*BOSS UNATAKA NA MIMBA HII* Sehemu ya 01 & 2 *___________________________________* Nilikuwa zangu nimekaa, nawaza apo nina kimimba cha miezi 3 natakiwa kuanza clinic, sina wakunipeleka mimba yenyewe aliyenipa kamuona binam yangu, ilihali alishanilipi
Lakini nikiwa natoa machozi alipita kaka mmoja kavaa kishua tu, aliingilia ile mada, kisha akawagombeza, alinishika mkono na kuniomba nikahudumiwe hosptal nyingine, atasimamia kila kitu, kwa ile aibu, sikuwa na pingamizi nilikubali akanichukua nakunipakia kwenye gari, alinipeleka hosptal nyingine ya private, nilipewa huduma nzuri mno, tena yeye ndie alikuwa Doctor mkuu wa pale, alinihudumia vizuri, nilipata amani, wakati naondoka, aliomba anisindikize, asante Doctor nashukuru sana kwa msaada wako, lakini pia usijal nitafika, wewe hudumia wa gonjwa, "Diana usihofu mimi leo niko off, nilikuja tu kwa ajili yako hapa, hivyo kama hutojari, naomba unipe kampan kwa leo...
Nilisita make apo natakiwa kazini nikizidi kuchelewa boss wangu namjua nitakuta kashafura kwa hasira nipewe mvua ya maneno, na mwezi huu natakiwa kulipa kodi, sina hata nusu ya hio kodi, na bado wiki tu, niliona bora tu nikatae ombi lake, samahani kaka angu, naomba unielewe natakiwa kazini nikizidi kuchelewa huenda nikakosa kazi, naomba kwa leo unisamehe sana...
"Dia nitakulipa kwa muda wako, nakuomba tafadhali, Doctor tatizo sio kunilipa tatizo ni nidham ya kazi naweza kukosa kazi milele kwa pesa ya siku moja Doctor, naomba unielewe, " ok unajishughulisha na nini? Ususi na mecup, "ok basi naaomba nikuwahishe kazini tafadhali hili pia usikatae, na kingine naitwa Alexander, nilikubali akanipatia lift adi jirani na salon ya pale mtaani kwetu, nilishuka kwenye gari, wakati na shuka, Doctor akaniomba no nikawa nimempa alidai kwa ajili ya afya yangu, nilishuka kwenye gari, nikasogea mpaka salon, kabla ata sijaingia, da Suz mwenye salon aliniporomoshea mvua ya matusi, nilikaa kimya nakuomba samahani, muda huo kumbe Suzi hakujua ata kama nimeletwa na gari nilijua tu hio itazua makubwa zaid, "kumbe ndio maana umetiwa mimba nakutelekezwa kwa mambo kama haya unaonekana kabisa hujatulla, Suzi alinifukuza kazini, nilijitahidi kumuomba lakini hakunisikiliza hata kidogo nililia nakupiga magoti lakini wapi, alianza kunipiga niondoke kazini kwake nisijekumtia nuksi, ilinibidi tu niondoke kuepuka mengi, wakati naondoka uku nafuta machozi na machozi yenyewe hayataki kukatika, nikashangaa ghafra tu nakumbatiwa...
Itaendelea.
Chapter 2
Niiikumbuka hii harufu nzuri, nimeisikia kwa Doctor Alex, nilijikaza nakumutoa kwenye kumbato, alinitizama kwa huruma nakuniomba, "Dia naomba usiongee chochote, nisikilize mimi tu, sikujibu chochote nilianza tu kwa kumsikiliza alinichukua nakuniingiza tena kwenye gari, yake kumbe hakuwa ameondoka alitaka ajue. mazingira yangu ya kazi, alihakikisha nimekaa vizuri, nikawa nahangaika kufunga mkanga, akaamua kunisogelea, kaka ananukia vizuri huyu adi pumzi yake kuna namna dah, nilijikuta naanza kuona aibu, make aliganda kunitizama uku mkono wake uko unatafuta mkanda ila macho yananitizama sana na pumzi zake zilikuwa kama zinakimbizwa, alivyoona nimeanza kuona aibu alinifungia akakaa kwanza. kwa muda akafunika macho kisha akatoa pumzi kwa nguvu, ndipo akafungua macho nakuanza kuendesha, aliendesha adi maeneo ya beach lakini hii beach, Ilionekana yakishua sana, alipack akanitolea mkanda, nakushuka akaja kunifungulia...
Alinishika mkono, akanipeleka eneo limetulia sana, aliniomba tuketi, tuliketi chini kabisa kwenye mchanga, bahati nzuri nilitembea na kitenge, nilitandika tukakaa, alisema haikuwa na haja apa huwa kuna jamvi, kweli zililetwa,tuliulizwa tunatumia nini, "Dia naomba uchague kinywaji na chakula, niliagiza soda na ugari samaki, ilikuwa mchana tayari, lakini Alex alizuia na kusema, "Dia samahani, kwa ajili ya afya bora yako na mtoto naomba usinywe soda, napendekeza utumie juice, naomba kwenye menyu yako pia ongeza matunda na chai au supu upashe tumbo kwanza naimani hujaonja chochote toka kumekucha...
Nilianza kuona masharti yanakuwa mengi, nikawaza kwanza ata pesa yakulipa apa mbona sina, ivi ninaakili kweli, nikiagiza afu asepe itakuwaje, nilijikuta naomba tu juice, ila Alex alilazimisha, chakula kilikuja nilikuwa nakiogopa, alihisi hofu yangu, akafanya kunitumia muamala kwenye simu yangu, ili mimi ndie nilipie, "Dia nimekutumia pesa apo utanisaidia kulipia bill kupitia simu yako, kucheki muamala ni ml 1, nilishtuka nikahisi huenda kuna mchezo, nilimuita mhudum....
Kulikuwa na no za wahudum, pale pale kwenye mkeka na vifaa vyao vyote waliweka по, mhudum alikuja nikamuomba no ya kulipia, alinipatia na bill ilikuwa ni 130k, nililipia kisha pesa ilivyobaki, niliirudisha kwa Alex, muamala ulivyomfikia akashangaa, naikataa akanirudishia tena ml1, Doctor kwa nini unafanya hivi, mimi hii pesa yako siihitaji, mda huo nanuka shida kwanza, nikitizama kila mtu apo tulowapita apo beach, niliona kabisa ni wakishua mno, mimi ndo nilikuwa wa kawaida...
Alijitahidi kunishawishi, ikabidi nimuulize kwa nini ananipa pesa yote hio? "Dia sikupi kwa nia mbaya, ila nimehisi kuna wakati unapitia hauko sawa, kibinadam tu nimeona nikupe angalau hicho kiasi kikusogeze, siwezi jua kesho nani atanisaidia, hii kwangu naichukulia kama sadaka, aliongea mengi, lakini kwa hekima mpaka nikamuelewa na kumshukuru, alinichangamsha mpaka nikaanza kufurahi, alivunja ukinya akaomba kujua historia yangu...
Nikimtizama nakuomba hio nimpe siku nyingine, alielewa, akaanza kuniimbia, nyie Doctor anasauti nzuri, kiume haswaa, kama hisia zako ni maharage ya mbea, maji mara moja, huwezi kutoboa, sauti yake inatetemesha hisia, unajikuta unaloa tu...
JE NINI
Makala nyingine zinazocheza na ladha yako
Mapendekezo haya yanatokana na kile unachosoma sasa + Endelea kugundua zaidi
Maoni