NILIUZWA KUWA MTUMWA WA BILIONEA 17 Ciara hakuonesha hofu hata kidogo, mjeledi uliokuwa mkononi kwa Mike haukumtisha
"Usiniambie hauelewi maana ya neno Mtumwa!...naweza kujua ulipata wapi ujasiri wa kutoroka bila ruhusa yangu?" Mike alifoka
"Nisamehe, lakini sikuwa na njia nyingine tofauti na hiyo"
"Mvueni nguo zote...." Mike alitoa amri
Basi Watumwa wawili wa kiume walimvua nguo akabakia mtupu.
Ililetwa meza kubwa kisha akalazwa kwa juu
Mike alikuwa amechafukwa, alianza kutembeza fimbo....si mtu wa kuchoka kama asingebahatika kuwa Bilionea basi angekuwa Mwanajeshi mwenye roho mbaya kuliko wote
Ciara naye ni binti mwenye roho ngumu kupita maelezo. Pamoja na kuchapwa mijeledi zaidi ya hamsini hakudondosha chozi wala kupiga kelele
Kiburi chake kilizidi kuziteka hisia za Mike.
Aliamuru koti likaletwa, alimfunika kisha akambeba mpaka bafuni kwake.
Alianza kumuogesha taratibu huku akimuomba msamaha
"Nakupenda pia....nimejua nakupenda baada ya kukaa mbali na wewe" Ciara aliongea
Basi kwa pamoja walikumbatiana kwa mahaba mazito
"Nilitarajia Mike atapendezwa na uzuri wako, sielewi ni kitu gani kinaendelea hata usionekana machoni kwake....." Katy aliongea akiwa anakata kucha zake
"Hata kama siwezi kuupata moyo wa Mike siyo mbaya kama nitaendelea kuishi hivi kama Mtumwa nayependeka na wewe" Jessa aliongea
"Jiandae tutoke out.....kuna namna najisikia vibaya kama nitakaa hapa huenda nikapoteza fahamu" Katy aliongea
Basi Jessa baada ya kusikia mambo ya out akili ilimruka.
Alivaa nguo nzuri kana kwamba anaenda kuonana na bwana yake. Hakika maisha mazuri yalimfaa kuliko kitu chochote
Waliingia supermarket kutafuta vitu vya kutafuna tafuna.
Wakati wanatoka walikutana na Jasinta.
Huwezi kuamini Jessa alivunga kabisa kama hamjui Mama yake
"Jessa ...." Jasinta aliamua kujipendekeza baada ya kuona anakaushiwa
"Uhusiano wetu uliisha ile siku uliyoamua kuniuza..."
"Nafurahi kuona unaendelea vizuri, unaweza kuendelea na safari yako" Jasinta aliondoka akiwa kakunja sura yake, hakuamini kama Jessa anaweza kumuoneshea jeuri
"Ms*nge huyu kama ningejua toka zamani ana roho ya kutu namna hii hata nisingempa kipaumbele kupita kiasi..." Jasinta aliongea huku akitembea kwa ghadhabu
Upande mwingine Mike aliingia chumbani kwa Suzy, hakutishwa na uchi wake kilichomleta hapa yalikuwa ni mazungumzo na si kingine
"Unaweza kuniambia kwanini Ciara alitoroka..... usiniambie Mama yangu ni tatizo"
"Jessa ndio tatizo, Ciara yupo tayari kujitoa kupita kiasi kwa ajili ya Mtoto wa Shangazi yake"
"Una uhakika kama nitamuondoa hapa Ciara hatasumbua akili yangu tena?"
"Ndiyo ..."
"Ahsante kwa kumleta Ciara...."
"Mama yako anapendezwa na Jessa kama utamuondoa hapa nadhani utakuwa umemkosea sana"
"Mara nyingi huwa napenda kufanya mambo kwa ajili yangu na si kwa ajili ya mtu yoyote yule hivyo sitajali kama atacheka au kununa" Mike aliongea kisha akaondoka
Wakati anatoka nje alimshuhudia Ciara akicheza na Mbwa.
Taratibu tu alijikuta akiachia tabasamu, ni mgumu wa kupenda lakini kwa Ciara amekuwa dhaifu.
"Namshukuru Jasinta kwa kukuleta hapa, nitaandaa zawadi kwa ajili yake" Mike aliongea kisha akaendelea na safari yake
Jasinta akiwa zake nyumbani akiangalia picha za Jessa alishtuliwa na hodi mlangoni.
"Mike kaomba kupata chakula cha jioni na wewe, hii nguo kakuchagulia yeye" Suzy aliongea kisha akasepa
"Montana Hotel...." Jasinta alisoma kikaratasi kilichokuwa kimeandikwa sehemu ya kukutania
Itaendelea ๐ฅ
Makala nyingine zinazocheza na ladha yako
Mapendekezo haya yanatokana na kile unachosoma sasa + Endelea kugundua zaidi



Maoni