VYOTE NDANI GONGA94
NISAMEHE MAMA π SEHEMU YA: 04
Usimulizi huu ni wa watu wazima. Chukua muda wako, tulia, kisha usome kwa utulivu kama machapisho yetu yanayoendelea moja kwa moja.
SONGA NAYO.......
Nililipa vijana ambak walimvamia mama usiku na kumpiga sana Kisha wakamuacha akiwa na hali mbaya Sana hakuweza hata kutumbua macho, wakati yote yakiendelea nilikuwa nimekaa pembeni nikiangalia, walivyomaliza waliondoka wakaniacha nilimsogelea na kuanza kuongea nae
" Ungekufa pamoja na kamili haya yote yasingekukuta mwanamke uko na roho ya paka wewe ujui hata maisha yako yakoje na Bado unaishi wachawi Ni wachawi tu unawezaje kulala sehemu kama hi na unaamka "
Ingawa mama akuweza kufumbua macho lakini aliweza kunijua alizungumza kwa tabu Sana
" Saada naomba unipeleke hospital Nina hali mbaya Sana usiniache hapa "
Nilibaki nikimuangalia kwa dharau mwisho wa yote nilimpiga na mguu Kisha nikandoka nikimuacha akiugulia maumivu makali ya kipigo.
Asubuhi wasamalia wema waliweza kumsaidia na kumpeleka hospital alipokelewa vizuri kabisa na walimpeleka hospital ambayo alitibiwa mwanzo, madaktari wa pale walijaribu kunipigia lakini hawakunipata kwani nilibadilisha line, kwa kuwa kulikuwa na namba ya Julius walimpigia na muda mfupi aliweza kufika hospital, Julius alikuta mama akiwa ICU ana hali mbaya Sana alinitafuta Sana lakini jitiada zikagonga mwamba
Baada ya wiiki mbili mama alikuwa sawa na aliruhusiwa Julius alimchukua Moja kwa Moja mpaka nyumbani kwao na kwa kuwa familia ya kina Julius ilikuwa Ni ya dini Sana walimpokea kwa heshima zote na kumfanya mmoja Kati ya wanafamilia, mama alianza kuwa na furaha lakini hakuwai kinisahau hata siku moja, alipewa kila aina ya upendo akaanzishiwa clinic kwaajili ya kansa ingawa ilikuwa imefikia stage ya mwisho lakini walikuwa na imani kuwa mama atapona na kuwa sawa kabisa, walikuwa wakimpeleka sehemu nzuri nzuri ili asiwe na mawazo kabisa kwani Julius aliwaambia kila kitu isipokuwa mahusiano yetu.
Siku moja nilienda shopping ya vyakula nilingia super market katika kutembea uku na uku nilikutana na mama uso kwa uso alitabasamu baada ya kuniona nilistuka sana kumuona alivyopendeza lakini pia alinawili sana nikaanza kucheka na kumsogelea Zaidi
" Wacha weeeeh Hatimaye mchawi Leo amekuja kuwanga supermarket kwa kujivesha vizuri kabisa ili asijulikane "
Kabla mama ajanijibu kitu muda huo huo alikuja Julius alishtuka kuniona lakini hakuwa na muda nami Zaidi alimgeukia mama na kumuuliza
" Mummy uko sawa....??"
Mama akatabasamu na kusema ndio mwanagu
Kama binadamu niliumia Sana nilipata kawivu flani hivi, muda huo huo akaja mama Julius
" Kuna Nini hapa...??"
" SI huyu.................."
Kabla ajaendelea mama alimkatisha, mama hakuwa akijua kama mimi na Julius tunajuana hivyo akataka mada ikatwe hapo
" Tunaweza kuondoka "
Alisema mama lakini mama Julius akauliza
" Nini kinaendelea mnajuana...??"
" Hapana , tumegongana tu ndo mara ya kwanza tunaonana "
Alijibu mama kiukweli hiyo iliniuma Zaidi mama kunikana mbele za watu na ajawai kufanya hivyo aiseee nilichukia nikajikuta nikiondoka kwa hasira sana.
Siku hiyo nilikuwa na mawazo sana niliumia kumuona mama anaishi katika maisha mazuri.
Siku ziliendelea kwenda ingawa mama alikuwa akipata kila tiba lakini Kansa na mawazo vilimuandama Sana hivyo Bado ilieababisha afya yake kuwa sio nzuri sana.
Akaanza kuumwa Sana ikawa wiki hospital wiki nyumbani.
Kuna siku aliumwa Sana akamuita Julius na kutaka kuongea nae
" Julius mwanangu Mimi siponi najiona kabisa lakini naomba umtafute saada nimuone mara ya mwisho najua amenikosea lakini Niko tayali kumsamehe Mimi kama mama napokea madhaifu ya mtoto wangu namba sana, najua umjui lakini unamkumbuka binti tuliyekutana nae supermarket yule ndo yeye "
Julius hakuwa na muda wa kupoteza haraka akatafuta marafiki zangu ili ajue naishi wapi lakini jitihada zake zilifanya kazi, tukakutana kinyerezi park nikisherehekea siku yangu ya kuzaliwa na marafiki zangu nilikuwa Nina furaha sana nikiwa nataka kukata cake Julius alifika na kuita jina langu, muda huo pembeni nilikuwa na boyfriend wangu mpya ambaye ndio ameniandalia hiyo sherehe nilifoka na kuwaomba walinzi wamtoe kwani anataka kuanzisha vurugu, walipokuwa wakimtoa alipiga kelele kwa kusema
"Saada mama yakoo anaumwa Sana anakuitaji mda huu Yuko hospital hile ile ya siku zote"
Mchumba wangu mpya alinigeukia na kuniuliza
" Mama yako gani na mama yako anaogelea kule "
"Baby huyu kichaa ananitaka ameanza kunifata mda Sana na sijui Nani kamuelekeza hapa"
Basi tukaendelea na sherehe........
ITAENDELEA........π₯°
SHUKRANI β Emidee ft. Mbacho Wizzy (Official Lyrics Video) ? Produced by: Gift Record ? Released: 20
Wimbo wenye ubunifu imechanga kiarabu kiswahili na amapiano wimbo wa kushukuru kwa maisha na upendo Sasa sikiliza na ku download hapa gonga94.com
Sikiliza Wimbo Kamili
Umesoma kwa utulivu Β· dakika chache tu Asante Endelea kusoma chagua hapo chini
Umependezwa ?? Asante Soma Zaidi nisamehe-mama-sehemu-ya
