*CHAGUO SAHIHI*
SEHEMU YA....5
Na
Mamuh Mohd
(0716730000)
Tulipoishia.....
"Na iwe kweli laaa sivyo nitakunyonga kwa mikono yangu".
Aliongea kwa hasira na uchungu sana Jarden....
SONGA NAYO.....
Chini ya serikali walifuatilia kesi ile na ukweli ikagundulika kwamba Jarden ni mtoto wa bwana Msame.
Baba Jarden kupokea majibu yake Palepale alidondoka chini presha ilipanda.
Hata kupelekwa hospital alifikishwa katika wodi ya uangalizi maalum kwani hali haikuwa nzuri kabisa kwake.
Huku nyuma sasa Ndipo bwana msame alimueleza kila kitu kijana wake ilivyokuwa ni kwamba,....
Miaka mingi iliyopita zaidi ya 30 msame akiwa kijana wa miaka 22 alitoka kijijini kwao na kufika mjini kwa ajili ya kutafuta kazi.
Alihangaika huku na kule lakini Baada ya miaka 2 ya shida na tabu alifanikiwa kupata kazi.
Ni katika familia ya kitajiri alipata kazi ya kuwa mtunza bustani wa nyumbani pale.
Alifanya kazi kwa takriban miaka 2 ikafika mahali aliaminika kabisa na familia ile mpaka wakamtuma kutafuta msichana wa kazi kutokea kijijini kwao.
Hapo sasa Ndipo Msame alimkumbuka mpenzi wake ambaye alimuacha kijijini (muna) akaona huo ndio wakati wa yeye kumpa nafasi hiyo ili waweze kuwa karibu.
Msame alifanya jitihada zote na mpaka Muna akafika mjini kufanya kazi katika nyumba hiyo ya kitajiri.
Wakati huo bado walikuwa wakiendelea na mahusiano yao kwani walikuwa na ndoto za kuja kuwa mke na mume.
Mwaka mmoja ulipita ndipo Muna alipata ujauzito na alimueleza ukweli msale kuwa ana mimba yake.
Msale alimtaka wafanye kazi hapo kabla mimba haijafikia hatua ya kujifungua warudi kijijini.
Muna aliendelea kufanya kazi pale lakini kumbe kwa wakati wote huo anafanya kazi ndani pale alikuwa akitumika kimapenzi na mtoto wa familia ile pasina kusema kwa mtu yoyote.
Alibainika kuwa ni mjamzito kwa Boss mama wa nyumba ile na alipouliza kuwa ujauzito ni wa nani, Muna alimtaja mtoto wa nyumba ile.
Kwa kuwa kijana wa familia ile Rich Jarden.
Alimpenda Muna kiukweli hakuwa na lengo la kumdanganya basi alikubali na kuwataka wazazi wake aishi na Muna.
Muna alikubali na neno alilomuambia msame ni kwamba anataka mtoto wao alelewe maisha mazuri.
Msale alishuhudia ndoa ilifungwa ya Muna na Rich Jarden mpaka mtoto anazaliwa kwa shangwe kubwa na kupewa jina Jarden.
Msame alikuwa ni wakilia tu kwani ilifika mahali hata nafasi ya kuzungumza na Muna akawa anaikosa na akiipata muna anamsihi akae mbali nae.
Basi kama haitoshi Muna alimzushia Wizi msame mpaka akafukuzwa kazi kabisa katika familia ile, lengo ni alitaka kuishi kwa amani na mumewe.
*******
"Alinigeuka mama yako maisha mazuri aliyataka pasina kunikumbuka mimi ambaye nilimtoa kijijini tujenge malengo yetu.
Muda wote huu nilikuwa nawafuatilia namna mnavyoishi natafuta kuingia katika familia hii ili wewe jarden unijue lakini haikuwa rahisi.
Tazama ni miaka mingapi imepita zaidi ya 30 ndio leo kupitia hili unanijua mimi nimehangaika kwa miaka mingi sana.
Mwanamke sio kiumbe wa kumuamini hata siku moja mwanangu nimejifunza kupitia mama yako".
Jarden alibaki akilia tu ukweli ule ulikuwa ni wa kuumiza sana kwake.
Akiwa hapo ndipo Jarden alipigiwa simu na binamu yake yule Tizo.
Alipewa habari ambazo zilimshtua sana.
"Baba hatunae amepoteza maisha".
Ndizo habari ambazo alipewa Jarden aliumia sio kawaida.
Saa ngapi asiinuke na kumkaba bwana msame.
"Yote kwa ajili yako umekuja kufanya nini katika maisha yetu ulikataliwa si basi ungeendelea na maisha yako ona sasa ona sasa maafa uliyoleta sitakusamehe kamweee mbwa wewe utaozea jela".
Alipata mchungu Sana Jarden yote yale aliyafanya kwa uchungu na maumivu.
