IN LOVE WITH ZURI* *Chapter 9&10*
SONGA NAYO........
Upande wangu nilikuwa zangu chumbani, nikijiandaa kwa ajiri ya kutoka kwenda kurefresh kidogo, nikiwa najiandaa mara Ethan huyu hapa alikuwa mnyinge kweli
"Vipi tena??"
Nilimuuliza baada ya kumuona amekuwa mnyonge gafla
"Acha tu Frank, huko Zuri amechukia sana hataki hata kuongea na mimi"
Sasa ndio ulikuwa unaniambia mimi niende nikamsaidie kubeba kapu, si ningepigwa kabisa.."
"Sema we nae unazingua sasa kulikuwa na kosa gani la kumgombeza hivyo..??"
"Niache bwana, kichwa changu hakipo sawa..."
Basi niliendelea kujiandaa pale huku Ethan na yeye akiwa ameenda chumbani kwake kujiandaa, baada ya kila kitu tulikutana sebleni, tukiwa ndani ya pamba kali sana
"Mama tunatoka kidogo, msituhesabie chakula cha usiku maana tutakula huko.."
Nilimwambia mama huku tukiondoka, basi baada ya kutoka nje tuliingia kwenye moja ya gari na kuondoka zetu.....
Safari yetu ilienda kuishia nje ya nyumba kubwa sana, ilikuwa nyumba ya kifahari mno, tuliingiza gari mpaka ndani na kushuka, tulikuja kupokelewa na mdada mrembo mno
Nimesahau kuwaambia huyu mdada ndio yule Nancy, na hapa tulikuwa tumekuja kwa sababu alituita, basi bwana akatukaribisha vizuri kabisa na kutupatia vinywaji
Huku story za hapa na pale ziliendelea, basi mida nao ulienda ilipofika saa kumi na mbili jioni ikabidi tuage tuondoke, lakini Nancy alipendekeza kuwa anataka kuongea na mimi
Sikuwa na sababu za kukataa hivyo tulisogea pembeni kwa ajiri ya mazungumzo zaidi.
"Kwanza samahani kwa kukusumbua.."
Nancy aliniambia
"Ah hakuna shida, jisikie huru tu.."
"Ouk, ah nafikiri Bruno alikwambia..??"
"Mh, unamaanisha nini..??"
Nilijizima data ila ukweli nilikuwa naelewa anataka kuniambia nini so nilikuwa nampima tu
"Ah Franksio hivyo bana, lakini mbona me aliniambia amekwambia..??"
"Nancy sifahamu chochote na nina week moja sijaonana na Bruno hata kuongea nae kwenye simu sijaongea nae, sasa unaposema kuwa aliniambia me ndio nikuelewe nini.."
"Basi samahani, sikujua but me nimetokewa kuvutiwa na wewe.."
"Ohoo asante na tena asante sana, am niko na mchumba.."
Nilimwambia, nikamuona Nancy anataka kulia
kabisa mapenzi haya dah
"Frank usinifanyie hivyo, lakini mbona sijawahi kukuona na mwanamke..??"
"Sina cha kukujibu swali lako, ila tambua ya kwamba nina mchumba na soon ninamvalisha pete, so asante kwa kuvutiwa na mimi lakini pia pole maana sijawahi kujua kuwa unanipenda
Najua kwamba unaumia ila siwezi kukuongopea uongo, na mwisho wa siku uumie, am sorry sana na asante kwa kutujali."
Nilisema na bila kupoteza muda nikaondoka zangu nikimuacha akiwa analia kama mtoto, mapenzi shida tupu yani dah au basi tu
Ila wanawake bana sijui huo mshipa wa aibu nyie huwa hamna mpaka mtongoze wanaume, lakini mbona mie siwezi eti jamani ??...
Itaendelea......
Makala nyingine zinazocheza na ladha yako
Mapendekezo haya yanatokana na kile unachosoma sasa + Endelea kugundua zaidi
Maoni