USIKU MMOJA TU ALIDATA SEHEMU YA 20
ENDELEA.......
"Acha kushangaa nina uhakika nilipokuwa na miaka saba 8 tulikutana kwenye hekalu la Watawa. Hiyo siku ulikuwa umevalia nguo nyeupe....sijui lengo lako lilikuwa ni nini lakini ulifanikiwa kuiba sadaka zilizokuwa zimewekwa kwenye kapu" Mfalme aliongea na kunifanya ni kumbuke, nikiwa na miaka 12 nilifanya hili tukio kwenye hekalu la Watawa.
"Kwahiyo Mimi na kuzidi miaka 4 π ni aibu kuzungumza mbele za watu. Kamwe usije kuongea kuhusu Uzee wangu" Niliongea......
"Miaka minne siyo kitu, umebarikiwa mwili mzuri kuliko watu wote wote niliowahi kuwaona....utachelewa kuzeeka" Mfalme aliongea......
Basi tuliendelea kupiga stori za hapa na pale.
Mida ya jioni ilipowadia tulirudi Ikulu.....
"Nimekusubiria kwa muda mrefu sana " Malkia Shamsa aliongea baada ya kufika malangoni kwangu.
"Unalipi la kuniambia?" Nilimuuliza
"Nimekupokea kama mke mwenza, kuanzia sasa na kuendelea naomba tuishi kwa upendo "
"Kwanini umebadilika ghafla namna hii ni kitu gani kimetokea?"
"Sheria zetu zinasema Mfalme ana haki ya kuoa Wanawake zaidi ya 100 kama nitamuonea wivu nitakuwa navunja sheria " Malkia Shamsa aliongea.
Mmmh maneno yake hayakuniingia akilini hata kidogo....huyu si mtu wa kubadilika kirahisi namna hii. Baada ya kuondoka tu nilimtuma Kijakazi wangu akachunguze
"Mfalme katoa onyo kwake na kwa Malkia Ada, endapo wataendelea kukuletea shida wewe basi atawafukuza mahali hapa. Nadhani hii ndio imewatisha " Kijakazi wangu aliongea.
Nilijikuta ni kitabasamu kuona Mfalme anajali kuhusu mimi. Basi Malkia Shamsa pamoja na Ada walikuwa wanashindana kuja kunisalimia na kuniletea zawadi.
Kuna baadhi ya zawadi zilikuwa zimewekwa sumu lakini nilifunika kombe mwana haramu apite kwani kama ningesema nizungumze kwa Mfalme basi wangekuwa kwenye hatari kubwa.
Hatimaye siku ya kujifungua iliwadia. Uchungu ulinipelekesha siku tatu mfulilizo.
"Nimesikia fununu Malkia Ada na Shamsa wapo wanafanya uchawi usitoke salama leba " Kijakazi wangu aliniletea maneno.
Hii ilinipa nguvu ya kujipambania, kama utani hivi lakini hatimaye nilifanikiwa kujifungua mtoto wa kike
Kama ningeleta mtoto wa kiume basi ningeheshimika zaidi.
Lakini pamoja na yote Mfalme hakuacha kunipenda.
Binti yangu Shaa alikuwa mwerevu kuliko hata Mwana wa Mfalme Ivan.
Watu wote wa Ufalme walitokea kumpenda sana.
Hata Malkia Shamsa pamoja na Ada walimpenda.
Baba yangu alijisalimisha kwa Mfalme kwa kuomba nafasi ya kuwa Mwalimu wa Shaa pamoja na Ivan.
Nilielewa lengo lake ni kuleta usawa.... halooo sikuwahi kufikiria kama Baba yangu ni Mwalimu mzuri namna hii.
Ivan alianza kuimarika pia, hii ilimpa nguvu Malkia Shamsa pamoja na Ada na hata wakaondoa unafiki waliokuwa nao juu yangu.
"Unajua Kwanini sijawahi kukupatia mafundisho ya aina yoyote ile?" Baba yangu aliniuliza asubuhi moja baada ya kumaliza kutoa masomo kwa Watoto Mfalme.
"Sijui...."
"Una maamuzi magumu kama Mwanaume, endapo tu ungepata elimu yangu hata kidogo ungelisumbua hili Taifa na sina uhakika kama ingeishi maisha materefu "
Niliachia tabasamu kwa maneno yake, na hata nilimshukuru kwa kujali kuhusu Mimi.
Niendelee kupendana na Mfalme, upendo wetu ulikuwa hauchuji hata kidogo....vijembe vya chini chini vilikuepo lakini havikunitisha............
Ahsanteni kwa kusoma kisa changu, kama utani hivi eeeh ila naitwa Malkia mdogo Sadiaπ₯°π₯°π₯°.
................MWISHO............
UBARIKIWE WOTE MLIONISHIKA MKONO KUPITIA SIMULIZI YANGU HII. MUNGU BABA AZIDI KUWABARIKI SANA SANAAAAA. ITOSHE KUSEMA NAWAPENDAπ«Άπ«Άπ«Άπ.
Makala nyingine zinazocheza na ladha yako
Mapendekezo haya yanatokana na kile unachosoma sasa + Endelea kugundua zaidi
Maoni