DADA WA KAZI EPISODE 8
Haya Tunaendelea pale pale tulipoishia ambapo Neema alikodowa macho baada ya kuona mlango wa house girl uko wazi. Na japo kwa mara ya kwanza taa ilikuwa inawaka lakini sasa imezima . Alisena leo ni siku ya fumanizi aliondoka mbio mbio kuelekea chumbani huko na kuwasha taaa akijuwa lazima mumewe awe ndani humo.
Lakini cha ajabu baada ya kuingia na kuwasha taa alimuona tu Aziza kalala hana jipya zaidi ya krooooooooo!!! Kama chura magamba ... Alijisemea moyoni mume wake atakuwa yuko wapi? Akaendelea kupepesa macho kufungua mapazia lakini hakumuona mtu . Aliinama na kutazama chini ya uvungu hakuona mtu..
Sasa huyu mwanaume kaenda wapi? Lakini kama kawaida alitazama ukuta wake dada w kazi kapigilia msumari kisha katundika kufuri lake la pinki?
" Hiii tabia ya kulala bila kufuri lazima niikemee siwezi kukubali huu ujinga yule mwanaume namjuwa vizuri sana huyu binti atakuja kuwa chakulaaaaaaaaaaa"
Hapo hapo akasikia maji bafuni akajua lazima mumewe ndo yupo bafuni anaoga alitoka mbio lakini baada ya kutoka muda huo huo dada wa kazi kumbe hakulala aliamka na kusema " huyu mwanaume mzembe sana atakuja kukamatwa sababu ya hiki kitu alikuwa akikitazama na kukigusa .... Kisha akacheka na kuendelea kuuchapa usingizi......
Baraka alirudi chumbani na kumkuta mkewe amemkazia macho akajichekesha chekesha sana.ili kuzugalakini mkewe kanyoosha kwenye point
" We mwanaume ulikuwa wapi?
" Nilikuwa kuoga "
" Tangu lini unaoga usiku?
" Kuanzia leo huoni joto kali?
" Mmmh sio unamvizia mfanyakazi?
" Mmmh wife tangu lini nikafanya hivyo?
"Weee! Umesahau Lissa? Umesahau Irene ?umemsahau vicky,,?wote hao niliwafukuza kwa tabia zako .......
" Mke wangu sahizi nimetulia "
Akamsogelea na kumlaza kwenye kifua chake mkewe naye alikubali na kumkumbatia vizuri mwanaume akawa anamkiss kwenye paji la uso lakini kichwani mwake alijisema" wewe ndio sababu ya yote haya . Kisha wakapitiwa na usingizi...
.......KWA UPANDE WA AZIZA ............
Aziza hakupata usingizi usiku huo. Akili yake haikupumzika. Kila alipojigeuza kitandani, picha ya Baraka ikimwangalia kwa jicho la upole na kutamani ilimjaa kichwani kama sinema za mapenzi Titanic ,Romeo &Juliet . Aliweza kusikia bado sauti ya Baraka alivyosema, "Neti ya mbu imepinda hapa," wakati jicho lake likiwa haliko kwenye neti, bali kwenye mapa.....yake.
Aziza alikuwa msichana wa kawaida kijijini, lakini baada ya kuishi mjini kwa siku kadhaa tu, alikuwa tayari amejifunza mbinu za kutumia akili kuliko nguvu. Na sasa, alikuwa na mpango mpya siku inayofuata ....
Siku Ya Mpango: Jumamosi
Kulipokucha Neema alishtuka baada ya simu yake kuita kuja kutazama ni bibi yake alitoka kifuani kwa mumewe kipenzi na kupokea simu
" Shikamooo bibi"
" Marhaba hujambo?
" Sijambo bibi kwema ?
" Hapana sio.kwema "
Alishtuka na kukaa vizuri" kuna nini?
" Shangazi yako anaumwa nipo hospitali"
" Mmmmh anaumwa nini? Na homa imeanza saa ngapi?
" Njoo utajua vyote huku huku"
" Haya nakuja " Aliinuka haraka na kwenda kuoga maana shangazi yake ndio ka mlea baada ya mama yake kufa siku anazaliwa yeye na sasa anamuona shangazi kama mama yake ....
Alielekea bafuni na kuoga kisha kuvaa haraka haraka na sasa kavurugwa chezea mama wewe.......
Aliwaaga lakini alimwita House girl na kumwambia kuwa " sitaki kukuona umelala bila kufuri wavamizi ni wengi kisha akaondoka " Haihitaji D2 kuelewa inahitaji tu akili za kawaida kuelewa kuwa Baraka ni simba mla nyama kila windo lililopo mbele yake kwake ni chakula muhmu
Aziza alicheka na kusema " mwenyewe nataka hivo hivo nataka mwindaji kama Mume wako maana mawindo yake yananikosha sana ...
Aliondoka asubuhi na kuacha nyumba kwa Aziza na Baraka. Baraka aliamka na kwenda zake dukani, kama kawaida.Aziza alisema leo najuwa Dada atachelewa kurudi leo lazima Baraka aonje tunda lililomshinda adam. Akacheka na kuruka ruka ....
