Ingia

Sema Jambo 2025

Unsplashb
750+ Trending Pictures | Download Free Images on gonga94
  gonga94 official track

MIMBA YA DHARURA 13 13---14

11th Sep, 2025 Views 79


Nadia alishindwa kuendelea kukaa pale ofisini alinyanyuka na kutoka huku kabir akiwa anamsindikiza kwa macho na kusahau kama Jayden yupo pale.
" Vipi kuna tatizo? Jayden aliuliza
" Hapana.
Jayden valimuonyesha sehemu ya kusain kisha akatoka na kuelekea moja kwa moja ofisini kwa Nadia.
" Vipi Nadia kuna jambo lina kusumbua?
" Hapana.
" Unajua haipaswi kujificha kitu Nadia.
" Naomba uniachie nataka kukaa pekee yangu .
" Kuna kitu kinaendelea kati yako na kabir na ndio maana siku ile kwenye sherehe ulikuwa huna amani hata kidogo.
Nadia hakuwa na cha kujitetea alinyamaza kimnya.
" Una uhusiano nae kimapenzi?
" Hapana.... Alijibu Nadia kwa sauti ya ukali.
Jayden nimesema toka ofisini kwangu sitaki maswali.
" Sawa natoka lakini nakuhakikishia nitajua kila kitu , hata kama sio leo basi siku za mbeleni nitajua tu Nadia.
Jayden alitoka ofisini kwa Nadia kwa hasira akabamiza mlango.

Kwa upande wa kabir bado alikuwa akimfikiria Nadia na kuona kama bahati imerudi tena kwa mara ya pili hakukumbuka kama yeye ni mume wa mtu bado tamaa zake zilikuwa ni ku mmiliki Nadia.
" Haijalishi nipo na nani au yupo na nani Nadia yupo kwenye nafasi yangu.
Maombi yangu yamefanya kazi na ndio maana yupo karibu na mimi hivi sasa. Hii ndio karma yangu.

Nadia alibaki ofisini kwake akiwa na mawazo Maneno ya Jayden bado yalikuwa yakirindima kichwani:
“Nitakuja kujua kila kitu, Nadia…”
Alijaribu kujishughulisha na faili lililokuwa mezani, lakini maandishi hayakuonekana, yalikuwa kama michoro isiyoeleweka. Kila akijaribu kushika kalamu mikono yake ilitetemeka.

Wakati huo Jayden alikuwa ameshuka chini kwenye parking, lakini hasira zake zilimfanya ashindwe hata kuendesha gari. Alijigonga kwenye kiti cha dereva, akapiga ngumi kwenye usukani.
“Huyu Kabir ana nini na Nadia? Na kwa nini moyo wangu unaniuma hivi?” aliwaza kwa uchungu.

Saa chache baadaye, Nadia alipokuwa anaondoka ofisini, Kabir alitokea na kumuita.
“Nadia,” Nadia alisimama kumsikiliza “tunahitaji kuongea.
Nadia akatikisa kichwa “Kabir, acha usinifanye nionekane dhaifu mbele ya kila mtu. Hii siyo sawa. Kama ni mambo ya zamani basi yaishi kila mtu aendelee na maisha yake .
Kabir alimshika mkono na kumvutia ndani ya lift .
" Niangalie usoni .
Nadia hakutaka kumuangalia aliangalia pembeni
“Kwa nini inakuwa tatizo ukiniangalia machoni? Kwa nini kila neno langu linafanya moyo wako kudunda?” Kabir alimvuta kidogo karibu, macho yao yakatazamana
Nadia alijaribu kujiokoa, akatazama pembeni, lakini pumzi yake ilikuwa nzito.
“Tafadhali… acha Kabir. Usinifanye tukarudia makosa yale yale.”
" Acha ijirudie na haitakuwa kosa tena.
Wakati huo huo, mlango wa lifti ulifunguka, na Jayden akatokea akiwa ameshika simu yake. Macho yake yalishitushwa na kile alichokiona Kabir alikuwa amesimama karibu mno na Nadia. Baada ya kumuona jayden alimuachia

Kimya kikali kikatawala kati ya watatu hao.
Huu ulikuwa mwanzo wa moto mpya, moto ambao ungeunguza kila kitu kama usipozimwa mapema…

MIMBA YA DHARURA 14

Jayden alisimama pale mlangoni huku akiwa anabonyeza simu yake, lakini alikuwa akimuangalia Nadia kwa jicho la pembeni.walifija ghorofa ya kwanza mlango wa lift ulifunguka kila mmoja alitegwa kutoka.
Nadia aliamua kutoka na kuwaacha jayden na kabir.
Alienda kuchukua usafiri wa pikipiki na kwenda nyumbani kwake.
Ile ameingia tu ndani huku nyuma mlango uligongwa.
" Dada kafungue mlango.
Alisema Nadia huku yeye alimchukua mtoto wake.
Baada ya mlango kufunguliwa Jayden aliingia ndani.

