Simulizi za Maisha,Mafunzo,Mapenzi ,Chombezo Habari za Michezo na Burudani vyote kwa Kiswahili ndani ya – Gonga94 Semajambo
Gonga94 · Stories
30 Nov -0001
103 views
VYOTE NDANI GONGA94
Ufafanuzi Wa 'Aqiyqah Anayofanyiwa Mtoto Mchanga Katika Sunnah
Usimulizi huu ni wa watu wazima. Chukua muda wako, tulia, kisha usome kwa utulivu kama machapisho yetu yanayoendelea moja kwa moja.
Ufafanuzi Wa 'Aqiyqah Anayofanyiwa Mtoto Mchanga Katika Sunnah
‘Aqiyqah maana yake ni kukata. Na katika sharia ni mbuzi anayechinjwa kwa ajili ya mtoto aliyezaliwa anapofika siku ya saba tokea kuzaliwa kwake.
‘Aqiyqah ni Sunnah iliyotiliwa mkazo kwa mwenye uwezo nayo.
Na hili ni jukumu la wazazi kumfanyia mtoto wao kwa kauli ya Mtume (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam)
“Kila mtoto amefungika na ‘Aqiyqah yake, itachinjwa kwa ajili yake siku ya saba na atapewa jina, na atanyolewa kichwa chake” (Ahmad na An-Nasaaiy).
Kwa ajili ya shughuli hiyo ni lazima achinjwe mnyama anayefaa kuchinjwa kwa ajili ya Udh-hiyah kwa kuzingatia kusalimika kwake na kasoro yoyote kama kuwa kilema au kukosa jicho na umri wake uwe zaidi ya mwaka.
Baada ya kuchinjwa mnyama huyo akiwa ni mbuzi au kondoo ni Sunnah kumgawa kama inavyogaiwa nyama ya Udh-hiyah. Baadhi ya nyama watakula watu wa nyumbani, na nyingine utatoa sadaka.
Ni vyema na ndio sahihi zaidi kuchinja siku ya 7 ama riwaya za siku ya 14 au 21 au 28 hazina uhakika sana. Kwa hiyo mtu ajihimu sana kuchinja siku hiyo ya saba. Ikiwa hakuweza kwa sababu fulani fulani, basi Maulamaa wanasema kuwa anaweza kufanya wakati wowote katika uhai wake.
‘Aqiyqah ya mtoto wa kiume ni mbuzi wawili na wa kike ni mbuzi mmoja kama alivyofanya Mtume (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam):
“Mtume (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) alichinja mbuzi wawili alipozaliwa Hassan” (At-Tirmidhiy).
Japokuwa zipo riwaya nyingine ambazo zinaonyesha kuwa mtoto wa kiume na wa kike wanachinjiwa mbuzi mmoja mmoja.
Wanachuoni wamekanusha riwaya hizi kwa kusema ni vyema kwa mvulana kuchinjiwa mbuzi wawili lakini ikiwa mzazi hana uwezo basi atachinja mmoja.
Ikiwa mtoto atakufa kabla ya siku ya saba basi hatochinjiwa.
Makala nyingine zinazocheza na ladha yako
Mapendekezo haya yanatokana na kile unachosoma sasa
+ Endelea kugundua zaidi
Wanangu hakuna jambo la muhimu kwenye malezi ya mtoto kama uwepo na sauti ya Baba
. Tofauti ni kubwa kati ya mtoto anayekuzwa na wazazi wote na yule anayelelewa na Mama pekee. Sauti ya Baba hujenga nidh...
MMMMMMMH UNIFANYE TARATIBU MM NI YATIMA❤️🔥 SEHEMU YA 01...05 Naitwa Leen ni mtoto wa kwanza kwa mama yangu nikifuatiwa na mdogo wangu wa kiume ambaye ni last born
Ibrahim tulilelewa na mama tu baada ya baba yetu mzazi kufariki kipindi nipo na miaka saba hapo mama yangu ndio ana uja...