Muda huo baraka anaenda kazini lakini akili zipo kwa Aziza kwa kile alichokiona jana usiku kimeanza kumvuruga alijisemea kimoyomoyo" saa tano lazima nirudi nyumbani angalau hata nimuone tu"
Huko alipiga mishe zake zote ikiwa ni pamoja na kuhudumia wateja mbalimbali wengine walikuwa wakitaka pembejeo wengine wakitaka vitu mbalimbali aliwahudumia na ilipofika saa tano
alirudi nyumbani kupumzika kidogo. Na hapo ndipo mtego ulipokuwa tayari kuchezwa na binti Aziza .......
Aziza alimpokea Baraka akiwa amevalia gauni la kijivu lililomkaa kama ngozi ya ndizi mbivu. Lilikuwa limefungwa kwa mkanda wa dhahabu kiunoni na kufanya sura yake ya kiuno na makalio kuonekana kwa ustadi mkubwa. Lakini kilichovutia zaidi ni mdomo wake: rangi nyekundu ya lipstick, iliyopakwa kwa ustadi, na kutabasamu kwa heshima, lakini ndani yake kukiwa na jambo zito......
Baraka alisalimia tu kwa mkato, akapita na kwenda sebuleni. Aziza alikuwa kashapika haraka tambi za mayai na juisi ya parachichi, kisha akamletea. Baraka alipokuwa anakula, Aziza alikaa pembeni na kuanza mazungumzo ya kuvuta akili:
"Shemeji, unajua... kuna mambo huwa ninawaza sana... lakini sikuwahi kuyasema."
Baraka alimtazama kwa jicho la mashaka, ila alinyamaza.
"Unajua nimekuwa nikijisomea vitabu vya saikolojia. Kuna kitu wanaita emotional exposure... unapomwambia mtu unavyohisi, bila hofu, unaweza kumfanya naye ajisikie yuko huru kukuambia yake."
Baraka alikuna kichwa. "Hivi kweli unasoma vitabu hivyo na umeanza lini ? Ikiwa elimu yako ni ya kidato cha tatu tu?"
"Ndio. Najifundisha mwenyewe. Kwa mfano, mimi najua kuna mwanaume nikimweleza ukweli, atanishangaa. Lakini wewe si mtu wa kawaida. Wewe ni mwanaume wa busara... na nikikukosea, utasamehe."
Baraka aliinamisha kichwa. Moyoni alianza kuhisi ukaribu wa kisaikolojia. Hakujua kama tayari Aziza alikuwa ameshaanza kutumia mbinu ya kuvuta roho kabla ya kuvuta mwili.
Baada ya chakula, Aziza alimletea kijikaratasi. "Hii ni barua niliyoandika kwa mtu ambaye siwezi kumwambia machoni. Niliamua kuiandika, kama mazoezi ya hisia. Lakini kwa sababu wewe ni mtu pekee ninayemwamini hapa nyumbani, naomba usome. Lakini ukimaliza, unifute kabisa kwenye akili yako kama haijakugusa."
Baraka alichukua barua. Aziza aliondoka sebuleni. Barua ilisomeka hivi:
"Mpendwa wangu usiyejua unapendwa, Kila ninapokuona najisikia amani na furaha ya moyo sijuwi umenipa nini? Sijuwi umenifanyia nini? Toka siku ile umekula asali yangu napata mawazo sana najuwa sina elimu ila nina moyo uliyojaa upendo naomba kama utanikataa usimwambie dada fanya kama sijakwambia naomba usinikasirikie mimi ni binadamu nina moyo na nina penda sikuwaza kuwa na wewe lakini asali ushaitia kidole naomba uendelee kuilamba am sorry kama nimekukosea ,moyo wangu unalia kwa utulivu. Sitaki chochote kwako... zaidi ya kukufanya ufurahie maisha yako.
Lakini najua, hata ukiniona mimi, huwezi kuona zaidi ya mfanyakazi wa ndani. Sikupendi kwa sababu una pesa au nyumba. Nakupenda kwa sababu ulisimama na kunipa kitu ambacho sijawahi kupewa .
Kama kuna siku utanihitaji, hata kwa saa moja, nitakuja. Na nikija, sitakutaka uniahidi kitu. Nitakuja kama vile jua linavyokuja bila kuitwa.
ukimaliza kusoma ichane pleaseeee.....
****************"*************************
Baraka alimaliza kusoma barua hiyo na moyo wake ulipasuliwa kwa silaha ya maandishi. Hakuwahi kutamkiwa maneno ya namna hii. .
Alipoinua macho, alimkuta Aziza kasimama mbele yake, kimya, macho yakiwa yanamtazama.
"Samahani kama nimekuudhi... Nimeamua niseme sasa, kabla moyo wangu haujaumia zaidi. Nenda, ukitaka kusahau yote haya. Mimi nitaendelea kuheshimu ndoa yako."
Aligeuka kuondoka, lakini Baraka alimshika mkono.
Follow the HADITHI ZA KELVIN MLOWE ❤️✋🔥 channel on WhatsApp: https://whatsapp.com/channel/0029Vaw5SzK7YSd3RKAO8G46
NB
SIJIBU MESEJI MESSENGER
WHATSAP TU
0699286085
Makala nyingine zinazocheza na ladha yako
Mapendekezo haya yanatokana na kile unachosoma sasa + Endelea kugundua zaidi




Maoni