Menu






Simulizi za Maisha,Mafunzo,Mapenzi ,Chombezo Habari za Michezo na Burudani vyote kwa Kiswahili ndani ya – Gonga94 Semajambo

ROWAN (Mine alone) 1 - 5
Gonga94 · Stories

ROWAN (Mine alone) 1 - 5

Usimulizi huu ni wa watu wazima. Chukua muda wako, tulia, kisha usome kwa utulivu kama machapisho yetu yanayoendelea moja kwa moja.


MTUNZI: Mr Burudan

Sehemu ya: 01

ANZA NAYO....

Niite Vee, jina la kifupisho cha jina langu la Vera, Vera ndio jina langu halisi nililopewa na wazazi wangu, nimezaliwa miaka kadhaa hapo ya 2000.

Mimi ni mtoto wa mwisho katika familia ya watoto watatu uku mimi ndio nikiwa wakike tu.

Niseme kuwa am blessed, yaani ikija kwenye upande wa kubarikiwa mimi nilikuwa nimebarikiwa Aswa, ukianzia kwenye akili kichwani walahi niko vizuri darasani, ukija kwenye umbo Mashallah niko vizuri, ukirudi kwenye sura hapa nisidanganye, sikuwa na sura nzuri sana ila mafuta mazuri na kujing'alisha kulinusaidia sana.

Nimezaliwa kwenye familia yenye pesa sana hivyo ghalama za skin care ni niliweza kuzimudu ipasavyo.

Niwanafunzi wa mwaka wa pili hapa chuoni UDSM, Nina marafiki wa kutosha jamani, yaani mimi kwa marafiki tu niseme kuwa niko vizuri, Vee mimi ni mtu ambaye nina muamimi mtu kirahisi sana, ukija kuchanganya na ucheshi ndio kabisa.

Katika maisha yangu nimepita kwenye mikono ya hovyo sana juu ya mapenzi, naweza kusema kuwa mapenzi sio vitu vyangu kabisa.

Nimebarikiwa kila kona ila sio mapenzi, kwa kumbukumbu yangu ya haraka haraka, nakumbuka nilianza mahusiano nikiwa kidato cha nne.

Mahusiano yangu ya kwanza hayakwenda sawa kutokana na kujifanya mtoto zaidi, nilikua sijui jinsi ya kuwa romantic na ukija kwenye masuala ya sex ndio unanivuluga Kabisa, sio kwamba nilikuwa sijui hapana, kujua najua ila aibu ilikuwa ni ya kiwango cha rami.

Mpaka nakuja kuingia chuoni,nilishaachana na wanaume kama wanne hivi, na wote nimeachana nao kwaajili tu ya kukataa sex, nilikuwa najiona mdogo sana hivyo niliamini kuwa nakosea na hivyo sikudumu kwenye mahusiano.

Nilipoingia chuoni mwaka wa kwanza, niliweza kukutana na kijana Mike, ni kijana ambaye nilimpenda kuliko maelezo.

Ninaposema kuwa nilimpenda Mike muwe mnanielewa jamani, Mike ni mvulana ambaye alikuwa anatoka kwenye maisha duni sana, lakini kutokana na kumpenda kwangu, nilihakikisha kuwa shida ndogo ndogo namsaidia.

Mike ndio mwanaume ambaye nilijipa asilimia Mia moja kuwa atakuja kuwa mume wangu wa ndoa, nilihakikisha kuwa najenga mahusino Imara sana na Mike.

Uaminifu wangu juu ya Mike ulikuwa ni wa hali ya juu ambapo sikuona hasara mimi kumuachia Mike mwili wangu ili achezee vyovyote awezavyo.

Katika moja na mbili, nilikuja kugundua kuwa Mike ni mkaka wa hovyo sana, kwanza uwa ana warekodi video wanawake wote ambao atabahatika kulala nao, lakini cha pili, Mike anatumia uzuri wake kuwadatisha wanawake wenye pesa, ili tu aweze kutumia pesa zao, na naweza nikasema kuwa Mike ni mzuri kitandani walahi na alituweza wanawake wengi.

Katika wanawake ambao Mike amefanikiwa kulala nao na kuwarekod na mimi nimo, na anatumia video yangu kuendelea kunitesa na kula pesa zangu.

Ouk ouk my zangu, tuachane na hizo brabrah za Mike njooni uku niwape fusho la kijana ROWAN.

SONGA NAYO.....

Ikiwa ni siku ya alhamisi, nikiwa darasani na mashoga zangu, tunapiga zetu picha uku na uku, gafla mkaka aliyejulikana kama Rowan alikuja na kusimama pembeni yangu na kuonekana kutaka kuzungumza kitu.

"Vee"

ROWAN aliita jina langu kwa sauti nzito kabisa kisha akakaa kimya akisubili niitike, nilimuangalia kwa muda kisha nikamuuliza.

"Unataka nini nawe, ata hivyo unaniziba si unaona napiga picha "

"ROWAN alivua kot lake ambalo alivaa pasi na kufunga zipu kisha akanipatia na kusema, jistili na hili kwanza"

Ila wanawake jamani, dharau na jeuri zitatuua na kutupeleka pabaya kabisa, nilikataa koti lake kata kata na kwa dharau nikainuka na kutoka eneo ilo.

Kitendo cha mimi kuinuka, kila mtu alibaki akininyooshea vidole na wengine kucheka, mwisho shoga angu akaniuliza.

"Kwani unaganya fashion show ya period mwenzetu au ? Maana inazidi kukuchafua lakini umo tu "

Kwa jazba na wasiwasi mkubwa, nikageuza mkono wangu nyuma na kuangalia, woiiiiih 🥺 nilijua kudhalilika jamani, yaani damu kama zote na vile nilikuwa nimevaa gauni nyeupe ndio kabisa.

Darasa zima lilinicheka isipokuwa ROWAN, yaani imagine, mpaka watu ambao nawaita marafiki wamebaki wakinicheka badala ya kunisaidia.

Kwa aibu nilitoka nje mbio na kukimbilia chooni, nilikaa uko kwa muda, nilivua gauni yangu na kulisafisha lakini alikutakata kabisa bado liliacha alama kubwa sana, na ni kama niliongezea hivi.

"Vee "

Ilisikia sauti nzito ya kiume ikiitilia jina langu kutoka nje ya choo.

"We nani ??" Niliuliza kwa sauti ya wasiwasi sana.

