MUME WANGU ALIVYONIOLEA MKE WA PILI SEHEMU YA : 15 🔥 Kwanza nilishtuka sana na haraka nikatoa mikono yangu ambayo ilikuwa imemkumbatia max vizuri
Max akanishika mkono wangu na tukaanza kuondoka lakini gafla hamad akadaka mkono wangu wa pili na kuzuungumza.
“Broh achia mkono wa mke wangu “
Max akaniangalia kwa muda kisha akaniachia mkono wangu na kubaki akimuangalia Hamad kana kwamba ananiambia haya fanya unachokitaka.
“Shamsa unafanya nini uku Saa hizi Tena mke wa mtu na mume wako Sijui kabisa “
Alizungumza hamd uku akitunisha kufua Kana kwamba alikuwa akimtambia max Kuwa huyu ni mke wangu Broh.
“Ina maana awakumbukani au ??”
Nilijiuliza kimoyomoyo tu, Yaani hamad na max walikutana Nyumbani kwetu kama umesahau ilikuwa ni siku ile ambayo Mimi nilienda shuleni kwa watoto wangu na kuwapelekea zawadi Mbili Tatu halafu hamad akagundua na kuja kufanya Fujo Nyumbani kwetu.
“Hamad tukutane ofisini”
Alizungumza max kisha akanishika mkono Mimi na kuanza kuniongozesha njia.
“Ofisini ? Kwani wanajuana au ? Aaah ni nini kinaendelea jamani au wananichezea michezo wawili hawa”
Nilijikuta nikipata wasiwasi wa hali ya juu sana, Yaani nilishindwa kuelewa ni kitu gani kilikuwa niliendelea jamani, Yaani Mimi najionea mapicha Picha lakini nilipofikia ni Kama Natakiwa Kuwa makini sana, akili yangu iliniambia Kuwa max na hamad ni wa najuaana na ni watu ambao mni team moja na wanaangalia njia ya kunichota Tu na kuharibu kila kitu kwenye maisha yangu.
Basi moja kWa moja nikiwa nikiwanimeshikwa mkono na max, safari ikaishia kwenye ofisi moja kubwa sana, ofisi ambayo ilikuwa na kila kitu muhimu, ofisi Fulani hivi kubwa na ya kisasa.
“Kaa pale “
Alizungumza max uku akinyooshea mkono sehemu Ambayo anataka Mimi nikae .
“Max kuna nini ??”
Nilijikuta nikiuliza kWa wasiwasi sana maana ni Kama max alikuwa serious sana na alionekana kuwa na hasira kiasi.
“Shamsa Kaa pale kwnza Nina mazungumzo ya muhimu sana kWa sasa”
Eeeh nini hiki jamani 🥹 ifikie hatua sasa na Mimi maisha yangu yapate utulivu jamni Yaani Nimekuwa ni mtu wa matukio Mapya kila iitwapo Leo khaaah.
“Hamad kuna chochote kile kinaendelea hapa ofisini na unataka kunijulisha ??”
Max alimuuliza hamad Kana kwamba yeye ndio boss wa ofisini nzima.
“Kitu gani ??”
Hamad alimuuliza max lakini macho yake yote yalikuwa yakiniangalia Mimi tu.
“Kwamba ujui kitu gani ? Hamad kuna upotevu wa Pesa nyingi sana za ofisi, Jambo ambalo niliamini Kuwa wewe ndio ulitakiwa Kuwa wa kwanza kabisa kunijulisha sasa sijajua shida ni nini “
KWa sauti ya dharau hamad akajibu.
“Na Kwanini nikushirikishe ikiwa hautaki kufika ofisini na upo bize kuangaika na wanawake za watu kwenye kila kona ya dunia”
“Hamad usiniletee masuala ya mapenzi kwenye ofisi yangu, usiniletee mahusiano kwenye Mali ambayo nimetumia nguvu nyingi sana kuifikisha hapa ilipo”
Hapo hamad akajikuta akicheka sana na na kuzungumza.
“Unavyozungumza Sijui ofisi yangu Sijui nini nini, utafikili hii ofisi ni yako peke yako “
Max alionekana kuchanganyikiwa sana alibaki Akizunguka uku na uku na kukuna kichwa chake tu.
“Hamad unasiikia ninachozungunza lakini au ? Nazani unaanza kusahau au labda baba yako alichelewa kukupa taarifa zangu, ngoja nikuambie kitu hamad, Mimi ndio mwanzilishi wa hii kampuni, Mimi ndio CEO wa kampuni nzima, lakini pia mimi ndiye mtu Mwenye shareholder kubwa, hapa ofisini namiliki asilimia 87 ya kila kitu hapa Kwahiyo unaweza kuona utofauti, sikiliza nakupa hii barua mfikishie baba yako kisha Mwambie baba yako Nina maongezi nae lakini Kuanzia sasa sitaki Tena kukuona kwenye ofisi hii mpaka nitakapokuita “
Eeeek kwanza nilikuwa nasahau Kuwaambia kitu jamani, Yaani Leo ndio Nimejua sehemu ambayo hamad anafanya kazi 😂🙌 Yaani miaka yote tuliyoishi sikuwai kujua sehemu halisi anayofanyia kazi hamad, hamad amekuwa mtu wa kunificha mambo yake.
