USIKU MMOJA TU ALIDATA SEHEMU YA 18
ENDELEA......
"Mke mwenza .....umesahau wadhifa wangu hata uniite mke mwenza" Malkia Shamsa alionesha hasira zake waziwazi.
"Furaha tu ndio imenifanya ni zungumze hivi, nakuomba unisamehe sana " Daktari alijitetea.
"Ni dharau, si wewe pekee yako tu...kuna watu sasa hivi nikipita mbele yao wananicheka kimtindo siku ya kesho kutakuwa na msako mkali juu ya watu hao. Sitakuwa na huruma na mtu yoyote yule.... hongera kwa ujauzito. Na hii ni zawadi yako " Malkia Shamsa alizungumza huku akinisogezea boksi .
Nilimpa ishara Kijakazi wangu alifungue tuone kilichomo.
Moyo wangu ulishtuka baada ya kukutana na panya waliokatwa katwa vipande.
"Hivi ndivyo itakuwa endapo utajitia kichwa ngumu, hivi ndivyo itakuwa endapo utajifanya unaijua Ikulu vyema kuliko hata Mimi uliyenikuta " Malkia Shamsa aliongea kisha akaondoka.
Si nilijikaza kupiga kelele lakini baada ya kuondoka kwake nilipiga kelele za kuogopa, hata Daktari alipiga kelele pia.
"Mnasubiri nini kutoa hilo boksi la panya " Nilifoka....
Vijakazi walikimbizana kama panya kutoa boksi. Sikuamini kama Mimi pia naheshimika...
"Ni muda wa Mimi kuvimba, ni lazima ni wavimbie pia. Ni lazima ni heshimike " Nilijisemea ndani ya moyo wangu kisha ni kapanda kitandani kupumzika kwanza.
Usingizi ulikuja basi, nilihitaji kuizungukia Ikulu yote nikiwa na Vijakazi wangu.
Askari walikuwa wanapita huku na kule kuwakamata watu wanaomchukulia poa Malkia Shamsa.
Mmmmh nilishtukia tu wamenifikia pia eti nipo chini ya Ulinzi.
"Naweza kujua kosa langu ni lipi " Niliuliza.
"Wewe pia ni miongoni mwa watu wanao muangalia Malkia Shamsa kwa kumkadiria na ndio sababu tupo hapa kukukamata "
Nilijikuta ni kiachia tabasamu kwa mashtaka nayopatiwa. Nilipiga hatua ni kamsogelea Kiongozi wa Askari.
"Endapo utaendelea kunizingua nitamueleza Mfalme kuwa ulikuwa unanitaka siyo kunitaka tu uliingia chumbani kwangu kwa lengo la kunibaka kama upo radhi kuhimili haya mashtaka fanya utakavyo" Niliongea.
Kiongozi wa Askari alinywea kwa mkwara niliomchimba.
"Ni muda wa Mimi kutafuta heshima " Nilijisemea kisha ni kaelekea malangoni kwa Malkia Shamsa.
Sikutaka kukaribishwa niliingia kibabe.
"Nini maana ya wewe kuingia bila hodi " Malkia Shamsa alinifokea.
Sikutaka kuongea badala yake nililwapua upanga kwa Askari ni kauzamisha tumboni kwa Kijakazi wake
"Hivi ndivyo kitakupata endapo utaendelea kunichukulia poa " Nilifoka.
"Mshenzi wewe ni kitu gani hiki unanionesha " Malkia Shamsa alifoka.
Niliuhamishia upanga wenye damu shingoni kwake.
"Kuanzia sasa unapaswa kuchagua maneno ya kuniambia tofauti na hapo tutakuwa na mgogoro usioisha " Niliongea kisha ni kautupa upanga chini nikasepa.
"Leo ni zamu ya Malkia Shamsa kuingia chumbani kwa Mfalme kwa bahati mbaya sasa nitaingia Mimi. Nahitaji kujua moyo wa Mfalme upo upande wa nani " Niliongea pekee yangu.
Vijakazi wangu waliishia kucheka.
"Kwanini mnacheka? "
"Ni kawaida kwa mtu kuongea pekee yake wanapokuwa Ikulu " Kijakazi wangu wa karibu aliongea
Nilijikuta ni kicheka pia.
Mida ya usiku nikiwa nimejiremba nilielekea langoni kwa Mfalme.
π’Mtukufu Mfalme, Malkia Shamsa na Malkia mdogo Sadia wako hapa. Nimruhusu nani aingie π’ Taarifa zilitumwa ndani.
Basi wote tulitulia kusikilizia majibu......
ITAENDELEA........
Makala nyingine zinazocheza na ladha yako
Mapendekezo haya yanatokana na kile unachosoma sasa + Endelea kugundua zaidi
Maoni