π£ππ‘ππ ππ πππππ‘π πͺπ πππππ‘ππ *1 - - - - - 5* SEHEMU YA 1 Naitwa Naima; ila wengi wananifahamu kwa jina la Ney. Naishi na mama yangu ambaye alinilea
"Mama samahani kesho nitawahi kurudi mapema usikasirike tu!"nilikuwa nikimuomba mama yangu msamaha na hiyo ni baada ya kurudi nyumbani saa kumi tangu alfajiri narudi nyumbani saa kumi.
"hata usijitetee najua sana ulikokuwa mjinga wewe!Ney najua wewe huwezi kutulia ukisikia ngoma hivo ulikuwa kwa kina shani vijora maana leo kaingiza mzigo.Na olewako utoke ety unaenda kuzindua tutagombana!"mama Ney aliniambia hivo nakuendelea kupanga uzi wake ili aendelee kufuma shuka.
Nyie huu mama Ney hajui tu utamu unaokuwaga kwenye ngoma aisee hasingeongea chochote hata π.Nilijipa shughuli ya kufua nikapika mwenzenu nikaoga na kukaa karibu yake sasa.Muda wote huo alikuwa kaacha kufuma ananitazama tu.
"mama nishamaliza sasa"niliongea huku nikitabasamuπ.
"nimeona .Yani ungekuwa hivi siku zote ungekuwa mtoto mzuri sana. Leo tutakula mapema sasa"mama aliongea huku akiachia tabasamu la upendoπ₯°.
"usijali mama nitafanya hivo siku zote. Haya mi natoka sas"niliongea huku nikinyanyuka.
"nilijua tu yaani huko kujituma kwako kuna jambo. Sasa huendi popote leo kama huna kazi kapumzuke hutaki njoo unisaidie kupanga uzi niendelee kufuma kabla umeme haujakata hapa"mama Ney alinikata maini baada ya kuongea hivo.Lakini kabla sijajibu kiliingia kikosi changu jeshi la watu 3 akiwemo mim sasa Naima a.k.a Ney tunakuwa 3. Swaumu na Jamilla walikuja kunichukuwa mida hiyo ha saa 12 jioni. Walisalimia kwa heshima na kukaa kwenye mkeka.
"baada ya salamu msijisumbue kumsumbiri huyu kifaranga wangu leo hatoki" mama aliongea na kuzidi kukazia hapo.
Basi kwa vile nampenda mama na hawezi kukubali mwanae nichukie au nilie akiwa anaona. Alinikubalia kwa sharti la kurudi mapema. Niliondoka na wenzangu ambapo sote tulivaa sare za vijora toka kwa vunja bei au Shani vijora. Sasa tukiwa njiani, ilipita ndinga kali na kuturushia matope tukaloa chakari!na vile kulikuwa kumenyesha mvua baasi tuliloeshwa wenzenu.Uzuri gari lilisimama akashuka mkaka ambaye sasa ni ex wangu anaitwa Saimon.
"aisee!samahanini sana!nilikuwa nawahi kumpeleka mgonjwa hospitali naombeni samahani sana"Saimon alituomba sana basi hatukumletea fujo kama alivyotuzoea, tukawa tumemruhusu aondoke. Sasa kabla hajageuka kurudi nyuma,akashuka mdada mrembo hadi tukashanga sote kama mwarabu au muhindi.
"hivi nyie mnataka tuwaguse miguu ndio mtusamehe au?"aliuliza mdada huyo baada ya kutufikia.
Sisi badala tujibu tuliangua kicheko maana kiswahili kilovyotamkwa aisee majanga!utafikiri anatonge la wali mdomoni π.
"Saimon niondoe hapa stupid girls!" kaliongea kadada kale na kuondoka.
Ndugu zangu mim Naima nitukane umalize ila usiweke lugha ambayo siisikii maana utakuwa umewasha moto. Kabla gari halijaondoka nilimfata na kusimama kwenye kioo.
"We paka shume! usirudie kuingia anga za wahuni tutakutega mjinga wewe. Kwanza ulivyonitukana sijakusikia ila nakujibu hivi tusi lile ni wewe na ukoo wenu mzima!"baada ya majibu gari liliondoka tukazidi kuzomea hadi lilivyoishia.
