BINAMU WEE UNGEKUWAZA? 1 na 2
๐ต๏ธ๐ต๏ธ๐ต๏ธ๐ต๏ธ๐ต๏ธ๐ต๏ธ๐ต๏ธ๐ต๏ธ๐ต๏ธ๐ต๏ธ๐ต๏ธ๐ต๏ธ๐ต๏ธ๐ต๏ธ
๐๐๐๐๐๐๐๐๐๐๐๐๐๐
SEHEMU 01
MWANZO........
Kitendo cha kutoka tu ndani kwangu nilistaajabu baada ya kumuona mchumba angu ambaye tayari alikuwa ashanichumbia amemshika binafu yangu kiuno huku akimuangalia kwa wasiwasi kidogo.
Binamu alikuwa wa mwanza kuniona hakuonyesha kustuka wala nini badala yake aliachia tabasamu alagu alimgeukia mchumba angu. Nilisikia akizungumza.
Naomba uniwaishe hospitali tumbo linaniuma sana, nilimwambia Nice lakini hakujali, napoelekea naweza kuzimia. Binamu alimwambia mchumba angu Sony huku akizidi kujilegeza na kujifanya mwenye maumivu.
"Huyu mtoto mbona ameanza kunifanyia drama, ananitafutia nini mimi?, nilijiuliza mwenyewe huku nikiwa nawaangalia na mpaka muda huo Sony hakuwa amenioan.
Sony alifika hapo nyumbani kwangu kwa lengo la kunitoa out ila safari iliingia doa. Nilimuona Sony anambeba binamu Manka kabda ya kumuingiza kwenye gari nilizungumza ndipo Sony alijua kuwa nipo eneo hilo.
"Kuna nini kinaendelea?".
" Nice huyu ni ndugu yako tena mdogo wako huyu kwanini hujali kuhusu yeye. Hivi unaweza kweli ukamtelekeza mwenzio ndani kwemye hali hii kisa tu unataka kutoka out na mimi?" Sony aliongea kwa paniki.
"Sina taarifa za yeye kuumwa. Eti Manka unaumwa nini?" Nilimuuliza Manka ila hakujibu alizidisha kuugulia. Sony alimpakia Manka mwenye gari alishika usukani hao wakaondoka.
Sikuwa na nguvu za kuludi tena ndani. Nilikaa hapo kibarazani nawaza na kuwazua kwanini Manka amebadilika namna hii....
Baada ya kukaa muda mrefu pale nje ya nyumba yangu niliingia ndani, nilibadili ngua nikavaa penzi na tisheti. Niliingia jikoni kwaajili ya kuandaa chakula kwaajili ya walioenda hospitali ila kabda sijaanza kupika simu yangu ilianza kuita.
"Mama anajisikia vibaya, amenikataza nisikwambie ila naogopa asije akazidiwa zaidi, kama hutojali naomba uje" Sauti ya mdogo wangu Joleen ilisikika simuni.
Sikuwa na chakujiandaa tena nilitoka chap kama nilivyo safari kwenda nyumbani kwetu.
Mama yangu alikuwa anasumbuliwa sana na presha haitaji mawazo kabisa. Alinishangaa baads ya kuniona hapo, alijua moja kwa moja Joleen amenipa taarifa.
"Naomba nikupeleke hospitali"
"Nipo sawa haikuwa na haja ya wewe kusumbuka namna hii. Joleen ni mtoto mpu bavu sana. Nikimwambia tu najisikia vibaya ataanza kusumbuwa watu, hapa navyokwambia kampigia mpaka baba yenu huko nje ya nchi".
" Anakupenda sana na ndo maana anajali kuhusu wewe. Jiandae basi nikupeleke hospitali "
"Nipo sawa kwa sasa wala usijali nadhani nilimiss uwepo wako karibu yangu ndo maana nilikuwa hovyo"
"Jamani mamaa!"
