Ingia

Sema Jambo

Unsplashb
750+ Trending Pictures | Download Free Images on gonga94

Hadithi ya "Mbweha 🐾 na Jogoo πŸ“

20th Jul, 2025 Views 87

Hadithi ya "Mbweha 🐾 na Jogoo πŸ“
Siku moja, mbweha alipita karibu na jogoo.
Akamwambia:
"Ewe jogoo, niliwahi kusikia sauti ya baba yako mara moja, ilinivutia sana na nikatamani kuisikia tena."

Jogoo akamjibu kwa majivuno na sifa;
"Sauti yangu ni nzuri kama ya baba yangu!"
Kisha akafumba macho yake ili apige kelele kwa sauti yake.

Mbweha alipoona jogoo amefumba macho, akamrukia maramoja na kumkamata, kisha akakimbia naye mbali.
Mbwa wote wa kijiji walipoona tukio hilo, wakaanza kumkimbiza mbweha.

Jogoo, akiwa mikononi mwa mbweha, akamwambia mbweha:
"Kama unataka kuwakimbiza mbwa hawa wasikufuate, waambie kuwa mimi (jogoo) sitoki kijijini kwao."

Mbweha alifumbua mdomo wake ili kuzungumza, lakini kabla hajamaliza kusema β€” jogoo akaanguka kutoka kinywani mwa mbweha na kukimbia akaokoka!

Mbweha akasema kwa hasira:
"Ulaaniwe mdomo unaoongea wakati ambao unatakiwa unyamaze!"

Jogoo akamjibu akisema;
"Na lilaaniwe jicho linalofumba wakati linapaswa kuwa macho!"

Mafunzo kutoka hadithi hii:
1. Usijivune au kuamini sifa unazosifiwa kirahisi, hasa mbele ya watu wenye nia mbaya kwako.

2. Mtu mjanja hujua wakati wa kunyamaza na wakati wa kusema, lazma ujue kusoma alama za nyakati, na huo ndio ujanja.

3. Uwe makini na hila za watu wenye tabia ya unafiki, mnafiki anahila nyingi pale anapotaka kufanikisha jambo lake lazima uwe makini mno juu ya hila za watu.

4. Usifumbe macho (kihisia au kimawazo) mbele ya hatari – kuwa macho kila wakati, kamwe usimuamini mtu moja kwa moja ajapokujia na sura nzuri ya Swahaba Abubakri Swiddyq.

5. Ujasiri na busara vinaweza kukuokoa hata katika hali ya hatari sana,.

Ni hadithi fupi yenye hekima nyingi!.
   

X
SHARE TO SOCIAL MEDIA

Hadithi ya "Mbweha 🐾 na Jogoo πŸ“   >>> https://gonga94.com/semajambo/hadithi-ya-mbweha-na-jogoo
#Nk #gonga94 #trending #instagood #explore #viral #challenge #simulizi #hadithi #israel #iran #war 

Share on Facebook
Share on Twitter
Share on LinkedIn
Share on Pinterest
 

SIMULIZI NA SAUTI
gonga94ads - The Best Popunder Adnetwork
karibu msagala furniture
karibu msagala furniture

HONGERA WEWE NDIO MSHINDI WA VOCHA YA LEO VOCHA NAMBA (499712343590381) MTANDAO VODACOM TUMA NENO NIMESHINDA KWENDA NAMBA 0768304821


majario rewards 100 Comments 0
 

A.J.A.D SE03 EP02

majario rewards 100 Comments 0
 

Simulizi: MAPEPE **

majario rewards 100 Comments 0
 

NDOA YA MKEKA 03

majario rewards 100 Comments 0
 

.BABAMKWE epsd 19.

majario rewards 100 Comments 0
 

ALINIINGIA BILA IDHINI

majario rewards 100 Comments 0
 

BABAMKWE..17..18

Home Login Signup
Top 20 Popular Contact us
Terms & Conditions About us Latest