VYOTE NDANI GONGA94
BINAMU WEWE UNGEWEZA? SEHEMU 13
Usimulizi huu ni wa watu wazima. Chukua muda wako, tulia, kisha usome kwa utulivu kama machapisho yetu yanayoendelea moja kwa moja.
ENDELEA.......
Manka alijifanya kupani alishtukia kapigwa kibao.
"Aaaaaah! Unanipiga mimi kisa Nice?"
"Huna tofauti na shetani. Kwanza toka chumbani kwangu na ikiwezekana ondoka kabisa nyumbani kwangu. Manka alipataka kuweka mgomo alitishiwa kuchakazwq sura.
Usiku huo kila mmoja alilala chumba chake. Maelewana hayakuwepo tena ndani ya nyumba.
Manka akimpigia simu nama yake ambaye ni shangazi yangu mimi.
"Mama naona mambo yameanza kwenda sivyo"
"Kwanini?"
"Sijui madawa yameisha nguvu au vipi? Lakini mbona ni mapema sana"
"Ebu niambie nini kimetokea"
Manka alimueleza mama yake. Mama yake alimshauri kesho mapema tu aende kwa mganga.
Manka alifanya hivyo kesho yake mapema tu alifika kwa mganga wake. Alipewa dawa nyengine tena. Safari hii alipewa limbwata.
Niliacha kazi kwa maelekezo ya Iron Ceo mwenye kampuni yake na haringi wala nini.
Jion moja nilivunja shauri la mahusiano kati yangu na Sony, nilivua pete ya uchumba aliyonivalisha Sony. Nilifanya hivyo ili nianze maisha mapya kabisa. Nilimuomba rafiki yangu Sophia ampelekee Sony bahasha ambayo ndani yake kulikuwa na ujumbe pamoja na hiyo pete.
Mama na baba walikubali kiroho safi mimi na Iron kwenda nje ya nchi. Mipango ya safari ilienda vizuri hatimaye tulienda Austaria.
Urafiki kati yangu na Iron ulizidi kupamba moto Iron alikuwa mtu wa kujali sana kuhusu mimi. Hatukuchukua muda mrefu tuliingia kwenye hausiano rasmi. Aiseee mwanaume huyu ananipenda vile navyotamani kuoendwa. Baba yake na mdogo wake ni watu wa zuri kwangu.
Sony baada ya madawa kumlolea alitangaza ndoa yake na Manka. Wazazi wake walikataa kata kata Sony asimuoe Manka ila madawa aliyopewa yalimfanya kuwa sikio la kufa yaani kila anachokisema Manka kwale jibu ndio sio hapana.
Mama Manka alikuja dar kwaajili ya ndoa ya mwanae na alifikia Nyumbani kwa Sony .
"Umasikini huo tumeuaga mwanangu"
"Umeona eeeeeh! Mganga kiboko haswaaa!
Mipango ya ndoa iliendeshwa na Manka mwenyewe yeye ndo alipanga kila kitu.
Taarifa za Sony kumuoa Manka zilinifikia. Haikunishtua sana maana nipo kwemye mahusioano yanayoeleweka na naimani nayo.
Jioni moja wazazi wa Sony walienda kwa mtumishi wa MUNGU walimuambia hitaji lao ni mtoto wao. Wanaoma hayupo sawa kabisa na siku za Usoni eti anaoa.
Mtumishi alifanya maombi ya nguvu na baada ya hapo aliomba waongozane wote mpaka nyumbani kwa Sony.
Walifika myumbani kwa Sony walikuta familia zima yaani Sony, Manka na mama Manka wapo kwenye meza ya chakula wanakula.
" Mmmmh!" Manka aliguna baada ya kaxi fungua mlango. Hawakumjali wsliingia ndani wote........ITAENDELEA........
Tume toka mbali na nyumbani kuja kwenye miji ya watu kutafuta maisha
Mwanangu Mungu ndio anae jua
Sikiliza Wimbo Kamili
Umesoma kwa utulivu ยท dakika chache tu Asante Endelea kusoma chagua hapo chini
Umependezwa ?? Asante Soma Zaidi binamu-wewe-ungeweza-sehemu