NAISHIWA PAWA💗 SEHEMU YA "1"💞 Ni majira ya jioni mida ambayo nilikuwa nimetoka kazini naelekea nyumbani
nilikuwa ndani ya gari langu naendesha mdogo mdogo huku nikiwa nayaangaza macho yangu kwa umakini zaidi barabarani ili nisije kusababisha ajali......kabla hata sijakaribia mtaa ninaoishi
Lilianza kunyesha bonge la mvua😫😫ni mvua iliyokuwa imeambatana na upepo mkali sana niliongeza mwendo kidogo wa gari.....nilipofika pembezoni mwa njia panda ya kuingilia nyumbani kwangu nilipunguza mwendo ili niweze kukata kona..
Wakati nakata kona mmhhh🤔🤔nikamuona mtu anahangaika katika baiskeli haikuwa baiskeli ya kawaida ni zile za walemavu🥹🥹
Mtu yule alikuwa anajisukuma mwenyewe na kutokana na upepo mkali uliombatana na mvua kubwa alijikuta kila akijisukuma hatua mbili mbele anarudi nyuma hatua kumi😭😭😭
Mimi na moyo wangu wa huruma nikajikuta namhurumia🥹🥹🥹nikajiambia ni lazima nimsaidie🥹😢 nilijisemea kimoyomoyo huku moyo wa huruma ukiwa unanisukuma kwenda kumsaidia...
mvua kubwa upepo mkali vilizidi kumtatiza ilifikia hatua yule mtu alishindwa kabisa kuisukuma baiskeli yake akabakia ametulia tu bila kufanya chochote🥹🥹😢 hapana siwezi kumuacha hapa peke yake natakiwa kumsaidia😢😢
nilijisemea hivyo huku nikiwa naufungua mlango wa gari langu haraka nikatelemka chini na kuelekea sehemu alipokuwepo yule mtu..
""Habari yako....... pole sana...... naomba nikusaidie""🥹😔
""Asante sana lakini siwezi kutembea """
"""Haina shida nitakusukuma hadi pale kwenye gari langu kisha nitakupandisha kwenye gari ili usinyeshewe...
Aliinua kichwa chake akawa ananitizama bila kusema chochote🥹🥹naitwa Pink niamini nachotaka kufanya ni kukusaidia tu........nilijitambulisha huku nikiwa namsukuma taratibu kuelekea sehemu ilipokuwepo gari yangu"""
""Asante sana Pink🥹🥹mimi naitwa Jordan"
Nilimsukuma Jordan hadi karibu kabisa na gari yangu nilijikaza nikamnyanyua kwa nguvu zote nikafanikiwa kumuingiza ndani ya gari baada ya hapo niliiweka baiskeli yake kwenye buti kisha nami nilipanda kwenye gari nikafunga milango
Nilipomtizama Jordan alikuwa anatetemeka sana kwa baridi nilizidi kumhurumia nilikichukua kimtandio changu kilichokuwa kwenye mkoba wangu nikamfunika ili angalau apate joto kidogo mwilini mwake.......
Asante sana Pink mwenyezi Mungu akubariki sana wasichana warembo kama wewe ni wachache sana wenye moyo wa huruma kwa wako🙏🏻🙏🏻 ni sawa Jordan usijali......unaishi wapi na unaishi na nani?! Kwanini uko peke yako hapa??
Nielekeze nyumbani kwako ili niweze kukupeleka na kama una ndugu au mtu yeyote unayeishi naye mpigie aweze kuja kukuchukua...... sina ndugu Pink niko peke yangu🥹🥹
Nyumbani kwangu ni mtaa fulani naomba unipeleke tafadhali...Jordan alinielekeza nyumbani kwake nami niligeuza gari safari ikaanza kuelekea nyumbani kwa Jordan......samahani ulipatwa na nini kwenye miguu yako?!.....
aah nilipata ajari ya gari iliyoifanya miguu yangu ikose uwezo wake wa kutembea..... pole sana Jordan...... asante Pink...... tayari tumeshafika katika nyumba uliyonielekeza lakini mvua ni kubwa sana nazani ni vyema tubakie kwanza kwenye gari hadi pale mvua itakapopungua.......
it's okay Pink lakini nahofia kukupotezea muda wako......samahani sana kwa kuchukua muda wako asante pia kwa msaada wako...... hahahaaa usijali Jordan sina haraka hata hivyo......