Hamad wa watu mwaya sijui ndio kuchanganyikiwa Sijui ni kitu gani maana kwa haraka sana akanishika mkono na kuniambia.
“Wewe na Mimi Tutamalizana Nyumbani “
Kisha akaanza kunivuta uku na uku akitaka tuondoke wote.
“Hamad Ebu Niache “
Nilizungumza kWa hasira sana kisha nikatoa mkono wangu na kurudi kukaa chini.
“Nitakufundisha adabu mbwa wewe “
Alizungumza hamad kWa hasira sana kisha akaondoka zake.
Baada ya hamad kuondoka, na Mimi nikamgeukia max na kumuuliza.
“Ilikuwa Unamaanisha nini kunileta uku na unajua hamad yupo uku au haujui Kuwa yeye ni mume wangu ??”
KWa mwendo wa taratibu max akaanisogelea na kuzungumza.
“Nafikili ilo Jina la mume wangu ungelitoa kinywani mwako Shamsa, hamad astahili kuitwa mume ata siku moja, halafu Nafikili labda unikumbuki tu Ila Mimi nakukumbuka, miaka kadhaa nyuma nilikuja Nyumbani kwako, nakumbuka wewe ndio kwanza ulikuwa umetoka kujifungua Mtoto wako wa kwanza lakini hamad akakutambulisha wewe Kama mfanyakazi wake wa kazi za Ndani na niliamini hivyo”
“Max sitaki kujua mambo ya nyuma Sawa nataka kujua sababu ya wewe kunileta uku na unajua kabisa hamad yupo, Lengo lako ni nini ?!”
“Sina Lengo baya na wewe ata kidogo, Kama unakumbuka nilikuambia Kuwa hakuna mtu mwingine anayejua Kama Mimi Nina ofisi nyingine Tena kubwa Kama hii “
“Max unanichanganya tu, Lengo lako ni nini Yaani 🥹”
Max baada ya kuona Kuwa Mimi Nimepaniki sana gafla tu Akalopoka.
“KWa sababu nakupenda Shamsa, kwa sababu wewe ni mwanamke wa maisha yangu “
Nyieeeeh kwanza nilishtuka sana na kujikuta nikinyanyuka kitini bila kupenda.
“Yaaaah najua utasema Kuwa wewe ni mke wa mtu lakini hamad hakustahili wewe ata kidogo, hamad hana hadhi ya kumiliki mwanamke Kama wewe, I love you Shamsa”
“Kimya, kimya max Kaa kimya “
Nilijikuta nikimfokea tu maana ni Kama alikuwa akinipigia Kelele, kitendo cha max kuniambia ukweli wa moyo wake kilinikimbusha mbali sana, kilinikumbusha enzi hizo za nyuma wakati hamad ananitongoza, siwezi kukataa Kuwa nampenda sana max na nanatamani sana awe mwenza wa maisha yangu lakini naogopa sana, ndoa yangu na hamad imenitengenezea Picha ya kutisha sana kwenye maisha yangu.
“Nipeleke Nyumbani “
Nilimwambia max.
Mkaka wa watu alielewa Kuwa siko sawa hivyo Wala hakufanya ajizi alichofanya ni kunishika mkono na kuniongoza njia maana sikuwa ata na nguvu kWa wakati huo.
Baada Kama ya masaa mawili hivi tayali nilikuwa Nyumbani wetu, Yaani tayali nilifika kWa wazazi wangu na mama na baba yangu wakanipokea wakiamini Kuwa Naumwa kutokana na maelezo ya uongo waliyopatiwa na hamad.
********
Siku ziliendelea kwenda na hatimaye siku ya mwisho ya maamuzi juu ya taraka yangu Mimi na hamad lakini pia juu ya malezi ya watoto, siku hiyo nilikuwa ni mtu Mwenye huzuni sana na Mwenye wasiwasi wa hali ya juu, kwa upande wangu Bwana nilikuwa na mama yangu, baba, max, Neha pamoja na mume wa Neha na wadogo zangu wengine.
KWa upande wa hamad alikuja na familia yake ambayo ilijionesha Kuwa na Pesa sana maana walikuja na ma gari ya kisasa sana.
Mwenye Pesa sio mwenzio bwnaaa 🥹💔 Yaani baada ya kutoa ushahidi wangu ulionyoka na kila kitu still hamad akainuka mshindi kwenye upande wa malezi ya watoto lakini pia kwenye taraka hamad alikataa kabisa kunipatia taraka akidai Kuwa ananipenda sana na anataka Mimi na yeye tulee watoto wetu kWa pamoja.
JE NI KITU GANİ KITAFUATA TUKUTANE SEHEMU INAYO.
Makala nyingine zinazocheza na ladha yako
Mapendekezo haya yanatokana na kile unachosoma sasa + Endelea kugundua zaidi



Maoni