Ingia

Sema Jambo 2025

Unsplashb
750+ Trending Pictures | Download Free Images on gonga94

PENZI LA MHALIFU 39

30th Nov, -0001 Views 68

PENZI LA MHALIFU 39

Sikutaka kumwambia Cyborg kuwa nimeamua kutumia uzazi wa mpango na iliendelea kuwa siri yangu.

Cyborg alizidi kuimalisha biashara yake huku gari ikibaki kwenye mikono yangu na kidogo ilisaidia kunipandisha thamani kwani ata wale asikari wenzangu hasa wakiume waliokuwa wakinisumbua mara kwa mara akiwemo Afande James walipunguza kunisumbua kutoka na mimi kumiliki gari kwani wengi wao walikuwa hawana.

Siku moja nikiwa kazini nilimuona mtu niliyepotezana nae miaka mingi iliyopita na hakuwa mwingine bali alikuwa x wangu wa zamani kipindi nasoma aliyekuwa akiitwa Dan.

Dan alikuwa ni mwanaume wa kwanza kwangu na kiukweli tulipendana sana na ilifika kipindi tulijiwekea malengo ya kuja kuoana hapo baadae. Dan alikuwa ni mwanaume aliyenitoa bikra na kidogo nilishikwa na aibu baada ya kumuona.

Dan baada ya kuniona hakuamini kunikuta kwenye kituo hicho cha polisi tena nikiwa kama asikari wa kituo hicho.

Alinisogea karibu na kunisalimia na mimi sikutaka kukataa kuipokea salamu yake sababu hatukuachana kiubaya na ni mazingira tu ndiyo yaliyotutenganisha ya utafutaji.
"Angel kumbe unafanya kazi hapa!?" aliniuliza na mimi nilimkubalia.
Baada ya kumkubalia kuwa nafanya kazi kwenye kitu hicho Dan aliniambia "Basi naomba unipatie namba yako ya simu ili tuwe tunawasiliana" Dan aliongea na mimi nilifikiria nakuona haina haja ya kumpa namba zangu kwani huenda tungejikuta tukirudisha mahusiano tuliyowahi kuwa nayo kipindi cha nyuma.

"Itakuwa ngumu kukupa namba zangu Dan maana tayari mimi ni mke wa mtu sasa ivi" niliamua kumjibu.
"Mmmh Angel ata mimi nimeoa kwa sasa ila nahitaji tuwe tunawasiliana na sio kama unavyofikiria wewe" aliniambia lakini mimi sikutaka kumpatia namba zangu za simu na baadae nilimwambia kama atakuwa na shida ya kuonana na mimi basi inatakiwa awe anakuja sehemu ninayofanyia kazi.

Dan alikubali kishingo upande na kuamua kuondoka na mimi niliendelea na mambo yangu.

Siku mbili zilipita na siku hiyo nilitafutwa na namba ngeni.
Nilipoipokea simu yangu niligundua kuwa ni Dan ndiye aliyekuwa kanipigia simu.

Nilishituka sababu sikutegemea kama atakuwa na namba yangu na ukizingatia nilikataa kumpa namba siku aliyoniomba "Dan namba yangu umetoa wapi!?" nilimuuliza baada ya kusikia sauti yake.
"Angel kwani sitakiwi kuwa na namba yako!!!? mimi kwa sasa ni rafiki yako na sio mpenzi wako japo na kumbuka wakati mzuri tuliokuwa pamoja Angel, naheshimu ndoa yako Angel lakini kwangu nahitaji unipe nafasi ya kuwa tunaongea na kupiga story" aliongea maneno mengine ambayo hata sikumuuliza na alidai kuwa namba yangu kaipata kutoka kwa asikari mwenzangu ila hakutaka kumtaja jina kwani alihofia nitaenda kumgombeza mtu aliyempatia namba.

Dan aliendelea kunipigia simu mara kwa mara na sababu kubwa alikuwa akisema kuwa ananijulia hali, na siku hiyo alipiga simu huku Cyborg akiwa karibu yangu lakini sikutaka kabisa kuipokea.
"Angel mbona unaiangalia simu yako au kuna mjinga anayekusumbua tena na anataka umpatie penzi!?" Cyborg aliongea.
"Ndiyo kuna asikari ananisumbua na ndiye anayenipigia simu kila mara" niliamua kumchoma Dan kwa Cyborg.

Cyborg aliichukua simu yangu na kuipokea kisha baada ya hapo aliongea.
"Ivi asikari wenzako hawajakupa habari zangu mpaka uendelee kumfatilia mke wangu sio!?" Baada ya Cyborg kuongea upande wa pili Dan aliamua kukata simu.

Tangu siku hiyo Dan alipunguza kunitafuta na ili kuepusha usumbufu niliamua kuiblock namba yake kwa ajili ya kupoteza mawasiliano nae na kila akitumia namba nyingine basi nilikuwa nikiiblock tu .

Wakati Dan akipunguza kunisumbua kuna mwingine alijitokeza na niseme tu kama kutongozwa basi nilitongozwa.

