BETWEEN SISTERS AND SECRET _____________________________________*6--7 *SEHEMU YA SITA* "Looh, msichana ana balaa yule! Kwahiyo anaona bora mapenzi kuliko undugu, na Mr. Gael wa watu alivyo mtaratibu na mu-handsome
"Acha ujinga! Sitaki kabisa mambo hayo, hasa kuwa karibu na mpenzi wa Mira. Kila siku ananilaumu mimi kuwa namletea mikosi kwenye mahusiano yake, au umesahau?" Mia alimuuliza. "Hata sijasahau shoga angu, hata hivyo Mr. Gael sio mtu wa kumzoea haraka haraka. Yupo busy na mambo yake, kumuona tu kwa mwaka unaweza ukamuona mara moja," Furaha na Mia walitembea huku wanaongea.
Siku zilienda, Mia alizidi kuwa mzoefu zaidi kazini. Siku moja Gael alienda dukani.
"Mama, unajua kabisa nina kazi nyingi sana ofisini, lakini bado umeamua unitumie mimi kwa shangazi kweli..." Gael alilalamika kwa mama G. "Sasa nisipokutuma wewe nimtume nani? Hata kama umekuwa na hizi ndevu na CEO wa kampuni kubwa, lakini kwangu bado wewe ni mtoto," alisema mama G huku anamtengeneza shati.
"Mimi sio kama nakataa mama, ila Gian si yupo likizo wala haendi kokote? Ungemtuma yeye nyumbani kwa shangazi, Gael aliendelea kulalamika.
"Mimi ndo ninawajua vizuri watoto wangu. Gavin anafanya mambo yake taratibu, Gian ni mvivu, anaweza kulalamika leo mpaka kesho na asiende. Lakini wewe ni mwepesi, ndomana napenda kukuagiza wewe," alisema mama G. "Okay, basi nipe huo mzigo niende," aliongea Gael huku anaangalia saa yake ya mkononi.
"Mia, lete huo mzigo," alisema mama G.
"Sawa madam, naleta," Mia alienda kuchukua
mfuko. Mama G alichukua akamkabidhi Gael.. "Huu hapa mzigo, lakini hautaenda peke yako. Utaenda na Mia," aliongea mama G huku anatabasamu. Mia na Gael waliangaliana.
"Mama, kama anaenda yeye pia kulikuwa kuna haja gani ya mimi kwenda? Lilikuwa ni suala tu la kumuita dereva wako akampeleka," Gael alisema.
"Ni kweli madam, acha tu niende mimi mwenyewe. Unaweza kunielekeza, muache kaka Gael arudi kazini," aliongea Mia kwa sauti yake ya upole.
"Mia, wewe ni mgeni. Nataka uende ili upajue. Siku nyingine naweza kukutuma ukaenda mwenyewe. Na kuhusu Baraka, leo yupo mapumziko, siwezi kumvunjia ratiba zake," mama G aliongea huku anamuangalia Gael. "Sawa basi, nitampeleka," Gael alisema.
Gael alichukua ule mzigo, Mia alimfuata nyuma.
Walipanda kwenye gari na safari ilianza. Kila mmoja alikuwa kimya. "Natumai leo itakuwa ni mara ya mwisho kukutana nae. Sitaki kabisa kugombana na Mira kwa vitu vya kijinga, Mia alijiongelea mwenyewe.
"Kwa kiasi fulani amefanana sana na Mira, lakini yeye... ni mrembo zaidi, na ni mpole, na anaonekana ana adabu, Gael alijikuta anamuangalia Mia kwenye kioo kila mara. "Unaweza ujinga gani... unawezaje kumfananisha mpenzi wako na msichana wa kawaida sana kama huyu," Gael alijisemea na akaacha kumuangalia, akaendelea kuendesha gari.
Walifika nyumbani kwa Bi Maua, shangazi wa
Gael. "Karibuni wageni!" Bi Maua alifurahi sana
kumuona Gael. "Asante shangazi, lakini sisi hata hatukai sana. Tumeleta tu huu mzigo," alisema Gael.
"Kaeni hata kidogo, namalizia malizia kupika jamani. Njoo mwaya binti yangu unisaidie kutenga," aliongea Bi Maua huku anatabasamu. Mia alimuangalia Gael kana kwamba alitaka ruhusa. "Nenda tu," alisema Gael.
Mia alitabasamu, akamfuata Bi Maua jikoni. "Bila shaka wewe ndo Mia?" aliuliza Bi Maua. "Ndiyo shangazi," alijibu Mia huku anatabasamu. "Kweli nimeamini, Hellen alikusifia kwa haki. Wewe ni mrembo na una heshima sana. Ningekuwa na kijana wa kiume ningekuozesha. Hellen sijui anasubiri nini, watoto wake wote hawajaoa," aliongea Bi Maua kwa utani.
Mia alitabasamu tu. Walitenga chakula, na baada ya hapo wakala kwa pamoja.
"Shangazi, chakula kilikuwa kitamu sana. Acha sisi tuondoke sasa," alisema Gael.
"Shangazi, asante kwa chakula," Mia alianza kutoa vyombo.