Tulifika kwenye uzinduzi huo tukasheherekea. Baadae nikaaga na kuondoka. Nikiwa nakaribia kufika nyumbani nikaona Mama amekaa na Saimon kwenye mkeka. Nikajua baasi saimon kampa mama mkasa mzima wa kilichotokea.Nikasogea nikasalimia nikataka kuingia moja kwa moja ndan.Lakini mama alinitaka nikae maana anamazungumzo na mimi.
"hata hivo mama ndio nilikuwa naondoka maana sijafika nyumbani"Saimon aliaga na kuodoka bila kuongea kitu.
Mama nae akanigeukia huku akipaga vigelegele na kusema "jamani mwanangu nimekuza!Mungu bariki hii furaha kwa soteπ! "jamani mama Ney duuh.
Itaendelea..........
SEHEMU YA 2
"Mama Ney jamani! tulia uniambie nijue nini kinafanya ushangilie hivo"
"mwanangu Naima leo nakwita Jina lako lote Naima Abdallah Shombe. Simon aliniletea taarifa nzuri nimezifurahia"
"Mama bana unazunguuka kama umepokea milioni. Mama Ney kama ni swala la kuolewa sahau kabisa mi siolewi sasa hivi.Na sio na Simon"
"Tulia kenge wa blue wewe!haya Simon anakasoro gani? na kwanza alivyo mtulivu siwezi kukubali apeleke moto kwake.Haya mwanangu ni hivi:Simon amenipatishia kazi huko anakofanyia yeye hivo kesho naanza kazi"
"Mama Ney π³ unaenda kufanya kazi kwa wahindi kweli duuh!sijui nitawaambia nini kina Swaumu sasa"
"Umeanza kunipa habari za hao mashankupe wenzio! koma we mtoto tena koma mara mia koma! mimi natafuta pesa sitaki kujua wewe na hao makenge wenzio mnawaza nini"
Baada ya kuongea hayo mama Ney aliingia ndani akaleta chakula tukala. Alikuwa na furaha sana maana kesho anaianza kazi yake rasmi kwa wahindi. Asubuhi aliniacha akaondoka huku akiniachia pesa za matumizi ya siku nzima na kuniambia atarudi usiku.
Ney wa kubaki nyumbani mmmh sio kweli. Na mimi niliondoka hapo hadi kwa kina Swaumu. Sikufika moja kwa moja mlangoni kwao ila nilisogea kwenye mti ulioko mbali kidogo na kwao. Nilimwita kwa ishara akaja haraka. Maana mama yake hapendi urafiki wetu.
"Ney unasemaje shosti maana mmmh!habari tunazo kwamba mama Ney sasa hivi anachezea matako ya wahindi!"
"Swaumu tutagombana sasa! habari hizo umetoa wapi?Mama Ney anatumika kwa wahindi lakini kazi ya kuuza bidhaa dukani"
Tukiwa tunaongea alifika Zuri shoga yetu nae akachangia kunicheka .Niliona hawa watakuja wanipe kesi ya kuumiza mtu bure niende jela. Nikaondoka haraka na upesi. Hasira sasa ilikuwa kama yote namsaka Simon mbwa huyu. Kaamua kwenda kutangaza. Ghafla nilimuona akiwa anakuja upande wangu.
"mshenzi mkubwa wewe! haya unautofauti gani na kina Swaumu wewe!mwanaume mzima kazi kuzagaza umbea ebu tulia utakuja uolewe !"
"Ney mamy tafadhali ongea taratibu utanidhalilisha sasa! ni hivi: pale napofanyia kazi mimi kuna mtu kajitoa kazini. Sasa wakanipa ruhsa ya kumpa mtu kazi pale. Nikaona fursa nimpe mama Ney"
"sasa ukaona mama yangu ndio anauwezo wa kuchezea makalio yao au?msamaha wako Simon ni wewe kunipeleka kwa mama yangu"
"Ney unajua kabisa nakupenda ndio maana siwezi kukataa niahidi basi tutarudiana"
"twende bana tutaongea tukirudi"
jamani Simon wangu nampenda hata kama kauzu. Alikubali tukapanda bajaji na kuondoka.Mwendo ulifika hadi kwenye nyumba kubwa sana geti jeusi kali kinoma yani.
Niligeuka nakumtazama kwa ukali Simon nae akawa kashapata jibu nini afanye. Basi taratibu alibisha getini hapo na akafunguliwa na mlinzi.
Tukakaribishwa hadi ndani.
