MMMM DADDY NIKIKUPA UTANIOWA KWELI?!* *SEASON TWO* *21--222 *__________* *SEHEMU YA 21* Tulipoishia msimu wa kwanza... mama Kingston aliniletea dawa za tumbo chumbani kwangu...
Na wakati huo kijana wake alishahisi huenda nikawa na ujauzito wasiwasi mzito ulimvaa Kingston akaamua kuja chumbani kwangu kuniuliza what's going on.
Kabla hatujasemezana chochote tulisikia mama Kingston anakuja hivyo ikabidi Kingston ajifiche kwenye pazia😰😰
Mama ni kama kuna kitu ameshaanza kukihisi mwilini mwangu🥹🥹nilitetemeka sana pale aliponigusa mapigo yangu ya moyo na kuniuliza kama kuna kitu ninamficha..
Hapo ndipo nilipotizama upande ule alipojificha Kingston ili niweze kumwonyesha ishara ya kuwa kwa hapa nilipofikia uyanisamehe lakini siwezi kudanganya tena🥹
Kabla sijafanya hivyo Kingston akaniwahi akaniambia please zarina niko chini ya miguu yako usiongee chochote na mama..
Nilibaki njia panda nifanya nini😰😰ilibidi kidanganye tena kwa ajili ya Kingston yani ukimpenda mtu bwana unakuwa kama mtumwa😂
Nilikuwa tayari kufanya chochote ilimradi nimuweke Kingston sehemu salama..
Mama aliniomba ninywe zile dawa mmmhh nilizishika mkononi zile dawa kichwani nikawa nawaza kama kweli nina mimba basi sitakiwi kuzinywa hizi dawa zinaeza kuniharibia ujauzito wangu..
Hata kama Kingston asipoukubali huu ujauzito mimi sitautoa nitahangaika nao mwenyewe mpaka nijifungue...
Wakati nayawaza hayo mama akawa anazidi tu kunishangaa😳😳😳wewe binti hebu kunywa dawa hizo..
Hapana mama kwa sasa tumbo haliumi we nenda ukalale niachie hizi dawa tumbo likianza kuuma nitazinywa🙏🙏
Mama alinielewa na akaniambia siku inayofuata kama hali yangu itakuwa mbaya basi nisiamke mapema kama ninavyoamka siku zote..
Aliniambia yeye atawahi kuamka afanye kazi zote baada ya hapo atanipeleka hospitalini kwenye vipimo..
Asante kwa kujali mama🥹🥹 mwenyezi Mungu akubariki🙏🙏it's okay zarina kuwa na usiku mwema..
Aliniaga na kuondoka zake bila kujua pale chumbani kuna Kingston🥱🥱..
Baada ya mama kuondoka Kingston alitoka pale alipojificha akanisogelea pale kitandani nilipokaa..
Aliniangalia sana huku mapigo yake ya moyo yakiwa yanamuenda mbio kuliko kawaida ..
Mwisho wa siku aliamua kunisemesha... aliniambia zarina nina imani siyo mimba😰😰..
Unamaanisha nini Kingston🥹🥹inamaana ikiwa ni mimba utaikataa???
Niliongea kwa sauti ya juu iliyojaa wasiwasi mwingi sana🙌🙌asikwambie mtu linapokuja swala kama hili utatamani ardhi ipasuke uingie😰😰
Hakuna mwanamke anayependa kutelekezewa mimba😓😓maisha ya usingo maza nimekua nikiyaona kwa mama yangu ni magumu hayaelezeki kuna muda mpaka mama yangu alikuwa analala bila kuoga wala kula kwa sababu ya mambo mengi kumtinga kichwani..
Itakuwaje Kwa upande wangu🥹🥹🥹...machozi ndo kitu pekee kilikuwa kinatiririka bila breki..
Wakati huo Kingston alikuwa ameniziba mdomo ili nisiendelee kushauti kwa sauti wazazi wakatusikia..
Nisikilize zarina..hakikisha mama na baba huwambii chochote kuhusu mimi na wala usiwambie chochote kilichotokea kati yetu..
Kesho ukiamka jifanye mzima kabisa ili mama asikupeleke hospital wakishaondoka mi nitakupeleka mwenyewe ukapime please mamaa..
Jamaa alishuka chini akapiga magoti alinisemesha kwa sauti ya chini ya kunibembeleza mimi nikawa nalia tu na moyo ukawa unazidi kuzama in love💔💔..
Kingston aliniomba kesho niamke muda kama niliozoea kuamka nifanye kazi zangu zote na mama akiniuliza nimwambie niko sawa haina haja ya kwenda hospital..
Nilikubaliana naye maskini ndo nishapenda nguvu ya kumpinga jamaa sikuwa nayo😔😔..
Baada ya kumkubalia alinikumbatia kisha akanibusu nyieeee niling'ang'ania kifuani kwake nikawa sitaki kumuachilia😣😣
Aliniomba nipumzike na nifanye kama tulivyokubaliana...
Nini kitafuata??...
*SEHEMU YA 22*
Nilimwambia sawa nitafanya hivyo... alinitakia usiku mwema kisha akaondoka zake..
Nilibakia peke yangu kule chumbani kusema kweli sikupata usingizi😓😓 nilikuwa nawaza tu nikikutwa na mimba itakuwaje??..
Niligala gala kitandani mpaka mida ya saa 11 alfajili nikaamka... nilinawa nikamaliza nikatoka kwenda kufanya usafi..
Wakati niko jikoni nakosha vyombo mama naye aliamka kumbuka aliniahidi kufanya kazi zote siku hiyo..
Hee zarina umeamka??.
Ndiyo mama😊😊we nenda tu ukaendelee kulala mimi nitafanya kazi zangu mwenyewe..