“Nadia…” aliita kwa sauti nzito yenye hasira “Kumbe kile ndicho alichokuwa unachojificha? Hii ndiyo sababu unasema hupendi kuulizwa maswali?”
Nadia alimpa mtoto dada wa kazi .
" Nendeni chumbani.
Waliondoka na kuwaacha wao wawili .
" Jayden kwanini unanifuatilia hivi? Kwani mimi na wewe tuna makubaliano gani?
" Hatuna makubaliano yoyote lakini huoni kuwa kabir ni mume wa mtu?
" Najua kama ni mume wa mtu.
" Kwahiyo imeridhika kuwa mchepuko wake?
Nadia alitoa tabasamu dogo.
" Unadhani sana ya kujua kila kitu lakini nasikitika kukwambia kuwa haiwezekani kujua kinachoendelea kati yangu na kabir.
" Kwahiyo kuna siri nzito ipo kati yenu?
" Sina la kujibu ila ni bora ukae mbali na hili.
" Sikiliza Nadia nasema lazima nitajua nini kinachoendelea na ikizidi nitahakikisha mke wa kabir anajua mchepuko wa mume wake. Nitahakikisha anakujua.
Mara amina akaingia .
" Hizi kelele nizanini?
Amina aliwaangalia usoni kwa zamu lakini hakuna alijibu . Jayden aliamua kuondoka na akina akimsindikiza kwa macho.
" Nadia nini kinaendelea?
Nadia alikaa kwenye kochi kama mtu aliechoka.
" Usiniambie leo tena umekuja na mapya.
" Hivi ni kubwa kuliko.
Eheeee....
Amina alikaa kwenye kochi ili kusikiliza
" Kabir ndio boss kwenye kampuni ninayofanyia kazi na amekuja kwa kasi ya ajabu anataka kuendekeza pale tulipoishia.
"Weweeeeeee.....
Amina alipiga kelele
" Acha ujinga kelele za nini?
" Nilikwambia rafiki yangu lazima ulikutana na kabir mambo yanaenda vizuri.
" Hakuna uzuri wowote kama unavyoona vita imeanza jayden ananifuatilia na kutaka kujua kinachoendelea kati yangu na kabir.
" Huyu nae chefuuu ananifuatilia kama nani? Kwani ulimkubalia?
" Hapana .
" Basi achana nae alafu mwambie kabir kuwa kuna kiume chake cha mbegu huku.
" Ni mapema sana kumueleza hivyo hilo linahitaji muda.
" Kujua ndio huki my dear ulichelewa kuuanika utautwanga mbichi.

Siku zilizidi kwenda kabir hakuchoka kumfuata Nadia na kumuomba mashairi matamu ya mapenzi ili kumvutia kwake.
Siku moja kabir alienda ofisini kwa Nadia , alimkuta kasimama moja kwa moja alienda na kumkumbatia.
" Unafanya nini .... Alisema Nadia huku akitaka kujitoa kwenye kumbatio. Lakini haikuwa rahisi kabir alimbana kwa nguvu
" Siwezi kuvumilia nilikuta usiku , nipe dakika moja nikumbatie huenda nitajisikia vizuri.
" Jiheshimu, wewe ni boss alafu ni mume wa mtu.
Mara mlango wa ofisi ya Nadia ulifunguliwa na jayden alizama ndani na kukuta wamekumbatiana.
" Hivi ni nini kinaendelea kati yenu nyie wawili?
Jayden alijikuta aliuliza kwa sauti ya ukali.
Kabir alivunja kumbatio na kumgeukia .
" Unauliza kama nani? Kaka, mjomba au baba yake Nadia?
" Wewe ni mume wa mtu kabir hiki unachofanya sio.
" Kwani mke wangu alikuwa kibarua cha kunilinda au kunichunga ninachofanya?
Hivi kwa nini kila anapokuwa Nadia na wewe upo kwani umekuwa kimvuli chake?
Jayden alijikuta anashindwa kujizuia alipaniki na kutaka kumvamia kabir.
Nadia akasimama katikati ya wanaume hao wawili, machozi yakianza kutoka. “Acheni! Kabir, Jayden… sihitaji vita hapa. Hii ni kazi tupo kazini sitaki mfaidishe watu.