"Simon karibu sana! naona una mgeni"
"aaah usijali huyu ni binti anaekuja kumuona mama yake yule mgeni aliyeshika nafasi ya mama Mwaju"
Tulizidi kusogea ambapo niliona bustani nzuri sana na kutamani kugusa mauwa yake. Lakini kwa mbali nikamuona mama Ney akiwa anampa bibi kizee moja hivi maji. Nilimuacha Simon akinitazama mi nikakimbia nikamkumbatia.
"mama ulidhani sikupati! nilikumiss mama yangu. Nilimiss uniseme kwa kitu kidogo tu"
"jamani Ney nani kakuleta hapa"
Mama hakusubiri jibu maana alimuona Simon akiwa anajifinya vidole.
"Ney nenda nyumbani nitakukuta"
Nilisita kumuacha mama yangu pale maana alikuwa kavuja jacho kuonyesha kafanya kazi sana.
"what's going on here?"
hawa watu si watutukane kwa kiswahili nipate kuwajibu vizuri.
Itaendelea............
SEHEMU YA 3
Ney?" Sote tuligeuka kutazama sauti ilipotokea. Tobaaaa!π³ jamani Ney leo kakamatika. Emu mtu aniazime uchawi halafu nitamrushia pesa kwa njia ya mpesa. Alikuwa ni yule mdada niliyempa maneno ya shombo siku ile akiwa na Simon kwenye gari. Alisogea na kumpa miwani bibi huyo. Bibi nae akavaa baadae kisha akauliza kwa upole.
"mama Ney nini kinaendelea?"
"samahani bibi Dadima ni binti yangu alikuja kuniona. Ameletwa na Simon"
"eh karibu mjukuu wangu we nimrembo sana"
Yule binti alikuja na miwani alisogea na kumkamata bibi vizuri tena kwa upole.
"bibi ungepumzika kwanza si unaona umekaa nje mda mrefu". Alimuondoa bibi kisha sote tukafuata ndani humo. Mwenzenu nilibaki kuwasha ambulance moyoni tu. Tuliingia hadi sebuleni tukakaa. Simon alikuwa akinitazama sana na kutabasamu. Nikamkonyeza kwamba nini?hakujibu chochote.
"Simon kaka Mohan ameenda kupokelewa. So i need kumpa zawadi aipendayo"
Aliongea binti yule mashauzi mengi nyuma ni mwenzangu na mimiπ.Simon alinyanyuka na kumfuata. Mimi nilibaki na bibi yule ."mwanangu unaitwa nani?""naitwa Naima ila Nazoeleka kwa jina la Ney". Mimi na bibi yule tulionekana kufanana akili. Hivyo, tulipiga story na kucheka kwa pamoja saana. Sikusahau kumpa story ya sambusa za mama Pili. Mzee wa watu alicheka hadi nikaona mapengo. Mida ya kula tuliweka chakula mezani kisha wafanyakazi tukajiweka kwenye meza yetu. Lakini bibi Dadima alitaka nile nae meza moja. Tukapewa chakula cha kiafrika maana pili pili situmii. Binti mashauzi bana alizidi kunitazama vibaya, mimi nikiwa kwenye msosi wala sikuwaza. Alichukuwa maji nakumpa bibi."asante sana Amla"
Hapo ndipo nikajua kama mashauzi anaitwa Amla. Kwenye meza ya wafanyakazi nilimuona binti rika langu. Baada ya chakula nikamfuata alipo tukaanza maongezi.
"mambo naitwa Naima au Ney"
"oh naitwa Mwaju"
Alijibu huku akiwa busy kuangalia mlangoni ."Kuna mtu unamsubiri hapa? mbona unaangalia mlangon?"
"we mwenyewe utamsubiri baada ya kumuona. Anakuja mtoto wa kwanza wa familia hii mjukuu pendwa wa Dadimaa handsome huwezi amini"
"eh ndio aliyekusubirisha hapa au?"
Mwaju badala anijibu alinionyesha kwa ishara mlangoni. Jamani jamani nyie nyie aliingia mkaka mmoja handsome kwanza kapaa hewani macho makubwa mweupe .Nikadhani Sharuh Khan sasaπ₯°.
"karibu sana mjukuu wangu handsome wangu. Alikaribishwa kijana huyo na ndipo nikashtuliwa na sauti hiyo ya Dadimaa.
"bibi yangu mrembo aisee naona umezidi kuwa mrembo sana lazima nikuowe sasa!"kijana alizidi kukumbatia familia yake.
