NILIUZWA KUWA MTUMWA WA BILIONEA 14,15 Mike alimuweka Ciara kitandani kwake kisha akaanza kumbusu kwa lazima.....hakuishia hapo alianza kupambana kumvua nguo ili wafanye mapenzi,
Ciara hakuonesha kushtuka wala kuogopa, alimuacha Mike afanye atakavyo. Ni wazi kabisa anaelewa nini maana ya kuwa Mtumwa.
Mike kuweza basi, alichukua shuka akamfunika. Ukishampenda mtu inakuwa changamoto sana kumfanyia ubaya na hivi ndivyo ilikuwa kwa bilionea.
"Kesho asubuhi nenda ukamsalimie Shangazi yako, nina uhakika una mengi ya kuzungumza naye"
"Kwanini unataka ni kamuone Shangazi yangu"
"Bila kujalisha alikuuza hapa lakini bado kabeba nafasi ya wazazi wako...." Mike aliongea kisha akageukia upande mwingine japo alikuwa na njaa lakini maneno ya Ciara yalivunja moyo wake
"Nisamehe kwa kuumiza moyo wako, naomba uishi katika huo ukweli kuwa hauna nafasi katika moyo wangu" Ciara alijisemea ndani ya moyo wake kisha akageukia upande mwingine pia
Kulivyo pambazuka alijikuta pekee yake, tayari Mike alikuwa ameamka.
Alisimama dirishani akachungulia, aliachia tabasamu baada ya kumuona Mike akisaidiana na Watumwa wengine kufanya usafi.
Japo huwa ana utajiri wa dharau lakini kuna muda huwa anakuwa na huruma kwa Watumwa wake.
Ciara alishika kalamu na karatasi kisha akaanza kumchora Mike na Watumwa wake.
Ilikuwa ni picha nzuri sana, baada ya kumaliza aliingia bafuni kuoga.
Mara nyingi huwa anapenda kuvaa kawaida tu ila siku ya leo kwa kuwa anaenda kwa Shangazi yake alijitahidi kupendeza....
Baada ya kumaliza kila kitu alitoka nje akiwa kashika picha aliyomchora Mike akiwa na Watumwa wengine.
Ile anataka kwenda kumuaga alizuiliwa na Katy
"Nasikia umeruhusiwa kwenda kumsalimia Shangazi yako, huna haja ya kupoteza muda nipatie hicho ulichobeba mkononi Jessa atampelekea"
Ciara hakuwa na shida alimkabidhi mchoro Katy kisha akamgeukia Jessa
"Naenda kumuona Shangazi, kama una chochote cha kuniambia zungumza"
"Usimuambie chochote kuhusu Mimi, nikipata nafasi kwa wakati wangu nitaenda kuzungumza naye"
"Ni muda sasa umepita itapendeza kama utaenda kumuona Mama yako" Katy alishauri
"Umesema unataka kwenda hospitali kufanya check-up, nitakusindikiza kuhusu Mama yangu nitatafuta nafasi kwa ajili yake"
Katy aliachia tabasamu baada ya kuona Jessa anamjali yeye kuliko Mama yake mzazi
Ciara aliondoka zake baada ya Jessa kukataa kwenda kumsalimia Mama yake..
Katy aliifungua picha aliyochora Ciara.
Ilikuwa ni picha nzuri sana na hata akajikuta akiachia tabasamu
Dada yako ni fundi mzuri sana katika kuchora, hii picha nitaiweka chumbani kwangu na si kumpatia Mike.
"Sikutarajia kama utaachia tabasamu sababu ya picha aliyochora Ciara"
"Huna haja ya kumuonea wivu Ciara kisha nimeachia tabasamu sababu ya mchoro wake...." Katy aliongea kisha akaendelea na safari
Jessa aliomba msamaha kisha akamgeukia Ciara aliyekuwa bado anazungumza na Mtumwa Jala.
Moyo wake ulichefukwa tu kiasi cha kutema mate
Upande mwingine Jasinta akiwa anakaanga zake chips aliishiwa pozi baada ya kumuona Ciara akiwa pekee yake.
"Jessa yuko wapi...."
