NILIUZWA KUWA MTUMWA WA BILIONEA 07/08 Wakati kisu kinanolewa, Ciara alijitahidi kupika chakula alichohisi kitamfaa Katy (Mama yake Mike)
Basi mida ya jioni Mike na Mama yake walikaa mezani.
Chakula kililetwa, Ciara hakuonesha hofu usoni mwake ukilinganisha na Watumwa wengine.
"Karibuni chakula...." Ciara aliongea
Vile Katy alikuwa na shauku ya kutoa adhabu endapo chakula kitakuwa kibaya aliwahi kushika kijiko.
Kadri alivyozidi kula ndivyo hasira na kisirani viliyeyuka.
"Hiki chakula kapika nani siamini kama kimepikwa na watu wengi" Katy aliuliza
"Kapika Katy....." Jala (Mtumwa mwenye umri mkubwa kuliko wote) alizungumza
Umepika vizuri kama unampikia Mama yako, na hivyo ndivyo inatakiwa kuwa bila kujalisha nyie ni Watumwa mahali hapa" Katy aliongea
Muda wote macho ya Mike yalikuwa kwa Ciara, ni vile Binti huyu hakujua tu kama anatazamwa.
Suzy pia alijikuta akimuangalia Ciara, hakuelewa kwanini Mike anamtazama Mtumwa huyu kwa umakini namna hii.
"Sioni maajabu yake, labda kama umbile lake limezidishiwa kipimo cha sukari..." Suzy alijisemea ndani ya moyo wake
Muda wa kulala ulivyofika Ciara hakuwa akikumbuka kama anatakiwa kulala chumbani kwa Mike.
Mike akiwa chumbani kwake aliendelea kumsubiria lakini hakutokea, uvumilivu ulimshinda. Alivaa koti lake kisha akaelekea chumbani kwa Ciara.
Wakati yote haya yanafanyika Katy na Suzy walikuwa juu ya kibaraza wakishuhudia
"Ulipaswa unipatie hii taarifa mapema. Macho yake hayaoneshi kuogopa chochote, huu ni udhaifu tosha kwa Mike. Kijana wangu anapenda Wanawake wanaojiamini na wasio na shobo kwake..... inaonekana Ciara anamfahamu Mike toka zamani. Nachotaka kusema ni kwamba siyo Watumwa wote wapo hapa kutii amri.... wengine wako hapa kumtega Mike" Katy aliongea
"Kwahiyo unataka kusema Ciara hakuuzwa hapa kwa bahati mbaya" Suzy aliuliza
"Na ndio maana nakupenda, siku zote huwa una uwezo wa kufikiria haraka. Hebu naomba uichunguze familia aliyotoka Ciara....kama utakuta wana utajiri wowote ule basi fikira zako zitakuwa sahihi kuwa hakuuzwa hapa bahati mbaya" Katy aliongea
"Nahitaji kufanya uchunguzi muda huu, pindi kutakapo pambazuka sitapata hiyo nafasi" Suzy aliongea kisha akasepa
Katy akiwa kasimama bado juu ya kibaraza alimshuhudia Mike akiwa kambeba Ciara.
Kuna namna moyo wake uliumia, mpaka sasa hajaona Mwanamke anayestahili kuwa na Kijana wake kama angekuepo basi angebariki ndoa.
Upande mwingine Suzy anafanikiwa kufika nyumbani kwa Jasinta baada ya kupeleleza kwa Walevi kwenye vilabu vya pombe.
Anafanikiwa kupuliza dawa ya usingizi kwenye vyumba vyao. Hii ilimpa urahisi wa kuvunja dirisha na kuingia ndani.
Uwezo wake wa kupekua sehemu anazohisi zitakuwa na hazina ulikuwa juu sana.
Kwa haraka alifanikiwa kuona saa mbili za dhahabu.
"Kama angeuza saa moja Jessa angesaidika bila hata kumuuza Ciara.... hivyo basi Ciara yupo kwenye jengo la Mike kwa majengo binafsi" Suzy alijisemea ndani ya moyo wake kisha akasepa.
Haraka aliyokuwa nayo miguuni kwake haikuelezeka. Wakati Mike anakazana kumpelekea moto Ciara, Suzy alifika mlangoni kwa Katy kutoa taarifa
"Ahsante kwa taarifa yako..... kuanzia kesho kila kitu kitabadilika. Ciara nitampitisha kwenye mitihani migumu ambayo hajawahi kuiona."
"Kuliko ufanye hivyo itapendeza kama tutamuondoa mahali hapa..."
"Mtumwa yoyote yule hawezi kuondoka hapa bila amri ya Mike. Usisahau kama hii si nyumba yangu, ni ngumu kuvunja sheria za Mike.....nitamuondoa hapa Ciara kwa akili kubwa. Ahsante kwa kuniletea taarifa sahihi" Katy aliongea
Suzy aliachia tabasamu kisha akaondoka, taratibu alisogea kwenye mlango wa Mike kuhakikisha usalama.