"Mohan yupo wapi Raj? maana aliaga anakuja kukuchukuwa airport" "mama amepitiliza club atakuja usiku" mama huyo alichukia baada ya kusikia mwanae ameenda club. Mohan alitambulishwa kwetu na sisi tukatambulishwa kwake. Mohan alinitazama sana na kutabasamu tu. Basi familia ilisambaratika kwenda kupumzika maana walihitaji Mohan apumzike. Wafanyakazi wote tuliambiwa tutabaki hapo maana kesho kuna kazi nyingi.
"excuse me!"
"eeh eeh mimi kaka Mohan"
"hapana huyo mwenzio" Mohan alimshushua Mwaju hadi aibu nyie. Mwaju alikereka na kuondoka kwa hasira. Mim nikamfuata Mohan.
Alinisogele hadi nikabanana na ukuta kisha akaiweka mikono yake ukutani hapo. Huyu Mohan naona anaanza uhuni mapema eheeeee.
Itaendelea......
SEHEMU YA 4
Mohan alinisogelea hadi nikahisi sitapumua tena. Akalisogelea sikio. Nikajua sasa anataka kunikiss. Kisha kwa sauti nzito ile ya kiume akasema nimtayarishie matunda. Baada ya hapo aliniacha na kupandisha ngazi chumbani kwake. Emu ngoja kwanza ndugu msomaji; hivi na mimi nilikuwa nasubiri kiss ya Mohan au shetani shindwa sitaki kumuacha Simon wangu. Aliponiachia sasa ndio nikapumua utadhani nilikuwa nimezamishwa baharini na huyu kiumbe anaitwa Mohan kuomba matunda ndio tubananishane ukutani chefuπ.Niliingia jikoni nikiwa na hasira. Mwaju nae alikuwa kajaa kuliko. Sikumsemesha kitu.
"sasa unavuta mdomo na wewe ulikuwa na handsome?acha maigizo!"
"Mwaju acha hujuwi tu kilichonikuta. Yaani saa hizi watu wamelala, yeye anataka atengenezewe matunda"
"eh fursa hii hapa!emu tengeneza nimpelekee mimi"
Baada ya kutengeneza nilimpa kisha akajiweka vizuri nakupokea.Nilimshangaa kawa na furaha ghafla wakati alikuwa kauvuta mdomo kama kibanio cha mtoto mdogo. Baada ya mwaju kuondoka ,nikaanza kufuata maelekezo ya chumba alichoko mama Ney. Lakini kabla nikifikie chumbani, nilivutwa nikazibwa na mdomo. Muda nafurukuta nijinasue nilihisi mwili unabaridi. Kutazama alikuwa ni Mohan akiwa kifua wazi amevalia taulo. Alionekana anatoka kuoga .Anilinishika kiuno na kunisogeza vizuri kifuani mwake. Mwenzenu kule kujivuruga niachiwe kukaisha shawaaaπ nikatulia huku sasa tukitazamana usoni.
"matunda nilikuagiza yapo wapi?"
"nili...Nili..."
"shuuuuutt!"
Mohan aliweka kidole chake cha shahada mdomon kwangu nikabak kimya.Nilimsukuma kidogo nikajitoka nakubaki nikiangalia chini. "Mohan hujalala mjukuu wangu?!" niliposikia sauti ya bibi nilijificha nyumba ya mlango."Ah bibi nimemaliza kuoga ndio nataka kulala"Bibi alimtakia usiku mwema kisha akaondoka. Sikusubiri nirudi kushikwa kiuno na huyu mshenzi niliondoka. Nikiwa naelekea chumban kwa mama yangu ghafla nikaitwa na bibi chumbani kwake. "bibi kumbe hujalala" "hapana nilikuwa nikisubiri Raj arudi nimseme lakini naona anakawia wacha nilale"nilimtakia usiku mwema nikaondoka huku nikiahidi kumuuliza maswali kuhsu mjukuu wake. Asubuhi kulikucha mama akiwa anahisi kuumwa hivo Simon akaambiwa ampeleke nyumbani na mimi nikimaliza kazi nitamkuta."Ney mpelekee Raj maji hapo bustanini na kisha Mohan yupo chumba cha Gim"mama aliniagiza akiwa kwenye hekaheka za yote. Nikaona bora nianze na Mohan maana akisikia nampelekea pia na Raj hatanifanya nichelewe. Na kweli nilivofikiria ndivyo ilikuwa. Raj alikuw akiruka kamba huku akiongea na simu. Wazi kwamba alik4uwa akiomba msamaha kwa demu wake sijui hata walikorofishana nini. Hakufua dafu demu alimkatia. Ndipo akageuka na kukutana na sura yangu."ah asante sana nipoze na hasira ziishe""unajua mimi nikiwa na hasira hua nakula tu sambusa za kwa mama Pili"
Raj alishtuka sana na kutaka kufaham meng kuhusu mama Pili huyo. Bas namimi nikampa umbea wote tulicheka kwa pamoja hadi nikasahau ninamgonjwa nyumbani. Msomaji siku zilikatika bila mimi kuonekana kwa kina Mohan tena kwasababu ya kumuangalia mama. Raj alikuja kuniona mara nyingi tu sana na alipenda kula sambusa za kwa mama Pili.Basi usiku mmoja nikiwa nimesharudi kufanya kazi nyumbani kwao,nilitoka kwenda jikoni nikachukue maji. Lakini kabla sijanywa Mohan alikuja na kunikumbatia kwa nyuma. Ghafla kuliwaka mwanga wa camera . Mohan aliniachia nakutoka kutazama ni nani ila hakukuta mtu.