"Atakuja kwa wakati mwingine..." Ciara aliongea akitaka kuchukua kipande cha chips aonje lakini hakufanikiwa baada ya Jasinta kuubana mkono na upawa
"Ingawa wewe ni Mtumwa kwenye jumba la Mike lakini nina uhakika kuwa una kula vyakula vizuri kuliko Watumwa wote"
Ciara aliachia tabasamu kwa maneno aliyoambiwa
"Nimeshaelewa kwanini umemuuza Jessa kwenye jengo la Mike"
"Kitu kipi hicho umeelewa"
"Unatamani aolewe na Mike"
"Siku zote huwa una uwezo wa kuelewa mambo kwa haraka, kama usingekuja kuzungumza na Mimi leo basi siku ya kesho ningekufuata. Hebu fanya kutoroka kwenye jengo la Mike.... nitafurahi kama utamuachia nafasi Jessa. Naamini uwepo wako hapo unaweka kikwazo"
"Yaani unataka Jessa awe na Mwanaume ambaye amekwisha lala na Mimi"
"Kulala na wewe haina shida hata, yule Mwanaume anaoga kila siku hivyo kama ni mabaki yako yataondolewa na maji"
Ciara alikaa kimya, alijikuta akikosa maneno ya kusema
"Siwezi kukufundisha namna ya kutoroka nina uhakika unazo mbinu kichwani" Jasinta aliomgea huku akimuwekea chips
Ciara hakuwa na noma alikula zote
"Hicho ni kiapo cha kunithibitishia kuwa utatoroka, sijakupa chips zangu bure. Pindi utakapo toroka hakikisha hauleti miguu yako hapa. Nadhani unaelewa nini kitatokea endapo utakuja kuishi hapa,"
Ciara alijikuta akitabasamu tu, hakutegemea kabisa kama Shangazi yake hampendi kiasi hiki
Itaendelea 💥
NILIUZWA KUWA MTUMWA WA BILIONEA 15
Ciara aliendelea kula chips taratibu, baada ya kumaliza alimpatia Shangazi yake kibunda cha pesa
"Hizi pesa ni kwa ajili yangu?" Jasinta aliuliza akiwa haamini
"Unataka nimpe nani na huku wewe ndio mzazi wangu uliyebakia? au hujaridhika nazo nizichukue" Ciara alitishia
"Acha ujinga...., kaa uendelee kula chips" Jasinta aliongeza zingine kwenye sahani
"Sitaki ni kuharibie ratiba yako ya usiku, uliponiuza Mimi pesa iliyopatikana ilitumika kumtibu Jessa. Ulipomuuza Jessa pesa iliyopatikana imeenda wapi?...."
"Kwanini unaniuliza...."
"Rekebisha hii nyumba, kwa sasa haupendezei kukaa kwenye nyumba iliyochoka kama hii."
"Ndiyo nilipatiwa pesa lakini sijui hata zilienda wapi, yaani ni kama zilikuwa na pepo hivi"
Ciara aliachia tabasamu, ana mfahamu Shangazi yake ni mtu wa bajeti sana.
"Tutaonana kwa wakati mwingine, pindi nitakapo toroka sijui nitaenda wapi lakini popote nitakapokuwa sitaacha kukumbuka. Kama ungechagua kunipatia sumu kipindi nikiwa na miaka minne sidhani kama ningeliona jua la leo hivyo Mimi hapa nipo tayari kufanya chochote kwa ajili ya Jessa"
Jasinta aliona aibu kwa namna Ciara anavyo mjali
"Nisamehe ipo siku hata wewe utakuwa Mama, nina uhakika utakuwa una mchagua Mtoto wako kwanza kwa kila kitu..."
"Ni wazi unajisikia hatia ndani ya moyo ndio maana unaomba msamaha. Huna haja ya kufanya hivi kwaheri" Ciara aliongea kisha akaondoka
Jasinta aliishia kuzitazama chips alizozibakiza Ciara. Moyo wake ulikuwa unauma kimtindo, alitaka kuangua kilio lakini alijizuia kwa kubugia chips zote.
Baada ya Ciara kurejea kwenye jengo la Mike, alijifungia chumbani kwake
"Naomba ufungue mlango..." Sauti ya Mtumwa Jala ilisikika
Kwa jinsi anavyo mchukulia Mwanamke huyu kama Mama yake alisimama akafungua mlango
"Kwanini unajifungia pekee yako, watu wote wako nje wakifurahia nyama na pombe zilizonunuliwa na Katy"
"Huenda tusionane tena, nipo nafikiria ni njia gani niitumie kutoka hapa..."
"Unafanya hivi kwa sababu Shangazi yako kasema"
"Ni kwa ajili ya Jessa, nafurahi kuona anaishi kama mtoto wa Mfalme mahali hapa, hivyo nitaondoka ili nisiwe sababu ya yeye kushindwa kuishi kama mtoto wa Malkia kabisa"
"Hii sehemu ina kustahili wewe hata kama utakimbia kwa sasa ni lazima utarudi hapa"
"Kama itatokea nimerudi basi sitakuwa na chaguo zaidi ya kukaa...."
Jala aliachia tabasamu kisha akampatia karanga
"Hizi ni nini...."
"Si umesema unataka kuondoka hapa!....kama utatumia hizi ni lazima wakukimbize hospitali hiyo ndio njia pekee ya wewe kutoroka" Jala aliongea
Basi Ciara akiwa katika uso wa kujiamini alitafuna karanga zote mpaka akamaliza.
Dakika tano zilikuwa ni nyingi alianza kutapika damu mfulilizo
Jala alipiga kelele za kuomba msaada, Acha Mike achanganyikiwe hasa baada ya kugundua Ciara ndio mahututi.
Alimuingiza kwenye gari kisha akaliondoa kama anakimbizwa na Majambazi
Ciara anapatiwa huduma za haraka,
"Sielewi ni kitu gani kina msumbua lakini kwa sasa anaendelea vizuri...." Daktari aliongea
Mike aliwahi chapu kumuona Ciara, moyo wake ulishtuka baada ya kukuta kitanda kikiwa tupu.
Kwa namna dirisha lilivyokuwa aligundua Ciara ametoroka.
Itaendelea 💥
Full 1000
Whatsapp 0657171961
KWETU Morogoro
Makala nyingine zinazocheza na ladha yako
Mapendekezo haya yanatokana na kile unachosoma sasa + Endelea kugundua zaidi



Maoni