VYOTE NDANI GONGA94
NISAMEHE MAMA π SEHEMU YA: 03
Usimulizi huu ni wa watu wazima. Chukua muda wako, tulia, kisha usome kwa utulivu kama machapisho yetu yanayoendelea moja kwa moja.
SONGA NAYO.......
Niliagana na baba angu Kisha nikarudi wodini kwa mama, yaani nilikuwa na furaha Sana siku hiyo hata mama alishangaa maana hakuwai kuniona nikiwa na furaha kiasi iko
"Mmmmh hili tabasamu lako Ni la kheri kabisa mwanangu sijawai kukuona ukiww hivyo"
" Umeanza unatakaga kuniona nikiwa na uzuni muda wote Mungu amtupi mja wake leo nimekutana na baba angu na Yuko na pesa na anafamilia nzuri sana kunakoelekea nitaenda kuishi nao "
" Baba yako, na mbona hajaja kutuona Angekuja hata akuone kamili jamani "
"Mmmmh ebu acha maigizo baada ya kumuwangia kwa muda mrefu Leo unasema unatamani angekuja kukuona, kwanza hata kumwambia kwamba uko hapa sijamwambia, kuwa na aibu ingekuwa sio uchawi wako na kibwengo chako hiki yote yasingetokea"
Niliongea kwa hasira Sana nikatoa pesa kiasi na kuwatupia tusisumbuane mkiruhusiwa nendeni nyumbani nimeshachoka kuwaona uvumilivu wangu umenishinda na nahisi leo ndio itakuwa mara yangu ya mwisho kuonana nanyi "
Niliondoka nikiwa na hasira kama zote , nikaenda kupiga unywaji na marafiki zangu, nilitaka kusahau kila kitu kuhusu familia yangu kwani chuki yangu ilipita kikomo.
Julius alikuwa akinipigia mda wote lakini sikutaka kupokea mwisho nikazima simu, siku hiyo nikalala kwa shoga zangu, siku iliyofuata nilimpigia simu baba na kuomba tuonane alikubali na tukakutana mlimanicity.
" Simu yako imenistua Sana Kuna shida yoyote.....??"
" Yaaah ipo shida baba Jana nilipoachana na wewe pale nilienda kumwambia mama pale hospital kwani amelazwa anaumwa, nilipomwambia kuhusu wewe amenifokea Sana na usiku aliruhusiwa akaamua kunifukuza nyumbani hapa Sina pa kwenda Jana nimelala kwa majilani "
"Yaani anaufukuza nyumbani kwangu mimi...?, Ile nyumba nilijenga kabla hatujaoana kiwanja niliachiwa na baba yangu anakufukuza kweli"
" Sijui kosa langu Nini mama ananichukia sana, siwezi kwenda kule amekuwa akinitesa tangu ulipoondoka mpaka Leo, alinisimamisha shule baba Mimi sijasoma nimeishia darasa la tatu kwaajili yake, kila siku ananituma mtaani kuuza mboga"
Nililia Sana ingawa nilikuwa naongea uongo baba hasira zilimpanda na kuahidi kuwa atamkomesha na hiyo ndio ilikuwa furaha yangu.
Baba akanichukua na kwenda nae nyumbani kwake kiukweli nyumba ya baba ilikuwa nzuri Sana Tena Sana kila kitu kilikuwemo, magari ya kifahari nilijikuta nikifurahi na kujiona wa kishua si ndio mimi.
Julius baada ya kunipigia sana bila mafanikio aliamua kwenda hospital na alikuta mama akiruhusiwa hivyo akawachukua na kuwapeleka nyumbani, alishangaa Sana baada ya kuona mazingira ya nyumbani yaan chumba changu Mimi tu ndo kilikuwa na godoro lakini kwa mama kulikuwa na mkeka na mito miwili ambao mmoja ulikuwa wa mama mwingine wa mdogo wangu kamili, alitamani kujua mengi saa na kwa kuwa mama alikuwa hajui yule Ni Nani ilikuwa rahisi yeye kupata ukweli
"Nashukuru sana mwanagu kwa kila kitu Nina imani wazazi wako wamebarikiwa Sana kuwa na mtoto kama wewe "
Alizungumza mama akimshukuru Julius
" Usijali mama kwa kuwa Mimi Niko katika shirika la msaada nitakusaidia Sana usijali, lakini naitaji kujua maisha yako kwa ufupi maana kampuni yetu inaitaji kuwafahamu watu Kisha wawasaidie"
"Aaaah yaani mwanangu sijui nianzie wapi kukuelezea, Mimi niliolewa nikiwa na miaka 15 niliozeshwa na mjomba angu baada ya wazazi wangu kifariki, nashukuru mume wangu alikuwa mtu mzuri, tulipata mtoto wa kwanza wa kiume, lakini wifi zangu walimchukua kwahiyo mpaka Sasa sijui yuko wapi aliondoka akiwa na mwaka mmoja, na wifi zangu Sina mawasiliano nao, nikapata wa pili anaitwa saada, ni binti sasa, na huyu kamili ndo wa mwisho, baada ya kamili kuzaliwa mume wangu akamkataa na kuondoka akituacha tukiteseka lakini pia Sasa hivi saada pia ameniacha na kuungana na baba ake wakidai Mimi mchawi "
Julius alistuka Sana kusikia Mimi ni mtoto wa yule mama lakini hakutaka kujionesha, waliongea mengi na mama mwisho akawachia kiasi Cha pesa na kuondoka.
