CHUMBANI KWETU 💚 Sehemu ya 10
Nilifurahi sana❤😘nikaletea mtoto wangu nikamuona nililia kwa furaha nikamshukuru sana Betty maana amekuwa msaada sana kwangu🙏❤
asubuhi ya siku iliyofuata mume wangu nae akaja kumuona mtoto nae alifurahi sana 🥰 akampa jina mtoto wetu kuwa aitwe faith🥰🙏 akasema anaenda kazini akirudi atapitia na tutarud nyumbani,basi nkaletewa chakula nikapiga👌💃
wifi zuu hakuja maana alivyoenda home akapata kahoma, nikasema sababu ya kukaa hospital siku zote hizo,sio mbaya tukirud nyumbani atamuona huyo alotuweka hospital wiki nzima🤣🤣🤣
mama mkwe ilibidi aende kwenye majukumu yake maana mume wangu alisema atatupitia kurudi nyumbani
basi ilivyofika jioni nilikua nishapewa ruhusa maana hatukuwa na tatizo lolote mimi na mtoto, tukawa tu tunamsubiri mume wangu aje ikafika mpaka saa kumi na mbili nikasema labda foleni😫
mama mkwe akapiga nkamwambia bado ajatufata mpaka saivi anawakalisha tu ngoja niwafate nyie mpaka mama mkwe amefika pale ilikuwa saa moja mume wangu akawa tulipiga hapatikani😳
nikaanza kuwa na waswas😭 tukarud nyumbani roho hainipi kabisa😿kila tukipiga hapatikani mama mkwe akajaribu kumtafuta rafik ake akamwambia walivyotoka kazini waliachana akasema anakuja hospital😫
usiku huo ata nililala sasa kila nikipga simu jibu ni lile lile haipatikani🥺 mama mkwe akasema nisiwe na waswas tulale asubuhi tutajua la kufanya,siku iliyofuata wakaenda ripoti polis kuwa mume wangu kapotea ,nikawaza kwahiyo mume wangu kaniacha hivi atakuwa mzima kweli😭😭😭
betty akasema usijali atakuwa salama tu,betty akaondoka kurud anapofanyia Kazi maana aliomba tu ruhusa,mamangu hakuondoka maana asingeondoka wakati hatujajua muafaka wa mume wangu,ikapita wiki hatujapata taarifa zozote za mume wangu😭😭😭
zaidi tu lilipatikana gari eti lilikutwa limepakiwa pale hospital🤔polis wakasema tutulie wanaendelea na uchunguzi roho inaniuma jamani nikikaa chumbani nawaza mwenyewe uko wapi mume wangu mtoto wetu tulompambania umeniachia mwenyewe hivi u mzima au ushakufa😭chumba nakiona kikubwa mimi nimemiss ucheshi wako😿
nikabaki kumuombea dua njema🤲awe salama uko aliko na arudi salama🥺 usiku nikawa nimembembeleza mtoto alivyolala na mimi nikalala , sasa usingizi umenikolea😴nikasikia simu inaita🤔nikaamka ni betty anataka nini usiku huu mamy mbona usiku hivi kuna tatizo?
hamna ila nimeota ndoto mbaya ebu naomba usali Kwa imani yako na mimi uku nasali hili jambo niloota liepushwe sasa niombe nini si uniambie niombee nini?
au unihadithie hiyo ndoto jamani😫weee muombee mtoto tu kesho nitakutumia voice note nkuhadithie sawa basi nikabidi nimuombee sana mtoto wangu🤲😔
nikalia sana Mungu amlinde betty sijui kaota nini...!!! niliomba kama lisaa nikamaliza nikapanda nilale betty akanipigia tena umesali? ndio sawa uyo mtoto ni moto haguswi ng'o Amina mama, tukalala asubuhi nikaamka nikawasha data nikute betty kanitumia hyo voice na nisipokuta nitampigia kawaida mbona😹😹😹
nikakuta kanitumia tu picha na maelezo mama faith mwenzio nimekabwa leo sasa Ile picha alinitumia ilikuwa ya shingo yake yaani nikaona Ina alama maana yeye ni mweupe pee basi alama ilikuwa inaonekana😳
nikampigia umekutwa na nini jana nimekabwa sana Kwa akili zangu timamu nimeshuhudia napigana na mtu ila sikumfahamu makubwa mwaka huu acha tu lakin usijali naenda job tutaongea bde ..
mama lakini kama huna waswas rafiki angu khaa ulopigana nae si itakua ni mchaw eeeh ndio sasa niwe na waswas wanini hata usiwaze bhana ya kawaida tu👌👌sawa dear baada ok siku njema msalimie faith sawa mama kalala saiv akiamka timbwili lake si mchezo
nikaamka sasa nifanye usafi ndani , ntoe na nguo chafu mama anifulie,nikaamka mama nae akawa amekuja akanipeleka kuoga,akatoka aende kufua na kazi zingine , nikachukua simu nijaribu kumpigi aman tena ikawa inaita🥲lakin haipokelewi🥲
nilipiga kama mara nne zote kimyaaaaa🤨 nikatoka nikaenda waambia kina mama simu ya amani inaita leo ila ndo hapokei🥲 aaah jamani angepokea tujue🥺
au twende polis tukaseme simu inapatikana wanaweza jua jinsi ya kumtafuta,mama na mama mkwe wakasema wanajiandaa waende wifi zuu akawa ana vihomahoma tangu tumerud hospital au una mimba shoga angu ata sielewi leo ndo najisikia vibaya sana ukapime kama unatuletea kitoto tujue wee naogopaje😭 si ulikuwa unancheka mimi😹😹😹
ngoja nikalale tu🏃🏃sawa mama
basi mimi nikabaki pale nje najaribu kupiga simu tena na tena lakini wapi😫 nikabidi niingie ndani tu nmuangalie na faith kama kaamka sasa nakaribia mlango wa chumbani nasikia faith analia sana😭😭😭
afu nasikia vishindo vya mtu kama anakimbia mule chumbani🏃🏃nikawahi kuingia nakuta yupo mwisho wa kitanda ananing'inia kwenye net nusu aanguke, kafikaje jamani mtoto mdogo hivii😳nikawahi kumchukua kuanza kumbembeleza😭😭 🙏
Makala nyingine zinazocheza na ladha yako
Mapendekezo haya yanatokana na kile unachosoma sasa + Endelea kugundua zaidi
Maoni