Follow: STORY ZA Zamrata
Mlango ulipogongwa, pumzi zetu zilihama kwa kasi.
Mimi na Juliet tulibaki tumezizima, macho yetu yakikutanisha hofu na shauku kwa wakati mmoja. Sauti ya kugonga haikuwa nzito, ilikuwa nyepesi, ya mtu asiye na haraka – lakini kwangu mimi ilisikika kama radi katikati ya usiku.
Juliet alinishika kifuani, akawa anatetemeka kidogo.
> “Vicent… nani huyo? Shangazi amerudi mapema?”
Nilinyamaza, nikainua mkono kuashiria tulie. Miguu yangu ilikuwa mizito, lakini nikavuta ujasiri, nikasogea taratibu kuelekea mlangoni. Nilipoweka sikio langu karibu, nilihisi pumzi ya mtu, lakini hakusema neno. Aliendelea tu kugonga mara ya pili – kwa nguvu kidogo kuliko ya mwanzo.
Juliet alinikodolea macho, moyo wake ukipiga kama ngoma ya sherehe.
Niliamua kufungua – kidogo tu, kwa mwanya.
Cha kushangaza… hakukuwa na mtu!
Njia ya korido ilikuwa wazi, taa ndogo ya ukutani ikiwaka, kimya kimetawala. Nilipogeuka kumtazama Juliet, tayari alikuwa amejifunika na shuka, macho yake yakinitafuta kama mtoto aliyeogopa giza.
Niliporudi kitandani, nilimkumbatia na kumnong’oneza:
“Usiogope, mpenzi… huenda ni upepo au mtoto wa jirani aliyepita tu.”
Lakini moyoni nilijua, hii haikuwa kazi ya upepo. Ilikuwa ni ishara – ama bahati mbaya, ama onyo.
Juliet alijikunyata kifuani mwangu, kisha taratibu akaanza kunong’ona:
> “Vicent… leo nimeamini mapenzi ni hatari. Lakini najua bila wewe, moyo wangu hauna pumzi.”
Nilimwangalia, macho yetu yakazama kwenye dimbwi moja la hisia. Nilipomsogelea tena, moto uliokuwa umepoa ghafla baada ya kugongwa mlango ulianza kurudi. Mikono yetu ikarudi pale pale – safari ya miili ikaanza upya, sasa kwa hamu yenye hofu ya kufumaniwa.
Pumzi zikawa nzito, sauti zikazimwa ndani ya mito, na jasho likaanza kudondoka tena kama awali…
Tulijua tunaiba muda. Tulijua tukifumaniwa, kila kitu kitakuwa kimekwisha.
Lakini nani anayeweza kuzima moto wa mapenzi mara unapowaka?
ITAENDELEA… 🔥.
Hakuna ratiba iliyopangwa kwa sasa.
Maoni
Click here to login and comments