Itaendelea.......
SEHEMU YA 5
Mohan baada ya kukuta hakuna mtu, alirudi nilipo. Kabla hajasema chochote nilimuwahi nikamwambia aniache nikalale. Alitabasamu tu. Ghafla sim yangu ikaingia ujumbe. Nikakumbuka kuwa Simon alisema atanitafuta. Mohan baada ya kuona natoa macho kwenye sim alininyang'anya nakusema kama naitaka nimfuate. Mi sikumfuata wala nini nikamuacha maana najua sim inapassword. Anataka tu nimfuate aanze kunishika kiunoπ. Asubuhi niliamka akiwa bado amelala. Basi nikaenda kumuona mama baada ya kumaliza kazi zangu. Simon alinisindikiza ,alikuwa kanuna balaaaπ .Nikaona nimuombe msamaha kwa kilichotokea jana .
"Simon jana simu..""Ney ushafika kwenu shuka niondoke nina kazi za kufanya nyingi tu"
"Simon nataka tuongee kwa kilichotokea sikuweza ku.."
"Ney mimi sio mtoto mdogo. Tazama ujinga huu na hivi unataka kusema nin"
Simon alinionesha upande wa sms .Msomaji nilishangaa kukuta mazungumzo na nakumbuka kama sim ilibaki na Mohan. Inamaana Mohan ndiye alikuwa akichatt na Simonπ³.Simon hakutaka nijieleze sana alirusha vumbi mbio nikabaki kukohoa tu. Nikamuona mama mida ya jioni nikarudi kazini.
"Ney emu njoo unisaidie kuinuka hapa nikapumzike miguu inauma"
"oh bibi wacha nikufanyie masaage tu"nilianza kumkanda bibi miguu hadi akasinzia. Nikawa natoka sasa nimfuate Mohan chumbani kwake anipe sim yangu. Amla alinijia kwa mbele nikiwa kwenye ngazi. Akanivuta hadi bustanini: Mohan na Raj ndio walikuwa wanawasili nyumbani hapo. Simon nae alikuwa na Mwaju.
"Hivi unataka kazi au unataka kushawishi vijana wa humu ndani?" mimi sikujibu zaidi nilimfuata Mohan na kumwambia nina maongezi nae. Walishtuka sana. Amla akauliza."maongezi gani hayo ambayo sisi hatutakiwi kuyajua?".Watu wote walioko hapo walionyesha kutaka kujua nini kinaendelea. Mohan nae alinisogelea na kusema."exactly kitu gani hicho kwann usiseme hapa hapa"Nilikereka na ujinga wa Mohan nikajikuta nimesema kwa sauti "Mohan naomba sim yangu"
"sim??!"Simon na Amla waliuliza kwa mshangao na mshtuko.
"Amla tafadhali wacha Mohan atoe majibu"niliongea hivo baada ya kuona Amla anakiherehere sana.
"sim aliacha chumbani akiwa kitandani kwangu"
Itaendelea.......
Makala nyingine zinazocheza na ladha yako
Mapendekezo haya yanatokana na kile unachosoma sasa + Endelea kugundua zaidi
Maoni