"Ondoa shaka mwanangu. Vipi mkwe hajambo?" Mama aliniuliza nilikaa kimya kwa sekunde kadhaaa........ITAENDELEA.........
SIMULIZI : BINAMU WEWE UNGEWEZA?
SEHEMU 02
ENDELEA......
"Hajambo kabisa"
"Na mipango mengine si inaenda vizuri?"
"Kabisa mama, tegemeeni mambo mazuri hivi karibuni"
"Hata mimi naona Japo unanificha mama yako kwa jambo kubwa kama hili labda unasubili mpaka tumbo lionekane ndo uniambie kama ni mjamzito" Mama aliongea hayo mie huyo nisiangue kicheko.
"Mama bhana umeanza mambo yako. Tangu lini nikakuficha mambo yangu na wewe ndo msiri wangu"
"Sasa mbona hili umenificha ndo maana nasema labda unasubiri tumbo likuwe"
"Ndo kwamba unamaanisha mimi huyu ni mjamzito?, mama bhana"
"Una kichaa wewe?, hujui kama una mimba au unanizuga mbwa wewe. Mtu mzima dawa popote anapokuwa mimi nimekuzaa wewe na ndo wa kwanza kuona jua unanificha mimba jinga kabisa wewe"
Nilifikiria kwa dakika chache huku nikipiga mahesabu kwenye kichwa changu.
"Inaweza kuwa kweli mbona sijaingia kwenye siku zangu karibia miezi miwili" niliongea hayo kwa sauti.
"Yaani Nice na utuuzima huo hujui hata dalili za mimba?"
"Mama nina tabia ya kupitiliza siku zangu ni ngumu kujua mapema kama nina mimba". Nilijitetee ila ni uongo mtupu.
Hata sikuamini kama ni kweli ni mjamzito. Majira ya jioni niliondoka nyumbani nilitaka nihakikishe kama kweli nina mimba. Moja kwa moja nilienda hospitali.
Nafika tu hospitali kwa mbali niliwaona Manka na Sony wanaelekea parking huku Sony akiwa amemshika Manka kwa uangalifu sana. Wivu wa mapenzi ulinikaba haswaaa! Niliendelea kuwatazama mpaka walipoondoka eneo hilo na wao wala hawakuniona.
Nilienda kuonana na doctor alinifanyia vipimo ni kweli nilikuwa mjamzito tena wa miezi miwili.
Nilifurahi sana maana ni matamanio yetu mimi na Sony kupata mtoto hasa Sony alikuwa na hamu sana ya kuitwa baba.
Niliondoka hospitali kwa mbwembwe zote. Nilijua muda huo Sony atakuwa nyumbani kwangu tu. Maana hawezi kuondoka akamuacha mgonjwa peke yake.
Nilifika nyumbani ile naingia ndani nikamkuta Manka amekaa kwemye sofa alafu miguu kainyoosha mezani. Mkononi kwake ana kipande cha rimao.
"Unaendeleaje?" Nilimuuliza kiroho safi.
"Salama" Alinijibu kwa mkato tu.
Sikutaka kumjali sana tena nina furaha zangu mwenyewe nilamuuliza kuhusu Sony.
"Ni muhimu kuliko mimi binamu yako?, Ok yupo jikoni ananiandalia supu" Sikutaka mambo yawe mengi nilielekea jikoni moja kwa moja.
Ni kweli nilimkuta Sony anaandaa supu. Nilimkumbatia nyuma ya mgongo kwa mahaba kama yote ila niliishiwa pawa kwa maneno aliyonitamkia. Wacha nilie kwanza ๐ญ๐ญ๐ญ๐ญ๐ญ๐ญ๐ญ.......
Je nini kitaendelea Pata mwendelezo
Makala nyingine zinazocheza na ladha yako
Mapendekezo haya yanatokana na kile unachosoma sasa + Endelea kugundua zaidi
Maoni