"ROWAN hapa, aaah nimekuletea pad kwaajili ya kujistili, lakini pia na koti ili "

Nyie, Rowan ni heaven sent walahi, yaani sijui nisemeje lakini alinisaidia sana, basi nilisogea mpaka mlangoni nikatoa mkono nje na kuchukua vitu kutoka kwa Rowan mwisho nikajistili na kutoka nje.

"Bado uko hapa ??" Nilimuuliza Rowan ambaye nilimkuta nje ya mlango mkubwa wa chooni.

"Yaaah nataka kujua kama uko sawa, are okay ??"

"Nisiwe muongo siko sawa kabisa "

"Naelewa, nafikili unaitaji kujisafisha zaidi, na sio hapa ni nyumbani "

"Ni kweli "

Rowan alinisindikiza mpaka nje ya chuo kabisa kisha akarudi darasani kuendelea na vipindi.

Kwa upande wangu niliitisha gari na kuondoka kwenda nyumbani.

JE UNATAKA KUJUA NINI KITAENDELEA ? TUKUTANE SEHEMU YA 2.
ROWAN (Mine alone )

MTUNZI: Mr Burudan

SEHEMU YA: 02

SONGA NAYO.....

Nilifika nyumbani nikajisafisha na kutulia zangu, nilijikuta nikijisikia aibu Sana walahi, ila sijui ni mimi tu au kuna wengine, jambo la period kuonekana mbele za watu kwa upande wangu ni aibu kubwa sana.

Kutokana na aibu ambayo nilikuwa nikijihisi, nilijikuta nikibaki tu nyumbani pasi na kwenda chuoni, yaani kitendo cha mimi kunyanyuka Na kwenda chuoni kilikuwa kizito sana.

*****

Hatimaye week nzima ilipita nikiwa bado naogopa kwenda chuoni, ila marafiki walahi ni wanafiki sana, ukiwa nao wanaigiza kukupenda na kukujali lakini ukiwa mbali uwiiiih ni Kama awakujui hivi.

Imagine tangu nimeondoka pale chuoni, hakuna ata rafiki yangu mmoja aliyenipigia simu kunijulia hali au kunipa pole kwaajili ya kile ambacho kilitokea.

Kwa upande wa Rowan amekuwa akipiga simu mfukulizo kwaajili ya kunijulia hali, lakini Rowan akuishia tu kunijulia hali, alinipigia pia kwaajili ya kunipa ujasili ili niweze kurudi chuoni.

***********

Ni siku nyingine tena, nimeamka zangu na naendelea na Mishe zangu za hapa na pale pasi na kuwaza kuwa natakiwa kwenda masomoni.

"Vee kuna mgeni wako nje "

Ilikuwa ni sauti ya mkaka wa getini, yaani mlinzi wa getini kwetu.

"Ni nani jamani ?"

"Aaah sijamuuliza,nikasema ngoja kwanza nimuulize small madam kama anatalajia kupokea mgeni " alizungumza mlinzi wetu na rafudhi yake ya kinyaturu.

"Unajua wewe hauna akili, badala ya kuuliza jina unakuja kwangu direct, me nitajuaje mama namjua au laaah "

"Basi, small madamu, kwahiyo nikamuulize ??"

"Haina haja wacha nikamuone "

Nilijibu na kujiweka sawa kisha nikatoka nje, ila mimi ni mtu ambaye nina uwoga wa hali ya juu, nilifika getini na kuchungulia ni nani kwanza.

"Rowan " nilishtuka baada ya kumuona Rowan akizunguka nje ya geti letu.

Haraka nikafungua geti, na kumkaribisha Rowan.

“Mkaka karibu “

"Asante za hapa ??"

"Aaah hapa ni njema Kwakweli, njema kabisa”

“aaaah pole nimekuja bila taarifa "

" usijali Rowan, karibu ndani "

"Hapana, nimepita kukuona, lakini pia kukuomba twende chuoni"

"Aaah hapana Kwakweli, niko radhi ni postpone for mwaka mzima kuliko kwenda kudhalilika uko chuoni "

"Ahaahahh Vee unajisikia kweli wewe ?, unajua ujasili unaanza na wewe kwanza, halafu iko kitu sio wewe tu, kila mwanamke anaingia mwezini, utasema kuwa unaogopa wanaume, nikutoe ofu, mimi kama Rowan nilishaitisha darasa kwa wanaume na kuongea nao na kila kitu kiko sawa "

Kwa namna moja au nyingine Rowan alijua kunipa moyo jamani, nilimkaribisha mpaka ndani na kumuacha sebuleni akipata ka juice.

Kwa upande wangu, niliingia chumbani kwangu na kwenda kujiandaa ili kuweza kwenda chuoni.

Kwa wakati huo, nilikuwa nikiogopa sana wanaume kutokana na matukio mfululizo ambayo nilipigwa na Mike.

Nilimaliza kujiandaa na hatimaye safari ya kwenda Chuoni Nikiwa na Rowan ikaanza, siku hii ndio nilijua kuwa Rowan ni kijana fulani hivi, Anaongea sana, Mcheshi mno lakini pia ana Huruma ya hali ya juu.

Tulifika chuoni na kwa kuwa muda wa darasani ulikuwa bado, mimi na Rowan tulishika njia na kwenda chini ya mti, sehemu ambayo ilikiwa tulivu sana lakini pia ilikiwa na ka upepo kakutosha.

“Ila Vee umejua kunishangaza Walahi, Yaani Mdomo wote huo, na heka heka uliyonayo kumbe ni muoga kiasi cha kwamba uwezi kujisimamia Mwenyewe ?”

Rowan aliniuliza uku akiniangalia sana usoni na akinicheka chini chini, kwa macho ya Aibu nikamuangalia Rowan Kisha nikajibu.

“Kwa Mimi naona ni kawaida sana aswa kwa Sisi wanawake, unajua Katika dunia yetu hii mwanamke anadhalilika sana kuliko Mwanaume, kwenye kila tukio mwanaume aangaliwi Kama ambavyo tunaangaliwa sisi mwanawake “

“Jifunze kujisimamia na uache kujitetea, simaanishi kwamba uliyosema ni uongo Ila kujitetea sana na kuangalia facts huo ni udhaifu “

Shoga yenu nilipoa hatari, nilibaki sura ndogo kama kidonge cha pilitoni, Rowan akiwa anaendelea kunipa somo, mashoga zangu Wawili walikuja na kuanza kunichangamkia.

“Shoga tulikumisii sana aiseeeh week nzima chuo uonekani “
Alizungumza Shoga Angu chuchu ambaye nilitokea kumpenda sana.

Nilitaka kujibu kitu lakini Rowan alinituliza kisha akawauliza.

“Baada ya kuona kuwa aonekani chuoni ni Hatua gani mlichukua ??”

