VYOTE NDANI GONGA94
BINAMU WEWE UNGEWEZA? SEHENU 06
Usimulizi huu ni wa watu wazima. Chukua muda wako, tulia, kisha usome kwa utulivu kama machapisho yetu yanayoendelea moja kwa moja.
ENDELEA........
Nilicheka huku nalia wao wenyewe walinishangaa huyu vipi?,
"Ni jambo jema na ni matamio yako kwa muda mrefu kuitwa baba. Hongere undugu wangu Manka". Niliongea hayo huku nikiwa nimepambwa na tabasamu lenye maumivu makali sana moyoni.
"Asante soon nampa heshima Sony ya kuitwa baba. Ok tusikuchoshe sana yetu ni hayo tu" Manka aliongea hayo bila hata aibu eti ndugu sisi tumeshea dudu la mwanaume mmoja na wote ni wajawazito na mimba ya huyo bwana Sony.
Nyie nilihisi uchizi mwenzenu.
"Baby nahitaji kupumzika nimechoka sana" Manka aliongea kwa madeko huku amemlalia Sony kifuano. Nyie nilikuwa nahisi labda naota jamani kumbe ni kitu halisi kabisa😭.
Walitoka chumbani kwangu ndipo nilipata nafasi ya kulia. Nililia sana usiku huo hata sijui nilipitiwa na usingizi saa ngapi. Nilikuja kushtuka majira ya Saa tatu asubuhi.
Nilichelewa sana kazini ila sikuacha kwenda.
Baada ya kumaliza kujiandaa nilitoka chumbani, milimkuta Manka amekaa sebleni anakula embe. Sikumsemesha nilimpita ila kabda sijaufikia mlango aliniongelesha.
"Nice haujaniona?" Hata sikumjibu niliendelea na safari yangu.
Nilifika kazini wafanya kazi wote walinishangaa siku hiyo nilikuwa kitofauti kabisa. Kwanza ukiniangalia tu utagundua kuwa naumwa.
Nilipeleka baadhi ya document kwa boss.
"Samahani boss sijisikii vizuri ndo maana unaona nimechewa kufika"
"Najua usiku wa Jana umekesha unalia sana mpaka macho yako yamevimba. Muda wa lunch nahitaji kupata chakula na wewe" Sony aliniambia hayo.
Nilimkabidhi document baada ya hapo nilitoka ofisini kwake.
"Huwezi kuamini Manka ana mimba ya Sony" nilimwambia hayo Sophia na nilishindwa kujizuia kulia.
"Mbona maajabu haya" imekuaje yani mmmh!"
"Moyo wangu umepasuka pasuka"
"Pole my dear. Amini kila kitu kinatokea kwasababu"
"Siamini kama mbwa hawa wanaweza kunikatili namna hii na mbaya sikuwai kuhisi kabisa kama wana mahusiano limekuwa jambo la gafla sana ndo maana naumia zaidi"
"Vipi Sony anasemaje kuhusu ujauzito wako?"
"Hata nguvu za kumwambia kuhusu hii mimba sina tena. Nina mpango wa kuitoa tu MUNGU atanisamehe. Ni aibu ndugu wawili ku share mwanaume mmoja na mbaya zaidi eti wote tumzalie hii ni laana Sophia"
"Ni kweli ila usisubutu kuharibu hii mimba unajua kila pito tunalopitia MUNGU ana makusudi yake".
" kwa sasa hata uongee nini sitokuelewa. Nisamehe kwa hilo my dear ila tambua nipo kwenye wakati mgumu sana"
Majira ya mchana kweli tulienda kula chakula cha pamoja na Sony, chakula chenyewe kilipanda basi?, Nilikubali tu wito wake ili kumsikiliza anataka kuniambia nini.
"Nice!" Sony aliniita kww sauti tulivu.
"Abeee!" Niliitika kwa unyonge.
"Nisamehe kwa kuuvunja vunja moyo wako"
"Ni sawa naamini ilipangwa iwe hivi" Mimi ni mwepesi sana kulia yaani kwenye kulia huwa ni ngumu sana kujizuia, nilianza kulia pasipo kujali uwepo wa watu wengine hapo hotelini.
"Ni kweli mimba ya Manka ni yako?"
"Ndiyo ila sikukusudia na hata ukiniambia nikueleze ilikuaje sielewi. Ila ukweli mimba ni yangu"
"Inawezekana vipi Sony?, kwaiyo nyie watu wa wawili mlipanga kunisaliti na kuurarua moyo wango, hakika umejua kuniumiza kupita kiasi, hichi kidonda sijui kama kitakuja kupona kwenye maisha yangu"
Niliongea hayo huku nikiwa nalia.
"Tuweke tofauti zetu pembeni kwanzu. Bado nakuhitaji kwenye naisha yangu. Manka kubeba mimba si jambo baya sana maana ni matamanio yangu kwa muda mrefu kuitwa baba. So ahadi yangu ipo pale pale wewe ndo mke wangu. Nakupenda sana Nice kama unajali Furaha yangu naomba uishi vizuri na Manka" Sony aliongea ni kama vile ni kitu cha kawaida tu........ITAENDELEA......
SIMULIZI :
Umesoma kwa utulivu · dakika chache tu Asante Endelea kusoma chagua hapo chini
Umependezwa ?? Asante Soma Zaidi binamu-wewe-ungeweza-sehenu