KIFAHAMU KITABU CHA DANIEL. Historia haijaandikwa kwa usawa. Mara nyingi inaandikwa na walioshinda vita
Kwa mfano, tunajua mengi kuhusu Babeli, Ashuru, kupitia vyanzo vya Biblia na baadaye kupitia tafsiri za Wagiriki na Waroma.
Lakini tunajua kidogo sana kuhusu simulizi za ndani za Nubia, Ethiopia, au hata Harappa–Indus kwa sababu maandiko yao yalipuuzwa na wana historia wa Kizungu.
Hebu fikiria, Danieli 2 na 7 zinatoa maono ya falme nne zinazopishana (Babeli, Umedi-Uajemi, Uyunani, na Rumi).
Na kwa hizi falme kuu nne, humwambii kitu msabato, labda kama unataka akuite mpinga kristo.
Humwambii kitu kuhusu Nebuchadnezzar na Babeli kama ufalme wa kwanza mkuu, humwambii kitu kuhusu ufalme wa Waamedi Na waajemi chini ya Dario na Koresh.
Humwambii kitu kuhusu Ugiriki na Alexander Mkuu, humwambii kitu kuhusu Roma na ukatili wake.
Babeli imepata umaarufu baada ya anguko la waashuru. Imeibuka ikawakuta Misri, Nubia, na hata india wakiwa na tawala imara sana.
Babeli sanjali na kupigiwa debe, haijawahi kushinda tawala hizi.
Swali linabakia: ni lini Babeli ilishinda tawala hizi na kuwa falme kuu ya dunia?
Ikumbukwe kuwa: baada ya muda mfupi tu, babeli aliangushwa chini, na kuziacha Misri, Nubia, Ethiopia, india, china na Amerika ya kale zikiwa zimesimama.
Sasa inapewaje hadhi ya kuwa super power wa kwanza wa dunia?
Hali hii inaunda simulizi kwamba historia nzima ya dunia “imepangwa kwa makusudi” kuelekea Rumi (ambapo baadaye Ukristo utazaliwa).
Hii ni framework ya Kiyahudi-Kikristo (Jewish–christian framework) ya historia, inayopuuza kabisa ustaarabu mataifa mengine (Misri, India, China, Amerika za kale).
Danieli si historia ya ulimwengu mzima, bali ni propaganda ya kifalsafa/kiimani ya eneo fulani, na sio ulimwengu mzima.
Biblia yenyewe iliandikwa katika mazingira ya Asia ya Kati na Afrika Kaskazini (sehemu za ngozi nyeusi).
Lakini ilipochukuliwa na Wagiriki, Waroma, na baadaye Ulaya ya Kikristo, simulizi hizi ziliwekwa kwenye muktadha wa “mashariki ni chanzo, magharibi ni kilele.”– wazungu ni hatari mno.
Mfano, Danieli anawaona Babeli, Uajemi, Uyunani, na Rumi kama nguzo za historia — hakuna neno kuhusu Misri (ambayo ilitawala muda mrefu zaidi).
Baadaye wanatheolojia wa Kikristo wanachukua hii kama blueprint ya historia ya binadamu, na wanaipa Ulaya (Rumi) nafasi ya juu kabisa katika simulizi.
Hii kiufupi ni white supremacy, kwa kuwa inamtukuza sana mzungu na kumbeza mtu mweusi.
Hainiingii akilini kuwa tawala nne za daniel 2 na 7 ndizo tawala kuu nne za ulimwengu, wakati kuna tawala kama vile:
✅Ashuru ( Chaldeans, Iraq ya Leo)– wababe waliotikisa kwa muda mrefu sana, hadi walipoanguka wakati ninawi iliposhambuliwa na Mchanganyiko wa Babeli na waamedi. Hawa hawatajwi kabisa kama super power, hadithi zao zina zimwa zimwa tu ndani ya biblia.
✅Misri– Taifa na ufalme wa ajabu uliotawala kwa muda mrefu sana hadi ulipovamiwa kwa mara ya kwanza na Waamedi na waajemi.
Simulizi yake inaminywa minywa tu, ili tusibaini ukuu wake.
✅India (Magadha, Maurya baadaye) —ilikuwa na falme kubwa, lakini haikuweza kufikiwa na mashambulizi yoyote yale ya hawa wanaopigiwa debe kama Wafalme wakuu wa dunia.
✅Nubia/Kush ilikuwa falme thabiti kusini mwa Misri, ambao haukuwahi kushindwa vita kutokana na uthabiti wake wa kijeshi.
Lakini Biblia inajifanya kana kwamba “ulimwengu wote” umepita ndani ya mzunguko wa Babeli → Uajemi → Uyunani → Rumi.
Huu ni uzushi na ubaguzi wa hali ya juu kabisa.
Historia ya Biblia (hasa kitabu cha Danieli) ni biased na regional, si historia kamili ya kiulimwengu.
Chaguo ni lako kuendelea kusoma tungo, ama kuamka na kuanza kuhoji.
Mimi kazi yangu ya kukuamsha nimeimaliza.
Ndo huyo mimi ninaelekea Nubia ( Sudani) kujifunza ukuu wa mtu mweusi.
Wenda mimi ni mtu wa kale sana niliyezaliwa upya, kurekebisha baadhi ya vipengele vya safari yangu
Makala nyingine zinazocheza na ladha yako
Mapendekezo haya yanatokana na kile unachosoma sasa + Endelea kugundua zaidi
Maoni