Swali langu lilionekana kuwa gumu sana jamani, Shoga zangu walibaki wakiangaliana tu, Rowan alipoona kuwa wameamua kuwa Kimya Akaamua kuendelea kuongea.

“Mliona kuwa Yuko kimya lakini na nyie mkakaa kimya, kwa hali ambayo aliondoka nayo Mwenzenu , ninyi mlipaswa kumfata na ata kumpa moyo cha ajabu nyie ndio mmekuwa wa kwanza kabisa kumcheka ikiwa aibu yake, siku moja inaweza kuwa ya kwenu”

Rowan aliongea sana tena kwa Hasira, Sawa Rowan Ali kuwa akifoka lakini aliongea ukweli mtupu.

“Sina nia ya kuwafanya mjisikie vibaya Ila mnatakiwa kujitambua, wanawake manadhalilika kutokana na upuuzi wenu , Aibu ya mwanamke mwenzio unaibebea bango badala ya kuweka uzio “

Rowan Alimaliza kuzungumza kisha huyo akaondoka kwa Mwendo wa haraka pasi na kuaga.

ITAENDELEA…………..
ROWAN (Mine alone )

MTUNZI: Mr Burudan

SEHEMU YA: 03

SONGA NAYO.....

Nilibaki na mashoga zangu pale waliniomba Msamaha Nani nikawasamehe na story zikaendelea.

Pole pole nikaanza kuzoeana na Rowan, akawa mtu Wangu wa Karibu sana ambaye nilijifunza mambo mengi sana kipitia yeye, nilijikuta nikiwa na amani sana Mbele ya Rowan.

Niwape kastory kafupi kuhusu Rowani, ni kijana ambaye amelelewa na single baba, mama Mzazi wa Rowan alifariki siku ya kwanza tu ambayo Rowan aliona uso wa dunia.

Rowan kwao ni Mtoto wa Mwisho kuzaliwa Yaani nia Kama Mimi tu, tofauti yetu ni kwamba Rowan kwao wako wanne na wote ni wanaume, Rowan Maisha Yake ameishi na wanaume tu uku ndugu wakike ni wale wa kutoka kwa ndugu wengine wengine.

Nilijua yote hapo baada ya kumzoea sana Rowan, nilijikuta nikimuuliza mengi sana kumuhusu lakini pia alinijibu pasi na kuchoka.

Mimi na Rowan tukiwa kwenye restaurant tunapata Chakula, gafla simu yangu iliita na nilipoangalia Namba ilikuwa ngeni kabisa, nilipokea chapu kisha nikasikiliza sauti ili kujua ni Nani.

“WhatsApp kuna ujumbe wako “

Sauti ilikiwa nzito sana walaahi ambapo kwa Namna moja au nyingine nilijikuta nikipata wasiwasi.

Chapu nikawasha data na kuingia mtandaoni.

Woiiiiih, Yaani ile nafungua tu ujumbe, uso kwa uso na video yangu ya utupu, nakumbuka video hiyo nilijirekodi Kipindi ambacho Nilikuwa na mahusiano na Mike na Nilimtumia yeye kwani aliniomba.

Katika vitu Najutia kwenye maisha yangu basi ni hii ya kumpa Mike utu Wangu wote, Yaani Mike nilimfanya Kama Mtoto Wangu wa mwisho kwamba chochote anachotaka natimiza.

Nilishindwa kuangalia kabisa na nikajikuta nikipata wasiwasi wa hali ya juu.

“Uko Sawa ?”
Rowani aliniuliza.

“Oooh yah, yaah am gud, eat eat” nilijibu nikiwa na wenge la kutosha , muda huo huo ujumbe ukaingia kwenye simu yangu na ulisomeka hivi.

“Bwana ako namdai laki mbili yangu, Mpaka kesho Saa mbili asubuhi asiporejesha Naachia video hizi”

Kijasho Chembamba kikaanza kunitililika mfululizo, Tumbo joto mpaka nikajihisi kuvimbiwa niliangalia uku na uku nikihisi uwenda kuna mtu ananiangalia.

Rowan alibaki akiniangalia jinsi ambavyo nilikuwa nikiangaika, Rowan wa watu akatoa reso yake na kunipatia ili niweze kujifuta jasho ambalo lilikuwa likinitililika mfululizo.

"Rowan nafikili tutaonana kesho "

Niliamua kumuaga tu Rowan maana nilikuwa nikihisi kuchanganyikiwa aiseeh, kwakuwa Rowan ni kijana fulani hivi, mtaratibu mtulivu na ana utu uliopitiliza hakuona vyema kuniacha niondoke Mwenyewe tena kwenye hali ya kichanganyikiwa hivyo akanifata nje.

"Vee, Vee, Vee "

Rowan aliniita mfululizo uku akiitaji nimsubili lakini niligoma kabisa, zaidi niliongeza mwendo, ila mwanaume ni mwanaume bwana, Rowan aliweza kunifikia na akiponifikia akanidaka mkono na kuniuliza.

"Kuna taarifa mbaya umepokea au ? Vee hauko sawa shida nini mama !"

Rowan alionekana kujali sana, lakini kwa upande wangu, akili ilishapaniki hivyo niliona kama ananichanganya, kwakuwa ni jambo la aibu niliendelea kukataa na kusema kuwa niko sawa.

"Vee please nini shida mama "

Rowan hakukata tamaa hivyo akaendelea kuniuliza, nilijikuta nikipatwa na hasira sana ambapo niliamua tu kumfokea Rowan.

"Niko sawa nimekuambia shida yako nini kwani "

Baada ya kujibu hivyo, sikutaka tena kusikia maswali yake, nilinyanyua viatu vyangu na kuondoka kwa kukimbia.

Upande wa na Rowan alibaki akishangaa na kujiuliza maswali ambayo majibu mimi ndio nilikuwa nayo.


ITAENDELEA
ROWAN (Mine alone )

MTUNZI: Mr Burudan

SEHEMU YA: 04

SONGA NAYO.....

Kwa upande wangu, niliita gari haraka na kuwai nyumbani kwetu, naweza nikasema siku hiyo ilikuwa ni ya mikosi kwangu walahi, ile nafika tu nyumbani, uso kwa uso na baba na mama, lakini pia na kaka zangu, kiufupi Ni familia nzima ambayo niliikuta sebuleni.

"Kulikoni mwenzetu saa hizi ??"

Mama aliniuliza baada ya kuniona pale tu nilipoingia sebuleni.