Usiku wa siku hiyo niliamua kuwasha simu Ili kutaka kumpigia Julius na kumuomba kiasi Cha pesa lakini nilikutana na sms moja matata sana ilinistua Sana iliandikwa hivi
" Nawaza kuwa Kati yako na mama ako Nani mchawi maana mmmh sijui hata nilikupendea Nini wewe Kama mama yako unamtreat hivyo Mimi na mam yangu itakuwaje...? Nimewaza Sana saada sijui uko wapi but it's over between us sikuhitaji katika maisha yangu yaani sijui nikutafsiri vipi ili uelewe chuki uliyojenga kwangu anyway maisha mema"
Niliogopa lakini ukizingatia Sasa nipo kwa baba yangu halafu familia nzima imenikubali sikuona haja ya kumuomba msamaha au kujielezea nikamtumia ujumbe mfupi
" Sikuwai kukupenda afadhali umenipunguzia idadi kwenye gari nipate kuongeza wengine "
Kusema kweli nilikuwa msichana rahisi Sana Tena Sana nilikuwa nikiangalia pesa tu nilikuwa sipendi mwanaume Mimi ila pesa hivyo sikuona shida kutumia mwili wangu katika kunipatia pesa.
Hasira za baba zilivuka kikomo baada ya kumwambia maneno Yale ya uongo kuhusu mama, usiku huo aliongozana na vijana wake wawili na kwenda kuchoma nyumba ya mama, na wote walikuwa ndani, moto ulikuwa mkali Sana mama alifanikiwa kutoka lakini hakuweza kumtoa kamili hivyo kamili alifia kwenye Moto ule.
Ilikuwa Ni uzuni kwa mama angu akuweza kabisa kuyashika maumivu, yake makali, kwakuwa nyumba iliungua Sana kabisa mama hakuwa na pa kukaa na ukizingatia majilani walikuwa wakimchukia Sana aliamua kuondoka kabisa mbagala na kwenda kutafuta maisha sehemu zingine.
Julius alifanya kazi kubwa Sana ya kumtafuta mama lakini pia haikuwezekana hivyo akakata tamaa..
Hatimaye miaka mitano ilipita nikiwa na miaka 23 najua ku drive Nina maisha mazuri nikiwa naishi kwa baba yangu sikuwaza kabisa kuhusu mama, lakini nilikuwa na ukaribu mzuri sana na mama yangu wa kambo kwani tabia zetu ziliendana kabisa ingawa tulifanya ujinga kwa Siri sana.
Nikiwa barabarani na mama yangu wa kambo kuelekea saloon nilipata kumuona mama akiwa anazurula barabarani alionekana kabisa Kama Ni chizi, na kwa kuwa nilikuwa Barabara ya vumbi nilimmwagia vumbi la kutosha, Kisha nikafungua kioo ili anione, mama alilia Sana lakini kwangu ndio ilikuwa furaha ya kutosha yaani nilikuwa nikifurahi tu muda wote.
Mama alikuwa akiishi majalalani na kula chakula vya jalalani, ukizingatia na Kansa aliyokuwa nayo, alidhoofu Sana ila Mungu allimpenda Sana mama maana na hali ile Bado alikuwa akitembea vizur tu.
Siku moja nilikutana na rafiki yangu ambaye alikuwa akiijua familia yangu vizuri kabisa tukaingia bar flani na kuanza kupiga story
"Hivi kumbe ulipona kwenye ule Moto ??"
"Mmmmh kwanza hata sikuwa nyumbani "
"Daaaah pole Sana masikini kamili amefariki akiwa na umri mdogo Sana "
" Umeanza Sasa hivi Ni kula maisha hizo habari sizitaki "
Alishangaa Sana maana rafiki yangu huyu hakuwai kujua kabisa kama naichukia familia yangu, niliinuka na kuondoka kwa hasira nikimuacha akinishagaa, kwa hasira nilizokuwa nazo nilianza kumtafuta mama kila Kona na nilifanikiwa kujua wapi anakaa
Baada ya siku mbili nklilipa vijana pesa na kuwaomba wakampige Sana lakini wasimuuwe naitaji ateseke tu.
ITAENDELEA......
MTAKATIFU GEMMA UTUOMBEE SHIRIKA LA MASISTA WA MT GEMMA WA DODOMA
Tunao Wapenda ndio wanao tuua baba
Sikiliza Wimbo Kamili
Umesoma kwa utulivu Β· dakika chache tu Asante Endelea kusoma chagua hapo chini
Umependezwa ?? Asante Soma Zaidi nisamehe-mama-sehemu-ya