Maongezi kati yangu na Jordan yaliendelea ndani ya gari ilikuwa ni kufahamiana tu Jordan alionekana kijana smart sana umri wake ni kati ya miaka 35 niliukadiria tu hata hivyo kwa haraka haraka ukimwangalia kama hayuko kwenye baiskeli yake ya walemavu wala huwezi kujua kama ni mlemavu🥹❤️
Yani😫😫nilijikuta namlaumu Mungu kwanini aruhusu mkaka mzuri kiasi kile awe kilema🥹🥹ni mzuri mnoo jamani yani lina macho mazuri hiyo sauti yake sasa dah😔💞nilizama deep kimawazo nikawa nawaza tu asingekuwa kilema huyu ndo angekuwa mume wangu..
baada ya masaa takribani mawili kupita hatimaye mvua nayo ilipungua yakabakia manyunyu kidogo tu...... nilipougeukia upande aliopo Jordan nilimkuta kaishapitiwa na usingizi mama weeeeeee nilishindwa namna ya kumwamsha ikabidi niwashe gari nisogee karibu kabisa na geti la kuingilia ndani kwake
hata hivyo nilipoiwasha gari naye alishtuka kutoka usingizini alinipatia ufunguo nikafungua geti nikamsaidia kuingia ndani ya nyumba yake ni nyumba nzuri lakini ilikuwa imepangiliwa ovyo ovyo..na ilikuwa chafu haswa..
Nilitamani nianze kufanya usafi lakini mmmhh usiku umeshaingia natakiwa kurudi nyumbani kwangu nikapumzike maana kesho mapema nilitakiwa kuingia kazini..
Kipindi hicho ndo kwanza nilikuwa mtoto mbichi na nilikuwa nakaa nchini Canada🥰🥰🥰huko nchini Canada nipo tu kikazi..nyumbani kwetu mimi ni Tanzania kabila langu ni muhaya kutokea kule Bukoba...
Nimezaliwa na kukulia jijini Dar es salaam nimepata elimu yangu ya mwanzo hukohuko Tanzania badae masomo yangu ya juu nilisomea nje ya nchi🥰🥰...
Vipi unajisikiaje Jordan...niko sawa Pink karibu nyumbani kwangu samahani lakini mazingira siyo ya kuridhisha...
Hahahaa hapana usijali mi niko sawa hata hivo nyumba yako ni nzuri sana hongera... wow asante sana Pink karibu sana karibu uketi natamani nikuandalie chochote kitu ninaishi peke yangu sina mke wala mtoto🙏🏻🙏🏻🙏🏻
hapana Jordan wala sitaki kukuchosha we pumzika tu mimi naomba nikuache🤝 kama unahitaji chochote naweza kukusaidia kabla sijaondoka....... nop asante sana pink usijali kuhusu mimi naweza kujihudumia😊😊😊
wow Good🤝🤝nilimpa Jordan mkono wangu kwa lengo la kuagana naye alipoushika mkono wangu hakuuachilia kwa haraka aliushikilia kwa muda huku akiwa ananitizama usoni kwangu niliachilia tabasamu kumpa moyo si mnajua tena walemavu hatutakiwi kuwatenga 😁😁
Nilitaka ajisikie vizuri...asijione mnyonge aliniangalia sana kisha akaniambia asante sana Pink aliniachilia mkono nami nikaanza kuondoka kule ndani kwake kabla sijapiga hatua nyingi Jordan aliniita na kuniomba nisubilie kidogo..
alijisukuma na baiskeli yake kuelekea katika chumba kimoja mi nikabaki nimesimama huku najiuliza kwanini amenisubilisha anataka nini kwani?????....🤔🤔
Itaendeleaaaaaaaa..
Makala nyingine zinazocheza na ladha yako
Mapendekezo haya yanatokana na kile unachosoma sasa + Endelea kugundua zaidi
Maoni