Nilitamani ata kuwa invisible kwa wakati huo lakini ni kitu ambacho hakikuwezekana kabisa, kwakuwa akili yangu ilipaniki, nilijikuta nikikosa Ata jibu la uongo la kumpatia mama.

Kwa wakati huo mama alikuwa na haki zote za kuniuliza kwani, niliwai sana kurudi nyumbani ikiwa nimetoka nyumbani masaa mawili yaliyopita.

Mama aliniangalia kwa muda kisha akaniuliza tena.

"Umekuwa bubu au ??"

Nilikosa majibu kabisa, nilikuwa nikitetemeka na wasiwasi ilikuwa ni ya kiwango cha juu sana, ilo jasho sasa mpaka nililoana nguo ya juu.

Nilipiga mahesabu yangu ya haraka haraka na mwisho niliamua tu kukimbilia chumbani kwangu, nilifika chumbani na kujifungia mlango, nilipofunga tu niliangusha kilio cha hali ya juu ambapo sikuweza ata kujizuia.

Familia yangu yote ilichanganyikiwa walahi, walibaki wakigonga tu mlangoni mwangu na kuitilia jina langu kwa kupokezana.

Kujali kwao ni kama ndio kulikuwa kunaniongezea maumivu hivi, akili yangu iliwaza na kuwazua sana, nilifikilia na kujiuliza, familia yangu itajisikiaje siku watakapoona video zangu chafu ?

Nyieeeh haya mambo yasikie tu na yasije yakakukuta, unajua mambo ya sex kwenye dunia yetu ni kawaida sana lakini yasiende public, ni watu wachache sana wanaweza kukuelewa, lakini je ubongo wako utakubali kupokea tukio kubwa la kudhalilisha kama ilo ?

Nililia sana na nilipotulia nilipaza sauti yangu na kusema.

"Msijali niko sawa jamani "

"Vera acha ujinga, uko Sawa na unalia ? Ebu fungua mlango"

Kwakuwa familia yangu ilikuwa na wasiwasi, waliendelea kukaa tu mlangoni, kwa upande wangu nilituliza kichwa na nilipopata wazo nikaamua kufungua mlango.

Kitendo cha kufungua mlango, baba yangu alinisogelea na kunikumbatia kwa nguvu na kuanza kunituliza kwa kupiga piga mgongoni.

"Vee nini shida dada ??" Kaka angu mkubwa aliniuliza.

Niliwaangalia kwa muda kisha nikamkumbatia baba kwa nguvu sana, kwa wakati huo, nilishapata uongo wangu kabambe kabisa, ndipo nikaamua kuwadanganya.

"Rafiki yangu kipenzi wa A level amefariki "

"Ni nani ??" Mama aliuliza haraka haraka.

Baba alinishika vizuri na kwa mwendo wa utulivu tukasogea mpaka kwenye kochi kubwa na kuniweka nitulie ili niweze kuzungumza vizuri.

"Nina rafiki yangu ambaye nilisoma nae A level, ni mtu ambaye tulipotezana muda mrefu sana, sasa leo nimeweza kupata namba yake na kumpigia, ajabu simu yake ilipokelewa na mama yake na akaniambia kuwa Irene amefariki week mbili nyuma "

Weeeh uongo wangu si ndio ukatiki sasa 🤣, sio kwa baba wala mama, kaka zangu ndio kabisa, yaani wote walibaki wakinibembeleza pasi na kujua sababu kuu ya mimi kulia 😆.

"Wazazi wangu mnisamehe tu lakini siwezi kuwa na huzuni Peke yangu ikiwa nyie mpo " nilizungumza kimoyo moyo.

Baada ya kubembelezwa sana, nilijikuta nikipitiwa na usingizi hivyo nikaachwa nilale tu kwenye kochi kwani ni kubwa mno.

*******

Nilikuja kustuka jioni ya saa 11, macho mekundu sana na yamevimba, kutokana na kulia sana na kulala.

Nilipokuja kushika simu yangu, nikiweza kukutana na missed call za kutosha kutoka kwa Rowan, naweza kusema kuwa Rowan ni mtu na nusu, yaani licha ya kumpa maneno na kumfokea hajakata tamaa na anataka kujua naendeleaje.

Kwakuwa niliona kuwa ana wasiwasi sana, niliamua kumpa uongo ambao niliwapa wazazi wangu kwa njia ya meseji.

Nilitumia muda huo pia kuwaza ni njia gani naweza kutumia ili kumaliza tatizo kubwa ambalo liko mbele yangu.

Niwaambie kuwa laki mbili kwangu si kubwa, lakini nilikuwa nikijiuliza maswali sana, yaani Mike amekuwa mtu wa kutumia video zangu kwaajili ya kupata pesa na anajua lazima nimpe.

Kwa safari hii, nilikuwa nashindwa kuelewa kama ni Mike tu ameamua kutumia njia nyingine ili kupata pesa kwangu au ni mtu kweli anamdai Mike, lakini kama ni mtu ambaye anamdai Mike, picha zangu ametoa wapi ?.

Nilijikuta nikiwa na maswali mengi ambayo hayana majibu mwisho niliamua kumpigia simu Mike ambapo niliamini kuwa anamajibu sahihi.

Kitendo tu cha kumpigia Mike chapu akapokea, kwa haraka haraka unaweza kusema kuwa alikuwa akisubilia simu yangu, yaani ni kama Mike alikuwa akisubili mimi nimpigie.

"Vee mama nisamehe mim"

Alizungumza mike kwa sauti ya chini sana na yenye wasiwasi sana.

Sikujali kuhusu utulivu wake hivyo nilimuuliza maswali nikiwa nimepaniki sana.

"Huyu mtu anayenitishia na video ni wewe sio ? , Mike unataka nini kwenye maisha yangu ? "

"Aaah Vee please usinifokee, me mwenyewe nimechanganyikiwa kama wewe sawa ? Iko hivi, huyo jamaa aliyekukutafuta, amewatafuta mademu zangu wote, yaani wote ambao nina video zao na kuanza kuwatisha kwakuwa tu ananidai laki mbili "

Alizungumza Mike akijifanya kuwa na yeye amechanyikiwa.

“Mike usinifanye mimi kama mtoto mdogo sawa ? Mimi ni mtu mzima na ninajielewa, huyo mtu amepataje hizo video ikiwa nilishakulipa zaidi ya milioni kwaajili ya wewe kufuta hizo picha na video zote "

"Huu sio muda wa kunilaumu, fanya hivi, njoo geto tuyamalize”

"Unakichaa wewe ??".

