NILIUZWA KUWA MTUMWA WA BILIONEA 09..10. "Vipi Mimi siyo Mwanaume nayefaa kwenye mizani yako?" Mike aliuliza
Ciara aliachia tabasamu, hakutaka kuonesha kuchanganyikiwa na wala hakutaka kuonesha kupuuzia alibakia kuwa vuguvugu
"Nipe muda nifikirie kuhusu hili suala"
"Muda?... usisahau kama nimekununua nina uwezo wa kufanya chochote kile bila kusubiria mtazamo wako"
Ciara aliachia tabasamu kisha akaendelea kukunja nguo. Kila alipoinua macho yake alikutana na macho ya Mike
Iliwachukua muda mrefu kumaliza kukunja nguo.
"Ni saa kamili usiku, sijisikii kula chakula cha hapa naomba tutoke out kidogo na hata hivyo nina muda mrefu bila kula hotelini" Mike aliongea
"Kuna ulazima wa Mimi kwenda?...." Ciara aliuliza kwa sababu alikuwa amechoka
"Nitafurahi kama tutatoka wote...." Mike aliongea
Ciara alienda chumbani kwake kujiandaa. Hakuwa na nguo nzuri ya mtoko hivyo alivaa kujisitiri na si kupendeza
"Naomba usinifuate, siku ya leo nahitaji kuwa huru zaidi" Mike alimzuia Suzy
Suzy alitikisa kichwa kuashiria ameelewa lakini ukweli ni hakufurahishwa na maamuzi ya Bilionea
Kwa mara ya kwanza Ciara aliingia kwenye gari la Mike.
"Sielewi ni vitu gani hivi umevaa, naomba uvue nitakununulia nguo kabla hatujaingia hotelini kupata chakula
"Sawa...." Ciara alijibu akiwa kamkazia macho
"Una macho mazuri...." Mike alimwaga sifa
Mike alisimamisha gari baada ya kufika shopping center ya nguo za kike
Kwa pamoja waliingia dukani, Ciara aseme nini sasa. Alikuwa ametulia zake akamuacha Mike achague nguo
Baada ya hapo waliingia kwa pamoja kwenye chumba cha kubadilisha nguo
Mike alinyoosha mkono wake taratibu akamfungulia Ciara zipu ya gauni alilovaa
Ciara alianza kujaribu nguo moja baada ya nyingine....
Nguo zote zilimpendezea, Mike alijipigia makofi kwa uchaguzi mzuri.
Ciara alivaa nguo moja nzuri kuliko zote, mezani kulikuwa na mapambo basi Mike aliingia jukumu la kumpendezesha
Mapigo ya moyo wa Ciara yalianza kwenda mbio pia hasa kila alipokutana macho na Mwanaume huyu
Wakati Ciara anatoka shopping center, alipozi kidogo baada ya kukutana na Jasinta (Shangazi yake)
Jasinta aliishia kukodoa macho, kwa namna Mike alivyokuwa amemshika mkono Ciara alitosha kuelewa ni kitu gani kinaendelea
"Shangazi...." Ciara aliita
"Nafurahi kuona unaendelea vizuri" Jasinta aliongea akataka kuondoka lakini alitulia kidogo baada ya kukumbuka uwepo wa Mike
"Ahsante kwa kumtunza vizuri Ciara wangu" Jasinta alishukuru kisha akasepa
Sijui nini kilimpata, usiku wake ulikuwa mgumu sana.
Alijikuta akimuonea wivu Ciara,
"Hiyo nafasi inapaswa kuwa ya Jessa na si yake... siwezi kuruhusu aolewe na Mike. Nitamuuza Jessa kwa huyo Bilionea.....binti yangu ni mrembo kuliko Wasichana wote duniani nina uhakika ataonekana machoni kwa Mike kwa wepesi zaidi." Jasinta alijisemea ndani ya moyo wake
Itaendelea π₯
NILIUZWA KUWA MTUMWA WA BILIONEA 10
Upande mwingine, Mike na Ciara waliendelea kufurahia chakula wakiwa katika hoteli ya Sunflower
Macho ya watu wengi yalikuwa kwao, Mike ni mtu mwenye jina kubwa hapa Mjini hivyo huchukuliwa kama kioo cha jamii.
Suzy pia alikuwa kabana kona kwa namna alivyokuwa amevaa isingekuwa rahisi kumtambua. Moyo wake ulikuwa unauma sana hasa kila alipoona Mike ana tabasamu sababu ya Ciara.
Alichomoa bastola kwenye mfuko wa suruali yake, lengo lake lilikuwa ni kumshambulia Ciara, kila alipotaka kulenga shabaha Mike alikuwa kikwazo.
"Una bahati nzuri Mbwa wewe....." Suzy alijisemea ndani ya moyo kisha akaondoka
Wawili hawa hawakurudi nyumbani, kwa mara ya kwanza kabisa Mike alilala nje ya jengo lake
Kulivyo pambazuka asubuhi alimpeleka Ciara nyumbani kisha yeye akaelekea kazini.