Kabir alimgeukia Nadia kisha akaingia kwa sauti nzito.
“USema hivyi Nadia lakini moyo wako unasema vingine kabisa.
Jayden alikuwa na hasira mpaka akarudia simu ukutani, ikapasuka. “Moyo wake sio mali yako Kabir! Na nitahakikisha unajua kuwa Nadia ni wangu. Wewe nenda katulie na mke wako ambae haujamaliza nae hata miezi sita.
" Nimeshasema mambo ya familia yangu hayakuhusu. Nataka ujue huyu Nadia nimeanza kumfahamu kabla yako au kabla ya huyo unasema ni mke wangu.
Nadia alisimama katikati yao huku akiwa anawaangalia wanavyotupiana maneno.

Nadia alifuta machozi haraka, akapumua kwa nguvu.
“Sitaki kumuumiza mtu yeyote lakini msinilazimishe kutoa maamuzi yangu.
Aliongea Nadia kisha akaondoka na kuwaacha ofisini. Kabir aliondoka akamuacha jayden akiwa haelewi .
" Hawa wamekutana lini na Nadia kampa nini kabir mpaka anasahau kuwa ni mume wa mtu na heshima yake hapa
Nadia alikaa akafikiria sana akaona mwisho wa siku mambo yanaweza kuwa magumu . Alimuomba jayden waongee ili kuweka mambo sawa.
Baada ya kazi walienda kukaa sehemu wakapata chakula.
" J kuna jambo nataka kuongea na wewe na naomba unielewe kwa jicho ninachokwambia.
" Ongea nakusikiliza ila usiniambie kuwa unampenda kabir na mimi ukanipotezea.
" Nataka kukwambie ukweli .
Jayden alitulia kimnya huku akiwa anamuangalia .
" Kabir ni baba wa mtoto wangu .
Jayden alishituka Alitaka kuongea lakini alijikuta anapata kigugumizi.
" Kwahiyo inakuwaje sasa Nadia, mimi mahitaji kuwa na wewe.
" Kabir hebu acha hili swala liende taratibu na kabir ajue kuhusu mtoto wake baada ya hapo.....
" Unamaana kabir hajui kuwa una mtoto nae?
" Ndio
" Basi naomba usimwambie kaa kimnya hivyo hivyo.
" Unamaanisha nini kusema nikae kimnya.
" Wewe tulia mimi nitajua la kufanya na pia nakuomba sana, nakuomba Nadia usirudishe mapenzi yako kwa kabir yeye ni mume wa mtu hata Kupa mapenzi ya kweli zaidi atakufa ya mwanamke wa kando hautakuwa na thamani , tofauti na mimi nitakupa thamani na heshima kama mke wa mtu.
Nadia alimuangalia jayden na kushusha pumzi ndefu.

Full 1000
Whatsp 0784468229.
   

X
SHARE TO SOCIAL MEDIA

MIMBA YA DHARURA 13 13---14  >>> https://gonga94.com/semajambo/mimba-ya-dharura-13-13-14

#Nk #gonga94 #trending #instagood #explore #viral #challenge #simulizi #hadithi #israel #iran #war 

Share on Facebook
Share on Twitter
Share on LinkedIn
Share on Pinterest
 

Maoni

You're not logged in
Click here to login and comments
gonga94ads - The Best Popunder Adnetwork
gonga94 official track
ZETU
SIMULIZI NA SAUTI ZETU
gonga94ads - The Best Popunder Adnetwork
Tangazo - PROMOTE YOUR BUSINESS FOR FREE
PROMOTE YOUR BUSINESS FOR FREE
PROMOTE YOUR BUSINESS FOR FREE

RATIBA YA SIMULI ZETU

Hakuna ratiba iliyopangwa kwa sasa.


Home Login Signup
Top 20 Popular Contact us
Terms & Conditions About us Latest