VYOTE NDANI GONGA94
NISAMEHE MAMA π SEHEMU YA: 02
Usimulizi huu ni wa watu wazima. Chukua muda wako, tulia, kisha usome kwa utulivu kama machapisho yetu yanayoendelea moja kwa moja.
SONGA NAYO..................
Nilistuka Sana baada ya kuona mama amevuja damu nyingi Sana maeneo ya kuchwani Kama binadamu huruma iliniingia haraka nikatoka nje na kuita tax, nilimuomba anisaidie tukampeleka mama hospital lakini pia sikuweza kumuacha kamili nyumbani nilienda nae muda wote alikuwa akilia njaa, ingawa kamili alikuwa na mapungufu yake lakini alikuwa na akili ya kuelewa Mambo kwa wepesi sana.
Tulifika hospital akapokelewa haraka na kuanza kupatiwa huduma kwa haraka sana, muda huo huo boy friend wangu ambaye alikuwa akiishi magomeni akanipigia
" Mbona simu zangu upokei eeeh ulikuwa wapi ...??"
" Ungeacha kwanza ilo gubu lako Niko hospital Jana tulivamiwa lakini Niko sawa ila shangazi yangu huyu ninayeishi nae amejeruiwa kichwani "
Nilianza kutoa kilio cha uongo na kweli, kipindi iko nilikuwa sitaki kabisa Kama watu wajue kuwa huyu Ni mama yangu yote kutokana na kuwa na muonekano mbaya, na wengi walikuwa wakimsema vibaya lakini sikujali wala Nini kikubwa wao hawajui kuwa Ni mama yangu
" Nakuja Sasa hivi "
Alizungumza boyfriend wangu aliyejulikana Kama Julius nilizoea kumuita baby J, baada ya muda aliwasili alikuta Bado mama amepoteza fahamu na muda huo huo dokta akaitaji kuongea na Mimi hivyo Julius alikuwa akifatilia kujua kiundani niliingia nae kwenye chumba Cha dokta
"Umemchelewesha Sana kumleta shangazi yako hiyo imepelekea hali yake kuwa mbaya Sana lakini usijali atakuwa sawa "
Julius alidakia
" Jitaidi dokta shangazi anatakiwa kuwa sawa "
" Tumuombe Mungu pia "
Muda wote nilikuwa nikijitilisha huruma tu, Julius alikuwa kijana mzuri sana ambaye amelelewa kwenye maisha mazuri lakini pia yangu dini na alikuwa na pesa nyingi baada ya kuwa na biashara nyingi nyingi na alijaaliwa huruma Sana
" Nikitaka kusahau yule mtoto anajaa Sana hivyo unaweza mnunulia chakula, mama akiamka tunataka kumfanyia vipimo Zaidi hiyo Ni Kama huduma ya kwanza tu "
Alimaliza kutoa maelezo pale tukainuka na kutoka nje
" Sikia subili nichukue chakula Cha kamili hapa nenda kakae nao"
Alizungumza Julius na kutoka nje niliingia wodini na kumkuta kamili akiwa amekaa akimuangalia mama kwa uzuni yote yaliyokuwa yakiendelea yalikuwa yananiboa tuu
" Huyu nae sijui amekuja kufanya Nini uku ningewaacha hapa nikaondoka zangu"
Nilichukua Simu na kumpigia Julius
" Eeeeh Kuna shida gani tena me Niko nje hapa nachukua chakula kwanza utakula nini....??"
" Nitakula nikarudi"
"Unaenda wapi Sasa....??"
"Naenda nyumbani kubadili nguo lakini pia kuchukua nguo za kamili na shangazi "
"Usichelewe"
" Usijali lakini pia ukishampa chakula naomba uondoke shangazi asije akaamka akakukuta sijui utamwambia wewe Ni Nani SI unajua shangazi yangu anaona me Bado mdogo ndomana hata kutoka tu saa 12 anataka uwe usharudi "
"Naelewa"
Nikakata simu na kuachia msonyo wa hatari, muda huo kamili alikuwa akiniangalia tu
" Kwani da saada huyu kumbe sio mama ako"
Nilimsogelea na kumvuta mashavu kisha nikaondoka alibaki akiniangalia "
Nilifika nyumbani na kubadilisha nguo Kisha huyo nikaondoka zangu kwenye mizunguko yangu mingine, nilizima na simu kwani Julius alikuwa akipiga sana nikaona kuwa ananisumbua tu na hakuna Cha maana ataniambia Zaidi ya mambo ya hospital.
Julius alikaa sana hospital mpaka giza likaingia, alipata wasiwasi Sana kuona sipatikani alisapigia marafiki zangu kadhaa lakini kila mtu Alisema ajui nilipo hi yote kwasababu niliwaambia wajibu hivyo
Asubuhi namapema nikaenda hospital nikiwa na laki na nusu mkononi kwaajili ya malipo na hii yote ilikuwa ni kipata sababu ya kujitetea kwa Julius, nilishangaa kumkuta Julius akiwa hospital Tena na mavazi yaleyale niliyomuacha nayo jana, alikuwa na hasira sana akanishika kwa nguvu na kunitoa nje Moja kwa Moja mpaka kwenye gari yake
" Ulikuwa wapi na simu iko wapi....??"
Nilianza kujiliza kwani namjua Julius Ni mtu wa huruma Sana akajiachia kwani alikuwa akinivuta nywele
" Sasa unalia Nini na wakati nauliza "
" Me nimechoka jamani nimechoka, kila siku Ni Mimi kila siku likitoka hili linaingia hili, Kama unavyojua shangazi yangu ametengwa na ukoo kwaajili ya uchawi mimi ndio nimeamua kumsaidia na huyu mtoto wake na nimetengwa na ukoo pia"
" Hayo si umewai kuniambia, nauliza Jana ulikuwa wapi na kwanink upatikani simu iko wapi kwanza ....??"