"Vee acha kufikilia upuuzi wewe, sina chochote ninachoitaji kwako sawa?, kwanza hautakuwa mwenyewe, jamaa atakuja nimemuita ili anirudishie simu yangu na ikiwezekana nilipe pesa, najua pesa sina ila nitajua nafanyaje, wanawake wenzio pia wanakuja "

Eeeh Mike anajua kupiga sound jamani uwiiiih, kwa maelezo yake, nilijikuta nikikubali tu kwenda uko.

Nilijiandaa na kuvaa nguo zangu za heshima, nikaaga na kuondoka.

Safari yangu ilikuja kuishia kwenye geto la mike ambapo sikukuta ata mtu mmoja kwakweli, Mike alinipokea pale na kuniaminisha kuwa wengine watakuja.

Kwa wakati wote huo, nliamua kuwa bize na simu tu sikutaka ata kupiga story na Mike.

Ila nyie upwiru sio kitu kizuri, nikiwa nimekaa, nilijikuta nikianza kukumbuka mambo ambayo nilishawai kufanya na Mike, tena kwenye chumba iko iko.

Mike alikuwa akiniangalia sana tena kwa Macho ya tamaa, kwakuwa mike anajua udhaifu wangu, hakuchukua muda kunichanganya na hatimaye tukapinduka kwa mara ya pili.

Nyie katika wanawake wapumbavu na mimi naomba mniweke 🥺💔mimi ni mjinga kabisa.

Baada ya kumaliza kupinduka na kila kitu, mike aliinuka na kusogelea laptop yake kisha akawasha, na kusema.

"Waooooh imetoka vizuri sana, imechukua kila angle yaani, daaah na sura yako imetoka karibu kabisa"

Nilistuka sana na hapo nikagundua kuwa nimerekodiwa kwa mara nyingine uwiiih Vee mimi kwisha habari yangu....

ITAENDELEA
ROWAN (Mine alone )

MTUNZI: Mr Burudan

SEHEMU YA: 05

SONGA NAYO.....

Nilikurupuka kama sijui ni kitu gani, kwa wakati huo nikasema liwalo na liwe, yaani akitaka Mike aniue tu lakini siwezi kuruhusu kudhalilika tena.

Nilimuwai Mike na kumkaba kwa nyuma, uku wazo langu likiwa ni kuiwai laptop na kuiteketeza na nashukuru Mungu niliweza kutumbukiza kwenye beseni la maji ambalo lilikuwa pembeni.

Hapo ni kama niliongeza hasira ya Mike jamani, alitaka kunipiga lakini gafla akaacha na kunitupia mavazi yangu kwa hasira sana na kuniambia.

"Vaa vibwende vyako na uondoke we kunguni wa kizungu "

Kwa haraka nikachukua nguo zangu na kuvaa, kwa wakati huo nilijikuta nikiwa na amani sana jamani, akili yangu ilinituma kuwa video zote ziliteketea pale tu nilipoharibu ile laptop yake.

Nilifika nyumbani na kuendelea kuigiza kuwa nina huzuni maana wanajua kuwa ninamsiba wa rafiki yangu.

*******

Siku iliyofuata nilijiandaa na kuwai chuoni, siku hiyo tulikuwa na vipindi vya asubuhi kwani kipindi cha kwanza kiliaanza saa 2 kamili asubuhi.

Nilifika na moja kwa moja nikapitiliza Darasani, ile naingia tu uso kwa uso na Mike ambapo alijiangalia na kunikonyeza, na mimi nilivyo na akili fyatu nikamzomea kwa kutoa ulimi nje.

Aaah sijawai kujiamini kama siku hii jamani, nilijikuta nikiwa na amani sana na nikijisikia raha isiyo kifani, siku hiyo nilicheza cheza na kuimba nyimbo mfululizo.

"Binti, leo naona umekuwa updated " alizungumza shoga angu.

"Ahhahahha, unajua nyimbo ya obby alpha wewe ? Ile anasema hivi unakajua kale ka feeling ka kujibiwa maombi, naona raha naona raha"

Ila mimi jamani, nilijikuta nikifurahi sana sana siku hiyo, muda wa lunch, niliamua kuwatoa rafiki zangu wote out, akiwemo na Rowan halafu bills on me, nyiee 😎.

********

Week nzima ilipita nikiwa na amani ya hali ya juu.

Ikiwa ni siku ya jumatano, nimekaa vibwetani mimi na Rowan, gafla akaja mvulana ambaye sikuwai kumuona kabla, yaani ilikuwa ni mara yangu ya kwanza kabisa kumuona, mvulana huyo alifika na pasi na kusalimia akaniambia.

"Mike anakuita yupo nyuma ya library "

"Sina ujinga huo mwambie siji " nilijibu kwa kujiamini sana walahi.

Mvulana yule wala hakutaka kueendelea kusubili jibu lingine kutoka kwangu hivyo akaondoka.

Kwa siku hiyo Mike alituma watu zaidi ya watatu na sikwenda, yaani nikiamua kukaza, yaani hapa dawa ya Moto ni moto na sio maji.

"Ni shemeji au mbona anakutumia watu mfululizo ??" Rowani aliniuliza.

"Ahahah yaani mimi nikatoke kimapenzi na Mike ? Yaani Mike huyu kilaza ? Mtu anakaa mbele na bado aelewi

Rowan aliniangalia kisha akatabasamu na kusema.

"Aaah ndo mnatusemaga hivyo tunaokaa mbele halafu tunafeli ?"

"Sio wewe bhana, ata hivyo sizani kama uwa unafanyaga Vibaya darasani”

“Unapima akili ya mtu na muonekano wa nje ?”

“Sina maana hiyo, Roman Sisi tumeshakuwa watu wa Karibu sana kwa sasa, naelewa uelewa wako, na niseme kuwa nimekuwa asilimia 99 Kama sio Mia Katika kukuamini “

Rowan alionesha kufurahia Maneno yangu mazuri ya kumsifia, maana alicheka kwa Furaha na kufanya niyaone meno yake yote ya kiutu uzima.

Tukiwa tunaendelea na maongezi, Mike alifika Akiwa na hasira Kama zote, alifika na kuanza kunivuta akitaka kunitoa kwenye Eneo ilo.

Walahi Rowan ni mwanaume na nusu, hakuweza kuruhusu mimi kuchukuliwa na Mike hivyo, akanishika mkono kwa nguvu kabisa na kunivutia upande wake.

"Oyaaaah broh kaa mbali na hili kabla sijakuchakaza " Mike akaanza kumfokea Rowan.

ROWAN hakuonesha kujali ata kudogo, kitu ambacho alijali Rowan kwa wakati huo ni kuhakikisha kuwa ananisaidia na nakuwa sawa.

