Simulizi za Maisha,Mafunzo,Mapenzi ,Chombezo Habari za Michezo na Burudani vyote kwa Kiswahili ndani ya – Gonga94 Semajambo
Gonga94 · Stories
11 Oct 2025
747 views
VYOTE NDANI GONGA94
BINTI MREMBO YATIMA NA KIJANA TAJIRI *SEHEMU YA 38* Kuna muuza magari mmoja hivi ni maarufu sana Dar..nilichukua namba yake Instagram tukamcheki..
Usimulizi huu ni wa watu wazima. Chukua muda wako, tulia, kisha usome kwa utulivu kama machapisho yetu yanayoendelea moja kwa moja.
Gari tulilolihitaji hakuwa nalo ila alisema kama tukikubaliana ataliagiza ndani ya siku 40 litafika nchini🤗🤗
Romy alikubali alimpa advance ya pesa alizohitaji then makubaliano ilikuwa gari likishafika tutamalizia pesa..
Inatakiwa uanze kujifunza how to drive right?.. nikamwambia yes babe 😍 hahahaaaa🥰🥰🥰nilitafuta mwalimu wa kunifundisha kudrive private..
Sikuweza kwenda Veta kwa sababu ya muda...muda mwingi nakuwa chuoni nisingepata muda wa kuwa nahudhuria vipindi vya Driving course..
Nilianza pia kufuatilia passport hii ndo ishu Romy aliipa kipaumbele kuliko ishu zingine😂😂😂Namshukuru Mungu ndani Three weeks nilifanikiwa kupata passport🥰
Huko chuoni nilikuwa naenda kwa mbinde sana😂😂🙌 yani kwa week nilikuwa nahudhuria chuo mara moja au mara mbili au week nzima siendi kabisa..
But nilikuwa najitahidi kufuatilia kwa wenzangu walichokisoma napitia ili kwenye mitihani nisitie aibu😂😂😂🙌..
Baada ya kupata passport Romy aliniuliza nchi gani nayotamani kwenda kutembea🙈🙈kusema kweli nilikuwa natamani sana kwenda Dubai😂
Ujue kwanini😂😂 nilikuwa natamani namimi nifike kule jangwani ambapo watu wakienda wanafunga tule tuvitambaa kichwani wanaendesha yale mapiki piki makubwa😂😂🙈
Nilikuwa naona hadi wasanii wakienda Dubai wanaenda huko basi namimi nikatamani sana siku Mungu akinijaalia nifike huko🙂🙂
Romy alikuwa anapitiliza kwenda nchini kwao niliona sio vizuri kuondoka bila kumuona mdogo wangu🙂 nilimkutanisha poppy na Romy...
Kabla ya kuwakutanisha nilimwelezea poppy kila kitu kilichotokea kati yangu na Hemed😰😰poppy alisikitika sana lakini akaniambia tumekua kwa shida sana dada..
Hatuwezi kuendelea kuishi maisha ya shida... kama Hemed amethubutu kukupiga kabla hajakuweka ndani basi hiyo ni dalili ya kuwa kwake hakutokuwa na amani yoyote..
Muda bado upo wa wewe kumchagua mwanaume sahihi ambaye ataelewa hali halisi ya kule tulikotoka akupende kama ulivo na si kukupiga💔💔 ..
Kama Romy ndo mtu anayekupa amani basi huyo ndo shemeji yangu mimi❤️🫂poppy aliniambia hivo na kisha alinitakia kila la kheri kwenye safari yangu ya mahusiano na Romy...
Tulimwachia nyumba kwa sababu nilipomchukua shule na kumleta pale aliponipangishia Romy..
Poppy alipapenda sana aliniomba nimuache kwanza afurahie maisha kwenye ule mjengo then Weekend ikiisha atarudi shuleni🥰🥰🥰❤️
Tuliagana naye poppy sisi tukaondoka kuelekea Dubai.. kumbuka hapo nyuma Romy aliniambia kuna surprise ataenda kunifanyia kabla ya kurudi kwao...
Hiyo surprise ndo inaenda kufanyikia hukooo Dubai..
Ni surprise gani????
HAYA WAZEE WAKUKOSOA SIMULIZI ZA WATU NA MNAJIFANYA WAJUAJI KWENYE COMMENT HUYO MDOGO WAKE MMEMUONA HAMJAMUONA?
KUNA MUDA MSUBIRI STORY IISHE KWANZA NDIO MUANZE HUKUMU
Itaendeleaaaaaa...
Maoni
You're not logged in
X
Login
X
signup
Makala nyingine zinazocheza na ladha yako
Mapendekezo haya yanatokana na kile unachosoma sasa
+ Endelea kugundua zaidi
AMINATA,BINTI AGEUKA NA KUWA MTU HATARI BAADA YA KUTEKWA, AMEOKOA MAELFU YA WAAFRIKA | Movie Recap
Huyu binti hapa anaitwa Aminata na ana umri wa miaka 11 tu. Aminata alikumbwa na changamoto ya biashara ya utumwa. Na b...
Tangazo - MY Wangu season one, season two, season 3, season 4 and season 5 final
MY Wangu season one, season two, season 3, season 4 and season 5 final
X
SHARE TO SOCIAL MEDIA
BINTI MREMBO YATIMA NA KIJANA TAJIRI *SEHEMU YA 38* Kuna muuza magari mmoja hivi ni maarufu sana Dar..nilichukua namba yake Instagram tukamcheki..
Gari tulilolihitaji hakuwa nalo ila alisema kama tukikubaliana ataliagiza ndani ya siku 40 litafika nchini🤗🤗
Romy alikubali alimpa advance ya pesa alizohitaji then makubaliano ilikuwa gari likishafika tutamalizia pesa..
Inatakiwa uanze kujifunza how to drive right?.. nikamwambia yes babe 😍 hahahaaaa🥰🥰🥰nilitafuta mwalimu wa kunifundisha kudrive private..
Sikuweza kwenda Veta kwa sababu ya muda...muda mwingi nakuwa chuoni nisingepata muda wa kuwa nahudhuria vipindi vya Driving course..
Nilianza pia kufuatilia passport hii ndo ishu Romy aliipa kipaumbele kuliko ishu zingine😂😂😂Namshukuru Mungu ndani Three weeks nilifanikiwa kupata passport🥰
Huko chuoni nilikuwa naenda kwa mbinde sana😂😂🙌 yani kwa week nilikuwa nahudhuria chuo mara moja au mara mbili au week...
👉 Soma zaidi hapa: https://www.gonga94.com/semajambo/binti-mrembo-yatima-na-kijana-tajiri-sehemu-ya-38-kuna-muuza-magari-mmoja-hivi-ni-maarufu-sana-dar-n
Maoni