" Unakuwaga na hasira tu wewe, nimeenda kazini Jana kwa muhindi hi yote nipate hela ya kulipa hospital, lakini pia nimefanya overtime mpaka mda huu wamenipa elfu 50 tu ikabidi niweke simu Bondi kwa laki moja "
Julius aliumia Sana alijikuta akinikumbatia na kuruhusu nilale kifuani kwangu, nikabaki nikimzomea chinichini tu
" Lakini Mimi si nipo na nimelipa ghalama za jana zote "
Niliinuka na kujifanya nimestuka ingawa nilikuwa najua kabisa lazima atalipa
" Jamani kila siku wewe unatatua matatizo yangu basi chukua hi pesa "
" Hapana itakusaidia Mambo madogo madogo, lakini pia inabidi uwe na nguvu ya kuvumilia ambayo naenda kukwambia mda huu"
" Kuna Nini Tena unanitisha sana "
" Shangazi aliamka usiku"
"Kauona....??"
Nilimuuliza kwa jazba Sana kutokana na wasiwasi niliokuwa nao
" Yaaaah lakini nilimwambia Mimi ni kijana ambaye natokea kwenye shirika la huruma la watoa huduma "
"Mmmmmmmmmmh"
Nilishusha pumzi ndefu
"Alifanyiwa vipimo na kuonekana kuwa Yuko na kansa kwenye ubongo ndio kwanza imeanza yaani Ni ndogo sana, lakini Kama ujuavyo mambo ya ubongo Ni hatari kufa kupona katika kufanyiwa upasuaji lakini anaweza kufanyiwa upasuaji"
"Hapana hapana naogopa sana Mimi jamani naogopa "
"Aaaah unatakiwa uwe na amani "
Mada hizo za kumzungumzia mama mda wote zilikuwa zinanikela Sana
" Naomba nikamuone mama kwanza unaweza kwenda nyumbani kupumzika "
" Usijali me Niko sawa nitakaa na wewe "
" Si unanipenda...??"
Nilimuuliza
" Ndio "
"Basi nenda kapumzike kipenzi π changu please nakuomba sana ..."
Akakubali Kisha akaniacha kiasi Cha pesa iliiuwa kama laki 5 hivi nilifurahi Sana , tukaagaa Kisha Mimi nikaenda wodini kwa mama
Nilimkuta akiwa anakula, akatabasamu asiponiona
" Kinachokuchekesha.....??"
Nilimuuliza nikiwa nimekasilika, alibaki akinichekea tu
" Kwahiyo unafurahi unavyosumbua watu mda wote tunaonekana kwenye majumba ya hospital si ndio, Sasa we SI mchawi konk na huu mzukure wako si ujiponye au mfe tu "
Nilizungumza kwa hasira uku machozi yakinitoka, nilikuwa nikiwachukia Sana , mama haujibu kitu Zaidi niliona akisogeza kile chakula na kukiweka pembeni Kisha akajilaza na kugeukia upande wa pili akilia kimya kimya, hakuwai kuruhusu machozi yake mbele yangu hata siku moja.
Nilitoka nje nikiwa na hasira niligongana na mbaba kwa na kumuangushia miwani yake, nilimuokotea na kumpatia, baada ya kumuangalia niliita
"Baba"
Ingawa baba aliondoka nikiwa mdogo sana lakini nilikuwa nikimjua Sana sikuweza kumsahau hata kidogo, aliniangalia tu kuonesha kuwa anikumbuki au anijui kabisa maana nimekuwa mdada mkubwa nimependeza na ule uzuri ndo kabisa, akanishika mkono na kunitoa nje kutaka kuongea na Mimi
"Binti unanijua Mimi au unavamia tu watu eti baba, unafikili mke wangu angesikia ingekuwaje ??"
" Na kuoa umeoa ukasahau Kama una mtoto kweli...??"
" Kwani wewe Ni Nani mbo......."
Kabla ajamaliza kuzungumza nilimkatisha kwa kutajia jina langu, alishtuka na kuniomba tusogee pembeni kabisa
" Daaaah saada mwanangu umekuwa kiasi iko vipi ulimaliza shule....??"
" Niliacha "
" Kwanini , nikuulize wewe kwanini uliniacha Bora ungenichukua kuliko kuniacha na yule mchawi na mtoto wake asiyeeleweka "
" Amekuloga na wewe, saada binti yangu sikuwa na Nia hiyo lakini mama ako alikataa Mimi kuondoka na wewe lakini pia ubaya wake ndio ulikuwa unanifanya nikose kuwa na maisha mazuri lakini sasa hivi Nina familia mpya na nashukuru kukutana na wee mwanangu "
" Yaani baba najua kabisa baba yangu una moyo mzuri hivi ulimtoa wapi yule mwanamke naona hata aibu kumuita mama "
" Tutaongea zaidi, chukua mawasiliano yangu haya utanipigia, Nina mdogo wake amevunjika mguu mpirani Yuko amelazwa hapa"
" Sawa baba nakupenda "
Akatoa kiasi Cha pesa na kunipatia Nika..............................
ITAENDELEA...............
Umesoma kwa utulivu Β· dakika chache tu Asante Endelea kusoma chagua hapo chini
Umependezwa ?? Asante Soma Zaidi nisamehe-mama-sehemu-ya
