Ingia

Sema Jambo

Unsplashb
750+ Trending Pictures | Download Free Images on gonga94
  Afande sele ft Belle 9 dini tumeletewa

BILIONEA NDANI YA HOTEL SEHEM YA 10

2nd Aug, 2025 Views 84



Rahul aliongeza mwendo wa gari kumuwahi Mr Alberto Airport ..

"HELLLO TANZANIAAAA..." Mr Alberto alitoka nje ya Airport akatazama Mbigu na kufumba macho akaisalimia Tanzania kwa bashasha zote ..

Alitazama huku na kule akiwa na Tabasam lake , baada ya dakika 20 ,Rahul akawa amefika
Umeniweka sana mzee" Mr Alberto alilalamika huku anasogea alipo Rahul

"Nisamehe kiongozi, Masha alitaka nimpeleke Bagamoyo ,nikashindwa kukataa unajua alivyo na Amri huyo"

"Lakini yupo salama "

"Yeah yupo salama kabisa, Ila Kiongozi mie aomba tuongee kama wanaume hapa tutoe kabisa Vyeo"
Rahul akashusha sauti kidogo , Mr Alberto akamsogelea Vizuri huku anaikunjia mikono yake juu ya kifua chake

"Mhuu"

"Upo serious swala la kumuoa Masha"

"Aah Rahul nimefanya kosa sina namna kuwajibika na kosa langu , Tangu nitembee na huyo mschana naweweseka sana usiku sina amani nahisi nina Deni kubwa sana linanizunguka ,Rahul sijasahau hata nukta ya ile saa ,Sijausahau mwili wake kabisa , Acha nionane nae kwanza"

"Yeye ni kama Gold Digger Tu "

"Rahullll please achaa "

" Aya sawa "

"Nitakwenda kumuona Masha , Nenda kamalizie tu kazi zako tutaonana jioni "

Rahul akachukua Tax gari alio kuja nayo akamuachia Mr Alberto kila mmoja akashika njia yake....

Baada Ya Vicky kuachana na Recho ,Alielekea kwenye kibarua chake huwa anauza uza Vitafunwa mtaani ..

Akiwa njiani na Ndoo yake alikuwa ameweka maandazi ndo anaingia mitaa yenye watu wengi na mishe mishe mingi

"ALBERTO!!! Kwanini namuwaza sanaa aah mtu mwenyewe hataa simjui lakini siachi kuliwaza hili jina" Alikuwa anatembea huku kichwa kinauma kwa kumuwaza Mr Alberto

Gafla tu alijikuta anapoteza umakini hata Barabarani, amefika kwenye Punda milia alivuka bila hata kusubiri wala kutazam kama ni salama yeye kuvuka

Mr Alberto alikuwa njian na hamu ya kumuona mschana alemsababishia matatizo kichwani alikuwa anapanga maneno ya kuongea nae pindi tu atakapo muona ,ataongea nae nini atatumia neno gani walau asimfikirie vibaya ..

Hakuwa tena na uhakika na barabara ili mradi hakuona Gari mbele aliona njia ni nyeupe akakanyaga mafuta kwenda mbele

Hapa na hapa anakuja kushtukaa kuna mtu mbele yake ,

Ndo muda huo na Vicky alikuwa akivuka kichwani ana yake
Nae anashtuka gari imefika miguuni kwakee
Hata kupiga kelele alishindwa alifumba macho akasema na mungu wake ..

Mr Alberto ilibidi afunge break kwa nguvuu huku akijaribu kukwepesha gari pembeni
Bahati mbaya alikuwa amechelewa akam sukuma pembeni Vicky bahati nzuri hakumgonga
Vicky alianguka pembeni kabisa akapoteza Faham

"Kila siku mimi wakusababisha matatizo tena kwenye Ardhi ya ugeni aah" alishuka akiwa na Hasira na woga kibao

Watu washajaa wamezunguka

"Mungu wangu ni mjamzitoo?? Jamani naombeni mnisaidie nimuweke kwenye gari"

Kwakua Mr Alberto alionekana ni mtu mwenye asili ya kizungu watu hata hawakupiga kelele kumzonga

Badala yake wakabaki kumlaumu Vicky hakuwa makini wakati wa kuvuka
Hawakujali ni mjamzito na hana faham kabisa