"Rowan nimesema muachie, huyu demu, utakuja kuniona mbaya muda sio mrefu "

Rowan alimuangalia Mike kwa muda kisha akaniachia mkono na kusema.

"Haya nimemuachia sasa na wewe mguse uone "

Mike kwakuwa ni mihuni sana na anajiamini kupitiliza, akashika mkoni wangu kwa nguvu na kuanza kunivuta, woiiiih Rowan sio mtu wa mchezo walahi, hakusubili nini wala nini zaidi alinyanyua mguu wake na kumtuliza Mike kwa teke la punda.

Mike pia hakuwa mzembe na hakupenda kabisa hivyo akaanza kujitetea, kwa wakati huo nilipambana na kumtuliza Rowan tu.

Walipigana kwa muda mrefu, mwisho walitulizwa na wanafunzi wengine na baada ya muda wakaondoka nami nikajikuta nikibaki mimi tu na mashoga huyoga, uwa nawaita mashoga huyoga kwani kuna muda wanakuwa chakula na kuna muda wanakuwa sumu, kiufupi ni watu wanafiki sana aiseeh.

"Eeeh shoga kwahiyo wote wawili umewachanganganya au ? Ata hivyo wewe na Rowan mmeanzia wapi jamani ? Mbona gafla "

Mashoga zangu wakaanza kunichimba.

Kwa wakati huo akili yangu ilikuwa imeshavulugwa hivyo nikaondoka pasi na kuwaaga.

*******

Siku ziliendelea kwenda, uku nikiwa karibu kabisa na Rowan, Rowan ni mkaka Powa sana ambapo alinifanya nijisikie ni mwenye bahati sana kumjua yeye.

Rowan alinilinda na kunifundisha mambo mengi sana.

Kwa upande wa pili ambapo ni kwa Mike, aliendelea kunitisha kuwa atanichafua kama sitampatia pesa, ila kwa wakati huo, nilikuwa nikijiamini sana sana, niliamini kuwa video Zote zimeteketea.

*******

Ikiwa ni siku Mpya tena, niliamka asubuhi na kujiandaa kwaajili ya kwenda chuoni, wazazi wangu na ndugu zangu pia walijiandaa na kwenda makazini kwao.

Nilianza Safari ya chuoni, , nikiwa njiani, nilijikuta nikipata simu mfululizo kutoka kwa watu tofauti tofauti, nilibaki nikiziangalia tu uku nikijiambia kuwa nitawapigia nikifika chuoni.

Nilifika chuoni na kitendo cha kufika tu getini, niliweza kukutana na wanafunzi wengi na Rowan akiwa mmoja wapo, kwa upande wangu, nilimsogelea Rowan na kumuuliza.

"Mbona mpo getini na sio ndani ? Kuna mgomo au ??"

Mwenyewe nilimuuliza Rowan nikiwa nacheka sina hili wala lile.

Wanafunzi wakaanza kunizonga, hapo nilijikuta NikiPata wasiwasi wa hali ya juu, sijui Rowan Ali request saa ngapi, lakini muda huo huo, gari kampuni ya huba ilifika na Rowan akaniwaisha kwenye gari.

"Dereva ondoa gari "

Rowan alimuimiza dereva uku akiwa na wasiwasi wa hali ya juu, safari ilipoanza Rowan akaniuliza.

"Uko sawa ?"

Nilimuangalia Rowan kisha nikatabasamu na kumwambia.

"Mimi ndio nikuulize wewe uko sawa, nashindwa kuelewa ujue, na uku unanpeleka wapi ??"

Rowan akuwa na maneno mengi, kwa upole na utulivu alishika simu yake na kunipatia.

Mtumeeeeeeeeh 😳 nafwaaa Vee mimi, woiiiiih Mike amejua kuniua mie, yaani ameachia video zangu zote, na nilikuwa na video zosizopungua 7, zingine ni za falagha, na zingine ni zile ambazo nilikuwa nikijirekod na kumtumia pale tu alipokuwa akiniomba.

Nilihisi kuzimia jamani 😭, Rowan alinikumbatia kwa nguvu kabisa na kuniruhusu kulia ili kupunguza maumivu makali ambayo nilikuwa nayo kwa wakati huo.

Hapo nilianza kuelewa ni kwanini nilikuwa nikipigiwa simu mfululizo namna ile.

Jumbe za mashoga zangu zilikuwa ni mbaya sana, zilikuwa ni jumbe za kunibeza na kujikejeri, walahi nilijua kudhalilika jamani, kwenye video zote Mike hakuweza kuonekana sura yale ata kidogo ni mikono ndio iliweza kuonekana.

Usafiri ule uliweza kutufikisha nyumbani kwetu kabisa.

"Aaah Rowan asante hapa panatosha nitakuwa sawa " nilimwambia Rowan ambaye alitaka kunifata ndani.

"Please usinikataze, naitaji kuwa na wewe kwa wakati huu, naelewa ni nini unapitia "

Natamani wanaume wote wangekua kama Rowan jamani, kwa pamoja mimi na Rowan tukaongozana na kuingia ndani.

Ile tunaingia tu sebuleni, ni uso kwa uso na familia yangu nzima, yaani ni wazi kuwa walishaona uchafu wangu na ndio umewafanya kuacha majukumu yao na kurudi nyumbani.

Baba aliponiona tu, akanirushia simu yake kwa hasira sana ambapo ilinipata kwenye kifua kwani sikuweza kukwepa.

Mama yangu alibaki akilia tu.

JE NINI KITAENDELEA .....

Maoni

You're not logged in


Tangazo - Sasa nakupenda fully episode
Sasa nakupenda fully episode
   
X
SHARE TO SOCIAL MEDIA

ROWAN (Mine alone) 1 - 5



MTUNZI: Mr Burudan

Sehemu ya: 01

ANZA NAYO....

Niite Vee, jina la kifupisho cha jina langu la Vera, Vera ndio jina langu halisi nililopewa na wazazi wangu, nimezaliwa miaka kadhaa hapo ya 2000.

Mimi ni mtoto wa mwisho katika familia ya watoto watatu uku mimi ndio nikiwa wakike tu.

Niseme kuwa am blessed, yaani ikija kwenye upande wa kubarikiwa mimi nilikuwa nimebarikiwa Aswa, ukianzia kwenye akili kichwani walahi niko vizuri darasani, ukija kwenye umbo Mashallah niko vizuri, ukirudi kwenye sura hapa nisidanganye, sikuwa na sura nzuri sana ila mafuta mazuri na kujing'alisha kulinusaidia sana.

