama Leti njoo uzime mshumaa na kukata keki tufungue hafla hii ndogo" kila mtu alinipongeza akiniita jina alilolizoea wengine langu na wengine la watoto wangu
"jamani asanteni sana kwa upendo wenu wa ajabu sana sina cha kuwalipa, keki nitakata lakini siwezi kukata peke yangu na kuzima mishumaa peke yangu bila mume wangu mpenzi ngoja nimuite tufungue shughuli hii yaani mmenishtua sana sijategemea" niliongea nikijawa na furaha wakapiga makofi na vigeregere hasa Margreth ambae alionekana kama ndiye mpambe mkuu, nikawaacha sebuleni na kurudi chumbani kumuita mume wangu
"vipi umeipenda hiyo zawadi?" nilimsikia mume wangu akiongea na simu kwa sauti ya chini
"mume wangu" nilimwita akashtuka na kunitazama
"ngoja" alimjibu aliyekuwa anaongea nae na kukata simu
"nakuhitaji sebuleni"
"ooh kula keki eeh?"
"kuzima mishumaa na kukata"
"sawa tangulia nakuja"
"hamna nataka tuongozane"
"basi twende mke wangu" alinijibu akiibeba simu yake
"simu si ungeiacha tu mume wangu?"
"nataka nichukue matukio" aliniambia tukatoka wote mpaka sebuleni na moja kwa moja kwenye keki tukazima mishumaa na kukata na kulishana na kuwalisha kila mtu na nikashangaa mdogo wangu Diana hajaja tangu mambo yote yanaendelea hata kutoka chumbani hajatoka ikabidi niingie chumbani kwake nikamkuta amelala kitandani siyo usingizi ila yuko bize na simu yake
"Diana upo sawa?"
"dada uuwiii" alinijibu akijinyoosha nyoosha
"mbona hauji sebuleni?"
"naumwa dada yaani kiuno chote hapa hakina kazi na mgongo pia unawaka moto natamani kuinuka kuja lakini nguvu sina usinione bize na simu kuna assignment za chuoni hapa nafanya hapa kwa kujilazimisha maana laptop nimemuazima rafiki yangu sijarudi nayo"
"pole basi ngoja nikuletee keki"
"usijisumbue dada nitakula na chakula baadae"
"sawa" niliitikia kiunyonge na kuanza kutoka chumbani kwake lakini nilipoufungua mlango ili kutoka
"dada!" aliniita nikageuka
"abee??!!"
"happy birthday to you!"
"asante mdogo wangu" nilitabasamu nae akatabasamu kisha nikatoka chumbani kwake taratibu nikamkuta mume wangu Dawson amekaa kwenye kochi akiwa bize na simu nikamfuata na kukaa karibu yake akiwa hajaniona, nilipomgusa akashtuka
"ooh mke wangu ulienda wapi?"
"mbona simu tu bize muda wote mme wangu?"
"kuna mambo ya kazini hapa hayajakaa sawa ndo nayaweka weka sawa mke wangu"
"ndo maana nilikwambia iache simu tu chumbani kwa sababu itakuchanganya leo huoni ni siku yangu ya furaha mume wangu jamani wewe bize na simu tu bize na simu?" nililalamika lakini tukiongea kwa kunong'ona watu wasije wakatusikia
"usijali mke wangu halafu nina zawadi yako!" aliniambia akaweka simu yake mfukoni akainuka kwenye sofa la watu wawili tulilokuwa tumekaa yeye akaenda chumbani, muziki wa taratibu ukiwa umefunguliwa watu wakinywa soda na vitafunwa vingine
"oooopppss mbona simuelewi elewi huyu mwanaume sikuhizi??" nilijiuliza kimoyomoyo huku nikishusha pumzi ndefu na nikageuka na ndipo nilipokutana na simu yake aliyodhani ameiweka mfukoni kwenye suruali aliyovaa na kumbe haikuingia iliponyoka, nikaishika na kuitazama na ndipo niliposhtukia napokonywa na mtu simu haraka haraka yaani kama naporwa na kutazama alikuwa ni mume wangu ambae sikujua hata amerudije rudije ndani ya sekunde chache hivyo nikabaki nimetoa macho....
FULL STORY TSH1000 TU, VIPANDE (50)
NJOO WHATSAPP 0675137453.
Hakuna ratiba iliyopangwa kwa sasa.
Maoni
Click here to login and comments