Huh lakini unaumwa wewe😳😳 hapana mama niko sawa tumbo haliumi tena yani najisikia vizuri kabisa..
Kwa hiyo hospital huendi tena???. Hahahaa mama sa hospital nifuate nini na wakati sijisikii vibaya...
Lbda ikitokea nimezidiwa ndo nitaenda hospital but for now I'm okay😊😊... hahahaa utakuwa muoga wa sindano wewe mi nishakugundua😂😂
Hahahaa tuliishia kucheka pale nikamuuliza mama yani kama vile ulikuwepo yani mimi na sindano ni maji na mafuta😂😂😂
Basi masikini mama wa watu aliniambia kwa vile nimeshaamka siwezi kurudi kulala hebu ngoja japo nikusaidiepo hivo vyombo we nenda ukasafishe huko hapa jikoni niachie mimi nishughulike napo..
Basi mamaa mi nilienda kufanya usafi ndani nikamuachia mama amalizie vile vyombo..
Kusema kweli siyo kwamba nilikuwa sawa hapana nilijikaza tu nisimkwaze Kingston...
Nyote mliozaa mnazijua tabia za mimba haswa mida kama hiyo zinakuwa kama zimepandwa na kuchaa😂
Nilianzia kudeki chini kupanda juu... wakati wote nahangaika na dekio kwenye flo ya chini kumbe Kingston alikuwa kajibanza sehemu ananichabo tu maskini🙈🙈
Nimedeki zangu chini nilipomaliza nikapanda juu wakati huo kushaanza kupambazuka...
Nilikuwa natembea nayumba kizungu zungu kama chote..
Vyote hivyo Kingston alikuwa anajionea tu...basi bwana nilipopanda juu nikashangaa nakutana na Kingston kwenye ngazi akanipokea ile ndoo ya kudekia nikashangaa😳
Nimatie mimi hii ndoo...nilimuachia ile ndoo lakini natetemeka kupita maelezo🙌..jamaa aliniangalia kwa macho ya huruma sana🥹🥹
Aliniuliza kwa sauti ya chini vipi unaendeleaje??. Polee unaonekana hauko sawa🙂 nilikaa tu kimya sikuweza kumjibu chochote😔😔
Kingston aliniambia nimuachie kazi iliyobakia ye ataimalizia wazazi wakiondoka nikamwambia sawa..
Alipitisha dekio zile sehemu zinazoonekana ili wazazi wakipita wajue tayari usafi ushafanyika kote..
Kwa ile hali ya kujali kidogo nikawa na matumaini juu ya Kingston 🙂🙂🙂..
Nilirudi chumbani kwangu nikapata na nguvu ya kutandika kitanda baada ya hapo nikaenda kuoga kidogo nikapata nguvu..
Ilipofika saa moja kuelekea saa mbili wazazi wa Kingston walitoka kuelekea kazini wakanisisitiza hali yangu ikibadilika nisisite kuwapigia simu..
Basi baada ya wazazi kusepa Kingston alikuja akanimiminia chai maskini akanipatia na vitafunwa akaniomba nile maana usiku wa jana sikula ndo maana kuzungu zungu kinanisumbua..
Lol mshikaji alionekana kujali vibaya mno🥹🥹alinisisitiza sana naomba ule zarina usijali kila kitu niachie mimi I'm a Man nitajua namna ya kufanya kikubwa tu uniamini..
Baada ya Kingston kuniambia hivyo aliondoka kwenda kumalizia usafi zile sehemu zilizobakia mimi nikabaki nakunywa chai..
Alifanya usafi akamaliza akaja kuniangalia... aliniuliza nilichoongea na mama nikamwelezea kila kitu akanishukuru kwa kuendelea kumfichia siri zake na akaniahidi kila kitu kitakaa sawa😰😰..
Aliniomba nikapumzike kidogo baada ya hapo tutaenda hospital kufanya vipimo😓😓yani kila niliposikia neno vipimo kimoyo kilikuwa kinafanya paaah😂😂😂
Mshikaji alinishikilia mkono mpaka chumbani kwangu akaniomba nijilaze pale nipumzike🤗🤗🤗..
Usingizi nilikuwa nao wa kufa mtu kumbuka usiku wa jana wote sikulala💔kwa ile hali ya kujali aliyonionyesha Kingston kidogo nikajikuta napata na amani ya kulala..
Nililala usingizi fofofo😴😴 nilikuja shituka saa nane mchana nimeloa jasho mwili mzima😺
Ilibidi nikoge tena baada ya hapo nikatoka kuelekea jikoni kwa ajili ya kupika..
Wakati nataka kuanza kupika Kingston alinifuata akaniambia nijiandae tutoke tutakula huko tunakoenda..
Nilimwambia sawaa... nilijiandaa chapu nikavaa nguo nzuri aloninunulia siku ile🙈🙈nayeye akajiandaa alipomaliza akaja kunigongea tuondoke..
Nilitoka kingston aliponiona nilivyotupia kwa mara ya kwanza akanisifiaaa🤗🤗🤗aliniambia wow you look good😽😽..
Nikamwambia thank youu🙈 ukisifiwa na wewe sifia😂😂nami nilimsifia The Boy maana lol Mungu alijua kumuumba kwa kweli🥰
Tulitoka mpaka parking familia ina kila aina ya magari jamani😴🙌 wakitaka kutoka wanajichagulia tu leo tutoke na ipi🤗🤗
Kingston alichagua gari moja wapo pale akaniambia nipande tukaondoka kuelekea hospital...
Nini kitafuata baada ya vipimo?.?fuatilia sehemu inayofuata...
Makala nyingine zinazocheza na ladha yako
Mapendekezo haya yanatokana na kile unachosoma sasa + Endelea kugundua zaidi
Maoni