Nimezaliwa kwenye...

👉 Soma zaidi hapa: https://www.gonga94.com/semajambo/rowan-mine-alone-1-5

#Nk #gonga94 #trending #simulizi #hadithi #viral #fictionwriter
#ShortDrama #fblifestyle #BeautyBattle #AfricaVsWorld #Tanzania #Kenya #Congo #Rwanda #Burundi #SouthAfrica #USA #VoteNow #DebateTime #Trending <br>

Share on Facebook
Share on Twitter
Share on LinkedIn
Share on Pinterest
 
Umesoma kwa utulivu · dakika chache tu Asante Endelea kusoma chagua hapo chini
Umependezwa ?? Asante Soma Zaidi rowan-mine-alone
Tafuta Simulizi,Hadithi,Michezo
Andika unacho taka.

Top 10 Kali za Leo

AFANDE MILLAN😎 Sehemu ya 77

AFANDE MILLAN😎 Sehemu ya 77

1.15K
AFANDE MILLAN😎 Sehemu ya 78 na 79

AFANDE MILLAN😎 Sehemu ya 78 na 79

1.15K
AFANDE MILLAN😎 Sehemu ya 80

AFANDE MILLAN😎 Sehemu ya 80

547
NAKUPENDA BILA  SEASON TWO 51 - 65

NAKUPENDA BILA SEASON TWO 51 - 65

256
BILLIONS OF LOVE💓💓   SEHEMU YA "12_13"💓😽

BILLIONS OF LOVE💓💓 SEHEMU YA "12_13"💓😽

216
JOGOO WA KIENYEJI sehemu ya 13

JOGOO WA KIENYEJI sehemu ya 13

197
IN LOVE WITH ZURI* *Sehemu YA SITA*

IN LOVE WITH ZURI* *Sehemu YA SITA*

180
IN LOVE WITH ZURI*   Chapter 7

IN LOVE WITH ZURI* Chapter 7

116
NAKUPENDA BILA MIPAKA 66 - 75 SEASON TWO

NAKUPENDA BILA MIPAKA 66 - 75 SEASON TWO

99
USISEME MTO MFUPI KABLA YA KUINGIA  Nimeshuhudia mchezo wa kiwango kibwa kunako Ligi Kuu , hii imekua mechi bora kuzidi Derby iliyopigwa pale Zanzibar.

USISEME MTO MFUPI KABLA YA KUINGIA Nimeshuhudia mchezo wa kiwango kibwa kunako Ligi Kuu , hii imekua mechi bora kuzidi Derby iliyopigwa pale Zanzibar.

15

ZIMESOMWA ZAIDI

‎TUNDA LA  DADA ‎ ‎SEHEMU YA KWANZA

‎TUNDA LA DADA ‎ ‎SEHEMU YA KWANZA

11.89K
RUNGU LA KIPOFU 22.

RUNGU LA KIPOFU 22.

7.6K
🙄 NILIONA MWENYEWE DADA YANGU ANAGEUZWA🔥  sehemu ya tisa.  👉 Akaanza kunipamp sasa...👇

🙄 NILIONA MWENYEWE DADA YANGU ANAGEUZWA🔥 sehemu ya tisa. 👉 Akaanza kunipamp sasa...👇

3.87K
🔥 UTANI WA SHEMEJI KAICHOMEKA..6..10  KWELI...Aaaaaaaaa chomoa🔥  Sehemu ya sita.  👉 Aaaaaaaaa chomoa...👇  Shemeji inauma utanichana.

🔥 UTANI WA SHEMEJI KAICHOMEKA..6..10 KWELI...Aaaaaaaaa chomoa🔥 Sehemu ya sita. 👉 Aaaaaaaaa chomoa...👇 Shemeji inauma utanichana.

3.41K
MY WANGU❤️ sehemu ya 108

MY WANGU❤️ sehemu ya 108

3K
MY WANGU❤️ sehemu ya 119 na 120.

MY WANGU❤️ sehemu ya 119 na 120.

2.98K
MY WANGU❤️ sehemu ya 116 na 117

MY WANGU❤️ sehemu ya 116 na 117

2.82K
 UTANI WA SHEMEJI KAICHOMEKA KWELI...Aaaaaaaaa chomoa🔥  Sehemu ya 20.  👉 Nikatanua mwenyewe miguu manuu..kazi kwake tu...👇

UTANI WA SHEMEJI KAICHOMEKA KWELI...Aaaaaaaaa chomoa🔥 Sehemu ya 20. 👉 Nikatanua mwenyewe miguu manuu..kazi kwake tu...👇

2.77K
MY WANGU❤️ sehemu ya 106 na 107

MY WANGU❤️ sehemu ya 106 na 107

2.7K
🔥 UTANI WA SHEMEJI KAICHOMEKA..16..20  KWELI...Aaaaaaaaa chomoa🔥  Sehemu ya 16.  👉 nakupenda pia...👇

🔥 UTANI WA SHEMEJI KAICHOMEKA..16..20 KWELI...Aaaaaaaaa chomoa🔥 Sehemu ya 16. 👉 nakupenda pia...👇

2.65K

RATIBA ZA MAKALA ZETU

Hakuna Ratiba kwa sasa

Machapisho Mapya
Vijipost vilivyotangazwa karibuni (yamekatwa hadi maneno 30)
ROWAN (Mine alone) 1 - 5 Post Mpya
ROWAN (Mine alone) 1 - 5
@majario LIVE

MTUNZI: Mr Burudan Sehemu ya: 01 ANZA NAYO.... Niite Vee, jina la kifupisho cha jina langu la Vera, Vera ndio jina langu halisi nililopewa...

NAKUPENDA BILA MIPAKA 66 - 75 SEASON TWO Post Mpya
NAKUPENDA BILA MIPAKA 66 - 75 SEASON TWO
@majario LIVE

:66 Mimi nilitoka nikiwa na furaha sana, Niliondoka hapa ni Kama nimezaliwa upya. Moyo wangu ulikuwa umechangamka mno. Ingawa nilifika kwa kujivuta sana lakini siku imeisha na tabasamu pana kwenye uso...

AFANDE MILLAN😎 Sehemu ya 80 Post Mpya
AFANDE MILLAN😎 Sehemu ya 80
@majario LIVE

🦈🦈🦈🦈🦈🦈🦈🦈🦈🦈🦈🦈🦈🦈🦈🦈🦈🦈🦈🦈🦈🦈🦈🦈🦈🦈🦈🦈🦈🦈🦈🦈🦈🦈🦈🦈🦈🦈🦈🦈🦈🦈🦈🦈🦈🦈🦈🦈🦈🦈🦈🦈🦈🦈🦈🦈 Basi nikaludi ndani sasa , nikamkuta zena ana mawazo sana, nikasema zena naomba nikupe chakula kwanza kisha tutaongea tu nitakuelezea kila kitu mke wangu, zena akanmbia sawa, wala hakuwa na...