Siku hiyo nakumbuka ilikuwa ni jumatano alikuja mtoto wa kiume wa mbunge mkubwa tu ndani ya nchi hii akiwa na gari lake (jina lake nalihifadhi) alitupita nikiwa mimi pamoja na asikari wenzangu.

Kijana huyo alishuka na kuingia kwenye ofisi ya mkuu wetu na baadae alivyotoka aliniangalia na  kuamua kuniita.

Niliamua kumfata na nilipomfikia aliamua kuniuliza.
"Unaitwa Afande nani!?"
Kijana wa mbunge aliniuliza na mimi niliamua kumjibu.
"Naitwa Angel"
"Ooh jina zuri unafanya kazi kwenye hichi kituo!?"
Aliniuliza swali ambalo jibu lake lilikuwa wazi ila niliamua tu kumjibu kuwa nafanya kazi kwenye kituo hicho.
Baada ya kumjibu alinipatia simu yake na kuniambia "Basi andika namba zako kwenye simu yangu na hii ni lazima sio ombi" aliongea kwa kujiamini na mimi sikutaka kuhangaika nae kwani niliamua kumuandikia namba za uongo na kumpatia.

"Vizuri nitakupigia" aliongea na kuondoka.
"Atajijua mwenyewe nimeshachoka kutongozwa tongozwa hovyo" niliongea mwenyewe na kwenda kuendelea na mambo yangu.

Siku mbili zilipita na siku ya tatu alikuja tena kwenye kituo chetu cha kazi na moja kwa moja alielekea kwenye ofisi ya mkuu wetu.

Nikiwa sina habari nilishangaa nikiitwa na mkuu.
"Mmmmh mkuu ananiita!?" niliongea mwenyewe na kuamua kwenda ndani ya ofisi yake ili nimsikilize ni kitu gani alichoniitia......ITAENDELEA.
   

X
SHARE TO SOCIAL MEDIA

PENZI LA MHALIFU 39  >>> https://gonga94.com/semajambo/penzi-la-mhalifu-39



#Nk #gonga94 #trending #instagood #explore #viral #challenge #simulizi #hadithi #israel #iran #war

#love #instagood #photooftheday #fashion #beautiful #happy #tbt #followme #picoftheday #art #nature #travel #fitness #motivation #life #fun #instagram #friends #smile #food


 

Share on Facebook
Share on Twitter
Share on LinkedIn
Share on Pinterest
 

Maoni

You're not logged in


Umependezwa ?? Asante Soma Zaidi penzi-la-mhalifu
PENZI LA MHALIFU 33.
PENZI LA MHALIFU 33.
PENZI LA MHALIFU 01.
PENZI LA MHALIFU 01.
PENZI LA MHALIFU 02
PENZI LA MHALIFU 02
PENZI LA MHALIFU 43 (FINAL).
PENZI LA MHALIFU 43 (FINAL).
PENZI LA MHALIFU 04.
PENZI LA MHALIFU 04.
PENZI LA MHALIFU 05.
PENZI LA MHALIFU 05.
PENZI LA MHALIFU 30
PENZI LA MHALIFU 30
PENZI LA MHALIFU 13.
PENZI LA MHALIFU 13.
PENZI LA MHALIFU 03
PENZI LA MHALIFU 03
PENZI LA MHALIFU 08
PENZI LA MHALIFU 08
PENZI LA MHALIFU 23.
PENZI LA MHALIFU 23.
PENZI LA MHALIFU 41
PENZI LA MHALIFU 41
PENZI LA MHALIFU 22
PENZI LA MHALIFU 22
PENZI LA MHALIFU 40
PENZI LA MHALIFU 40
PENZI LA MHALIFU 15.
PENZI LA MHALIFU 15.
PENZI LA MHALIFU 06
PENZI LA MHALIFU 06
PENZI LA MHALIFU 09
PENZI LA MHALIFU 09
PENZI LA MHALIFU 36
PENZI LA MHALIFU 36
PENZI LA MHALIFU 24
PENZI LA MHALIFU 24
PENZI LA MHALIFU 10
PENZI LA MHALIFU 10
PENZI LA MHALIFU 20
PENZI LA MHALIFU 20
PENZI LA MHALIFU 29
PENZI LA MHALIFU 29
PENZI LA MHALIFU 35.
PENZI LA MHALIFU 35.
PENZI LA MHALIFU 11.
PENZI LA MHALIFU 11.
PENZI LA MHALIFU 26
PENZI LA MHALIFU 26
PENZI LA MHALIFU 42
PENZI LA MHALIFU 42
PENZI LA MHALIFU 07.
PENZI LA MHALIFU 07.
PENZI LA MHALIFU 27
PENZI LA MHALIFU 27
PENZI LA MHALIFU 28
PENZI LA MHALIFU 28
PENZI LA MHALIFU 12
PENZI LA MHALIFU 12
SIMULIZI NA SAUTI ZETU
You're not logged in