Mr Alberto hakujali maneno yao., mwenyewe alijisikia unyonge kwa sababu alikuwa na uhakika yeye ndio sababu ya kumsabishia bint wa watu shida

Aliangalia maandazi yalivyokuwa yamesambaa barabara yote lakini hamuwa na jinsi aliamua kumuwahisha hospital kwa kuulizia hospital iliyopo Karibu
Alielekezwa lakini alipo fika aliona hospital ndogo yaan ipo ipo akasema Noo bibie Vumilia kidogo tunafika hospital ambayo nina uhakika nayo

Alikanyaga mafuta mpaka kwenye Hospital iliyopo mwananyamala Hospital kubwa sana ya kisasa ma daktari bingwa vifaa vya kisasa na vipimo vya uhakika

Hospital hii ndio kwanza ina wiki tangu ianze kufanya kazi sasa ndio Alberto alimleta huku Vicky

Hakuana muhudumu hata mmoja anaemjua Mmiliki wa hii Hospital zaidi ya msaidizi wake wa karibu Rahul

Wahudumu walimchukua wakaanza kumpa huduma ...

Rahul baada ya mizunguko kuisha alimpigia simu sana Mr Alberto lakini haikuwa inapokelewa akaamua kwenda nyumbani kwa Masha

"Yaan wewe unaniambia leo kuwa Mr Alberto amekujaa yaan sasa hivi ndio unaniambia??" Masha hakuwa na Taarifa za ujio wa Mr Alberto ndo kwanza anapewa tena baada ya Rahul kumkosa kwenye simu

"Alisema anataka kukufanyia surprise "

"Hayaa yupo wapiii sasaa"

"Kama hajafika basi atafika tu hapa "
Rahul aliondoka baada ya kuona hapo hakuna cha maana zaidi ya kupewa lawama

"Waooooh siamini hahah et ananifanyia Surprise ,Mhuu ngoja sasaaa" Masha alianza kuandaa haraka haraka mazingira ili Mr Alberto atakapo fika akute mambo ya mahaba kama yotee
Kwanza akafukuza wafanyakazi wake wotee
Na amejaza wafanyakazi kila idala , hakuna anachofanya hata kusuuza nguo yake ya ndani alishasahauu

Akachagua vinguo vya kimitego mitego

"Yaan hapa hachomoii penzi nitakalo mpaa hehehe mbona atajuta kuchelewa"
Akajiandaa masha kumpokea Mr Alberto

Huku Mr Alberto yeye alishindwa kabisa kumuacha Vicky katika hali ile , Haraka zake zikaishia pale ..

ITAENDELEA....
KWETU morogoro.
   

X
SHARE TO SOCIAL MEDIA

BILIONEA NDANI YA HOTEL SEHEM YA 10  >>> https://gonga94.com/semajambo/bilionea-ndani-ya-hotel-sehem-ya-10
#Nk #gonga94 #trending #instagood #explore #viral #challenge #simulizi #hadithi #israel #iran #war 

Share on Facebook
Share on Twitter
Share on LinkedIn
Share on Pinterest
 

Afande sele ft Belle 9 dini tumeletewa
SIMULIZI NA SAUTI
gonga94ads - The Best Popunder Adnetwork
Mambo ya wakubwa hayo soma kwa uangalifu 18+
Mambo ya wakubwa hayo soma kwa uangalifu 18+

HONGERA WEWE NDIO MSHINDI WA VOCHA YA LEO VOCHA NAMBA (499712343590381) MTANDAO VODACOM TUMA NENO NIMESHINDA KWENDA NAMBA 0768304821


majario rewards 100 Comments 0
 

BLOOD MOON EPISODE 1

mjukuu rewards 100 Comments 0
 

CHANZO NI BOSS 03

mjukuu rewards 100 Comments 0
 

CHANZO NI BOSS 02

mjukuu rewards 100 Comments 0
 

CHANZO NI BOSS 01

majario rewards 100 Comments 0
 

MTOTO WA MAMA LISHE

majario rewards 100 Comments 0
 

MY LUNA SEHEMU YA : 06

majario rewards 100 Comments 0
 

NDOA YA MIE ... 8...

majario rewards 100 Comments 0
 

LUVIE binti wa malaya

Home Login Signup
Top 20 Popular Contact us
Terms & Conditions About us Latest