IN LOVE WITH ZURI*   Chapter 7 Post Mpya
IN LOVE WITH ZURI* Chapter 7
@majario LIVE

SONGA NAYO..... Kitendo cha mimi kuongea kwa ukali kiasi hicho kiliwashtua sana Idress lakini pia na Ethan, Ethan yeye mpaka alinyanyuka na kuja sehemu niliyokaa kisha akachukua hiyo chai ambayo nasemea...

IN LOVE WITH ZURI* *Sehemu YA SITA* Post Mpya
IN LOVE WITH ZURI* *Sehemu YA SITA*
@majario LIVE

SONGA NAYO..... Kimya kifupi kilipita hii ni baada ya mimi kusikia kuwa Zuri ni mke wa mtu nilikuwa naumia sana sio siri jamani ila sema nilijikaza mbele ya mama asigundue "Unamaanisha kwamba...

AFANDE MILLAN😎 Sehemu ya 78 na 79 Post Mpya
AFANDE MILLAN😎 Sehemu ya 78 na 79
@majario LIVE

Basi ikawa hivyo, na ikakat mwez amani ndani hakuna kabisaa, zena ni kanuna , yani hacheki na mm kabisaa, hatuna story ata, na mala nyingi nikiludi nyumbana namkuta kashalala et...

AFANDE MILLAN😎 Sehemu ya 77 Post Mpya
AFANDE MILLAN😎 Sehemu ya 77
@majario LIVE

Mwandiishi; LISSA Nikasema.mm ndo nanukia ayo malashi mke wangu, akanmbia ndio.kwani apa si nipo mimi na ww. Nasikia marashi ya kialabu, mh nikajinusa sasa na mm. Eeh ni.kweli aya ni...

NAKUPENDA BILA  SEASON TWO 51 - 65 Post Mpya
NAKUPENDA BILA SEASON TWO 51 - 65
@majario LIVE

NAKUPENDA BILA MIPAKA:51 Nilitoka nikiwa nishapendeza hata mama alishtuka na kusema “kulikoni tena? Nilishusha pumzi na kusema “Acha tu mama ndiyo nishaitwa.” Mama alinitazama na kusema “huna namna nenda. Sasa vipi pesa ya...

BILLIONS OF LOVE💓💓   SEHEMU YA "12_13"💓😽 Post Mpya
BILLIONS OF LOVE💓💓 SEHEMU YA "12_13"💓😽
@majario LIVE

“Leo hakuandaa boss , but i promise u kesho unazipata, alijibu jamaa “Okay , dont worry just do it …..alisema yule boss wake kitandani “We dada wewe ni...

JOGOO WA KIENYEJI sehemu ya 13 Post Mpya
JOGOO WA KIENYEJI sehemu ya 13
@majario LIVE

Mwandishi:lissa mwalla Sikuamin macho yangu, hiv n huyu kweli naemuona hapa mbele yangu? Yy alionesha kama ananifananisha mana alikua ananiangalia kwa makini sana, alionitendea yalinirudia akilini niliumia niliona kama nimeona mnyama...

USISEME MTO MFUPI KABLA YA KUINGIA  Nimeshuhudia mchezo wa kiwango kibwa kunako Ligi Kuu , hii imekua mechi bora kuzidi Derby iliyopigwa pale Zanzibar. Post Mpya
USISEME MTO MFUPI KABLA YA KUINGIA Nimeshuhudia mchezo wa kiwango kibwa kunako Ligi Kuu , hii imekua mechi bora kuzidi Derby iliyopigwa pale Zanzibar.
@majario LIVE

Pamba Jiji football club walikua kwenye ubora mkubwa zaidi kwa dakika zote, kuna muda Simba SC Tanzania walikua hawana tofauti na Jkt Tanzania football club. Mechi imechezeka kwa dakika tisini...

🚨😱 imebainika kwamba shati ya kocha mkuu wa Manchester City, aliyoivaa Kwenye mchezo dhidi ya Real Madrid, ina thamani ya Euro 290. Post Mpya
🚨😱 imebainika kwamba shati ya kocha mkuu wa Manchester City, aliyoivaa Kwenye mchezo dhidi ya Real Madrid, ina thamani ya Euro 290.
@majario LIVE

kwa makadirio ya kubadilisha fedha, Euro 290 ni takriban shilingi za tanzania (TZS) 750,000 hadi 780,000 (kulingana na kiwango cha ubadilishaji cha sasa cha karibu TZS 2,600–2,700 kwa dola 1). hii...

BILLIONS OF LOVE💓💓   SEHEMU YA "11"💓😽 Post Mpya
BILLIONS OF LOVE💓💓 SEHEMU YA "11"💓😽
@majario LIVE

"BY BABIE LOVE" "(Alikuja kama muuza chai)" “Twende huko na wewe mi siyo mchawi nilikuwa najilinda tu Faster boda akaongeza speed ili asilipoteze lile gari Yule jamaa akaendesha mpaka huko mjini zaidi...

 Increase Earnings from Pakistan → Get +10% Bonus!  Hello Partner! This week the spotlight is on Pakistan 🇵🇰 Post Mpya
Increase Earnings from Pakistan → Get +10% Bonus! Hello Partner! This week the spotlight is on Pakistan 🇵🇰
@majario LIVE

. If you increase your earnings from this GEO by 25% or more compared to last week, we’ll reward you with a +10% bonus on top. How Your Earnings Can Grow...

Fainali ya SIMBA 🆚 RS BERKANE ilipopagwa tu Zanzibar nilijuwa ni mipango ya huyu jama FAOUZI LEKJAA Post Mpya
Fainali ya SIMBA 🆚 RS BERKANE ilipopagwa tu Zanzibar nilijuwa ni mipango ya huyu jama FAOUZI LEKJAA
@majario LIVE

ona sasa anaanza kuumbuka kwa kuendesha mpira wa Afrika kwa Upendeleo FAOUZI LEKJAA yeye ni ✅️Makamu wa Rais CAF ✅️Mwenyekiti wa Fedha CAF ✅️Waziri wa Fedha Morocco 🇲🇦 ✅️Mjumbe wa kamati ya...

Home Login Signup
Top 20 Privacy Policy Contact us
Terms & Conditions About us Latest