Hata Mama Jarden nae alichanganyikiwa alilia sio kawaida aliumia kupita kiasi.
Ukweli uliojulikana ndio umepelekea hadi Baba Jarden kupata mshtuko na presha kupanda kwa kasi ukawa ndio mwisho wake.
Basi tena familia ilitoneshwa kidonda kingine tena,palepale kwenye mshono wa maumivu ya Kumpoteza Yasinta Ndipo palikuja Kutoneshwa upya baba Mr rich Jarden alipoteza maisha.
Simanzi,huzuni vilitawala lakini ilibidi mipango yote ikamilike na kumuhifadhi mzee huyo.
Upande wa kijana Tizo sasa aliona nae huo ni wakati sahihi wa kujiweka karibu apate mali.
Yeye alikuwa ni mtoto wa dada yake na Rich Jarden kwa maana alikuwa anakaa hapo kwa mjomba wake.
Kitendo cha mjomba kupoteza maisha na ukweli kujulikana kuwa Jarden sio mtoto wa Mr rich Jarden kwa maana alijua urithi wa mali wote utakuwa ni wa binti Joan ambaye sasa tunapata kujua amechangangia mama mmoja na Jarden.
Anatambua kuwa Joan huwaga anampenda sana Kimapenzi ila yeye ndo akawa anamkataa basi akaona kwa wakati huo ni wa yeye kumkubali Joan ili katika mali nae ahusike.
Basi alimfuata Joan ambaye alikuwa amekaa eneo la nnje katika bembea na marafiki zake.
"Joan tunaweza kuzungumza kidogo".
"Yes niambie"
"Faragha".
Joan aliwatazama rafiki zake wale na kuwataka waondoke kwanza pale.
Kweli marafiki wale wakaondoka.
"Pole sana kipenzi kwa kumpoteza baba yako na hata mimi nimempoteza mjomba wangu mlezi Kwaiyo tuna maumivu japo wewe ni zaidi pole sana".
"Usijali Tizo nimeshapoa".
"Mhhh vipi kuhusu Jarden unatakiwa kuwa makini asije kukudhulumu mali hizi sasa ni za kwako peke yako asije kwenda kutajirisha ubabani kwake".
"Mhhh namsubiri sana hapa nasikia yeye ndio kabaki malaloni eti anajiliza hataki kuondoka anadhani akilala pale ndio itabadilika na awe mtoto wa hapa.
Atarudisha kila kitu cha baba yangu naomba uwe nyuma yangu Tizo.
Najua hanipendi ila kwa hili nisaidie ".
"Nakupenda Joan nipo hapa kukupa faraja"
"Unamaanisha nini Tizo tuende hoteli leo ukaniliwaze?"
"Joan itakuwa mapema sana mpenzi ".
"Nani atajua? Tuende plzzz sipo sawa mwili mzima trust me.... mapenzi yanatesa Tizo si unaona Mzee mzima kadondoka kisa mapenzi...akaaa mimi nataka mapenzi yawe dawa kwangu nipone mwili mzima".
"Ok sawa Joan tutaenda".
Basi walikumbatiana pale kinababa kabisa huku wetu wa pembeni waliwaona hawakuisha kunong'ona.
Manga sasa ndio nae anakuja kutoka njje baada ya kumuacha mtoto nafsa amelala chumbani.
Akawaona Tizo na Joan wamekumbatiana wenyewe huku wakiambizana mahaba wetu wanawatazama.
Akaona awafuate ili waachane maana aibu kwa mazingira kama yale.
"Mhhhh mhhhh samahanini Kaka Tizo umemuona boss Jarden yupo wapi?".
"Mhhh anajiliza huko wetu wamerudi yeye anajiliza huko malaloni sijui".
Manga alishangaa alitambua Sehemu ambayo mzee rich Jarden nakwenda kupumzishwa ivyo alikodi boda boda hadi Sehemu hiyo.
Jua lilikuwa limezama lakini akamkuta Jaden analia ameinama peke yake.
Manga akamsogelea hadi pale,
"Boss kulia kutwa nzima hakuwezi kubadilisha ukweli twende nyumbani".
Jarden ndo kama alishtuka maana mwanzo alikuwa amechanganyikiwa.
"Manga umefikaje hapa na wewe "
"Haijalishi ila twende nyumbani tafadhali nafsa anakuita".
Manga aliona aseme ivyo akijua Jarden anampenda sana mwanae ivyo atakubali kwa urahisi.
Manga alimshika mkono boss wake huyo Taratibu walielekea katika boda boda ile wakapanda wote mishikaki kurudi nyumbani.....
Full 1000.
Ianze weekend leo kwa package ya simulizi ya Chaguo sahihi, anana, binti mpelelezi,anana kwa bei ya weekend ofa.
Nichek kwa Whatsapp no 0716730000.
Sijui itakuwaje?
Tukutane Sehemu ya 6.