"Hata usipate tabu binti yangu, nitavitoa tu. Nyie nendeni," alisema Bi Maua.
"Shangazi, acha nivitoe tu."
"Sawa kama ndo ulivyoamua." Mia alitoa vyombo.
"Unamuonaje huyu binti, Gael?" Bi Maua alimuuliza kwa sauti ya chini.
Chapter 7
"Unamuonaje huyu binti, Gael?" Bi Maua alimuuliza Gael kwa sauti ya chini.
"Mbona sikuelewi shangazi, unamaanisha nini?"
Gael alimuangalia Bi Maua kwa makini.
"Mmmh sio kama hujanielewa ila umechagua tu kusema hujaelewa. Huyu binti anafaa kabisa kuwa mke, Gael." Aliongea Bi Maua kwa msisitizo.
"Shangazi, nina mpenzi na tunapendana sana, na wote mnalijua hilo. Siku sio nyingi tutafunga ndoa."
"Mchumba yupi? Yule mwanamke aliyekosa adabu? Hakuna atakayekuruhusu kumuoa mwanamke kama yule! Sijui mbele ya wazazi wake anavaa vile... yani amekosa haya kabisa!"
"Shangazi, sitaki kukuvunjia heshima, haya ni maisha yangu, na mimi ndiye nitakaye muoa Mira, na sio familia yangu!" Gael alisimama kwa hasira, akatoka nje, aliwasha gari, akaondoka.
"Mia, binti yangu!" Aliita Bi Maua.
"Abee, shangazi," alitikia Mia akiwa jikoni.
Bi Maua alimfuata. "Umeamua kuosha vyombo kabisa?"
"Ndiyo shangazi, isingekuwa tabia nzuri kuacha vyombo vichafu."
Mia alimalizia kupanga vyombo kabatini.
"Asante mwaya binti yangu, ngoja nimpigie John aje akurudishe kazini, maana huyu kisirani ameondoka hata bila kuaga, Bi Maua alimuita dereva, akampeleka Mia kwenye nyumba waliyofikia kwani muda ulikuwa umeenda sana.
"Ukaamua kuhamia kwa watu?" Dora alimuuliza Mia.
"Alitenga chakula, na sikuweza kumwachia kazi,
nilimsaidia kuosha vyombo, ndomana nimechelewa." Mia alijilaza kwenye kochi.
"Sawa, ila kesho mama G amesema hakutakuwa na kazi," alisema Dora.
"Kwanini hakuna kazi, na ni katikati ya wiki?" Aliuliza Mia.
"Sio kama tutakaa tu nyumbani, siku kama ya kesho tarehe 20 mwezi wa 11 huwa tunaenda vituo mbali mbali vya yatima. Tunashinda nao, tunakula nao, kuna michezo, yani kwa ujumla ni vitu vingi sana," alisema Furaha.
"Jamani, hadi raha! Mama G kweli ana moyo wa kipekee sana, sio kama matajiri wengine," alisema Mia.
"Ndiyo, yani ana roho nzuri, sijawahi kuona," alisema Judith.
Kwa upande wa Bi Hellen, alipigiwa simu na Bi Maua.
"Eeeh, niambie wifi yangu kipenzi, ilikuwaje?" aliuliza Bi Hellen kwa shauku ya kutaka kujua. "Mmmh aseme nini zaidi ya kusema hataki kuingiliwa kwenye mambo yake, na aliondoka kwa hasira sana. Sijui kama mtaweza kumzuia kumuoa yule mwanamke."
"Wifi, tunatakiwa kushirikiana kwa pamoja kulizuia hili, usituachie huu mzigo peke yetu. Unajua kabisa yule mwanamke hafai, si kwa mavazi tu, hata tabia!" Aliongea Bi Hellen kwa kulalamika.
"Nitaendelea kujaribu kuongea naye, lakini yeye ni mtu mzima. Kama ameona Mira anamfaa, muacheni mwenyewe. Yakija kumshinda huko mbele, atajua afanye nini," alisema Bi Maua. "Sawa, ngoja tuone mwisho wake," Bi Hellen alikata simu.
Kesho yake asubuhi kwenye kampuni ya Purenex, Gael alimuita Mira ofisini kwake. "Babe, nimeitikia wito," Mira alienda
kumkumbatia Gael.
"Sweetheart, leo nataka tutoke pamoja, kuna sehemu nzuri nataka twende pamoja."
"Kweli babe?" Mira alifurahi sana. "Ndiyo, tena tunatakiwa kuondoka sasa hivi."
Gael na Mira waliongozana mpaka nje ya kituo cha watoto yatima kilichoitwa Tumaini Jipya. "Babe, hapa ni wapi?" Mira aliuliza huku anapaangalia.
"Sweetheart, hapa ni kituo cha watoto yatima.
Kila mwaka huwa tunakuja kupata nao chakula, kucheza nao..." Mira alimkatisha Gael.
"Kwahiyo hii ndo sehemu nzuri uliyoniambia?" Mira alimuuliza Gael.
Full 1000
Whatsp 0784468229
Makala nyingine zinazocheza na ladha yako
Mapendekezo haya yanatokana na kile unachosoma sasa + Endelea kugundua zaidi

Maoni