"Naomba uniitie Ciara hapa au acha nitamfuata mwenyewe" Katy aliongea kisha akaongoza njia
Hakupiga hodi wala nini alisukuma tu mlango kisha akaingia
"Karibu....."Ciara alizungumza
"Unanikaribisha?....mbona ni ajabu sana" Katy aliongea huku akikaa
Ciara alikuwa amechoka lakini kwa kuwa ni Mtumwa ilimlazimu kusimamia.
"Siku ya jana ulienda wapi na Mike? hebu naomba kujua ni kitu gani umepatia Kijana wangu mpaka akose hata muda wa kuzungumza na Mimi!" Katy alifoka
"Nisamehe, nitamkumbusha atenge muda kwa ajili yako"
"Hakika una kauli zinazo kera moyo wa mtu, hebu vua nione ni kitu gani hicho unacho kinacho changanya akili ya Mike"
"Kuvua? siwezi kufanya hivyo mbele yako...."
"Kwanini?"
"Huu mwili ni wa Mike si kila mtu anatakiwa kuuona"
"Mimi ndio umenijibu hivi?" Katy aliuliza akionekana kuchanganyikiwa kupita kiasi
"Nisamehe kama maneno yangu yana ukakasi"
"Msamaha hauwezi kutolewa kirahisi namna hiyo, naomba unifuate" Katy aliongea kisha akaongoza njia akiwa mwenye ghadhabu
Ciara alimfuata kwa nyuma akiwa mwenye uso wa kujiamini.
Mahali hapa kuna Mbwa wanne wenye ukubwa mfano wa ndama.
Mbwa hawa aliwaleta Katy wakiwa wadogo kabisa kutoka Urusi.
"Utalala na hawa mbwa wote" Katy aliongea kisha akawafungulia
Miingurumo yao tu ilikuwa inatisha mfano wa Simba jike.
Ciara hakutishwa na hawa Mbwa hata kidogo.....
"Mnasubiria nini?....mvulisheni nguo huyu kisha mmpelekee moto" Katy aliongea na mbwa
Hakuna hata Mbwa mmoja aliyediriki kumvamia Ciara......waliishia tu kuunguruma
"Mimi ni Mtumwa wa Mike si rahisi kwa Mbwa hawa kunidharau bila ruhusa ya Bilionea" Ciara aliongea
Hasira ya Katy ilifika mwisho sasa, aliwaita Watumwa wanne wa kiume.
Walimshika Ciara kisha wakamlaza chini.
Katy aliletewa mjeledi, alianza kumchapa
Kitendo cha Ciara kutolia wala kuomba msamaha kilimpandisha hasira, alijikuta akimchapa zaidi na zaidi
"Muondoeni huyu mbwa hapa....." Katy alifoka kisha akatupa mjeledi, alikuwa amechoka kupita kiasi
Badala ya Ciara kulia, yeye ndio alianza kulia sababu ya maumivu ya mkono. Kama utani hivi lakini alishikwa homa kabisa alipatiwa dawa kisha akajifunika gubigubi.
"Hakuna mafanikio yanayokuja kirahisi bila kupitia changamoto" Jala (Mtumwa wa kike mwenye umri mkubwa kuliko wote) alizungumza huku akimpaka dawa Ciara kwenye makalio yake
Ciara aliachia tabasamu kimtindo, si mtu wa kukasirika..... adhabu aliyopatiwa na Katy ilikuwa ni ya kitoto wala haikumuumiza moyo wake
Si kawaida ya Mike kurejea nyumbani mapema kabla ya masaa ya kazi kuisha lakini siku ya leo alifanya hivyo.
"Mama yako anaumwa...." Suzy alimpatia taarifa
"Nitamuona baadae...." Mike alizungumza huku akiwahi chumbani kwa Ciara
Suzy aliishia kukodoa macho, yaani pamoja na kutoa taarifa kuhusu kuumwa kwa Katy lakini Mike alikuwa na uchu wa kumuona Ciara na si Mama yake.
Ciara akiwa amekaa alishtukia tu mlango una funguliwa kisha Mike akaingia
"Kwanini hunipigii simu wala kutuma ujumbe kunijulia hali?"
"Sina simu, ulisema Mtumwa hatakiwi kumiliki simu"
"Nitakununulia simu.... ukweli nimeshindwa kufanya kazi kwa sababu yako" Mike aliongea huku akimvua nguo Ciara
Moyo wake ulishtuka baada ya kuona alama za mijeledi mwilini kwa Ciara
"Ni kitu gani hiki...."
"Naomba uvunge kama huoni...."
Mike alichukua dawa iliyokuwa mezani akaanza kumpaka majeraha yote.
Wakiwa katika kubembelezana taarifa zililetwa
"Jasinta yupo hapa kufanya biashara na wewe" Sauti ya Suzy ilisikika
Itaendelea π₯
FULL Tsh 2000
Whatsapp 0657171961
KWETU Morogoro
Makala nyingine zinazocheza na ladha yako
Mapendekezo haya yanatokana na kile unachosoma sasa + Endelea kugundua zaidi



Maoni