Anakutana na vicheko, yaani Mike na Ciara walikuwa wanafurahi kana kwamba wamefahamiana kwa muda mrefu
Itaendelea π₯
NILIUZWA KUWA MTUMWA WA BILIONEA 08
Kulivyo pambazuka asubuhi, Katy aliamka akiwa na nguvu mpya na hali mpya.
Bila kupoteza muda aliomba kuitiwa Ciara.
"Nitakuwa bustanini naomba afanye haraka kuja...." Katy aliongea kisha akaelekea bustanini
Ciara alichanganyikiwa kidogo hii nyumba ina bustani mbili alishindwa kuelewa Katy atakuwa wapi hivyo alijikuta akienda huku na kule..... bahati nzuri alimkuta kwenye bustani inayopendelewa zaidi na Mike
"Nisamehe kwa kuchelewa...." Ciara alijitetea
"Ni kama unanilazimisha ni kusamehe...."
"Hapana, uzito wa sauti yangu naomba usiiufikirie"
"Sawa.....nimemwaga mchele bahati mbaya kwenye bustani pendwa ya Mike, sijui utautoaje naomba unisaidie kuiweka sawa"
"Usiwe na shaka nitautoa wote" Ciara aliongea
Mchele ulikuwa umetapakaa bustani nzima tena kwenye nyasi fupi.
Ciara alianza kuokota, masaa yalizidi kutembea.....Katy alisepa zake akamuacha.
Mpaka jua linazama alikuwa hajamaliza
"Ni kitu gani unafanya...." Mike aliuliza
"Natoa mchele...."
Mike aliangalia kwa haraka haraka kila sehemu ilikuwa imetapakaa mchele
"Hii ni adhabu au ni nini..."
"Siyo adhabu, ni jukumu langu kutoa uchafu kwenye bustani yako"
"Kuna kazi nataka unifanyie, hii naomba uachane nayo watakuja kumalizia watu wengine"
"Kama nitakusikiliza wewe nitaonekana na mdharau Mama yako..."
Mike aliachia tabasamu kisha akamnyanyua Ciara
"Wewe ni Mtumwa wangu nilikununua kwa pesa zangu hivyo nitafurahi kama utayapa maneno yangu kipaumbele kuliko ya mtu mwingine...."
"Ni kazi gani hiyo unataka nikufanyie...."
"Njoo utaiona..."
Basi kwa pamoja waliongozana, Katy akiwa anaongea na Suzy alishangaa kumuona Mike akiongozana na Ciara kuelekea ndani.
"Hebu nenda kaangalie kama kazi niliyompatia imekamilika...." Katy aliongea
Suzy alienda kuangalia, alikuta Watumwa wengine wakifanya kazi aliyopatiwa Ciara
"Si rahisi yeye kukusikiliza wewe kwa sababu ni Mtumwa wa Mike...." Suzy aliongea kisha akaondoka
Katy alijihisi kudhalilika kupita kiasi....alienda mwenyewe bustanini kushuhudia, ni kweli aliwakuta Watumwa wengine wakiokota mchele
Upande mwingine, Mike aliporomoa nguo zote za kabatini kwake akaanza kupanga na Ciara
"Mara nyingi huwa nakosa usingizi usiku...." Ciara aliongea
"Kwanini...."
"Sielewi, huwa natamani nipate usingizi lakini huwa inakuwa changamoto..."
"Niambie ukweli, ulitamani uwe nani kwenye maisha yako kama ungebahatika kutimiza ndoto zako"
"Mbali na kumpikia Jessa chakula kizuri nilitamani kuwa Mwanajeshi mwenye cheo kikubwa kuliko wote...."
"Mwanamke kabisa unatamani kuwa na ndoto ngumu kama hiyo...."
"Siyo ndoto ngumu ni vile tu sikubahatika kutimiza ndoto zangu"
"Ni afadhali hata hukufanikiwa, sidhani kama Mimi na wewe tungeonana...."
"Hauna tofauti na Wachawi, nilitarajia utahuzunika kwa kushindwa kufikia malengo yangu cha ajabu umefurahi"
"Nina sababu ya kunifanya nifurahie kufeli kwako"
Ciara alisitisha kukunja nguo kisha akamtazama
"Ni sababu ipi hiyo...."
Mike alisogeza mdomo wake akambusu Ciara kwenye paji la uso
"Nakupenda, kama ungefanikiwa kutimiza ndoto yako sidhani kama tungeonana....namshukuru Shangazi yako kwa kukuuza kwangu"
Maneno haya yalipasua moyo wa Ciara alijikuta akitetemeka kabisa kwa kutangaziwa upendo
Itaendelea π₯
Full 2000
Whatsapp 0657171961
KWETU Morogoro
Makala nyingine zinazocheza na ladha yako
Mapendekezo haya yanatokana na kile unachosoma sasa + Endelea kugundua zaidi



Maoni